Sikonge
JF-Expert Member
- Jan 19, 2008
- 11,550
- 6,062
Jee kuna ukweli kuwa hiyo gari ni made out of gold? Nadhani imepigwa rangi ya gold tu...
Nema,
Hapo umesema kweli kabisa ingawa si kuwa wamepaka. Kuna Mwaarabu mmoja alitaka kutengenezewa gari la dhahabu tupu. Walimwambia itabidi alipe pesa watengeze gari la kwanza na walifanyie crushing test na kupata uimara wake. Na wakisharidhika, ndiyo watatengeneza la pili wampe.
Nafikiri hayo juu watakuwa wame-coat na si ku-paint. Ila wanaweza kuwa wametengeneza layer ya mwisho ya dhahabu. Kumbuka kuwa hata mikufu yote ya dhahabu unayoiona, hakuna PURE GOLD. Inabidi watengeneze ALLOY (mchanganyiko wa gold na vyuma vingine) na ndipo wanatengeneza mkufu maana dhahabu yenyewe ni LAINI sana na kui-process inakuwa kasheshe. Sasa ulaini wake huo unafanya isiwe inafaa kutengenezea gari. Ukiwa na gari la dhahabu na ukakutana na Tyson/Hayman kachukukia kama siyo Shaq, basi atalikunjakunja gari lako na linakuwa kama limefanya crush test.