Bububu: CUF kuiburuza tume mahakamani kupinga matokeo

Kakke

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,883
1,482
vvvvvv.jpg

Salim Bimani

Chama cha wananchi CUF kinajiandaa kwenda mahakamani kupinga ushindi wa mgombea wa CCM Hussein Ibrahim Makungu katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Bububu uliofanyika Jumapili iliyopita.

Akizungumza na Zenji FM radio, mkuregenzi wa mawasiliano na haki za binadamu wa CUF Salim Bimani amesema wanasheria wa chama hicho wanaandaa taratibu za kisheria ili kufungua kesi hiyo.

Amesema wana ushahidi wa kutosha wa kukiukwa taratibu za uchaguzi ikiwemo upandikizaji wa wapiga kura.

Bimani amesema taratibu za kisheria za kufungua madai hayo zinatarajiwa kukamilika ndani ya siku 14 tokea kutangazwa mshindi huyo.

Chama cha wananchi CUF kimepinga matokeo ya uchaguzi yaliompa ushindi mgombea wa CCM Makungu kwa kupata asilimi 50.7 ya kura dhidi ya mgombea wa CUF Issa Khamis Issa aliepata asilimia 48.2 ya kura.

Wakati huo huo mbunge wa jimbo la Mtoni Faki Haji Makame amekanusha taarifa za kukamatwa na jeshi la polisi na kufikishwa mahakamani akidaiwa kupigana hadharani siku ya uchaguzi huo.

Akizungumza na wandishi wa habari huko afisi ya wilaya CUF Vuga amesema taarifa hizo alizonukuliwa kamishna wa polisi Zanzibar zina lengo la kupotosha ushahidi dhidi ya kadhia ya kupigwa iliyomkuta siku hiyo.

Makame amesema siku ya tukio hilo alipigwa na vijana watatu kati yao wawili walikamatwa na jeshi la polisi kituo cha Bububu, lakina anashangazwa bado hawajafunguliwa mashtaka

Wacha UAMSHO wachukue jukumu la kuingo'a SIASA Chafu ya Democrasia huko Zanzibari na badala yake waweke Mfumo wa SHARIAH ili heshima ya Zenji irejee kama ilivokuwa mwanzo.

Safi sana Cuf waburuzeni hao wezi mpaka kieleweke!

Dawa si kwenda mahakamani kwa CUF bali kuvunja ndoa ya mkeka ya Maalim Seif na CCM. Vinginevyo wanatwanga maji. Bila kuvunja hiyo ndoa wataendelea kuliwa na CCM mchana kweupe.

Kazi bado mbichi!.. Rais wa urusi Josef Stalin aliwahi kusema, ..Siwaogopi wapiga kura, bali wale wanaohesabu kura ndiyo wanaofanya maamuzi makubwa zaidi. Zanzibar bado kuna tatizo kubwa. Kwa mtaji huu, Serikali ya umoja wa kitaifa mwisho 2015.

Hongereni wanaCUF wenzangu tupo nyuma kati ya hili ila wa kulaumiwa ni nyinyi viongozi wetu mna tulikwambieni kua CCM sio binadamu hao ni midudu tu ila mumedharau kauli zetu....HAKIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII

Huo ndio ukweli mkuu,mke anajua mumewe mdokozi sasa kwa nini kumpeleka mahakamani kwa nini mambo ya unyumba msiyamalize ndani ya nyumaba?

Ivi wewe uliyeleta mada ebu acha kutuchezea tuna mambo muhimu ya kufanya na kujadili sio upuuzi huu wa CUF ivi hapa tunataka ulete hoja imetimia sasa kama wanakwenda mahakamani utwambie kwa makosa yepi waliyofanyiwa ili tupime kuwa wanalogic au hawana

kwa kweli hawa wa CUF wamezowea kulalamika tu hali ya kuwa makosa wanayo wao kama fujo wameanza wao kama wizi au maamluki basi yawezekana pia wameanza wao hawa jaamaa wana penda fujo sana

Na kama mahakamani wangeanza kupelekwa wao kwa kuwepo kwa mawaziri ambao wanaongoza serikali ambayo wanaoongozwa ni ccm na cuf na wananchi waso vyama  kwa nini mawaziri wale waje pale kwa sababu za CUF na huhisi kama wamevuja haki ya mpiga kura na kumshawishi afanye maamuzi ya uwoga

Wacha waende na kama huamini ni tishia ***** tu hawendi popote kozi hawana mashiko

Sasa CUF waligombea kama chama pinzani au kama wana ndoa? Coz nijuavyo mimi wako kwenye ndoa ya kuongoza huko visiwani

Back
Top Bottom