Bila bila
JF-Expert Member
- Dec 20, 2016
- 21,498
- 37,792
Ibara ya 63(3)(e) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inalipa mamlaka Bunge la nchi kujadili na kupitisha mikataba inayoingiwa Kati ya Tanzania na Mataifa mengine. Siku ya majadiliano nilimsikia Spika Tulia na baadhi ya Wabunge akiwemo Kitila Mkumbo wakinukuu Ibara hii kwamba ndiyo imewaba Bunge nguvu ya kujadili na kisha kupitisha mkataba na Dubai Emirate.
Cha kushangaza Jana Spika Tulia kageuka anasema walichopitisha si Mkataba ni makubaliano.
Sasa naomba Wapambe wake mtusaidie ni Ibara ipi ya Katiba inayosema makubaliano nayo yatajadiliwa na kupitishwa na Bunge? Vinginevyo mtuambie labda Spika Tulia analazimisha kutofautisha Mkataba na makubaliano!!