Gurudumu
JF-Expert Member
- Feb 5, 2008
- 2,349
- 261
Kuanzia jioni hii tarehe 8 Februari 2011, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tz litajadili hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyoitoa Bungeni hapo mwezi Novemba 2010. Bunge lina wabunge 350 ambao wengi wao wanahudhuria kikao hiki, pamoja na watendaji wote wa Ofisi ya Bunge na baadhi ya maafisa wa serikali.
Wote hawa wanahitaji kulipwa posho na marupurupu mengine ambayo wanastahili. Nitaomba mwenye hesabu ya haya marupurupu atupatie kwa wabunge na watendaji wote hao kwa siku tano ili tujue ni kiasi gani cha pesa kitatumika kujadili hotuba ya rais.
Nadhani hii hotuba iliwahi kujadiliwa sana na wananchi na mijadala ilikuwa inaripotiwa na vyombo vya habari. Mengine aliyoyasema yalionekana ya maana na mengine yalionekana porojo tu.
Sasa, tunatumia pesa za walipa kodi kujadili hotoba ambayo ilikwishajadiliwa? Je hizi pesa hazingeweza kutumika kutatua matatizo ya wananchi kama vile maji, umeme, elimu, afya, n.k? Pengine huu muda ambao wabunge wanatumia kujadili hii hotuba wangeweza kutumia kujadili mambo yanayowakera wananchi. Au warudi kwenye majimbo yao kuhudumia wananchi.
Naomba anayeona umuhimu wa kutumia pesa na muda wote huo kujadili hotuba hii anishawishi vinginevyo, it is misuse of public resource and abuse of powers