THE SPIRIT THINKER
JF-Expert Member
- Sep 9, 2019
- 392
- 555
THE SPIRIT THINKER.
UTANGULIZI
Berlin, Ujerumani
SONJA VERBRUGGE HAKUWA anafahamu kwamba leo ingelikuwa ni siku yake ya mwisho kuishi duniani. Alikuwa anatembea kwa taabu kuwapita watalii waliokuwa wamefurika kwenye barabara ya Unter den Linden.
Usikurupuke, alijiambia. Lazima uwe mtulivu.
Ile meseji ya ghafla kwenye kioo cha kompyuta yake kutoka kwa Franz ilikuwa inatisha: Kimbia, Sonja. Nenda hadi Hotelini Artemisia usitoke hadi upigiwe na-
Meseji ilikuwa imekatia njiani hivyo. Kwanini Franz hakuwa amemaliza kuandika ujumbe wote? Kulikuwa na nini? Usiku uliopita alikuwa amemsikia mume wake akiongea na mtu kwenye simu kwamba Prima lazima atulizwe. Prima alikuwa ni nani?
Sonja alikuwa ameikaribia Brandenburgische, hoteli ambayo ilikuwa ni kwaajili ya wanawake tu. Nitamsubiria Franz hapo aje kunieleza kuna nini.
Wakati alipokata kona, taa za barabarani ziliwaka nyekundu. Magari yakasimama halafu ghafla mmoja kati ya watalii waliokuwa wakitembea akamsukuma barabarani. Hapohapo gari moja lililokuwa limeegeshwa kwa mbele likaanza kuunguruma na kumgonga kiasi cha kumfanya aanguke chini. Watu wakaanza kumzunguka.
“Kafa?”
“Ist ihr etwas passiert?”
“Puet-elle marcher?”
Muda huohuo ambulance fulani ilifika na kuegeshwa jirani. Wahudumu wawili walishuka kutoka kwenye ile ambulance na kuongea, “Tutamhudumia.”
Sonja alijikuta akibebwa na kuwekwa ndani ya ambulance halafu mlango wa gari ukafungwa, na dakika chache baadae gari likachochewa moto.
Sonja alikuwa amefungwa kwenye kitanda, alijaribu kujiinua. “Mimi nipo sawa. Sijaumia.” Alisema.
Mmoja kati ya wale wahudumu aliinama usoni kwa Sonja. “Kila kitu kipo sawa, Frau Verbrugge. Tulia.”
Sonja alimtazama yule mhudumu kwa mshtuko. “Umelifahamu vipi...?”
Lakini hakumaliza kauli yake. Alihisi sindano ikimchoma mkononi mwake, na dakika moja baadae alitulia tuli.
Paris, Ufaransa
MARK HARRIS ALIKUWA amesimama peke yake kwenye eneo la kuutazama mnara wa Eiffel, huku mvua ikimnyeshea. Muda hadi muda kulikuwa na radi ikipiga huku manyunyu ya mvua yakichuruzika. Lakini mawazo yake yalikuwa mbali. Akili yake yote ilikuwa ipo kwa Prima na habari ya kushtusha ambayo ilikuwa ipo mbioni kutangazwa kwenye ulimwengu wote.
Mvua ilikuwa imeanza kukata. Mark Harris aliinua mkono wake kuangalia saa. Wamechelewa. Na kwanza kwanini walikuwa wamesisitiza tukutane hapa, Usiku wa manane? Akiwa anajiuliza alisikia mlango wa mnara ukifunguka. Wanaume wawili walikuwa wanamfuata aliposimama.
Mark Harris aliwatambua, akajihisi amani. “Mmechelewa.”
“Hii hali ya hewa, Mark. Samahani.”
“Hata hivyo mmefika. Kwahivyo kikao cha Washington tayari kimepangwa?”
“Hili ndilo suala tunalotaka kuongea na wewe. Hata hivyo asubuhi tulijadiliana kwa kina sana namna ya kushughulikia hili suala na tukaamua...”
Wakiwa wanaongea, mwanaume wa pili aliyekuwa kimya alimzunguka Mark Harris kwa nyuma halafu mambo mawili yakatokea. Ilikuwa ni kwa kasi na ghafla kitu kizito kilitua kichwani kwa Mark, na muda kidogo alijisikia akibebwa na kutupwa chini kutokea ngazi ya 80 ya mnara wa Eiffel.
Denver, Colorado
GARY REYNOLDS ALIKUWA amekulia Kelowna huko Canada, jirani kabisa na Vancouver, na huko ndiko alikojifunzia urubani kwahivyo alikuwa mzoefu sana wa kupaisha ndege kwenye mazingira ya milima. Na leo alikuwa anapaisha ndege aina ya Cessna Citation II akiwa makini na milima iliyokuwa mbele yake.
Ndege yenyewe ilikuwa imetengenezwa kwaajili ya kupaishwa na marubani wawili, lakini leo hakukuwa na rubani msaidizi.
Gary alikuwa ametoa ripoti kuwa alikuwa anaelekea uwanja wa ndege wa Kennedy. Kwahivyo hakuna mtu yeyote ambaye angeweza kufikiria kumtafuta Denver.
Angeutumia muda wa usiku na dada yake, halafu asubuhi angeelekea kukutana na wenzake. Mipango yote ya kumuondoa Prima ilikuwa kamili na…
Sauti kwenye kiredio ilimkata kwenye mawazo yake, “Citation one one Lima Foxfort, hii ni sauti toka chumba cha maelekezo cha uwanja wa ndege wa kimataifa Denver, tunakusikiliza…”
Gray Reynolds alibofya kitufe. “Hii ni Citation one one Lima Foxfort, naomba kutua.”
“One Lima Foxfort, tuambie ulipo.”
“One Lima Foxfort. Nipo maili kumi na tano mashariki mwa uwanja. Umbali wa futi kumi na tano kutoka ardhini.”
Ukimya ukapita kidogo. Halafu sauti ikasikika. “One Lima Foxfort una ruhusa ya kushuka njia ya two-six. Narudia two-six.”
“One Lima Foxfort, nimeelewa.”
Ghafla na bila onyo lolote Gary aliisikia ndege ikitikisika ghafla, alipochungulia kupitia dirishani kulikuwa na upepo na ndani ya sekunde chache tu upepo mkali uliikumba ndege na kuizungusha. Alijitahidi kuvuta usukani, lakini haikusaidia chochote. Alikuwa kanaswa na hakukuwa na namna ya kuiondoa ndege. Alibofya kitufe kwenye kiredio.
“One Lima Foxfort. Nina dharura.”
“One Lima Foxfort, dharura yako ni nini?”
Gary Reynolds alikuwa anapiga kelele, “Nipo kwenye upepo mkali!”
“One Lima Foxfort, upo umbali wa dakika nne tu hadi uwanja wa ndege na hatuoni dalili ya upepo kwenye skrini zetu.”
“Sijali mnaona nini kwenye skrini. Nakuambia wewe…” Halafu sauti yake ikapanda. “Mayday! May..”
Kwenye jengo la uongozaji ndege uwanjani walitazama kwa mshtuko kadri alama ya radar ilivyopotelea kwenye skrini.
Manhattan, New York
ALFAJIRI, ENEO MOJA karibu na daraja la Manhattan unapopita mto wa mashariki kulikuwa na umati wa askari polisi waliovalia sare zao na wapelelezi kadhaa ambao hawakuwa na sare. Wote walikuwa wamekusanyika kutazama maiti iliyokuwa pembeni ya ukingo wa mto. Ni kama mwili ulikuwa umetupwa.
Asakari kiongozi wa zamu, Earl Greenburg, kutokea kikosi cha upelelezi wa mauaji Manhattan alikuwa amemaliza kutoa maelekezo ya awali. Hakuna mtu kuusogelea na kuugusa mwili hadi utakapopigwa picha, aliandika maneno fulanifulani kwenye notebook huku askari wengine wakijaribu kutafuta kama kuna ushahidi wowote. Mikono ya ile maiti iliyokuwa imekwatwa ilikuwa imewekwa kwenye mfuko wa plastiki.
Daktari Carl Ward, alimaliza uchunguzi wake wa awali. Alisimama na kujipangusa uchafu kwenye suruali yake. Akawatazama askari wapelelezi waliokuwa zamu. Wa kwanza, Greenburg, huyu alikuwa mzoefu. Halafu mpelelezi wa pili alikuwa ni Robert Praegitzer, mzee ambaye umri wake uliashiria ameona mengi sana.
Ward alimgeukia Greenburg, “Maiti ni mali yako kuanzia sasa.”
“Umegundua nini?”
“Chanzo cha kifo ni shingo iliyochomwa ncha kali kwenye mshipa wa Carotid. Magoti yake yamevunjika pia. Na mbavu kadhaa pia. Inaonesha kuna bwana alimshughulia kwelikweli.”
“Na muda aliofariki?”
Ward aliitazama maiti. “Ni ngumu kusema, pengine walimtupa hapa usiku wa manane. Ila nitakupa ripoti kamili mwili wake ukifika hospitali kwa uchunguzi zaidi.”
Greenburg aligeuza macho yake kuitazama maiti. Koti la kijivu, suruali ya bluu mpauko, na saa ya bei ghali kwenye mkono wa kushoto.
Greenburg alipiga magoti na kuanza kukagua mifuko ya koti ya ile maiti.
Kwenye mfuko mmoja alikuta kikaratasi, alikivuta halafu akakisoma. Kilikuwa kimeandikwa: Washington jumatatu saa nne asubuhi. Prima.
Alikiangalia kile kikaratasi bila kuelewa chochote.
Kwenye mfuko mwingine alikuta kikaratasi kingine. “Hii imeandikwa kwa kiitalia.” Alizungusha macho yake halafu akaita, “Gianelli!”
Mmoja kati ya maafisa alimwendea. “Naam, mkuu.”
Greenburg alimpa ile karatasi. “Unaweza kunitafsiria?”
Gianelli alisoma kilichoandikwa huku akitafsiri: Nafasi ya mwisho. Tukutane Pier Seventeen ukiwa na mzigo uliobakia au utajikuta unaogelea kama samaki.”
Robert Praegitzer alisema kwa mshangao. “Hili ni tukio la genge la kihalifu? Kwanini sasa walikuja kumtupa hapa? Sehemu ya wazi kama hii?”
“Swali zuri.” Greenburg alikuwa anaendelea kukagua mifuko ya marehemu. Alipata waleti na kuifungua. Ilikuwa imejaa pesa za noti nyingi. “Bila shaka waliofanya hivi hawakuwa na shida na hela zake.”
Alitoa kadi kwenye waleti, “Anaitwa Richard Stevens.”
Praegitzer alitetemeka, “Richard Stevens… Hilo jina kama tumelisoma juzijuzi tu kwenye magazeti.”
Greenburg alisema, “Mke wake ni Diane Stevens. Na anatoa ushahidi kwenye kesi ya mauaji ya Tony Altieri.”
Praegitzer alisema, “Ndiyo. Anatoa ushahidi dhidi ya capo di capos.”
Halafu wote wakageuka kuutazama mwili wa Richard Stevens.
TUMEANZIA HAPA .
HAKIKISHA UNASOMA KWA MAKINI. NA UKIPENDA KUSOMA TENA NITAFUTE NIPACHIKE TENA.