Bro wangu kanichosha sana, nampiga chini leo leo! Nimechoka!

Bora huyo kaka yako,nikikuhadithia ya kaka yangu,mbona kaka yako utamsifia??anyway solve kifamilia!
 
Hii imekaa kifamilia zaidi! Busara inahitajika sana,wasiliana na nduguzo. Naungana nawe kumuondoa kwako,kaeni kifamilia na umueleze sababu zinokufanya ushindwe kuishi nae pamoja,mueleze wazi upo tayari kumsaidia akiwa nje ya nyumbani kwako.
 
he is 38 n living to his younger brothers???...UKIMZOEA MBWA UNATIA NAYE MAGUU MASJID...dogo horse power naona uliamua kumzoea mbwaa sasa umejikuta naye kunako mswala ndani ya masjidi....

wewe nani alikuambia kaka analelewa na mdogo wake and not vice versa??..hujui kaka ndio anamlea mdogo wake???
....kwa hiyo wewe umeenda kinyume cha nature...kaka maji hayapandi mlima milele maji hufuata mkondo kunako mteremko...

SASA UNALOOOO...toka kwa kakako acha kumbanabana...aftrall ushakuwa unahitaji kujitegemea mpishe broo wako 38yrs aweze kuoa na atumie nyumba na gari zake kwa nafasi na mademu wake...

horsepowerrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr...chezea kakako weyeeeeeeeeee...unalooooo.
 
Kaka kweli umenichoka, yaani niondoke tena nyumbani kwangu? abadani asilani siwezi!!!
 
Huyu ni kaka yangu kabisa, mama mmoja baba mmoja. Ana miaka 38 na kabla ya kuzaliwa mimi, walizaliwa kaka na dada zangu wengine 2, hivyo mimi ni mdogo wake wa 3, na hapo unaweza kujua tumepishana umri kiasi gani!

Haileweki. Alimaliza form akafeli. Wazazi walimlazimisha shule akakataa kata kata. Akawa anashinda anazurura na kufanya kazi za udalali huku akiishi kwa sisi wadogo zake. Alikuwa anakaa kwa kaka zangu mwanzo, akawa na tabia za ulevi wa kupindukia na kuiba vitu vidgo vidogo na kusumbua shemeji zake. Tumemkalisha vikao na kumuonya kashindwa kubadili tabia.

Kila mtu alimchoka tukaamua kumuacha na kuanza kuishi maisha kama chokoraa! Nilimuonea huruma, nikamchukua akae nyumbani kwangu. Nilijaribu kumfungulia miradi ikafa kwa maana ni muhongaji mzuri wa wanawake! Nilimpa hela aenda driving, na kupata leseni ili nifanyie mpango kazini kwangu akala hela zote na leseni hakupata. Niliamua kumtafutia leseni kwa juhudi zangu na kumpeleka akawe dereva kwenye kampuni moja kubwa ya kusafirisha mizigo, akaishia kutumia magari kubebea vimwana. Akafukuzwa kazi

Sasa kaanza tabia ya udokozi wa vitu vya ndani na kuuza na kuleta wanawake huku akiwadanganya kuwa nyumba na usafiri wangu vyote ni vyake, ila kaamua kuniachia mdogo wake. Na sasa kuna msichana wake kanitumia meseji eti kwa nini nang'ang'ania nyumba na usafiri wa kaka badala ya kujitafutia maisha yangu mwenyewe! Thats is to say, hata wasichana wake wanaamini kuwa mimi ndo ninaishi kwa kaka! Wananisumbua, eti nawabana! - Sijui wana upeo mdogo kiasi gani!

Sasa mtu kama huyu hasaidiki, nitampeleka wapi? Nampiga chini leo leo. Namfukuzia mbali! Nimechoka!
Naomba ushauri!

HorsePower

Waswahili walinena "ndugu wakigombana chukua jembe ukalime" Uamuzi ni wako wewe mwenyewe.

Kama wewe ni mpenzi wa filamu tafuta ile ya catoons inayoitwa "The Lion King". Kuna Character anaitwa Zazu, wakati mfalme Mufasa amegombana na mdogo wake Scar, Zazu alimwambia " There is one in every family, two in mine actually". maana yake ni kwamba, kila familia ina matatizo yake na hakuna ukoo utakaokuwa hauna matatizo kama hayo yako au mengine.

Nakushauri mkae kama familia na kuweka msimamo namna ya kumsaidia huyo ndugu yenu. Kwa kawaida hatuchoki kwa kuwa hata akikutwa ameiba, ameugua au amekufa bado ndugu zake mtatafutwa. Mara nyingi hamtaweza kukataa au kumkimbia!
 
Mtathmini utambue kama anafanya makusudi au la, kama anafanya makusudi mfukuzie mbali kwa mwl dunia ambaye mimi binafsi sikubali kufundishwa nae!
 
Mwambie ukweli kwamba kakushinda".. Mtaftie chumba mbali aende,
 
Bora huyo kaka yako,nikikuhadithia ya kaka yangu,mbona kaka yako utamsifia??anyway solve kifamilia!

Duuu, kumbe tuko wengi wenye haya matatizo! Itabidi uni-pm nijue mwenzangu ulisolve vipi maana kama familia tumekaa vikao mpaka suruali zinatoboka!
 
Huyu ni kaka yangu kabisa, mama mmoja baba mmoja. Ana miaka 38 na kabla ya kuzaliwa mimi, walizaliwa kaka na dada zangu wengine 2, hivyo mimi ni mdogo wake wa 3, na hapo unaweza kujua tumepishana umri kiasi gani!

Haileweki. Alimaliza form akafeli. Wazazi walimlazimisha shule akakataa kata kata. Akawa anashinda anazurura na kufanya kazi za udalali huku akiishi kwa sisi wadogo zake. Alikuwa anakaa kwa kaka zangu mwanzo, akawa na tabia za ulevi wa kupindukia na kuiba vitu vidgo vidogo na kusumbua shemeji zake. Tumemkalisha vikao na kumuonya kashindwa kubadili tabia.

Kila mtu alimchoka tukaamua kumuacha na kuanza kuishi maisha kama chokoraa! Nilimuonea huruma, nikamchukua akae nyumbani kwangu. Nilijaribu kumfungulia miradi ikafa kwa maana ni muhongaji mzuri wa wanawake! Nilimpa hela aenda driving, na kupata leseni ili nifanyie mpango kazini kwangu akala hela zote na leseni hakupata. Niliamua kumtafutia leseni kwa juhudi zangu na kumpeleka akawe dereva kwenye kampuni moja kubwa ya kusafirisha mizigo, akaishia kutumia magari kubebea vimwana. Akafukuzwa kazi

Sasa kaanza tabia ya udokozi wa vitu vya ndani na kuuza na kuleta wanawake huku akiwadanganya kuwa nyumba na usafiri wangu vyote ni vyake, ila kaamua kuniachia mdogo wake. Na sasa kuna msichana wake kanitumia meseji eti kwa nini nang'ang'ania nyumba na usafiri wa kaka badala ya kujitafutia maisha yangu mwenyewe! Thats is to say, hata wasichana wake wanaamini kuwa mimi ndo ninaishi kwa kaka! Wananisumbua, eti nawabana! - Sijui wana upeo mdogo kiasi gani!

Sasa mtu kama huyu hasaidiki, nitampeleka wapi? Nampiga chini leo leo. Namfukuzia mbali! Nimechoka!
Naomba ushauri!

HorsePower

usimfukuze, mpeleke kwa watu wa counciling wamfanyie social counselling, afanyiwe rehabilitation.
 
Usimfukuze hata kidogo.

Huyu ni kaka yako, na yanayomsibu ni mtihani tu, mmetoka tumbo moja, jifikirie ingekuwa ni wewe badala ya yeye ungependa kufukuzwa na kunyanyaswa? Inabidi umuenzi na kumheshimu na mapungufu yake yote.

Utamfukuza leo hujui ya kesho.
 
jf atutatui matatizo ya kifamilia kama yenu tena uache kuchezea na kudharau jukwa ahili malizana na ndugu zako atuitaji hata kujua umwamwaga ujammwaga ..ukioa njoo tukufunde hayo ndiomambo tunasaidia ahumu mwisho utatanza kutuandikia jamani nimepigwa na mama yangu mzazi...then tukusaidieje???
I see, wakati mwingine ni vizuri kunyamaza kuliko kutoa majibu usiyoyajua. Mara ngapi watu wanaleta habari za kutofautiana na wake zao au waume zao au kutokuridhishwa na wapendwa wao, na mnayajadili kwenye jukwaa hili hili? Au ya mme na mke si ya kifamilia kulinganisha na kaka na mdogo wake? Kama hatuna majibu sahihi tusikurupuke kujibu.

HorsePower, kakako ni kakako, huyo ni ndugu yako. Hakuna namna nzuri ya kumtosa kabisa. Nafikiri huhitaji kumtimua badala yake unahitaji kuongea naye vizuri na umpe onyo juu ya uwezekano wa kumvukuza hapo nyumbani iwapo atashindwa kubadilika. Na idea nzuri isiwe kumfukuza, pengine ni vizuri kumpangishia nyumba na kumwambia ajaribu maisha yake binafsi kuliko kukaa nyumbani kwako.
 
Hiyo kweli ni ngumu.Kitu cha msingi ni kwwanza kumsaidia huyo kaka yenu mapepo yamtoke ili naye aishi kama mtu.Tafuteni msaada wa maombi na ushauri nasaha kwa wanasaikolojia kabla ya kumtimua.
 
Busara itawale kwa ishu hiyo, huyo ni ndugu yako wa damu hata iweje atabaki kuwa ndugu, mpangie chumba kicha mkabidhi na weka mipaka ya yeye kukanyaga kwako usimwadhibu, mwachi dunia imwadhibu lakini msaidie kumlipia chumba chake tu!
 
Ningekuwa ni mimi ningemtafutie mwanaume wa kumuoa, nadhani ndo kazi anayoweza kuifanya, lol! keirooo!!!!!
 
Huyo dawa yake ndogo! Mpe nauli ya kwenda kijijini, mpe na kama shilingi elfu 50 akawapelekee wazee kule. Najua hatofikisha, na ndio itakuwa tiketi yake ya kumtoa hiyo! Huyo hakufai hata kama ni ndugu yako!
 
Busara itawale kwa ishu hiyo, huyo ni ndugu yako wa damu hata iweje atabaki kuwa ndugu, mpangie chumba kicha mkabidhi na weka mipaka ya yeye kukanyaga kwako usimwadhibu, mwachi dunia imwadhibu lakini msaidie kumlipia chumba chake tu!

Hili nalo Neno!
 
Huyu ni kaka yangu kabisa, mama mmoja baba mmoja. Ana miaka 38 na kabla ya kuzaliwa mimi, walizaliwa kaka na dada zangu wengine 2, hivyo mimi ni mdogo wake wa 3, na hapo unaweza kujua tumepishana umri kiasi gani!

Haileweki. Alimaliza form akafeli. Wazazi walimlazimisha shule akakataa kata kata. Akawa anashinda anazurura na kufanya kazi za udalali huku akiishi kwa sisi wadogo zake. Alikuwa anakaa kwa kaka zangu mwanzo, akawa na tabia za ulevi wa kupindukia na kuiba vitu vidgo vidogo na kusumbua shemeji zake. Tumemkalisha vikao na kumuonya kashindwa kubadili tabia.

Kila mtu alimchoka tukaamua kumuacha na kuanza kuishi maisha kama chokoraa! Nilimuonea huruma, nikamchukua akae nyumbani kwangu. Nilijaribu kumfungulia miradi ikafa kwa maana ni muhongaji mzuri wa wanawake! Nilimpa hela aenda driving, na kupata leseni ili nifanyie mpango kazini kwangu akala hela zote na leseni hakupata. Niliamua kumtafutia leseni kwa juhudi zangu na kumpeleka akawe dereva kwenye kampuni moja kubwa ya kusafirisha mizigo, akaishia kutumia magari kubebea vimwana. Akafukuzwa kazi

Sasa kaanza tabia ya udokozi wa vitu vya ndani na kuuza na kuleta wanawake huku akiwadanganya kuwa nyumba na usafiri wangu vyote ni vyake, ila kaamua kuniachia mdogo wake. Na sasa kuna msichana wake kanitumia meseji eti kwa nini nang'ang'ania nyumba na usafiri wa kaka badala ya kujitafutia maisha yangu mwenyewe! Thats is to say, hata wasichana wake wanaamini kuwa mimi ndo ninaishi kwa kaka! Wananisumbua, eti nawabana! - Sijui wana upeo mdogo kiasi gani!

Sasa mtu kama huyu hasaidiki, nitampeleka wapi? Nampiga chini leo leo. Namfukuzia mbali! Nimechoka!
Naomba ushauri!

HorsePower

kama kweli hayo yote umemfanyia na bado anazingua, bora mpe mtaji kisha mwambie home kwako aondoke kumbuka nakwambia ndugu wanasumbua sana ni bora aondoke kwa amani...otherwise atakuwa kero kwako na mwisho majirani na ndugu wengine watasema anamnyanyasa ndugu yako kisa unapesa. the sooner the better
 
Back
Top Bottom