Bro wangu kanichosha sana, nampiga chini leo leo! Nimechoka!

HorsePower

JF-Expert Member
Aug 22, 2008
3,612
2,566
Huyu ni kaka yangu kabisa, mama mmoja baba mmoja. Ana miaka 38 na kabla ya kuzaliwa mimi, walizaliwa kaka na dada zangu wengine 2, hivyo mimi ni mdogo wake wa 3, na hapo unaweza kujua tumepishana umri kiasi gani!

Haileweki. Alimaliza form akafeli. Wazazi walimlazimisha shule akakataa kata kata. Akawa anashinda anazurura na kufanya kazi za udalali huku akiishi kwa sisi wadogo zake. Alikuwa anakaa kwa kaka zangu mwanzo, akawa na tabia za ulevi wa kupindukia na kuiba vitu vidgo vidogo na kusumbua shemeji zake. Tumemkalisha vikao na kumuonya kashindwa kubadili tabia.

Kila mtu alimchoka tukaamua kumuacha na kuanza kuishi maisha kama chokoraa! Nilimuonea huruma, nikamchukua akae nyumbani kwangu. Nilijaribu kumfungulia miradi ikafa kwa maana ni muhongaji mzuri wa wanawake! Nilimpa hela aenda driving, na kupata leseni ili nifanyie mpango kazini kwangu akala hela zote na leseni hakupata. Niliamua kumtafutia leseni kwa juhudi zangu na kumpeleka akawe dereva kwenye kampuni moja kubwa ya kusafirisha mizigo, akaishia kutumia magari kubebea vimwana. Akafukuzwa kazi

Sasa kaanza tabia ya udokozi wa vitu vya ndani na kuuza na kuleta wanawake huku akiwadanganya kuwa nyumba na usafiri wangu vyote ni vyake, ila kaamua kuniachia mdogo wake. Na sasa kuna msichana wake kanitumia meseji eti kwa nini nang'ang'ania nyumba na usafiri wa kaka badala ya kujitafutia maisha yangu mwenyewe! Thats is to say, hata wasichana wake wanaamini kuwa mimi ndo ninaishi kwa kaka! Wananisumbua, eti nawabana! - Sijui wana upeo mdogo kiasi gani!

Sasa mtu kama huyu hasaidiki, nitampeleka wapi? Nampiga chini leo leo. Namfukuzia mbali! Nimechoka!
Naomba ushauri!

HorsePower
 
Damu ni nzito kuliko maji, hayo ni mambo ya Familia, kama ni mali yako ni mali yako tu.......by the way mwenye mali siku zote haitaji kutambulishwa bali status yenyewe itajieleza.

Usijaribu kuja kuchukuwa ushauri wa Familia hapa jamvini familia zetu hazifanani, labda nikupe mfano mdogo tu nina shemeji yangu niliwahi kumtembelea nyumbani kwake watoto wake wote wapo Uganda shule na mmoja yupo hapa Bongo kwenye chuo kikukuu x, lakini pale nyumbani kwake nilikuta extended family ya watoto 15 wanaomtegemea yeye kura kulala, sasa huyu angeniomba ushauri ningemwambia timuwa wote angalau wabaki wawili, je unajuwa asili ya familia yao?
 
wewew huo ni undugu sio rafiki huyo, ongea nae na aondoke kwa amani, hapa si mahala pake mpwa
 
Unapomuadhibu mtoto si kwamba humpendi, ila unapenda awe na maisha mazuri hapo baadaye. Hivyo kumfukuza kaka yako ambaye hasidiki si kumuonea ni kumtaka ajirekebishe kwani anavuna alichopanda huenda akili ikavujia japo kusikia kwa kenge ni mpaka damu ivujie masikioni, au sikio la kufa...
 
jf atutatui matatizo ya kifamilia kama yenu tena uache kuchezea na kudharau jukwa ahili malizana na ndugu zako atuitaji hata kujua umwamwaga ujammwaga ..ukioa njoo tukufunde hayo ndiomambo tunasaidia ahumu mwisho utatanza kutuandikia jamani nimepigwa na mama yangu mzazi...then tukusaidieje???
 
Mkuu huyu ni ndugu yako tuu hata ukimfukuza utamtafuta tuuu!
wengine wanahitaji maombi eeeti!
 
Tumia busara zaidi. Utamtimua leo, kesho anauawa na wananchi wenye hasira kali kisa kadokoa sufuria la wali. Sijui utajisikiaje?
Watu wengine wanapata baraka/riziki kwa sababu ya watu wanaowasaidia. Mungu anajua ni mzigo gani ulionao na ndiyo maana unafanikiwa.

Case yako haitofautiani na ya kwangu, lakini siwezi kukata mkono wangu eti kwa kuwa nimeunyea.
Kaa naye, usichoke kumkosoa.
 
jf atutatui matatizo ya kifamilia kama yenu tena uache kuchezea na kudharau jukwa ahili malizana na ndugu zako atuitaji hata kujua umwamwaga ujammwaga ..ukioa njoo tukufunde hayo ndiomambo tunasaidia ahumu mwisho utatanza kutuandikia jamani nimepigwa na mama yangu mzazi...then tukusaidieje???

Ninavyofahamu hili ni jukwaa la MMU yaani Mahusiano, Mapenzi na Urafiki, nafikiri mahusiano ni pamoja na hilo nililoliandika!
 
Huyo aliyekuambia ni mbeya NA ANAMUONEA WIVU KAKA YAKO.

Mnvumilie tu kaka yako huyo!

Unataka umtimulie wapi sasa?
 
Mkuu kuna kitu unatakiwa kuelewa,huyo bro wako bado hajapata akili ya maisha,tunatofautiana wengine wanapata akili ya maisha wakiwa wadogo wengine wanapata wakiwa wakubwa,nakushauri ongea naye fresh,kama anakunywa na wewe unakunywa nenda naye mahali agiza moja baridi moja moto pale ndio umpe hayo maneno yako,lakini atakuja kupata akili huyo utamshangaa ndugu,usifanye kosa la kumfukuza ndugu yako ni mbaya kinoma leo kwake kesho kwako
 
jf atutatui matatizo ya kifamilia kama yenu tena uache kuchezea na kudharau jukwa ahili malizana na ndugu zako atuitaji hata kujua umwamwaga ujammwaga ..ukioa njoo tukufunde hayo ndiomambo tunasaidia ahumu mwisho utatanza kutuandikia jamani nimepigwa na mama yangu mzazi...then tukusaidieje???
wacha maneno mbofumbofu wewe, we unataka uletewe habari za demu wangu kaniacha, au mchumba wangu haniridhishi ndo utoe ushauri?
 
Mkuu kuna kitu unatakiwa kuelewa,huyo bro wako bado hajapata akili ya maisha,tunatofautiana wengine wanapata akili ya maisha wakiwa wadogo wengine wanapata wakiwa wakubwa,nakushauri ongea naye fresh,kama anakunywa na wewe unakunywa nenda naye mahali agiza moja baridi moja moto pale ndio umpe hayo maneno yako,lakini atakuja kupata akili huyo utamshangaa ndugu,usifanye kosa la kumfukuza ndugu yako ni mbaya kinoma leo kwake kesho kwako

Miaka 38 jamani bado hajakuwa?
 
watu wa namna hii wapo kwenye familia kama unaweza kukutana na ndugu wa karibu kuweza kuongea swala hili upate mawazo tofauti kabla ya kumfukuza ikiwezekana umfukuze ndugu wakiwepo kuondoa lawama baadae
 
Back
Top Bottom