Bituro Kazeri, Huyu si mchambuzi bali ni kada wa CCM

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,034
144,388
Habari wadau,

Huyu bwana amekuwa akialikwa star tv mara kwa mara kama mchambuzi wa siasa lakini ukimsikiliza hoja zake mara nyingi ni kuponda wapinzani na kusifia serikali ya CCM.

Kwa mfano,anasema wapinzani kutoka Bungeni ni utoto.

Madai ya katiba mpya yalikuwa na agenda za kisiasa.

Mwaka 2005 Raisi Kikwete ndie aliekuwa mtia nia mwenye sifa kuliko wote ndani ya CCM.

Anahoji kwanini tv za binafsi zilipinga kujiunga TBC kwa ajili ya taarifa ya habari ya saa mbili usiku lakini tv hizo ziko tayari kujiunga na tv za nje kama CNN n.k

Uzuri mtangazaji kamjibu kuwa wanajiunga na tv za kimataiga kwasababu wanatekeleza maagizo ya TCRA kuwa local tv stations hizo zinatakiwa zimpe mwananchi habari za ndani na za kimataifa kupitia stations za nje hivyo ndio maana wanajiunga na station za nje.

Anasema mgombea kumpa mpiga kura hela kama shilingi 100,000 ili ampigie kura haiwezi kuwa rushwa moja kwa moja kwasababu kura ni siri hivyo mtu anaweza kupewa hiyo 100,000 na bado asimpigie kura hivyo ni lazima kwanza ithibitishwe kama alimipigia kura ya ndio kabla kusema hiyo hela ni rushwa au laa!!

Hayo ni baadhi tu ya mengi aliyoongea na si leo tu bali anapoalikwa ni kuponda tu wapinzani!

Msikilizeni mjue kama ni mchambuzi au kada.
 
Huyu aliwahi kugombea Ubunge jimbo la Mwibara, akashindwa. Anaendesha mgahawa unaitwa Pizzeria karibu na mWanza hoteli, Mwanza. Ule mgahawa ukifika na kuanza kusifia wapinzani ama kuiponda CCM usishangae ukatimuliwa. Ni kijiwe cha karibu mwanaCCM atafutaye uongozi. Cha ajabu huyu Bituro mapenzi yake kwa CCM yamezidi kiwango, labda ili asiendelee kuudhi watu apewe cheo atulie, maana anashusha hata hadhi ya Star Tv.
 
Juzi na jana mwenyewe nilikuwepo STAR TV Kuchambua juzi kuhusu mwenendo wa uandikishwaji wa daftari la kudumu la wapiga kura na jana nikiwa mwanza na mwenzangu Rioba akiwa studio za Dar tulichambua kuhusu mwenendo wa bunge hili linalomaliza muda wake na pia nilipata nafasi ya kuongea na watangazaji offline, nilichokiona ni kwamba hata waandishi huwa wanakwazika mtu anapochambua kwa kuonyesha ushabiki wake kwa jambo fulani badala ya masilahi ya nchi.

Pamoja na watu wengi kusema nilichambua vizuri bila kuegemea upande mmoja lakini bado baadaye nilipata simu kutoka kwa mkurugenzi mmoja wa Halmashauri akiniambia kuwa nilimshambulia Waziri wa Fedha pale nilipogusia suala la ESCROW ambapo yeye waziri na gavana waliomba kinga ya kulindwa ili wasiwajibishwe kwa ESCROW SCANDAL Na suala BOT kutowajibika ipasavyo kwenye suala zima la uchumi wa nchi na hasa suala la shilingi kuporomoka na kutokuwa na mfumo madhubuti kwenye masuala ya fedha pamoja na riba kubwa kubwa za ma benki ambazo kisheria ziko chini ya BOT.

Kwa kifupi ni kwamba watangazaji huwa wanapata lawama zisizo za msingi kwa sababu unamwalika mtu ukitegemea ataongelea masilahi ya Taifa lakini ataongelea masilahi ya chama chake.
 
alikuwa mzee mmoja mwenye busara kipind anasoma saut lakn kwa sas yuko kimasrahi zaid kwa maana anafanya biashara katkat ya jiji la mwanza akiwa tofaut na ccm ni hatar kwa biashara yake
 
Ndio maana nikafungua JF nipate mawazo yenu kuhusu huyu jamaa maana sielewi anaongea nini? Star TV wanajishusha sana kumleta studio huyu jamaa hana anachoongea utumbo mtupu
 
Huyu Bituro Kazeri ni kada mwaminifu wa CCM. Na kama mnavyojua CCM is a mental disease, ndiyo maana hata hawezi kuwa objective because brain yake imeshatafunwa na huo ugonjwa.

Mwaka 2010 aligombea jimbo la Mwibara na Kangi Lugola. Bahati mbaya akashindwa na Kangi kwenye kura za maoni.

Yeye aliamini kwamba ameshindwa na Kangi kwasababu alikuwa hana degree. Hivyo baada ya kushindwa maoni akajiunga na SAUT ili kuipata hiyo degree, ili 2015 awe level moja na Kangi kugombea jimbo la Mwibara.

STAR TV ni ya Mhe Diallo, M/Kiti wa Mkoa wa Mwanza. Hivyo Bituro Kazeri anaitwa mara kwa mara Star TV kuchambua masuala ya siasa because Birds of the same feather flocks together. In deed sio mchambuzi wa Siasa bali ni mpiga debe wa CCM.

The BIG question is Je 2015, ataweza kumung'oa Kangi Lugola baada ya kupata hiyo degree ya SAUT?! It remains to be seen.
 
alikuwa mzee mmoja mwenye busara kipind anasoma saut lakn kwa sas yuko kimasrahi zaid kwa maana anafanya biashara katkat ya jiji la mwanza akiwa tofaut na ccm ni hatar kwa biashara yake

Haya ndio matatizo ya kutojiamini. Kwani kuwa mfanyabiashara na unafuata sheria unahofu ya nini kuwa na msimamo tofauti na chama tawala?
Mbona wazee kama Ndesamburo ni wafanyabiashara wakubwa na wa siku nyingi na wanaendelea kufanya biashara miaka nenda rudi?
 
Mkuu wala usihangaike nae, huyo ni kada wa siku nyingi sana wa CCM, nimemfahamu tokea mwaka 2009 kule Mwanza, akiwa kiongozi wa CCM, kwanza hata kuongea hajui
 
Bila shaka anaitumikia CCM kwa madai kwamba uendeshaji wa mgahawa ule pale Pizzeria una mgogoro.

Asipounga CCM mkono, atatimuliwa. Ni kweli Tv inayomwalika mtu ambaye si mchambuzi, bali kada wa CCM na mawazo mfu kama yale hushusha hadhi ya tv yenyewe.

Ni mapenzi haya haya ndiyo yalimkosesha ubunge Mwibara. Badala ya kumwaga sera na alitaka kuwafanyia nini watu wa Mwibara yeye kila siku akiimba CCM ni nzuri, CCM ni baba na mama, CCM nakupenda nk wapiga kura wakampuuza.

Anaipenda CCM kama tulivyokuwa tunalazimishwa kuiimba ilivyo nzuri tukiwa darasa la nne. Huyo ni mtu ana Masters katika Sociology.

Kwa vile amejipambanua ni mkereketwa halisi wa CCM, mwakani ateuliwe kuongoza mbio za mwenge, atakuwa amekichangia chama chake kwa kukimbia nchi nzima.
 
Mzee huyu ni kada tena mtiania ubunge Ukerewe!Ukiachana na ukada akijikita kwenye uhalisiha ni mtu mzuri sana,tena msomi wa hali ya juu tu,mwanzilishi wa taasisi ya sayansi jamii,
www.tasaja.org
 
Pizeria iko kwenye eneo linalotakiwa kuwa wazi,ngoja chadema ikamate halmashauri ya jiji mwanza tukapavunje
 
Mzee huyu ni kada tena mtiania ubunge Ukerewe!Ukiachana na ukada akijikita kwenye uhalisiha ni mtu mzuri sana,tena msomi wa hali ya juu tu,mwanzilishi wa taasisi ya sayansi jamii,
www.tasaja.org
wenzako wanasema mwibara,wewe unasema ukerewe,wenzako wanasema usomi wake umechagizwa na kangi lugora,wewe unasema ni msomi wa haja,###$&#*-@-@+@-@(@*$+@*#+@
 
Bituro ni kada wa ccm, mnazi wa msimbazi, amewahi kuwa Teller wa NBC kabla ya kubinafsishwa baadaye alikuwa kama Cashier wa kampuni ya utafiti wa madini JCI kabla nayo haijafilisika. Baadaye alipolipwa mafao yake alikwenda kwa mgongo wa kuanzisha mradi wa kuwasaidia watoto wa mitaani walio chini ya kuleana. sina hakika kama huo mradi unawanufaisha watoto su la....

kuwepo studio mara kwa mara ni kwa sababu ya akina David Lata na kaka yake Kuleana ndo kijiwe chao ila na hakika hana muda wa kujisomea na kuwa mchambuzi mzuri....
 
Sijajua kwa nini Star TV wanamtumia sana huyu jamaa. Mara kadhaa nimemuona akifanya uchambuzi Star Tv lakini hamna kitu cha maana anachoongea. Labda kupitia jukwaa hili Star Tv watatuelewa wadau wa vipindi vyao.
 
Sijajua kwa nini Star TV wanamtumia sana huyu jamaa. Mara kadhaa nimemuona akifanya uchambuzi Star Tv lakini hamna kitu cha maana anachoongea. Labda kupitia jukwaa hili Star Tv watatuelewa wadau wa vipindi vyao.

Kuna mwingine huwa anapenda kujiita mwandishi wa habari aliyebobea anaitwa Moses Mathew, Star TV wanamtumia sana ila uchambuzi wake huwa haueleweki kabisa.
 
Bituro ni kada wa CCM na sio mchambuzi wa masuala ya siasa.

Aligombea jimbo la Mwibara 2010 akashindwa na Kangi kwenye kura ya maoni CCM.

Akafikiri Kangi amemshinda kwasababu hana degree, baada ya kushindwa akaenda kusoma SAUT.

Mwaka huu 2015 anajiandaa tena kwenda kugombea akifikirii degree itamsaidia kumushinda Kangi.

Bituro anaitwa mara kwa mara Star TV sio kwamba ana weledi wa siasa, ila kwasababu ni mpiga debe wa CCM na Star Tv ni ya M/Kiti wa CCM wa mkoa Mwanza Mr. Diallo. Bituro ni kada wa CCM, Period.
 
Anachoongea ni ujinga tu, nimeshindwa hata kuendelea kumsikiliza.

Ndio maana nikafungua JF nipate mawazo yenu kuhusu huyu jamaa maana sielewi anaongea nini? Star TV wanajishusha sana kumleta studio huyu jamaa hana anachoongea utumbo mtupu.

Huyo jamaa ni kada maarufu wa ccm ila huwa anajitahidi kuficha ukada wake na ndio maana star tv huwa wanapenda Kumpa muda wa kusikika sana hewani,si unajua mmiliki wa hiyo tv?
 
Back
Top Bottom