BoT yawaonya wanaotumia pesa kutengeneza mashada ya maua ya zawadi

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imeonya matumizi mabaya ya pesa ikiwemo wale wanaotumia pesa hizo kutengeneza mashada na maua kwa ajili ya kuwatunuku wapendwa wao.

Akizungumza na Swahili Times, Meneja Msaidizi Kitengo cha Mawasiliano, Noves Moses amesema pesa inapotumika kufanya shughuli nyingine tofauti ni kukiuka utaratibu pamoja na kuipa gharama Serikali kutengeneza pesa mpya kutokana uchakavu wa pesa.

“Tuligundua pia maeneo mengi tu ya nchi utakuta noti zinatengenezewa mashada, zinatengenezewa maua, watu wengine wanatupa chini pesa au labda mtu anatoa burudani ile noti inachukuliwa inaenda kubandikwa sehemu yenye jasho, kichwani, kwenye paji la uso.

Kwahiyo matumizi ya namna hiyo ndiyo ambayo tunatolea ufafanuzi kwamba mnapofanya hivyo mnakiuka sheria, hizi ni pesa ambazo zinatumia gharama ambayo ingeweza kutumika kufanyia mambo mengine kwaajili ya ustawi wa jamii lakini sasa zinatumika kutengenezea noti mpya,” ameeleza.

Aidha, amesema elimu hiyo haikuwa imewafikia watu wengi, hivyo baada ya elimu inayoendelea kutolewa na BoT katika maeneo mbalimbali, hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa watakaovunja taratibu hizo.

Hata hivyo, BoT imewataka wananchi hususani wanawake kuepuka kukunja pesa au kuziweka kwenye maziwa na badala yake waweke kwenye pochi zitakazowawezesha kuweka noti ikiwa imenyooka.

Chanzo: SwahiliTimes
 
BOT wamevimbiwa na pesa za madafu ndio maana wana discuss ishu zisizo na mashiko.

Siku hizi watu wana safe zao za kuhifadhi pesa majumbani kwao.

Wafanye utafiti kwenye maduka yanayouza safe za kuhifadhia fedha ndio watapata picha kamili.

Mzunguko wa pesa kitaa haupo vizuri wao wanazungumzia petty issues!

Waache mambo ya kisengerema.
 
Tushaanza kupangiana matumizi ya pesa sasa.

PAMBANENI KUKUZA THAMANI YA TSH NA SIO KUTUPANGIA MATUMIZI YA PESA ZETU.

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom