Bunge kujadili Hotuba ya Rais kwa Siku Tano, Ni matumizi sahihi ya rasilimali zetu?

Gurudumu

JF-Expert Member
Feb 5, 2008
2,349
261
Kuanzia jioni hii tarehe 8 Februari 2011, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tz litajadili hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyoitoa Bungeni hapo mwezi Novemba 2010. Bunge lina wabunge 350 ambao wengi wao wanahudhuria kikao hiki, pamoja na watendaji wote wa Ofisi ya Bunge na baadhi ya maafisa wa serikali.

Wote hawa wanahitaji kulipwa posho na marupurupu mengine ambayo wanastahili. Nitaomba mwenye hesabu ya haya marupurupu atupatie kwa wabunge na watendaji wote hao kwa siku tano ili tujue ni kiasi gani cha pesa kitatumika kujadili hotuba ya rais.

Nadhani hii hotuba iliwahi kujadiliwa sana na wananchi na mijadala ilikuwa inaripotiwa na vyombo vya habari. Mengine aliyoyasema yalionekana ya maana na mengine yalionekana porojo tu.

Sasa, tunatumia pesa za walipa kodi kujadili hotoba ambayo ilikwishajadiliwa? Je hizi pesa hazingeweza kutumika kutatua matatizo ya wananchi kama vile maji, umeme, elimu, afya, n.k? Pengine huu muda ambao wabunge wanatumia kujadili hii hotuba wangeweza kutumia kujadili mambo yanayowakera wananchi. Au warudi kwenye majimbo yao kuhudumia wananchi.

Naomba anayeona umuhimu wa kutumia pesa na muda wote huo kujadili hotuba hii anishawishi vinginevyo, it is misuse of public resource and abuse of powers
 
Yaaan ni aibu na kero tupu haiezekan maswala ya rais yatumike cku 5 uku jasho le2 linaishia kwa wachache...eti watafte mbinu mbadala ya kuwakaba walipa kodi il wackwepe...yaan i rily hate dic party CCM kwa kujpenda wao 2!
 
Wastage of time na kodi za walipa kodi, kwani aliongea nini cha maana. Bunge litapoteza mvuto kwa wa tz.
 
Mmeona eeh? Yaan hpa c ni sawa kabsa et mckie spika wa bunge alvo mpumbav..yaan nataman npigane na tv hpa!
 
Tupe data bunge lililopita walijadili kwa siku ngapi?

Je ni utaratibu wa kawaida au unataka kuubadili pia?
 
Kwa nini kila mbunge asiandike maoni yake kuhusu hiyo hotuba badala ya kila mmoja kurudia ambayo wananchi wameshasema au wabunge waliomtangulia wameshasema.
 
Ni upuuzi wa mwaka eti kuchangia hotuba iliyoandikwa kisanii namna ile. Kwanza inawezekana hata aliyeitoa hiyo hotuba amesahau ilikuwa inahusu nini. So, it is just wastage of time.
 
ni kweli hakuna umhimu wowote wa hiyo hotuba kwani hain amasilahi yeyote kwa taifa, hotuba ya Mkwere? ndiyo wana discuss kwaa siku tano?
hivi hawana kazi za kufanya? kweli hii serikali ni ya kisaniii sio mchezo.
Tumeona wanafunzi pale UD wameambiwa hakuna pesa kwa sasa hadi bajeti ya mwakani...hivi hawa jamaa huwa wanaakili kweli?
 
Ni upuuzi wa mwaka eti kuchangia hotuba iliyoandikwa kisanii namna ile. Kwanza inawezekana hata aliyeitoa hiyo hotuba amesahau ilikuwa inahusu nini. So, it is just wastage of time.
ur absolutely right, kweli hata aliyeitoa akiulizwa leo hawezi akaielezea, maana ilijaa usanii tu.
 
Tupe data bunge lililopita walijadili kwa siku ngapi?

Je ni utaratibu wa kawaida au unataka kuubadili pia?
we know that ur the ccm sevant
watu kama ninyi hamtakiwi kbisa ktika hiii nchi na ingekuwa nchi zingine wangelishakuuza kabisa maana ni mtoto asiyekuwa na riziki hata kidogo
 
ni kweli hakuna umhimu wowote wa hiyo hotuba kwani hain amasilahi yeyote kwa taifa, hotuba ya Mkwere? ndiyo wana discuss kwaa siku tano?
hivi hawana kazi za kufanya? kweli hii serikali ni ya kisaniii sio mchezo.
Tumeona wanafunzi pale UD wameambiwa hakuna pesa kwa sasa hadi bajeti ya mwakani...hivi hawa jamaa huwa wanaakili kweli?

Hao wanafunzi wa vyuo vikuu ndo sasa wapige hizo hesabu na umuhimu wa hiyo hotuba kutumia pesa nyingi na muda wa watu wengi hivyo kuijadili. Wajiulize nini cha muhimu zaidi kati ya hotuba ya rais au elimu ya juu.
 
Kati ya mbinu chafu za CCM kutaka kuhakikisha kwamba matakwa ya umma hayapitishwi kokote huko bungeni, hii ni mojawapo na tunaendelea kuwatazama kwa jicho la kuuliza zaidi.
 
hata wakipiga unadhania hiyo serikali ya kinyanganyi na kilaghai itawasikia?
 
Kati ya mbinu chafu za CCM kutaka kuhakikisha kwamba matakwa ya umma hayapitishwi kokote huko bungeni, hii ni mojawapo na tunaendelea kuwatazama kwa jicho la kuuliza zaidi.
hapo kwenye red hapo, u mean question mark right?
 
Ni ukweli usiopingika kuwa siyo matumizi mazuri ya rasilimali zetu. Naomba tuwe makini ili mwisho tupime kama kweli kuna 'VALUE FOR MONEY' wote tunajua kikao hiki kinatugharimu shs ngapi kwa kila siku.

I bet 75% ya muda huo utatumika kushukuru na kupongezana.

Kumbuka wakati wengine wako pale kuona jambo linaamuliwa kumkwamua Mwananchi wengi wapo kuona hakitoki chochote kitakacho affect status cuo
 
Nimepata taarifa kuwa bunge litatumia muda wa siku tano kujadili hotuba ya rais ya ufunguzi wa bunge. Pamoja na kuungana na wale wanaosema kuwa ni kupoteza muda, binafsi nina wasiwasi hata aliyeitoa hiyo hotuba kama atakuwa anakumbuka alichoongea. Ni bahati mbaya hatuna namna ya kufanya majaribio ya hicho ninachosema.
 
Anne kilango alitumia dakika zake zote kutupa vijembe kwa Chadema. Je hiyo nayo ilikuwa kwenye hotuba ya rais?

Halafu sijui ni macho yangu au kweli yu mjamzito? Kama kweli hongera zake
 
Anne kilango alitumia dakika zake zote kutupa vijembe kwa Chadema. Je hiyo nayo ilikuwa kwenye hotuba ya rais?

Halafu sijui ni macho yangu au kweli yu mjamzito? Kama kweli hongera zake
labda amenenepa? au anakitambi si unajua tnea wanawake siku hizi wanakuwa na vitambi:msela:
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom