Riwaya: Kiza kinakutisha?

Kenii

Member
Apr 29, 2023
8
5
UTANGULIZI

Berlin, Ujerumani
SONJA VERBRUGGE HAKUWA anafahamu kwamba leo ingelikuwa ni siku yake ya mwisho kuishi duniani. Alikuwa anatembea kwa taabu kuwapita watalii waliokuwa wamefurika kwenye barabara ya Unter den Linden.

Usikurupuke, alijiambia. Lazima uwe mtulivu.

Ile meseji ya ghafla kwenye kioo cha kompyuta yake kutoka kwa Franz ilikuwa inatisha: Kimbia, Sonja. Nenda hadi Hotelini Artemisia usitoke hadi upigiwe na-

Meseji ilikuwa imekatia njiani hivyo. Kwanini Franz hakuwa amemaliza kuandika ujumbe wote? Kulikuwa na nini? Usiku uliopita alikuwa amemsikia mume wake akiongea na mtu kwenye simu kwamba Prima lazima atulizwe. Prima alikuwa ni nani?

Sonja alikuwa ameikaribia Brandenburgische, hoteli ambayo ilikuwa ni kwaajili ya wanawake tu. Nitamsubiria Franz hapo aje kunieleza kuna nini.

Wakati alipokata kona, taa za barabarani ziliwaka nyekundu. Magari yakasimama halafu ghafla mmoja kati ya watalii waliokuwa wakitembea akamsukuma barabarani. Hapohapo gari moja lililokuwa limeegeshwa kwa mbele likaanza kuunguruma na kumgonga kiasi cha kumfanya aanguke chini. Watu wakaanza kumzunguka.

“Kafa?”

“Ist ihr etwas passiert?”

“Puet-elle marcher?”

Muda huohuo gari la dharura la wagonjwa lilifika na kuegeshwa jirani. Wahudumu wawili walishuka kutoka kwenye ile gari na kuongea, “Tutamhudumia.”

Sonja alijikuta akibebwa na kuwekwa ndani ya gari ile ya wagonjwa mahututi halafu mlango wa gari ukafungwa, na dakika chache baadae gari likachochewa moto.

Alipokurupuka alikuwa amefungwa kwenye kitanda, alijaribu kujiinua. “Mimi nipo sawa. Sijaumia.” Alisema.

Mmoja kati ya wale wahudumu aliinama usoni kwa Sonja. “Kila kitu kipo sawa, Frau Verbrugge. Tulia.”

Alimtazama yule mhudumu kwa mshtuko. “Umelifahamu vipi...?”

Kabla hajamaliza kauli yake alihisi sindano ikimchoma mkononi mwake, na dakika moja baadae alitulia tuli.

Paris, Ufaransa
MARK HARRIS ALIKUWA amesimama peke yake kwenye eneo la kuutazama mnara wa Eiffel kwa ndani, huku mvua ikimnyeshea. Muda hadi muda kulikuwa na radi ikipiga huku manyunyu ya mvua yakichuruzika. Lakini mawazo yake yalikuwa mbali. Akili yake yote ilikuwa ipo kwa Prima na habari ya kushtusha ambayo ilikuwa ipo mbioni kutangazwa kwa ulimwengu wote.

Mvua ilikuwa imeanza kukata. Mark Harris aliinua mkono wake kuangalia saa. Wamechelewa. Na kwanza kwanini walikuwa wamesisitiza tukutane hapa, Usiku wa manane? Akiwa anajiuliza alisikia mlango wa mnara ukifunguka. Wanaume wawili walikuwa wanamfuata aliposimama.

Mark Harris aliwatambua, akajihisi amani. “Mmechelewa.”

“Hii hali ya hewa, Mark. Samahani.”

“Hata hivyo mmefika. Kwahivyo kikao cha Washington tayari kimepangwa?”

“Hili ndilo suala tunalotaka kuongea na wewe. Hata hivyo asubuhi tulijadiliana kwa kina sana namna ya kushughulikia hili suala na tukaamua...”

Wakiwa wanaongea yule mwanaume wa pili aliyekuwa kimya alimzunguka Mark Harris kwa nyuma halafu mambo mawili yakatokea ndani ya muda mfupi. Moja, kitu kizito kilitua kichwani kwa Mark. Pili, akapoteza fahamu. Na muda kidogo baadae alijihisi akibebwa na kutupwa chini kutokea ngazi ya 80 ya mnara wa Eiffel.

Denver, Colorado
GARY REYNOLDS ALIKULIA Kelowna, huko Canada jirani kabisa na Vancouver, na huko ndiko alikopata mafunzo yake ya urubani kwahivyo alikuwa mzoefu sana wa kupaisha ndege kwenye mazingira ya milima. Na leo alikuwa anapaisha ndege aina ya Cessna Citation II akiwa makini na milima iliyokuwa mbele yake.

Ndege yenyewe ilikuwa imetengenezwa kwaajili ya kupaishwa na marubani wawili, lakini leo ilikuwa na rubani mmoja tu ndani.

Gary alikuwa ametoa ripoti kazini. Kwamba alikuwa anaelekea uwanja wa ndege wa Kennedy. Kwahivyo hakuna mtu yeyote ambaye angeweza kufikiria kumtafutia Denver nyumbani kwao.

Angeutumia muda wa usiku na dada yake, halafu asubuhi angeelekea kukutana na wenzake. Mipango yote ya kumuondoa Prima ilikuwa kamili na…

Sauti kwenye kiredio ilimkata kwenye mawazo yake, “Citation one one Lima Foxfort, hii ni sauti toka chumba cha maelekezo cha uwanja wa ndege wa kimataifa Denver, tunakusikiliza…”

Gray Reynolds alibofya kitufe. “Hii ni Citation one one Lima Foxfort, naomba kutua.”

“One Lima Foxfort, tuambie ulipo.”

“One Lima Foxfort. Nipo maili kumi na tano mashariki mwa uwanja. Umbali wa futi kumi na tano kutoka usawa wa bahari.”

Ukimya ukapita kidogo. Halafu sauti ikasikika. “One Lima Foxfort una ruhusa ya kushuka njia ya two-six. Narudia two-six.”

“One Lima Foxfort, nimeelewa.”

Ghafla na bila onyo lolote Gary aliisikia ndege ikitikisika, alipochungulia kupitia dirisha kulikuwa na upepo na ndani ya sekunde chache tu upepo mkali uliikumba ndege na kuizungusha. Alijitahidi kuvuta usukani, lakini haikusaidia chochote. Alikuwa kanaswa na hakukuwa na namna ya kuiondoza ndege. Alibofya kitufe.

“One Lima Foxfort. Nina dharura.”

“One Lima Foxfort, dharura yako ni nini?”

Gary Reynolds alikuwa anapiga kelele, “Nipo kwenye upepo mkali!”

“One Lima Foxfort, upo umbali wa dakika nne tu kufika uwanjani na hatuoni dalili ya upepo kwenye skrini zetu.”

“Sijali mnaona nini kwenye skrini. Nakuambia wewe…” Halafu sauti yake ikapanda. “Mayday! May..”

Kwenye jengo la uongozaji ndege uwanjani waliitazama kwa mshtuko kadri alama ya radar ilivyopotelea kwenye skrini.

Manhattan, New York
ALFAJIRI, ENEO MOJA karibu na daraja la Manhattan unapopita mto wa mashariki, kulikuwa na umati wa askari polisi waliovalia sare zao na wapelelezi kadhaa ambao hakuwa na sare. Wote walikuwa wamekusanyika kutazama maiti iliyokuwa pembeni ya ukingo wa mto. Ni kama mwili ulikuwa umetupwa.

Asakari kiongozi wa zamu, Earl Greenburg, kutokea kikosi cha upelelezi wa mauaji Manhattan alikuwa amemaliza kutoa maelekezo ya awali. Hakuna mtu kuusogelea na kuugusa mwili hadi utakapopigwa picha, aliandika maneno fulanifulani huku askari wengine wakijaribu kutafuta kama kuna ushahidi wowote. Mikono ya ile maiti iliyokuwa imekwatwa ilikuwa imewekwa kwenye mfuko wa plastiki.

Carl Ward, mchunguzi kutoka hospitali, alimaliza uchunguzi wake wa awali. Alisimama na kujipangusa uchafu kwenye suruali yake. Aliwatazama askari wapelelezi waliokuwa zamu. Greenburg, huyu alikuwa mzoefu. Halafu mpelelezi wa pili alikuwa ni Robert Praegitzer, mzee ambaye muonekano wake ulionesha ameona mengi sana.

Ward alimgeukia Greenburg, “Maiti ni mali yako kuanzia sasa.”

“Umegundua nini?”

“Chanzo cha kifo ni shingo iliyochomwa na kitu chenye ncha kali kwenye mshipa wa Carotid. Magoti yake yamevunjika. Na mbavu kadhaa pia. Inaonesha kuna mabwana walimshughulia kwelikweli.”

“Na muda aliofariki?”

Ward aliitazama maiti. “Ni ngumu kusema, pengine walimtupa hapa usiku wa manane. Ila nitakupa ripoti kamili mwili wake ukifika ofisini kwa uchunguzi zaidi.”

Greenburg aligeuza macho yake kwenye mwili. Koti la kijivu, suruali ya bluu mpauko, na saa ya bei ghali kwenye mkono wa kushoto.

Greenburg alipiga magoti na kuanza kuukagua koti la ile maiti.

Kwenye mfuko mmoja alikuta kikaratasi, Alikivuta halafu akakisoma. Kilikuwa kimeandikwa; Washington jumatatu saa nne asubuhi. Prima.

Alikiangalia kwa mshtuko kile kikaratasi.

Kwenye mfuko mwingine alikuta kikaratasi kingine. “Hii imeandikwa kwa kiitalia.” Alizungusha macho yake halafu akaita, “Gianelli!”

Mmoja kati ya maafisa waliokuwepo alisogea. “Naam, mkuu.”

Greenburg alimpa ile karatasi. “Unaweza kunitafsiria?”

Gianelli alisoma kilichoandikwa: Nafasi ya mwisho. Tukutane Pier Seventeen ukiwa na mzigo uliobakia au utajikuta unaogelea kwenye bwawa la samaki.”

Robert Praegitzer alisema kwa mshangao. “Hili ni tukio la genge la kihalifu? Kwanini sasa walikuja kumtupa hapa? Sehemu ya wazi kama hii?”

“Swali zuri.” Greenburg alikuwa anaendelea kukagua mifuko ya marehemu. Alipata waleti na kuifungua. Ilikuwa imejaa noti nyingi. “Bila shaka waliofanya hivi hawakuwa na shida na hela zake.”

Alitoa kadi kwenye waleti, “Anaitwa Richard Stevens.”

Praegitzer alitetemeka, “Richard Stevens… Hilo jina kama tumelisoma juzijuzi tu kwenye magazeti.”

Greenburg alisema, “Mke wake ni Diane Stevens. Na anatoa ushahidi kwenye kesi ya mauaji dhidi ya Tony Altieri.”

Praegitzer alisema, “Ndiyo. Anatoa ushahidi dhidi ya capo di capos - bosi wa mabosi.”

Halafu wote wakageuka kuutazama mwili wa Richard Stevens.

SEHEMU YA KWANZA
 
SEHEMU YA KWANZA.

Shauri la Anthony (Tony) Altieri lilikuwa linasikilizwa lilipo jengo la mahakama kuu iliyopo Manhattan. Chumba hicho kikubwa cha mahakama kilikuwa kimefulikwa na waandishi wa habari na watu mbalimbali waliokuja kujionea kilichokuwa kinaendelea.

Kwenye meza ya mtuhumiwa alikuwa amekaa Anthony Altieri, akiwa ndani ya kiti chake cha walemavu, huku akionekana kama chura mnene aliyejikunyata. Macho yake tu ndiyo yalionesha yana uhai, na kila muda alikuwa anamtazama Dianne Stevens aliyekuwa amekaa kwenye kiti cha mashahidi.

Pembeni ya Altieri alikuwa amekaa Jake Rubenstein, Wakili wa utetezi. Rubenstein alifahamika kwa mambo makuu mawili: Kwanza ni wateja wake mashuhuri, wengi wakiwa ni magenge ya uhalifu, na jambo la pili ni uwezo wa kuwanasua kwenye mitego iliyowanasa wateja wake.

Rubenstein alikuwa na umbo dogo na akili inayofanya kazi kwa kasi sana na fikra yake ndiyo iliyombeba. Alikuwa hakaririki. Mara nyingi angewashinda wapinzani wake kwa kutafuta udhaifu wao. Kuna nyakati Rubenstein alijiona kama simba anayenyatia windo lake tayari kwa kulirarua... au kama utando wa buibui ambao utanasa windo lake likikosea njia. Kuna muda alijiona kama mvuvi, anayetupa ndoano yake kwenye maji na kusubiria mpaka mashahidi wanase na kujiingiza kwenye mtego.

Alikuwa anamtazama shahidi aliyekuwa amesimama kizimbani. Diane Stevens. Rubenstein alimkadiria umri wake kuwa miaka thelathini. Muonekano wa kuvutia. Macho ya kijani na nywele nyeusi. Umbo la Diane pia lilikuwa ni zuri. Alikuwa amekamilika kuitwa mwanamke. Alikuwa amevaa suti nyeusi na Jake Rubenstein alifahamu fika kuna namna angeweza kuteka akili za baraza. Angetakiwa kuwa makini na namna atakavyommudu. Nitakuwa mvuvi, aliamua.

Rubenstein alichukua muda wake alipokuwa akikisogelea kizimba cha shahidi, na alipozungumza sauti yake ilikuwa ni ya upole.

“Mrs. Stevens, Jana ulikiri kwamba mnamo mwezi wa kumi tarehe kumi na nne, ulikuwa unaendesha gari kusini mwa barabara ya Henry Hudson ambapo tairi lako moja liliishiwa upepo ukaamua kuegesha nje kidogo ya barabara kuu ilipo Fort Washington?”

“Ndiyo,” Sauti ya Diane ilikuwa laini.

“Nini kilikufanya usimame hapo na sio sehemu nyingine?”

“Kwa sababu ya ile pancha ilinibidi nipishe barabara kuu nisogee pembeni kidogo na kuna kinyumba nilikiona pembeni mbele kidogo ya miti nikahisi kuna mtu ataweza kunisaidia hapo.”

“Lakini una fundi wa gari lako?”

“Ndiyo.”

“Na una namba zake?”

“Ndiyo.”

“Sasa kwanini haukumpigia?”

“Ingechukua muda mrefu mpaka afike.”

Rubenstein alianza kuongea kwa upole zaidi, “Sahihi, na pia kulikuwa kuna kinyumba karibu na ungeweza kuomba msaada hapo.”

“Ndiyo.”

“Kwahivyo ulisogea kilipo hiko kinyumba upate msaada?”

“Ndiyo.”

“Nje palikuwa na mwanga?”

“Ndiyo. Ilikuwa ni kama saa kumi na moja jioni.”

“Kwahivyo ulikuwa unaweza kuona vizuri?”

“Ndiyo.”

“Uliona nini, Mrs. Stevens?”

“Nilimuona Anthony Altieri.....”

“Oh. Ulikuwa umewahi kukutana naye kabla ya hapo?”

“Hapana.”

“Nini kilikufanya uwe na hakika kwamba uliyemuona ni Anthony Altieri?”

“Nilikuwa nimewahi kuiona picha yake kwenye gazeti na...”

“Kwahivyo unasema uliwahi kuona picha ambayo inafanana na mlalamikiwaji?”

“Kiukweli ile...”

“Uliona nini kwenye kijumba?”

Dianne Stevens alivuta pumzi ndefu. Akaanza kuongea taratibu huku tukio alilolishuhudia likipita taratibu akilini mwake. “Kulikuwa na wanaume wawili kwenye kile chumba. Mmoja alikuwa amekaa kwenye kiti, akiwa amefungwa. Altieri alikuwa kama anamhoji maswali huku wanaume wengine wawili wakiwa wamesimama pembeni yake.”

Sauti ya Dianne ikakwama. Alipoipata tena akaendelea. “Altieri alichomoa bunduki, akafoka maneno fulani, na... na akampiga risasi nyuma ya kichwa yule mwanaume aliyefungwa kwenye kiti.”

Jake Rubenstein akageuza macho yake kulitazama baraza. Walikuwa wamevutwa na ushuhuda wa Diane.

“Ukafanya nini baada ya hapo sasa?”

“Nilikimbia kurudi nilipokacha gari yangu na kupiga 911.”

“Halafu?”

“Nikaendesha gari kuondoka pale.”

“Huku tairi yako moja ikiwa haina upepo?”

“Ndiyo.”

Wakati wa kucheza na ndoano kidogo ndani ya maji. “Kwanini haukuwasubiria polisi wafike?”

Diane alitupa macho yake ilipokuwa meza ya utetezi. Alteri alikuwa akimwangalia kwa jicho la chuki iliyo wazi kabisa.

Dianne alihamisha macho. “Sikuendelea kukaa pale kwa sababu nilihofia wangenikuta endapo wangetoka kwenye kile kijumba.”

“Jambo la busara.” Halafu sauti ya Rubeinstein ikawa na ukali kidogo. “Ila jambo ambalo nashindwa kuelewa ni kwamba polisi walipofika eneo la tukio na kwenda kwenye kile kijumba , sio tu hakukuwa na mtu mule, Mrs. Diane, ila hawakukuta hata ishara kwamba palikuwa na mtu mule ndani, achilia mbali mtu kuuliwa.”

“Siwezi ku...”

“Wewe ni msanii, sio?”

Swali lilimshtua Diane. “Ndiyo, nina...”

“Sanaa yako inakulipa?”

“Sio sana, lakini haihu...”

Ilikuwa ni wakati wa kuvuta ndoano. Samaki kashanasa!

“Umaarufu kidogo hauumizi, au sio? Nchi yote inakutazama kwenye taarifa ya habari na magazeti yanaandika kuhusu wewe tena kurasa za mbele kabisa...”

Diane alimtazama Rubeinstein kwa jicho la hasira. “Sijaja kutoa ushahidi kwaajili ya umaarufu. Siwezi kumtolea ushahidi mtu asiye na hatia aende ge..”

“Neno ni mtu asiye na hatia, Mrs. Stevens. Na nitawathibitishia mabibi na mbwana wa baraza la mahakama hii kwamba ndugu Altieri hana hatia. Asante. Umemaliza.”

Diane Stevens alipuuza maneno yale. Alipokikaribia kiti chake alikuwa anahema kwa hasira. Alimnong’oneza mwendesha mashtaka, “Ninaweza kwenda?”

“Ndiyo. Nitakupa mtu akusindikize.”

“Haina haja. Nashukuru sana.”

Aliuelekea mlango na kutoka nje hadi yalipo maegesho ya magari mahakamani hapo, wakati huu maneno ya wakili wa utetezi yalikuwa yakipita kwenye akili yake. Wewe ni msanii, sio?... Umaarufu kidogo hauumizi, au sio? Ilikuwa ni udhalilishaji. Hata hivyo bado alikuwa ameridhika na namna alivyotoa ushuhuda wake. Alikuwa ameiambia mahakama kile alichokiona kama kilivyotokea. Anthony Altieri lazima afungwe gerezani kwa kipindi chote cha maisha yake. Lakini kila Diane alipolikumbuka jicho la Anthony, alihisi uoga fulani.

Alimpatia mhudumu wa eneo la maegesho tiketi ya maegesho na kuingia kwenye gari lake. Dakika mbili baadae, Diane alikuwa mtaani, akielekea kaskazini, kuelekea nyumbani kwake.

Baada ya mwendo kidogo barabarani, kwenye kona alikutana na alama ya Stop. Diane alikanyaga breki, na kulikuwa na kijana aliyevalia kitanashati alilisogelea gari lake.

“Samahani. Nimepotea njia.”

Diane alishusha kioo chake.

“Unaweza kunielekeza nawezaje kufika Holland Tunnel.” Yule kijana aliongea kwa lafudhi ya kiitalia.

“Ni rahisi. Pita hii njia...”

Yule kijana aliinua mkono wake na alikuwa na bunduki ikiwa na kiwambo cha kuzuia sauti. “Shuka kwenye gari. Haraka.”

Diane alishtuka. “Sawa. Tafadhali.” Alipoanza kufungua mlango, yule kijana alirudi hatua kadhaa nyuma, na hapo ndipo Diane akakanyaga mguu wake kutia moto na gari likaondoka kwa kasi ya ghafla. Alisikia kioo cha nyuma kikipasuka baada ya risasi kukipiga, na mlio mwingine wa risasi ukigonga gari kwa nyuma.

Moyo wa Dianne ulikuwa unaenda kasi sana kiasi kwamba alikuwa anapumua kwa taabu.

Diane Stevens alikuwa amesoma makala kadhaa kuhusu wizi wa magari, lakini haikuwahi kumtokea hata mara moja. Na yule kijana alikuw a amejaribu kumuua. Je, wezi wa magari hufika hadi hatua hiyo? Diane aliichukua simu yake na kupiga 911. Ilichukua dakika mbili kabla haijapokelewa upande wa pili.

“Tisa moja moja. Una shida gani?”

Ingawa Diane alielezea kilichotokea, ila alijua hakuna matumaini. Yule kijana lazima atakuwa ameondoka zamani sana.

“Nitatuma afisa afike hilo eneo. Naomba jina lako, anuani na namba yako ya simu.”

Diane alitaja. Lakini alijua havikuwa na maana yeyote kwa muda ule. Aligeuka nyuma na kukiangalia kile kioo na kutetemeka. Alitamani sana ampigie Richard na kumsimulia kilichotokea, lakini aliacha kwa sababu alijua Richard alikuwa anafanya kazi ya muhimu sana ofisini kwake. Kama angempigia na kumwambia kilichotokea, Richard angehuzunika na kuahirisha mambo yake ili aje kumfariji na hakutaka iwe hivyo. Atamwambia kilichotokea watakapokuwa pamoja nyumbani.

Ghafla wazo la kustusha kidogo likamjia. Inawezekana Yule kijana alikuwa anamsubiria, au ilikuwa ni bahati mbaya amekutana naye? Akakumbuka maneno ya Richard kipindi ambacho shauri lilikuwa linaanza: “Nadhani usiongee chochote, Diane. Utajitafutaia mabalaa.”

“Usijali, kipenzi. Altieri atapatwa na hatia na atafungwa milele.”

“Lakini ana marafiki na...”

“Richard, nisipofanya hivi nitaishi na hatia kubwa moyoni.”

Kilichotokea lazima ni bahati mbaya tu, Diane alijiambia. Altieri sio mjinga kiasi cha kufanya jambo lolote la kunidhuru, hasa wakati huu wa shauri lake.

Alikata kona kuelekea magharibi na kufika mpaka ilipo nyumba yake mashariki mwa mtaa namba sabini na tano. Kabla hajaingiza gari kwenye sehemu yake ya maegesho, aliangalia nyuma kupitia kioo cha pembeni. Kila kitu kilionekana kuwa sawa tu.

Nyumba yenyewe ilikuwa na sebule kubwa, yenye madirisha yaliyotokea sakafuni hadi ilipo ceiling, na kulikuwa na sehemu ya kuota moto. Kulikuwa na masofa, viti, kabati ya vitabu na televisheni. Kuta za sebule zilikuwa zimepambwa na michoro ya rangi mbalimbali.

Ilikuwepo michoro ya Childe Hassam, Jules Pascin, Thomas Birch, Diane Hitchcok na ukuta mmoja ulikuwa na michoro ya Diane.

Ghorofa ya juu ilikuwa na chumba kimoja chenye bafu ndani kwaajili ya Diane, na kulikuwa na chumba kingine kwaajili ya wageni, sehemu ya kuotea jua ambako ndiko Diane alipatumia kuchora. Baadhi ya michoro ilikuwa inaning’inia ukutani. Kwenye kiti kimoja wapo katikati ya chumba hicho kulikuwa na mchoro ambao ulikuwa haujakamilika. Jambo la kwanza alilolifanya Diane alipoingia ndani ilikuwa ni kuutoa ule mchoro kwenye kiti na kuweka karatasi ambayo haikuwa imechorwa chochote. Alianza kuchora sura ya yule kijana aliyejaribu kumuua, lakini mikono yake ilikuwa inatetemeka sana kiasi kwamba ilibidi aache.

***

Mpelelezi Earl Greenburg alikuwa akiendesha gari yake kuelekea ilipo nyumba ya Diane Stevens huku akilalamika, “Hakuna kazi ninayochukia kama hii.”

Robert Praegitzer alisema, “Ni bora tuwaambie kuliko wasikie kwenye taarifa ya habari.” Akamtazama Greenburg. “Si unaenda kumwambia mwenyewe?”

Earl Greenburg alitikisa kichwa kukubali. Akajikuta anakumbuka kisa cha askari mmoja aliyeenda kumpatia Mrs. Adams taarifa kuwa mumewe ameuliwa.

***

DIANE ALISHTUSHWA na sauti ya kengele mlangoni. Alisogea na kuuliza. “Nani?”

“Askari mpelelezi. Naitwa Earl GreenBurg. Ninaomba kuzungumza na wewe.”

Ni kuhusu tukio la kutaka kuibiwa gari yangu, Diane aliwaza. Polisi wamefika mapema.

Diane aliufungua mlango na Greenburg aliingia koridoni na kusimama mlangoni.

“Habari.”

“Wewe ndiye Mrs. Stevens?”

“Ndiyo, asante sana kwa kuja mapema. Nilikuwa nimeanza kuchora uso wa yule kijana, lakini...” Alitulia kuvuta pumzi. “Alikuwa na sura ya ajabu, ana macho ya kahawia na ana kidoti shavuni. Bunduki yake ilikuwa na kiwambo cha kuzuia sauti, na...”

Greenburg alikuwa anamuangalia Diane kwa mshangao. “Sielewi unazungumzia nini?”

“Mwizi wa gari. Nilipiga 911 na...” Diane aliuona uso wa Greenburg. “Kwahivyo ujio wako hauhusu tukio la gari yangu?”

“Hapana,” Greenburg alisema. “Naweza kuingia ndani.”

“Karibu.”

Greenburg aliingia sebuleni.

Diane alikuwa anamtazama, akiwa haelewei. “Kuna tatizo?”

Maneno sahihi ya kuongea yalikuwa hayamjii Greenburg. “Ndiyo. Pole. Ni- Nina habari mbaya. Ni kuhusu mume wako.”

“Kimetokea nini?” Sauti yake ilikuwa inakwaruzika.

“Amepata ajali.”

Dianne alihisi baridi ikimpiga. “Ajali ya aina gani?”

Greenburg alivuta pumzi. “Ameuawa jana usiku. Mwili wake umekutwa chini ya daraja linalopitisha maji Mto mashariki asubuhi hii.”

Diane alibaki ametoa tu macho, halafu akaanza kutikisa kichwa chake kukataa.

“Umekosea nyumba, afande. Mimi mume wangu yupo kazini, maabara kwake.”

Suala lilikuwa linaenda kuwa gumu kuliko Greenburg alivyotazamia. “Mrs. Stevens, mume wako alirudi nyumbani jana usiku?”

“Hapana. Lakini Richard mara nyingi huwa anakesha kazini kwake. Ni mtafiti.” Diane alikuwa anazidi kutafuta sababu za kukataa habari iliyoletwa.

“Mrs. Stevens unafahamu kwamba mume wako alikuwa anajihusisha na kundi la uhalifu?”

Diane alifoka. “Uhalifu? Umechanganyikiwa?”

“Tumekuta..”

Diane alikuwa ameanza kufoka tena. “Naomba nione kitambulisho chako.”

“Sawa.” Greenburg alivuta kitambulisho chake na kumuonesha.

Diane alikitazama na kukirudisha kitambulisho, halafu akampiga kofi kali Greenburg usoni. “Serikali inakulipa pesa bure ili uzunguke kuwatisha wananchi? Mume wangu hajafa! Yupo kazini.” Diane alikuwa anafoka.

Greenburg alimtazama machoni halafu akaona mshtuko na hali ya kuukataa mshtuko kwa pamoja. “Mrs. Stevens ungehitaji labda nitume mtu kwaajili ya kukuangalia na...?”

“Wewe ndiye unayehitaji mtu wa kukuangalia. Haya toka hapa.”

“Mrs. Stevens...”

“Toka!”

Greenburg alitoa business card na kuiweka mezani. “Kama utahitaji kuongea na mimi tena namba yangu ipo hapo.”

Alipotoka nje ya mlango, Greenburg alishukuru kwa kumaliza hicho kibarua.

Huku nyuma Diane alifunga mlango na kuvuta pumzi ndefu ya uoga. Yule mjinga! Anakosea nyumba na kujaribu kunidanganya. Nitamripoti. Aliitazama saa yake. Richard atafika nyumbani muda sio mrefu. Ni muda wa kuanza kuandaa chakula cha jioni. Angepika Paella, chakula pendwa cha Richard. Alienda jikoni na kuanza kuandaa paella yenyewe.

Kutokana na mazingira ya kisiri ya kazi ya Richard, Diane hakuwa na mtindo wa kumsumbua akiwa ofisini, na ingetokea Richard asipige simu basi ilikuwa ni ishara kwamba atachelewa kurudi. Ilipofika saa mbili kamili chakula kilikuwa tayari. Diane alikionja na kutabasamu. Kilikuwa kipo kama ambavyo Richard hupendelea chakula chake kiwe. Saa nne, na Richard hakuwa bado amewasili, aliichukua paella akaiweka kwenye jokofu halafu akaweka kikaratasi kwenye mlango wa jokofu: Mpenzi, chakula kipo ndani ya jokofu. Naomba uje kuniamsha tule wote.

Lazima Richard angekuwa na njaa wakati atakapofika.

Diane alijihisi uchovu wa ghafla. Alielekea chumbani na kuvua nguo na kuvaa gauni la kulalia, akapiga mswaki halafu akapanda kitandani. Ndani ya dakika chache tu, akasinzia na kulala fofofo.

Ilipofika saa tisa usiku, aliamka akiwa anapiga kelele za uchungu.

BOFYA HAPA KUSOMA SEHEMU YA PILI
 
UTANGULIZI

Berlin, Ujerumani
SONJA VERBRUGGE HAKUWA anafahamu kwamba leo ingelikuwa ni siku yake ya mwisho kuishi duniani. Alikuwa anatembea kwa taabu kuwapita watalii waliokuwa wamefurika kwenye barabara ya Unter den Linden.

Usikurupuke, alijiambia. Lazima uwe mtulivu.

Ile meseji ya ghafla kwenye kioo cha kompyuta yake kutoka kwa Franz ilikuwa inatisha: Kimbia, Sonja. Nenda hadi Hotelini Artemisia usitoke hadi upigiwe na-

Meseji ilikuwa imekatia njiani hivyo. Kwanini Franz hakuwa amemaliza kuandika ujumbe wote? Kulikuwa na nini? Usiku uliopita alikuwa amemsikia mume wake akiongea na mtu kwenye simu kwamba Prima lazima atulizwe. Prima alikuwa ni nani?

Sonja alikuwa ameikaribia Brandenburgische, hoteli ambayo ilikuwa ni kwaajili ya wanawake tu. Nitamsubiria Franz hapo aje kunieleza kuna nini.

Wakati alipokata kona, taa za barabarani ziliwaka nyekundu. Magari yakasimama halafu ghafla mmoja kati ya watalii waliokuwa wakitembea akamsukuma barabarani. Hapohapo gari moja lililokuwa limeegeshwa kwa mbele likaanza kuunguruma na kumgonga kiasi cha kumfanya aanguke chini. Watu wakaanza kumzunguka.

“Kafa?”

“Ist ihr etwas passiert?”

“Puet-elle marcher?”

Muda huohuo gari la dharura la wagonjwa lilifika na kuegeshwa jirani. Wahudumu wawili walishuka kutoka kwenye ile gari na kuongea, “Tutamhudumia.”

Sonja alijikuta akibebwa na kuwekwa ndani ya gari ile ya wagonjwa mahututi halafu mlango wa gari ukafungwa, na dakika chache baadae gari likachochewa moto.

Alipokurupuka alikuwa amefungwa kwenye kitanda, alijaribu kujiinua. “Mimi nipo sawa. Sijaumia.” Alisema.

Mmoja kati ya wale wahudumu aliinama usoni kwa Sonja. “Kila kitu kipo sawa, Frau Verbrugge. Tulia.”

Alimtazama yule mhudumu kwa mshtuko. “Umelifahamu vipi...?”

Kabla hajamaliza kauli yake alihisi sindano ikimchoma mkononi mwake, na dakika moja baadae alitulia tuli.

Paris, Ufaransa
MARK HARRIS ALIKUWA amesimama peke yake kwenye eneo la kuutazama mnara wa Eiffel kwa ndani, huku mvua ikimnyeshea. Muda hadi muda kulikuwa na radi ikipiga huku manyunyu ya mvua yakichuruzika. Lakini mawazo yake yalikuwa mbali. Akili yake yote ilikuwa ipo kwa Prima na habari ya kushtusha ambayo ilikuwa ipo mbioni kutangazwa kwa ulimwengu wote.

Mvua ilikuwa imeanza kukata. Mark Harris aliinua mkono wake kuangalia saa. Wamechelewa. Na kwanza kwanini walikuwa wamesisitiza tukutane hapa, Usiku wa manane? Akiwa anajiuliza alisikia mlango wa mnara ukifunguka. Wanaume wawili walikuwa wanamfuata aliposimama.

Mark Harris aliwatambua, akajihisi amani. “Mmechelewa.”

“Hii hali ya hewa, Mark. Samahani.”

“Hata hivyo mmefika. Kwahivyo kikao cha Washington tayari kimepangwa?”

“Hili ndilo suala tunalotaka kuongea na wewe. Hata hivyo asubuhi tulijadiliana kwa kina sana namna ya kushughulikia hili suala na tukaamua...”

Wakiwa wanaongea yule mwanaume wa pili aliyekuwa kimya alimzunguka Mark Harris kwa nyuma halafu mambo mawili yakatokea ndani ya muda mfupi. Moja, kitu kizito kilitua kichwani kwa Mark. Pili, akapoteza fahamu. Na muda kidogo baadae alijihisi akibebwa na kutupwa chini kutokea ngazi ya 80 ya mnara wa Eiffel.

Denver, Colorado
GARY REYNOLDS ALIKULIA Kelowna, huko Canada jirani kabisa na Vancouver, na huko ndiko alikopata mafunzo yake ya urubani kwahivyo alikuwa mzoefu sana wa kupaisha ndege kwenye mazingira ya milima. Na leo alikuwa anapaisha ndege aina ya Cessna Citation II akiwa makini na milima iliyokuwa mbele yake.

Ndege yenyewe ilikuwa imetengenezwa kwaajili ya kupaishwa na marubani wawili, lakini leo ilikuwa na rubani mmoja tu ndani.

Gary alikuwa ametoa ripoti kazini. Kwamba alikuwa anaelekea uwanja wa ndege wa Kennedy. Kwahivyo hakuna mtu yeyote ambaye angeweza kufikiria kumtafutia Denver nyumbani kwao.

Angeutumia muda wa usiku na dada yake, halafu asubuhi angeelekea kukutana na wenzake. Mipango yote ya kumuondoa Prima ilikuwa kamili na…

Sauti kwenye kiredio ilimkata kwenye mawazo yake, “Citation one one Lima Foxfort, hii ni sauti toka chumba cha maelekezo cha uwanja wa ndege wa kimataifa Denver, tunakusikiliza…”

Gray Reynolds alibofya kitufe. “Hii ni Citation one one Lima Foxfort, naomba kutua.”

“One Lima Foxfort, tuambie ulipo.”

“One Lima Foxfort. Nipo maili kumi na tano mashariki mwa uwanja. Umbali wa futi kumi na tano kutoka usawa wa bahari.”

Ukimya ukapita kidogo. Halafu sauti ikasikika. “One Lima Foxfort una ruhusa ya kushuka njia ya two-six. Narudia two-six.”

“One Lima Foxfort, nimeelewa.”

Ghafla na bila onyo lolote Gary aliisikia ndege ikitikisika, alipochungulia kupitia dirisha kulikuwa na upepo na ndani ya sekunde chache tu upepo mkali uliikumba ndege na kuizungusha. Alijitahidi kuvuta usukani, lakini haikusaidia chochote. Alikuwa kanaswa na hakukuwa na namna ya kuiondoza ndege. Alibofya kitufe.

“One Lima Foxfort. Nina dharura.”

“One Lima Foxfort, dharura yako ni nini?”

Gary Reynolds alikuwa anapiga kelele, “Nipo kwenye upepo mkali!”

“One Lima Foxfort, upo umbali wa dakika nne tu kufika uwanjani na hatuoni dalili ya upepo kwenye skrini zetu.”

“Sijali mnaona nini kwenye skrini. Nakuambia wewe…” Halafu sauti yake ikapanda. “Mayday! May..”

Kwenye jengo la uongozaji ndege uwanjani waliitazama kwa mshtuko kadri alama ya radar ilivyopotelea kwenye skrini.

Manhattan, New York
ALFAJIRI, ENEO MOJA karibu na daraja la Manhattan unapopita mto wa mashariki, kulikuwa na umati wa askari polisi waliovalia sare zao na wapelelezi kadhaa ambao hakuwa na sare. Wote walikuwa wamekusanyika kutazama maiti iliyokuwa pembeni ya ukingo wa mto. Ni kama mwili ulikuwa umetupwa.

Asakari kiongozi wa zamu, Earl Greenburg, kutokea kikosi cha upelelezi wa mauaji Manhattan alikuwa amemaliza kutoa maelekezo ya awali. Hakuna mtu kuusogelea na kuugusa mwili hadi utakapopigwa picha, aliandika maneno fulanifulani huku askari wengine wakijaribu kutafuta kama kuna ushahidi wowote. Mikono ya ile maiti iliyokuwa imekwatwa ilikuwa imewekwa kwenye mfuko wa plastiki.

Carl Ward, mchunguzi kutoka hospitali, alimaliza uchunguzi wake wa awali. Alisimama na kujipangusa uchafu kwenye suruali yake. Aliwatazama askari wapelelezi waliokuwa zamu. Greenburg, huyu alikuwa mzoefu. Halafu mpelelezi wa pili alikuwa ni Robert Praegitzer, mzee ambaye muonekano wake ulionesha ameona mengi sana.

Ward alimgeukia Greenburg, “Maiti ni mali yako kuanzia sasa.”

“Umegundua nini?”

“Chanzo cha kifo ni shingo iliyochomwa na kitu chenye ncha kali kwenye mshipa wa Carotid. Magoti yake yamevunjika. Na mbavu kadhaa pia. Inaonesha kuna mabwana walimshughulia kwelikweli.”

“Na muda aliofariki?”

Ward aliitazama maiti. “Ni ngumu kusema, pengine walimtupa hapa usiku wa manane. Ila nitakupa ripoti kamili mwili wake ukifika ofisini kwa uchunguzi zaidi.”

Greenburg aligeuza macho yake kwenye mwili. Koti la kijivu, suruali ya bluu mpauko, na saa ya bei ghali kwenye mkono wa kushoto.

Greenburg alipiga magoti na kuanza kuukagua koti la ile maiti.

Kwenye mfuko mmoja alikuta kikaratasi, Alikivuta halafu akakisoma. Kilikuwa kimeandikwa; Washington jumatatu saa nne asubuhi. Prima.

Alikiangalia kwa mshtuko kile kikaratasi.

Kwenye mfuko mwingine alikuta kikaratasi kingine. “Hii imeandikwa kwa kiitalia.” Alizungusha macho yake halafu akaita, “Gianelli!”

Mmoja kati ya maafisa waliokuwepo alisogea. “Naam, mkuu.”

Greenburg alimpa ile karatasi. “Unaweza kunitafsiria?”

Gianelli alisoma kilichoandikwa: Nafasi ya mwisho. Tukutane Pier Seventeen ukiwa na mzigo uliobakia au utajikuta unaogelea kwenye bwawa la samaki.”

Robert Praegitzer alisema kwa mshangao. “Hili ni tukio la genge la kihalifu? Kwanini sasa walikuja kumtupa hapa? Sehemu ya wazi kama hii?”

“Swali zuri.” Greenburg alikuwa anaendelea kukagua mifuko ya marehemu. Alipata waleti na kuifungua. Ilikuwa imejaa noti nyingi. “Bila shaka waliofanya hivi hawakuwa na shida na hela zake.”

Alitoa kadi kwenye waleti, “Anaitwa Richard Stevens.”

Praegitzer alitetemeka, “Richard Stevens… Hilo jina kama tumelisoma juzijuzi tu kwenye magazeti.”

Greenburg alisema, “Mke wake ni Diane Stevens. Na anatoa ushahidi kwenye kesi ya mauaji dhidi ya Tony Altieri.”

Praegitzer alisema, “Ndiyo. Anatoa ushahidi dhidi ya capo di capos - bosi wa mabosi.”

Halafu wote wakageuka kuutazama mwili wa Richard Stevens.

SEHEMU YA KWANZA
Screenshot_2023-05-01-08-02-38-162_com.android.chrome.jpg
 
SEHEMU YA PILI

Diane aliacha kutetemeka ilipofika alfajiri. Baridi aliyokuwa akihisi ilikuwa imehamia kwenye moyo na mifupa sasa. Ni kweli Richard alikuwa amekufa. Hakuna siku angewahi kumuona tena, au kusikia sauti yake, au kuhisi mwili wake ukigusana na wa Richard. Na ni kosa langu. Sikupaswa kwenda kusimama mahakamani. Oh, Richard, Nisamehe... Tafadhali nisamehe... Sidhani kama nitaweza bila wewe. Ulikuwa ndiye maisha yangu, sababu ya mimi kuwepo. Na sasa sina hata sababu ya kuendelea kuwa hai.

Alitamani dunia ipasuke aingie.

Alitamani apotee tu.

Alitamani afe.

Alibaki amelala akitafakari kuhusu maisha yake ya zamani, namna alivyokutana na Richard na namna Richard alivyobadilisha maisha yake.

Diane West alikuwa amekulia Sands Point huko New York. Baba yake alikuwa ni daktari wa upasuaji na mama yake alikuwa ni mchoraji, na Diane alianza kuchora alipokuwa na umri wa miaka mitatu tu. Alienda shule ya St. Paul na alikuwa na matokeo mazuri chuoni kwa sababu alikuwa na mahusiano na mwalimu wake wa hesabu. Mwalimu wake huyo alimwambia anataka kumuoa kwa sababu yeye ndiye mwanamke pekee anayempenda duniani. Lakini baadae Diane aligundua mwalimu wake huyo alikuwa na mke na watoto watatu, hapo Diane akaamua labda huyo mwalimu wake alikuwa na matatizo ya kumbukumbu na kuamua kuchukua uhamisho kwenda Wellesley College.

Diane alivutiwa sana na michoro na muda wake mwingi aliutumia kuchora tu. Kufikia kipindi anahitimu, alikuwa ameanza kuuza michoro yake na wengi walimtazamia kama msanii mkubwa baadae.

Na msimu huo, Fifth Avenue art gallery ilimpa Diane nafasi ya kuandaa tamasha lake na tamasha lilifanikiwa kwa kiwango kikubwa. Mmiliki wa ukumbi huo, Paul Deacon, alikuwa ni bwana mmoja tajiri aliyesaidia kwa kiasi kikubwa kukilea na kukikuza kipaji cha Diane.

Usiku wa tamasha eneo lilikuwa limefurikwa. Deacon alimfuata Diane, huku tabasamu kubwa likiwa usoni kwake. “Hongera! Tumekwishauza baadhi ya michoro yako. Nitaandaa tamasha linguine baada ya miezi michache, ukiwa tayari niambie.”

Diane alisema, “Asante sana, Paul.”

“Unastahili kila kitu.” Paul alisema na kumshika Diane began a kuondoka.

Diane alikuwa anaweka sahihi yake kwa huyu na yule alipotokea mwanamume mmoja nyuma yake na kusema, “Napenda michirizi yako.”

Diane alistuka. Kwa hasira aligeuka na kufungua mdomo wake kuongea jambo, lakini hakutoa sauti. Yule mwanaume alikuwa tayari ameanza kuongea.

“Zina ladha fulani ya Rossetti au Manet.” Yule mwanaume alikuwa anauangalia mchoro mmoja uliokuwa ukutani.

Diane alijizuia kwa wakati. “Oh.” Akamtazama yule mwanaume kwa umakini. Alionekana kuwa na umri kati ya miaka ya katikati thelathini. Urefu wake ulikuwa ni futi sita, na mwili wa mazoezi, na macho ya bluu iliyokoza. Alikuwa amevalia suti, shati jeupe na tai ya kahawia.

“Ahsante.”

“Umeanza kuchora lini?”

“Nilipokuwa mtoto. Mama yangu alikuwa ni mchoraji.”

Yule mwanaume alitabasamu. “Mbona mama yangu mimi alikuwa mpishi mzuri, ila mimi siwezi kupika. Jina lako nalifahamu. La kwangu ni Richard Stevens.”

Wakati huohuo Paul Deacon alifika akiwa na vifurushi vitatu. “Michoro uliyochagua hii hapa Mr. Stevens. Natumai utaifurahia.”

Richard alivyopokea vifurushi, Deacon aliondoka.

Diane alimtazama kwa jicho la mshangao, “Umenunua michoro yangu mitatu?”

“Ninayo miwili mingine nyumbani kwangu.”

“Ni- Nimefurahi kusikia hivyo.”

“Mimi nathamini sana vipaji.”

“Asante.”

Alisita kidogo, “Naona upo bize, kwahivyo nitakuacha- ”

Diane alijikuta akisema, “Hapana. Siko bize mbona.”

Tabasamu la Richard likaongezeka, “Basi unaweza kunisaidia jambo moja, Miss.”

Diane akautazama mkono wake wa kushoto. Alikuwa hajavaa pete. “Nakusikiliza.”

“Nina tiketi mbili kwaajili ya uzinduzi wa kinywaji cha Noel Coward kesho usiku, na sina mtu wa kwenda naye. Kama haupo bize- ?”

Diane alibaki anamtazama kwa muda kidogo. Alimuona anavutia, lakini, yote kwa yote, alikuwa hamfahamu. Hatari sana. Hatari kubwa sana, lakini mwisho wa siku alijikuta akisema, “Nitafurahi kukupa kampani.”

Jioni ya kesho yake ilitokea kuwa ya kufurahisha sana. Richard Stevens alikuwa ni mtu mcheshi, na kuna vitu vingi sana ambavyo wote walikuwa wanavutiwa navyo. Walikuwa wanapenda sanaa na muziki, na zaidi ya yote Diane alijikuta akivutiwa na Richard, lakini hakuwa na uhakika kama mwenzake alikuwa na hisia hizo kwake pia.

Mwishoni Richard aliuliza, “Utakuwa na nafasi kesho jioni?”

Jibu la Diane lilikuwa ni, “Ndiyo.”

Jioni iliyofuata walikuwa wanapata chakula cha jioni kwenye mgawa mmoja mtulivu uliopo SoHo.

“Niambie kuhusu wewe, Richard.”

“Sina historia ndefu. Nimezaliwa Chicago. Baba yangu alikuwa mhandisi wa michoro ya majengo na amefanya kazi nyingi karibu kila sehemu duniani, na mara nyingi tulisafiri naye. Nimeenda nchi nyingi na nimejifunza lugha mbalimbali kwa sababu kila tulipohama nchi nilihama na shule.”

“Unafanya nini? Kwaajili ya kipato”

“Ninafanya kazi KIG – Kingsley International Group. Ni taasisi kubwa na inahitaji watu wenye akili sana.”

“Acha basi.”

“Kweli. Tunanya tafiti za teknolojia ya hali ya juu. Kama tungelikuwa na kauli mbiu ingekuwa inasema, ‘Kama hatujapata jibu sasa hivi, tupeni hadi kesho tu.”

Baada ya chakula, Richard alimpeleka Diane nyumbani. Wakiwa mlangoni, aliishika mikono yake na kusema, “Nimwifurahia jioni ya leo. Asante.”

Na akaaondoka.

Diane alibaki amesimama akimtazama kwa nyuma. Nashukuru huyu bwana ni mkarimu na sio kama wanaume wengine.

Walikuwa pamoja kila usiku tangu jioni hiyo, na kila Diane alipomuona Richard alijihisi faraja kubwa.

Ijumaa moja, Richard alisema, “Huwa ninafundisha timu fulani mazoezi kila Jumamosi. Unaweza kuja kuangalia kidogo?”

Diana alijibu, “Nitafurahi, Kocha.”

Asubuhi ya kesho yake Diane alimtazama Richard akifanya mazoezi na wachezaji wachanga. Alikuwa ni mpole na mwenye kujali na mvumilivu, na ilikuwa ni wazi wachezaji wale walimpenda Richard.

Diane alijiwazia, Nimeanza kupata hisia za mapenzi kwa huyu mtu. Ninampenda!

Siku chache baadae, Diane alikuwa anapata chakula cha mchana na marafiki zake wa kike, na walipokuwa wanaondoka mgahawani hapo, njiani walimpita mnajimu mmoja.

Na kama utani Diane akasema, “Tujaribu kupata utabiri wa maisha yetu.”

“Sina muda, Diane. Mimi narudi kazini.”

“Mimi pia.”

“Ninatakiwa kumchukua Johnny shule.”

“Embu wewe nenda halafu utatuambia kakuambia nini.”

“Sawa.”

Dakika tano baadae, Diane alijikuta akiwa amekaa peke yake mbele ya mwanamke yule mzee aliyejaa meno ya dhahabu mdomoni na uso uliochafuliwa kwa alama za michoro huku akiwa kajifunga tambala chafuchafu kichwani.

Huu ni upuuzi, Diane aliwaza. Kwanini nafanya huu ujinga.? Lakini alijua ni kwanini alikuwa anafanya huo ujinga. Alitaka kujua kama yeye na Richard wangekuwa na maisha ya pamoja siku za usoni.

Diane alimtazama yule mwanamke mzee ambaye alikuwa anachezacheza na karata, bila kuunia uso wake juu.

“Nilikuwa nataka kujua kama...”

“Shh.” Yule mwanamke aligeuza karata moja. Ilikuwa ni karata yenye picha ya ‘Joker’ akiwa amevaa nguo zenye rangirangi huku kashika kishoka. Yule mwanamke mzee aliitazama kwa muda. “Kuna siri nyingi sana unatakiwa kuzijua.” Akageuza karata nyingine tena. “Huu ni mwezi. Una mambo mengi unayohitaji na hauyajui.”

Diane alisita na kutikisa kichwa kukubali.

“Je, ujio wako hapa ni kuhusu mwanamume?”

“Ndiyo”

Yule mwanamke mzee akageuza karata iliyofuata. “Hii ni karata ya wapendanao.”

Diane akatabasamu. “Ni ishara nzuri?”

“Tutaona. Karata tatu zinazofuata zitatuambia.” Alipomaliza kuongea hivyo akageuza karata nyingine.

“Mwanamume aliyenyongwa.” Alisita, halafu akageuza karata nyingine. “Shetani,” alinong’ona.

“Ni ishara mbaya?” Diane aliuliza kwa upole.

Mnajimu hakutoa jibu lolote.

Diane aliendelea kumuangalia yule mwanamke mzee akifunua karata inayofuata.

Yule mwanamke alitikisa kichwa chake kuonesha huzuni. Sauti yake ilitoka kwa chini sana. “Karata ya kifo.”

Diane alisimama. “Muongo mtupu! Siamini chochote utakachokisema,” Aliongea kwa hasira.

Yule mwanamke mzee aliinua macho yake juu, na alipofungua midomo yake kuongea, sauti yake ilikuwa ni ya kutia mkazo. “Haijalishi unaamini nini. Ukweli ni kwamba mauti imekuzunguka kila unapokanyaga unyayo wako.”

SEHEMU YA TATU
 
SEHEMU YA TATU

Berlin, Ujerumani.
Kamanda wa polisi, Otto Schiffer, akiwa na maafisa wa polisi wawili waliokuwa ndani ya sare zao, na msimamizi wa jengo lenyewe, Herr Karl Goetz, walikuwa wanaushangaa mwili wa maiti ya mwanamke- ukiwa uchi- uliokuwa umelala ndani ya beseni la kuogea lililokuwa linavujisha maji. Uvimbe kidogo ulikuwa umezunguka shingo ya mwanamke huyo.

Kamanda wa polisi alinyoosha kidole chake hadi kwenye mkono wa bomba lililokuwa linatoa maji. Akamaliza akanusa chupa ya kilevi iliyokuwa wazi pembeni kidogo ya beseni lile la kuogea halafu akamgeukia yule msimamizi wa jengo, “Jina lake?”

“Sonja Verbrugge. Mume wake anaitwa Franz Verbrugge. Ni mtafiti wa mambo ya kisayansi.”

“Marehemu alikuwa anaishi na mume wake?”

“Ndiyo. Wameishi hapa kwa miaka saba na walikuwa ni wapangaji wazuri. Kodi walikuwa wanalipa kwa wakati sahihi. Sikuwahi kupata shida nao. Kila mtu alipenda...” Yule msimamizi aligundua alikuwa anataka kusema nini kwahivyo akanyamaza.

“Kwani Sonja alikuwa anafanya kazi gani?”

“Alikuwa na kazi Cyberlin internet cafe, sehemu ambayo watu wanalipa ili...”

“Nini kilikufanya ukagundua kuna maiti humu?”

“Ni kwa sababu ya hilo bomba linalovujisha maji. Huwa ni bovu na nimejaribu kulirekebisha mara kadhaa ila halijakaa vizuri.”

“Kwahivyo?”

“Kwahivyo asubuhi mpangaji wa ghorofa ya chini alilalamika maji yanachuruzika kutoka juu. Ndiyo nikaja huku, nikagonga mlango, na nilipoona sijibiwi, nikaufungua na funguo zangu. Nikaingia mpaka bafuni na kukuta...” Sauti yake ikakwama.

Mwanaume mwingine alikuwa ameingia mule bafuni. “Hakuna chupa za vilevi kwenye kabati au chumbani, kuna waini tu.”

Kamanda wa polisi alitikisa kichwa halafu akamgeukia tena Karl Goetz. “Unaweza ukawa unafahamu alipo Franz Verbrugge?”

“Hapana. Huwa namuona asubuhi tu akiwa anatoka kwenda kazini, lakini...” Halafu akaonesha alama ya kutokuwa wa msaada zaidi.

“Leo asubuhi haujamuona?”

“Hapana.”

“Unaweza ukawa una taarifa kwamba Franz Verbrugge alikuwa na mpango wa kusafiri labda?”

“Hapana. Sina hiyo taarifa.”

Kamanda alimgeukia yule mwanamume mpelelezi aliyekuwa ameingia muda sio mrefu. “Ongea na wapangaji wengine. Chunguza kama Sonja Verbrugee alionekana kuwa na mawazo siku za hivi karibuni, au kama yeye na mume wake walikuwa na ugomvi, na kama alikuwa ni mlevi wa pombe. Tafuta kila taarifa unayoweza kuipata.”

Halafu akamgeukia tena Karl Goetz. “Tutamcheki mume wake. Kama utakumbuka jambo lolote linaloweza kuwa la muhimu...”

Carl Goetz alisema kwa mashaka, “Sijui kama hili lina umuhimu au msaada, lakini kuna mpangaji mmoja aliniambia kuna ambulance ilionekana imeegeshwa nje, na aliniuliza kama kuna mgonjwa. Wakati ambao nilifika nje kuonana nini kilikuwa kinaendelea, ile ambulance ilikuwa tayari imeondoka. Inaweza kuwa na msaada hiyo taarifa?”

Kamanda alisema, “Tutacheki pia.”

“Na vipi... Vipi kuhusu mwili wake?” Karl Goetz aliuliza kwa uoga.

“Mtu wa hospitali anakuja kufanya uchunguzi. Kwa sasa hivi uachwe hapohapo tu.”

SEHEMU YA NNE
 
SEHEMU YA NNE

Nina habari mbaya... Ameuawa jana usiku... Mwili wake umekutwa chini ya daraja...

Muda, kwa Diane Stevens, ulikuwa umesimama. Alikuwa anatembeatembea kwenye nyumba yake iliyojawa kumbukumbu nyingi. Nyumba haikuwa na amani tena bila Richard. Haikuwa nyumba tena ila mkusanyiko wa tofali tu. Hakuna siku nyumba ile itakuja kuwa hai tena.

Diane alikaa kwenye sofa moja wapo na kufumba macho yake. Richard mpenzi, siku tulipofunga ndoa uliniuliza ninataka zawadi gani. Nilikujibu sitaki kitu chochote ila uwepo wako tu. Ila sasa hivi kuna kitu nakitaka.

Rudi kwangu. Haijalishi kwamba sitaweza kukuona tena. Ila nataka unikumbatie mikononi mwako. Najua upo hapa. Nahitaji kujihisi unanigusa angalau mara moja tu. Nataka nihisi ninaweza kuisikia sauti yako ikisema ninajua kupika paella kuliko mtu yeyote duniani. Nataka nisikie sauti yako ikiniambia kwamba unanipenda. Alijaribu kuzuia machozi ambayo tayari yalikuwa yanatiririka, lakini hakuweza.

Kuanzia wakati ambao Diane aligundua kuwa Richard alikuwa amekufa, alitumia muda wa siku zake akiwa amejifungia ndani ya nyumba yake, bila kupokea simu au kufungua mlango ulipobishwa. Alikuwa kama mnyama aliyeumia akiwa kajificha.

Alitaka kuwa peke yake na maumivu yake. Richard, kuna nyakati nyingi sana nilitamani nikuambie nakupenda ili ujibu unanipenda pia. Lakini sikutaka kuonekana kama nina uhitaji sana. Nilikuwa mjinga.

Hatimaye simu zilipozidi sana, na mlango ulipogongwa sana, Diane aliamua kufungua mlango.

Carolyn Ter, mmoja kati ya marafiki zake wa karibu alikuwa amesimama mlangoni. Alimtazama Diane na kusema, “Umetupatia wasiwasi sana. Kila mtu anakupigia simu haupokei.”

“Samahani, Carolyn, lakini siwezi...”

Carolyn alimshika Diane mkono, “Nafahamu. Lakini unao marafiki wengi sana wanataka kukuona.”

Diane alitikisa kichwa kukataa. “Hapana. Ni...”

“Diane, maisha ya Richard yameisha, lakini yako bado hayajaisha. Usiwafungie milango watu wanaokupenda. Acha nipige simu kuwataarifu watu upo salama.”

Rafiki za Diane na Richard wakaanza kupiga simu na kuja nyumbani, na Diane akajikuta akisikiliza misemo ileile kuhusu kifo:

“Ifikirie hivi, Diane. Richard ana amani huko aliko..”

“Mungu kampenda zaidi...”

“Najua Richard yupo mbinguni anakuangalia...”

“Ameenda sehemu bora zaidi...”

“Ameungana na malaika...”

Kila mara Diane aliposikia hiyo misemo alitamani kulia kwa nguvu.

Lakini mnyororo wa wageni haukuisha. Paul Deacon, yule mmiliki wa jumba la maonesho ya kazi za sanaa alikuja pia. Alianza kuongea, “Nimejaribu kukutafuta, lakini...”

“Nafahamu.”

“Kwanza pole kuhusu Richard. Alikuwa ni mwanaume bora, lakini Diane hauwezi kukaa hivi siku zote. Watu wanatamani waendelee kuona kazi zako.”

“Siwezi kuendelea na kazi. Haina umuhimu wowote tena kwangu, Paul.”

Ilikuwa ni ngumu kumshawishi.

Siku iliyofuata kengele ya mlango ilipogongwa, Diane alienda kufungua mlango. Alichungulia kupitia kitundu kidogo mlangoni, na palionekana kama kuna kundi kubwa la watu nje.

Akiwa na mshtuko, Diane alifungua mlango. Kulikuwa na kundi la vijana nje. Mmoja kati yao alikuwa ameshika maua.

“Shikamoo, Mrs. Stevens.” Aliongea huku akimpatia yale maua Diane.

“Ahsante.” Akawakumbuka wale vijana walikuwa ni akina nani. Walikuwa ni vijana ambao Richard alikuwa anawafundisha mpira.

Kiukweli, Diane alikuwa amepokea maua yasiyo na idadi, bahasha za pole na barua pepe nyingi, lakini hii ndiyo ilikuwa zawadi iliyougusa moyo wake kuliko zote.

“Ingieni ndani,” Diane alisema.

Wale vijana walivamia sebule. “Tulitaka kukuambia tumejisikia huzuni sana.”

“Mume wako alikuwa mtu mzuri.”

“Na alikuwa ni kocha mzuri.”

Kitu pekee alichoweza kusema Diane kuzuia machozi yake ilikuwa ni, “Asante.” Halafu akaongeza, “Mngependelea vinywaji gani?”

Tim Holm alijibu kwa niaba ya wenzake, “Hapana, Asante. Tulikuja kukuambia tu tutammiss mwalimu. Na wote tulichangia kununua hayo maua.”

Diane aliwatazama na kusema kimyakimya, “Asanteni sana.”

Aliwasindikiza na kuwatazama wakiondoka. Wakati huo Diane alianza kukumbuka mara ya kwanza alivyoshuhudia Richard akiwafundisha. Akakumbuka hiyo ndiyo siku aliyoanza kumpenda Richard.

Diane alisikia muungurumo wa radi kwa nje na manyunyu ya mvua yalianza kushuka, kama machozi ya Mungu akihuzunika naye. Mvua. Akaanza kuikumbuka siku moja ya mapumziko walipokuwa na Richard...

“Unapenda picnic?” Richard aliuliza.

“Nazipenda ndiyo.”

Richard alitabasamu. “Nilijua. Nitaandaa picnic kwaajili yetu. Nitakupitia mchana wa kesho.”

Kesho yake ilipofika ilikuwa nzuri, yenye hali ya jua na Richard aliandaa picnic kama alivyomuahidi Diane. Kulikuwa na vikapu viwili. Diane alipoona kilichokuwemo aliishia kucheka. Kulikuwa na nyama ya kukaanga ya ng’ombe na chipsi na sahani mbili kubwa na mkusanyiko wa vinywaji kadhaa na vitinda mlo.

“Chakula kingi! Kuna watu wengine tunaungana nao”

Richard alikuwa anamuangalia. “Upo sawa?”

Nipo sawa? Sijawahi kujihisi raha hivi. “Ndiyo, Richard. Nipo sawa.”

“Hatutawasubiri wanaokuja kuungana na sisi. Tuanze kula.”

Wakiwa wanakula waliongea mengi na kila neno liliwafanya wawe na ukaribu zaidi. Kulikuwa na nguvu ya ajabu iliyokuwa inaaongezeka kati yao – kama sumaku iliyowekwa karibu na chuma, na kila mmoja aliihisi. Halafu katikati ya siku yenye anga la jua mvua ikaanza kunyesha. Ndani ya dakika moja tu walikuwa wamelowana chapachapa.

Richard alisema, “Pole sana. Sikujua hali ya hewa itabadilika – Utabiri wa hali ya hewa jana hawakutabiri mvua. Pole sana hii mvua imeharibu...”

“Imeharibu?” Diane aliuliza kwa sauti ya chini.

Na kabla Richard hajajibu, Diane alikuwa amejitupa kifuani mwake na kumkumbatia. Aliyahisi mapigo ya moyo ya Richard yakienda kasi. Alipojiachia aliongea, “Itabidi tubadilishe hizi nguo zilizolowana.”

Richard alicheka, “Upo sawa. Tunaweza kuugu..”

Diane alisema, “Kwako au kwangu?”

Hapo Richard akabaki ameganda. “Diane, una uhakika? Ninauliza kwa sababu... Isije ikawa ni tendo la moja tu.”

Diane alijibu, “Ninafahamu.”

Na nusu saa baadae walikuwa nyumbani kwa Diane, wakiwa wanavua nguo huku mikono yao ikitalii mwili wa kila mwenza katika sehemu zenye kusisimua, na hatimaye uvumilivu uliwashinda wakapanda kitandani.

Richard alikuwa mtaratibu na mkorofi na mwenye hamu na aliyeridhika, na kila kitu kilikuwa ni miujiza. Ulimi wake uligusana na mwili wa Diane ukitambaa hapa na pale na hatimaye alimwingia.

Waliutumia mchana wote, na karibu usiku wote wakiongea na kuoneshana ufundi, na wakafungua mioyo yao kupena nafasi. Na ilikuwa ni faraja kuliko maneno yanavyoweza kueleza.

Asubuhi wakati Diane akiandaa kifungua kinywa, Richard aliuliza, “Naomba nikuoe, Diane?”

Diane aligeuka akamwambia. “Hauhitaji kuomba. Sema lini?”

Na ndoa yao ilifungwa mwezi mmoja baadae. Sherehe ilifaana huku marafiki na familia zikiwapongeza wanandoa wapya. Diane aliutazama uso wa Richard na kuyakumbuka maneno ya uongo ya yule mnajimu msoma nyota na kutabasamu.

Fungate yao walipanga ifanyike Ufaransa wiki moja baada ya ndoa, lakini Richard alimpigia simu kutokea kazini. “Kuna project mpya imekuja ofisini na siwezi kutoka. Unaonaje tukifanya fungate baada ya miezi michache? Samahani, mpenzi.”

Diane alijibu, “Usijali, mpenzi.”

“Ungependa tupate chakula cha mchana pamoja leo?”

“Ndiyo.”

“Kuna mgahawa unapika mapishi mazuri ya ufaransa. Nitakupitia twende tukale hapo baada ya lisaa limoja.

Nusu saa baadae, Richard alikuwa nje akimsubiri Dianne. “Za kushinda, mpenzi. Kuna mteja wa ofisini mmoja namsindikiza. Anaenda Ulaya. Tutaagana naye halafu tutaendelea na ratiba zetu.”

Diane alimkumbatia. “Sawa.”

Walipofika uwanja wa ndege wa Kennedy Airport, Richard alisema. “Jamaa ana ndege binafsi. Tutakutana naye kwa ndani.”

Mlinzi aliwaruhusu wapiti kuelekea eneo ambalo ilikuwa ni marufuku kupita, ambako ndege aina ya Challenger ilikuwa imeegeshwa. “Jamaa hajafika. Itabidi tumsubirie ndani ya ndege.”

“Sawa.”

Walipiga hatua kupanda ngazi na kupanda ndege hiyo ya kifahari. Injini ilikuwa inaunguruma.

Mhudumu wa ndege alikuwepo karibu na mlango. “Habari za asubuhi.”

“Nzuri.” Richard alisema.

Diane alitabasamu, “Nzuri.”

Waliingia ndani na kumtazama mhudumu akifunga mlango.

Diane alimgeukia Richard. “Huyu mteja wenu atatumia muda kiasi gani kufika?”

“Haitomchukua muda mrefu.”

Mlio wa injini uliongezeka na ndege ikaanza kupaa.

Diane alichungulia dirishani, na uso wake ukabadilika rangi. “Richard, Ndege inaondoka.”

Richard aligeuka kumtazama Diane kwa mshtuko, “Una uhakika?”

“Angalia nje ya dirisha.” Halafu akaongeza, “Mwambie rubani.”

“Nimwambie nini?” Richard aliuliza.

“Mwambie ashushe ndege chini, sisi sio abiria wake.”

“Siwezi. Ashapandisha ndege.”

Kulikuwa na ukimya halafu Diane akamtazama Richard, macho yake akiwa kayakodoa. “Tunaenda wapi?”

“Oh, sikukuambia? Tunaenda Paris. Si huwa unapenda mapishi ya ufaransa.”

Diane aslishtuka. Muonekano wake ukabadilika. “Richard, Siwezi kwenda Paris sasa hivi. Sina nguo. Sijafanya make-up. Sina...”

Richard alisema, “Kuna mtu aliniambia Paris kuna maduka mengi tu ya hivyo vitu.”

Diane alimtazama kwa muda, halafu akarusha mikono yake kumkumbatia. “Nakupenda sana, Richard.”

Richard akaguna, “Ulitaka fungate. Ndiyo hii sasa.”

Itaendelea...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom