Brain za Prison Break

Scoflield alikuwa kama actor Mkuu na alicheza vizuri, lakini TBAG ndio aliyecheza vizuri zaidi kwenye nafasi yake, scene almost zote alizocheza zilikuwa zinauhalisia zaidi ya hata zile za Michael

Hili neno nimelisikia sana bongo, especially kenye movies za Tanzania, mara nyingi kama mtu akilia au akifoka wanasema ameonyesha uhalisia, hivi maana yake ni nini hasa?..
 
Allex mahone ndiye mwisho wa matatizo aliweza kusoma michezo yote ya michael s..
 
Ndugu Mbimbinho, hakua dhamira yangu, kuwafanya wanajukwaa kama vilaza, ila jambo nilikuwa najaribu kusisitiza ni ulichokisema wewe yaani "kumatchisha characters na uhalisia wake" kitu ambacho, huwafanya characters wafanikiwe kwa kiasi kikubwa katika movie wanazotoa. Ila sasa si kila character anaweza ku-match na uhallisia na hapa linakuja swala la kipaji na education background, Mfano Ray au Kanumba wote si ni waigizaji na wato husema au husemwa kama ni watu wenye vipaji ila kuna baadhi ya scene ukimpa hawezi kucheza na ata akizicheza haziwezi vutia sana...mathali, wampe Kanumba sehemu aliocheza Scofield, hata kama hiyo movie itakua ni ya Kiswahili hakita toka kitu kama alicho kitoa Scofield, utofauti mkubwa hapa ikiwa Shule za hawa wawili, na hapa kwenye shule hasa kwa waigizaji wa Nyumbani ndipo ninapo sisitiza (Ila kuna aina nyingi vilevile ya Kujielimisha si lazima sana uingie darasani) unaweza ukaamua kujiendeleza out of the class na bado ukawa very knowledgeable, kiasi ukiongea na mtu akakiri unavijua vitu vingi na unajua namna ya kujieleza kitu ambacho ni silaha kubwa kwenye industry nzima ya filamu
 
Vijana wanstaili pongezi as wamejipanga vizuri sana ila ili jina la tea bag huwa linaniacha hoi sana
 
Aaaaaaah T-bag mkali mkuu aibu.

I'm all the laws of karma come down wrong - T-bag

 
duh nashindwa kabisa kuamua kati ya alexander mahone na T-Bag.....Ila nadhani Mahone alikua juu kidogo...no T-bag dah hapana looh
hii kitu ni ngumu kuamua asee...ila wote waliuvaa uhusika 100% yaani ni mshike mshike
 
Hakuna mwenye akili unayoifikiria wewe kati ya hao uliowaandika ila unachokiona kama ni uwezo wao mkubwa wa akili wameumbiwa na mtunzi pamoja na director wa hiyo series. Mfano Michael Scofield, amembwa kama mtu mwenye ujuzi mkubwa katika fani ya uhandisi na unaweza ukadhani amesoma na kuhitimu shahada ya juu ya Uhandisi. Ina ukweli ni kuwa . "He graduated from Princeton University completing his bachelor's degree in English Literature". source:Wentworth Miller - Wikipedia, the free encyclopedia. Mi ninacho weza kuchangia hapoa ni kuwa hao jamaa wote uliowaandika hapo juu wanauwezo mkubwa sana wa kuigiza, ila pamoja na uwezo huo wameza kuupiga msasa au kukipiga msasa kipaji chao walicho nacho kwa kwenda shule and therefore their talent is supplemented by their educational background. Kitu ambacho ni nadra sana kukikuta kwa waigizaji wetu wa Nyumbani. Hebu fikiria mtu kamaliza darasa la saba alafu unampa scene ambayo itamkata yeye aigize kama lawyer...Hata iweza hata kama atahudhuria mahakamani mara mia ili kujifunza kile mawakili wanacho kifanya. Alafu kitu cha pili ni kuwa wenzetu wale wanavyoigiza hujua kama wanaigiza unaona kama ni uhalisia na ndio maana unaweza kuhadaika kuwa Scofueld ni Mhandisi kumbe sio. Ila huku kwetu mtu anaigiza afu anaigiza kuigiza...unamwona kabisa jamaa anaigiza hapa. Tunasafari ndefu waungwana


Mkuu hebu google tena C.V ya Michael huyu jamaa ni engeneer kweli na ana award kama mbili hivi za engeneering with a GPA of 3.8.Huyu jamaa sio kiuigiza tu ni kichwa kweli
 
Kama ninavyolionaga hilo likitu kwamba limekaa kiume kiume ndio ninavyohisi humu wamechangia wanaume tu!
 
Back
Top Bottom