Bunduki Mpya ya Marekani Yenye Uwezo Kumlenga Adui Sehemu Aliyojificha

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,354
33,192
Bunduki Mpya ya Marekani Yenye Uwezo Kumlenga Adui Sehemu Aliyojificha
2194066.jpg

Bunduki mpya ya Marekani XM25 yenye uwezo wa kumtungua adui hata kama amejificha nyuma ya ukuta Monday, June 08, 2009 4:57 PM
Jeshi la Marekani limetengeneza bunduki mpya ambayo ina uwezo wa kumtungua mtu popote pale alipojificha iwe ni nyuma ya ukuta au kwenye mabonde. Picha za bunduki hiyo mwisho wa habari hii. Bunduki hiyo iitwayo XM25 inatumia risasi ambazo hulipuka na kusababisha mvua ya risasi nyingi ndogo ndogo baada ya kwenda umbali uliosetiwa na mtumiaji wa bunduki hiyo.

Jeshi la Marekani litatumia bunduki hizo kuwatungua maadui zao wanaojificha nyuma ya ukuta au kwenye mashimo kwani risasi za bunduki hiyo zikishafika eneo ambalo wamejificha hulipuka na kutoa risasi zingine ndogo ndogo nyingi sana ambazo kuzikwepa ni vigumu sana.

Kwa mfano fikiria mtu amejificha kwenye shimo liliopo nyuma ya mwinuko wa ardhi na kwa mazingira ya kawaida risasi haiwezi kumpata kwa kuwa mwinuko utakuwa kama kinga yake, lakini kwa kutumia bunduki hiyo mpya, risasi itapigwa kwa juu hadi kwenye sehemu ambayo shimo hilo lilipo na itakapofika juu ya shimo hilo italipuka na kutoa risasi ndogo ndogo ambazo zitaelekezwa kwenye shimo hilo.

Bunduki hizo zinatumia mfumo kama wa kompyuta kupiga mahesabu ya sehemu inayotakiwa kulengwa na risasi zake pia zina uwezo wa kupiga mahesabu zimesafiri umbali gani kabla hazijalipuka.

XM25 zimeelezewa na kampuni iliyozitengeneza ya Alliant Techsystems kwamba zitasaidia kupunguza gharama kwani badala ya kurusha bomu ambalo lingerimu maelfu ya dola, bunduki hiyo ikitumika itagharimu dola 20 tu. Bunduki Mpya ya Marekani Yenye Uwezo Kumlenga
541.jpg
Jeshi la Marekani limetengeneza bunduki mpya iitwayo XM25 ambayo ina uwezo wa kumtungua mtu popote pale alipojificha iwe ni nyuma ya ukuta au kwenye mabonde.

Inatumika kufyatua 25 mm grenade.
 
Last edited:
ushahidi vile ambavyo hawajali kuua wananchi ... so-called 'collateral deaths'
... badala ya kutengeneza darubini ambazo zitamuona adui aliejificha nyuma ya ukuta, wanatengeneza bunduki itakayolipua yeyote aliejificha nyuma ya ukuta... sa watoto na wanawake wakijificha, watajulikana vipi ka wao si adui?
...mfano, kule Iraki, so-called adui hawavai nguo za kijeshi, sa watajuaje nani ni adui ???
 
dunia hii inakwisha tena watu badala ya kumrudia mungu ndo kwanza wanatengeneza madubwana ya kuangamizana.
 
Mkuu nakubaliana na wewe,
Sasa subiri uone waarabu na waafrica tutakavyo zinunua kwa wingi ili tufyekane sawasawa!! Wamarekani wenyewe kimyaaaa kwao!
 
zote hizi ni za kummaliza binadamu huyu huyu nayemfahamu ambaye "mbu" (sio wa jf) anamdhibiti???!!
 
[
Marekani inamiliki silaha za nyuklia zenye uwezo wa kuangamiza dunia mara tatu(sijui naeleweka), wana bomu linaloitwa AMOEBI ambalo exploding power yakE ni mara nane ya kombora la nyuklia.isitoshe wana neutron bombs ambayo yana uwezo wa kuua viumbe hai tu na kuacha miji ikiwa ni mizima bila kuharibika.
kwa hizi bunduki mpya sio ajabu,bali cha kujiuliza ni kwamba,wanajiandaa kwa vita ili waje wapigane na nani? THINK ABOUT IT........
 
Naweza ipata wapi niitumie kwa JF members wanaonikera? teh teh teh teh....
 
Duuu hiyo binduki balaaa....sasa sisi africa tunahangaika na mlo mmoja kwa siku wenzetu ......wanafikiriaa mambo mengine kabisa.....
 
Niliposoma kichwa cha habari, nikajua hizo risasi zinakata kona mpaka adui alipo!

Malengo ya kutengeneza madubwesha yote haya, adui anayekusudiwa ni nani? Mimi nafikiri upande wa silaha, wafike mahali waseme sasa basi, kwa sababu watatumaliza!
 
dunia hii inakwisha tena watu badala ya kumrudia mungu ndo kwanza wanatengeneza madubwana ya kuangamizana.
Mwalimi wangu wa Falsafa, aliwahi kunambia...

"Mtawala Mwenye kuwapa Haki Raiya zake, Hana haja ya kununua Silaha"

Hii yote ni dalili ya ubabe na ukandamizaji, wa kutaka kutawala hata wale wasio kuwa kwenye territory yako.
 
Back
Top Bottom