Bro wangu kanichosha sana, nampiga chini leo leo! Nimechoka!

kaka wa namna hiyo ukifumba macho anakomba kila kitu wanao hawataambulia hata ndururu...
 
Kaka Mistari imetulia mno!!!
Mi nakuhakikishia kama tukiingia studio ukampata mtu akakuingizia korasi mbona utatoka tu mwana!!!!
 
Kaka inabidi uwe na maneno machache sana. NAOMBA UENDE UKATAFUTE SEHEMU NYINGINE YA KUKAA, NITAKUSAIDIA UKIWA HUKO.
Hili limeshanitokea ila ni kwa dogo alikuwa kila nikirudi home namkuta na demu home vinywaji vyote kwenye friji wamefuta na anasema ananilea mimi, nilifanya maamuzi magumu na kumtimua. Kuanzia hapo nawasaidia huko huko waliko sitaki wafike kwangu bila ya mimi kuwaita. Heri lawama kuliko fedheha bro. Wewe ni mtoto wa Kiume
 
Huyu ni kaka yangu kabisa, mama mmoja baba mmoja. Ana miaka 38 na kabla ya kuzaliwa mimi, walizaliwa kaka na dada zangu wengine 2, hivyo mimi ni mdogo wake wa 3, na hapo unaweza kujua tumepishana umri kiasi gani!

Haileweki. Alimaliza form akafeli. Wazazi walimlazimisha shule akakataa kata kata. Akawa anashinda anazurura na kufanya kazi za udalali huku akiishi kwa sisi wadogo zake. Alikuwa anakaa kwa kaka zangu mwanzo, akawa na tabia za ulevi wa kupindukia na kuiba vitu vidgo vidogo na kusumbua shemeji zake. Tumemkalisha vikao na kumuonya kashindwa kubadili tabia.

Kila mtu alimchoka tukaamua kumuacha na kuanza kuishi maisha kama chokoraa! Nilimuonea huruma, nikamchukua akae nyumbani kwangu. Nilijaribu kumfungulia miradi ikafa kwa maana ni muhongaji mzuri wa wanawake! Nilimpa hela aenda driving, na kupata leseni ili nifanyie mpango kazini kwangu akala hela zote na leseni hakupata. Niliamua kumtafutia leseni kwa juhudi zangu na kumpeleka akawe dereva kwenye kampuni moja kubwa ya kusafirisha mizigo, akaishia kutumia magari kubebea vimwana. Akafukuzwa kazi

Sasa kaanza tabia ya udokozi wa vitu vya ndani na kuuza na kuleta wanawake huku akiwadanganya kuwa nyumba na usafiri wangu vyote ni vyake, ila kaamua kuniachia mdogo wake. Na sasa kuna msichana wake kanitumia meseji eti kwa nini nang'ang'ania nyumba na usafiri wa kaka badala ya kujitafutia maisha yangu mwenyewe! Thats is to say, hata wasichana wake wanaamini kuwa mimi ndo ninaishi kwa kaka! Wananisumbua, eti nawabana! - Sijui wana upeo mdogo kiasi gani!

Sasa mtu kama huyu hasaidiki, nitampeleka wapi? Nampiga chini leo leo. Namfukuzia mbali! Nimechoka!
Naomba ushauri!

HorsePower

Duh, mkuu pole sana asee, Yule demu kakumwaga bado kaka mtu naye analeta zakuleta hapa.. Mpe onyo la mwisho.
 
Kama una ushauri mbadala, please nipatie, vinginevyo kanichosha! Nampiga chini!

Kaeni ndugu wote kwa pamoja, shaurianeni, mtafutieni chumba chake, mlipie, ndugu wote mchange mmpe mtaji akiharibu tena baaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaasi! Wewe utakuwa umenawa mikono na huyo mwanamke utajua ukweli kwamba wewe ndo baba mwenye nyumba.
 
pole sana aise....kwakweli me naona bora 2 ubakia mwenyewe uishi kwa amani......ama ongea nae na ujaribu kumpa ushauri juu ya maisha japo ameshakua ivo...
 
Pole sana ndugu. kama una uwezo mtafuties mtaji wa biashara kisha mpangishie chumba miezi sita uachane nae klwa amani tu.
 
Pole sana bro hali hiyo. Mimi nafikiri hayo maneno ya shemeji zako yasikusumbue kabisa coz huyo ni ndugu yako tena wa damu so maneno ya mashemeji yasikuumize kichwa. Kwa kuwa ni ndugu yako wakati mwingine unatakiwa kuibeba aibu yake huo ndo udugu.... si unaona umepata mashemeji kwa kupitia vitu vyako wasichana wanamwona brother wako wa maana kwa ajili ya vitu vyako!!!!! Jambo la kufanya ni kumshauri kuhusu kupunguza au kuachana kabisa anasa (ulevi na wanawake) ili awe na uwezo. Pia kama una nafasi jaribu kumtafutia sehemu nyingine za kazi. Usimfungulie miradi kwa sasa kwani utajikuta unapoteza hela bure ila akipata kazi akaweza kuifanya vizuri baada ya kutulia unaweza kumfungulia kamradi akafanya
Endelea kumsaidia kwani huyo ni nduguyo. vitu kama ni vyako basi ni vyako tu maneno hayawezi kubadili umiliki wa vitu hivo.
Thanks
 
Actually umechelewa kumfukuza, mpangie room weka kitanda mtoe, we Ndo umemwaribu, kwa nini alipopata kazi ukaendelea mlea? Mtafutie mahali Ndo umeondoe, akishindwa lipa achana Naye.

Huyu ni kaka yangu kabisa, mama mmoja baba mmoja. Ana miaka 38 na kabla ya kuzaliwa mimi, walizaliwa kaka na dada zangu wengine 2, hivyo mimi ni mdogo wake wa 3, na hapo unaweza kujua tumepishana umri kiasi gani!

Haileweki. Alimaliza form akafeli. Wazazi walimlazimisha shule akakataa kata kata. Akawa anashinda anazurura na kufanya kazi za udalali huku akiishi kwa sisi wadogo zake. Alikuwa anakaa kwa kaka zangu mwanzo, akawa na tabia za ulevi wa kupindukia na kuiba vitu vidgo vidogo na kusumbua shemeji zake. Tumemkalisha vikao na kumuonya kashindwa kubadili tabia.

Kila mtu alimchoka tukaamua kumuacha na kuanza kuishi maisha kama chokoraa! Nilimuonea huruma, nikamchukua akae nyumbani kwangu. Nilijaribu kumfungulia miradi ikafa kwa maana ni muhongaji mzuri wa wanawake! Nilimpa hela aenda driving, na kupata leseni ili nifanyie mpango kazini kwangu akala hela zote na leseni hakupata. Niliamua kumtafutia leseni kwa juhudi zangu na kumpeleka akawe dereva kwenye kampuni moja kubwa ya kusafirisha mizigo, akaishia kutumia magari kubebea vimwana. Akafukuzwa kazi

Sasa kaanza tabia ya udokozi wa vitu vya ndani na kuuza na kuleta wanawake huku akiwadanganya kuwa nyumba na usafiri wangu vyote ni vyake, ila kaamua kuniachia mdogo wake. Na sasa kuna msichana wake kanitumia meseji eti kwa nini nang'ang'ania nyumba na usafiri wa kaka badala ya kujitafutia maisha yangu mwenyewe! Thats is to say, hata wasichana wake wanaamini kuwa mimi ndo ninaishi kwa kaka! Wananisumbua, eti nawabana! - Sijui wana upeo mdogo kiasi gani!

Sasa mtu kama huyu hasaidiki, nitampeleka wapi? Nampiga chini leo leo. Namfukuzia mbali! Nimechoka!
Naomba ushauri!

HorsePower
 
Tumia busara zaidi. Utamtimua leo, kesho anauawa na wananchi wenye hasira kali kisa kadokoa sufuria la wali. Sijui utajisikiaje?
Watu wengine wanapata baraka/riziki kwa sababu ya watu wanaowasaidia. Mungu anajua ni mzigo gani ulionao na ndiyo maana unafanikiwa.

Case yako haitofautiani na ya kwangu, lakini siwezi kukata mkono wangu eti kwa kuwa nimeunyea.
Kaa naye, usichoke kumkosoa.

Umeongea sana kaka.......not only that but also dunia hii mungu kaweka watu wa kuwaokoa wengine kama hapa kwenye case ya HP...ni mtihani mgumu sana huu ila ajue kwamba ni wake na ni lazima aufaulu..

HP - Watakukatisha watu tamaa kwa majibu ya hovyo lakini be a man and take a leading role.....watu wa aina ya kaka yako huwa wanapewa majukumu na si mamlaka sababu hawakupewa uwezo wa kufikiria na kupanga miradi ilikufa kwa sababu hii . Get another one na yeye awe mmoja wa watendaji but decisions should rest with you...a company mode

Always muombe muumba akusaidie huku ukimshukuru kwa mtihani huu. Namfahamu mzee mmoja ana watoto wake wa kuwazaa watatu wote wana mtindio wa ubongo!!!! Can you imagine na bado anawahudumia kwa moyo mmoja na halalamiki hadharani?????
 
Back
Top Bottom