Binti wa Karume azua mtafaruku kortini Dar

Hii stori inatuambia mengi. Kwanza bado nina msimamo kuwa yule Hakimu ni kilaza, kwa sababu kwa nini asingemchukulia hatua huyo wakili? mbona kuna mkuu wa wilaya alimjia juu Lowassa pale iLowassa alivyojaribu kumdhalilisha mbele za watu?

Kutokana na maelezo ya rushwa hapo mahakamini nina hisia kuwa huyo Hakimu kilichomzuia kumfundisha adabu Wakili ilikuwa si kuogopa jina la Karume, bali huyo Hakimu ana jambo lingine analoogopa in this case ni hayo mambo ya rushwa. Hapa ni shari kuzaa heri, maofisa wa kuzuia rushwa wanatakiwa wateremke pale wawapige watu jamba jamba hata kama hawatamkamata mtu basi waonyeshe presence yao pale na wachimbe biti kishenzi kwamba tumeweka mitego na tunawatumiwa washtaki na washtakiwa kwa hiyo muhusika wa kesi akiombwa rushwa tu tutajua na Hakimu anayeshughulikia kesi hiyo tutamuabisha, yaani hapo ni scare tactics za kuzuia watu kuomba rushwa kabla hata hawajaomba, unajua unaweza kuzuia rushwa kisaikolojia tu! Mambondia kama kina Mohamed Ally walikuwa kwanza kabla ya ngumi wanampiga mtu kisaikolojia mtu anatishwa wewe ntakufanyizia leo ntakuteremshia ngumi kama nyuki, jamaa anakuwa anapigwa pambano la kifikra kabla la ngumi halijaanza.

Hii inawezekana mahakamani, mahakimu wataogopa kupokea rushwa na serikali iwaongezee mishahara na mambo yataenda na haki itatendeka.


Wel said, but who said pccb officers are angels? they are also corrupt like hakimuz, nao wanazimwa vilevile wakitaka ku act. kuna law of protectionism hapa, ma godfathers, na wanaoozea magerezani ni wanyonge tu. This whole thing confuses me, mahakimu wanaofunga wala rushwa nao ni cwala rushwa, pccb wanaopambana na rushwa nao wala rushwa, viongozi wakubwa nao wala rushwa, watoto wao pia waliolewa madaraka ya wazazi wao hata kutohehimu mamlaka ya mahakama kwa kujitetea kwamba wanazuia rushwa nao wala rushwa, i am so fed up with this nation, May God help us.
 
Huyu Dada inaonekana ni katili sana sasa hii inaturahisishia kumuelewa kwamba hata mumewe ana shida kubwa katika mawasiliano na huyu mkewe.
 
Mimi tokea jana nilihisi hili suala haliko simple hivyo!
Nadhani kwamba hili swala la Wakili Karume linahitaji kugeuzwa na kuwa swala la rushwa mahakamani!
Vitu hivi vinaweza vikamathiri Fatma na akajikuta amefungiwa lakini angalau ameanzisha mjadala kuhusu rushwa! Mi nadhani kutokana na hilo tungeanza thread nyingine mpya kuhusu rushwa katika vyombo vya dola.
 
Leo asubuhi Binti Karume ametembelea Claoud FM katika "Power Break Fast" kinachoendeshwa na Masoud Kipanya na Finna Mango. Kitu cha kwanza ambacho nimegundua ni kuwa huyu Binti ni jasiri sana (labda kwa kuwa ni mtoo wa Kigogo). Lakini kitu cha pili ni kuwa huenda hii story ikawa imekuzwa na Wahandisi wa habari.

Kwa mujibu wa madai yake ni kuwa hakufanya kama jinsi ilivyolipotiwa na magazeti na tena Mahakamani hakukuwa na Waandishi wa Habari. Kwa mijibu wa madai yake ni kuwa Wahandisi hao wa habari waliitwa na Hakimu Addy Mamuya baadaye kabisa na Hakimu huyo akaanza kuwaeleza hayo yaliyotolewa kwenye Magazeti. Binti KArume anasema kuwa habari hizo amepewa na mmoja wa Waandishi wa Habari yaani Hakimu Mamuya aliwaita Wanahabari na kuwaeleza hayo ili kumkomoa.

KAtika kipindi hicho cha Clouds FM pia Wakili Karume alieleza kuhusu kujitoa kwa hakimu wa awali anayejulikana kwa jina kla Euphemia Mingi amabcho pia ni kichekesho!

Swali la kujiuliza hapa ni hili: ikiwa ni kweli Wakili KArume alimvamia Hakimu Lyamuya; Je, kwa nini hakuripoti suala hilo kwa Polisi wa Pale Mahakamani au kwenda Kituo chsa Polisi kulalamika, au hata kutoa amri ya kumkamata Wakili huyo na kutoa adhabu papo hapo kwa kosa la kuidharau Mahakama au kuhatarisha Amani?

Mambo mengine hata kama ni mabaya, yanaotkea ili kutufunulia yaliyojificha na kutusaidia kujifunza na kujirekebisha. Naamini ninaelekea pazuri zaidi.

Ibra napenda jinsi unavyotumia neno "wahandisi" (kiingereza ni engineers). Probably they "engineered the news" i.e the journalists used some "engineering principles" to fabricate the news. Hawa tunao wengi.
 
Je, unakubali kuwa mawakili ni maofisa wa mahakama?

Kitu ambacho hufahamu ni tafsiri yako kutoka kiingereza ya 'an officer of the High Court' kwa kiswahili kumfanya advocate kuwa na authority juu ya jaji, kitu ambacho ni kichekesho. Kiswahili hakina neno fasaha katika nyanja hii kwa maoni yangu pengine watafutwe wanaoelewa Kiswahili sanifu wakusaidie.

The principal argument ni hiyo ya authority, mengine yote ni mazungumzo baada ya habari.
 
Nadhani umefika wakati wa wachangiaji kuacha kuandika habari za kufikirika, je unaweza kutuambia unamfahamu vipi Wakili Fatma? je ni mtu wa namna gani?

Pundamilia,

Do not be naive dude! The first story was about Miss. Karume being a bully. And so are many other stories about her character. You do not need to know her as a friend or a buddy to figure two and two is four.

What everyone had written was due to news that had been published and the fact that TLS has already sent a request for investigation citing previous incidents that she was involved.
 
HAKIMU MWANGESI AKAMILISHA RIPOTI

Na Grace Michael

HAKIMU Mkuu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Bw. Sivangilwa Mwangesi, amesema kuwa ni kweli Wakili wa kujitegemea ambaye ni mtoto wa Rais wa Zanzibar, Bi Fatma Karume, alifanya vurugu mahakamani.

Kutokana na sakata hilo ambalo Bw. Mwangesi alitakiwa kulifanyia uchunguzi na kutoa taarifa katika ngazi husika na tayari amekamilisha uchunguzi huo na kukabidhi ripoti sehemu husika kwa uamuzi zaidi.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Bw. Mwangesi alisema kutokana na uchunguzi alioufanya kutoka kwa watu mbalimbali waliokuwa eneo la tukio imeonekana ni kweli Bi. Fatuma alifanya vurugu hizo.

"Nimefanya uchunguzi wangu na tayari suala hili nimelipeleka ngazi za juu kwa uamuzi zaidi, lakini kwa maoni yangu ni kweli nimethibitisha kuwa wakili alifanya vurugu hizo," alisema Bw. Mwangesi.

Bw. Mwangesi alipotakiwa kufafanua ni kwa nini Bibi Addy Lyamuya hakumchukulia hatua yoyote wakili huyo, alisema alipigwa butwaa na hakutarajia kama wakili anayefahamu kanuni na maadili, angeweza kufanya hivyo.

Kuhusiana na suala la Hakimu anayetuhumiwa na Bi Fatma kupokea rushwa kwa mteja wake kuwa amesimamishwa kazi, Bw. Mwangesi alifafanua kuwa hajawahi kupokea maelekezo yoyote ya kusimamishwa kazi kwa Hakimu huyo na ndiyo maana mpaka sasa bado anaendelea na kazi mahakamani hapo.

"Ninachokijua, siku ya tukio alilolifanya Bi Fatma, alikuja hapa na kunipa taarifa za kuwa tayari amepeleka malalamiko katika Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (PCCB), hivyo mambo mengine yanayosemwa ni maoni yao na suala la kuwa Mahakama inanuka rushwa si kweli, kwani Kisutu ni nzuri na inapingana na rushwa vilivyo," alisema.

Kutokana na vurugu hizo mpaka sasa kesi hiyo hajapangiwa Hakimu mwingine wa kusikiliza, kutokana na tuhuma zilizopo kuwa mahakimu wote Kisutu ni wala rushwa, hivyo Bw. Mwangesi bado anafikiria aipange kwa nani.

"Nasubiri barua ya kuhamisha kesi hii kutoka kwa Fatma kwani tayari alishasema ataihamisha, hivyo nasubiri maneno hayo kwa maandishi," alisema Bw. Mwangesi.

Sakata hilo lilitokea Jumatano baada ya Bibi Lyamuya kuahirisha kesi hiyo na kuipangia siku nyingine, ambayo Bi Fatma aliipinga kwa nguvu zote hali iliyozua tafrani kubwa kutokana na maneno makali aliyokuwa akiyatoa wakili huyo.

Kutoka: Majira
 
I beg to differ

Sioni kosa la Fatma

-Kuzungumza kwa sauti kubwa ?- haikatazwi mahakamani

-Kusema ataandika barua kwa wakubwa wake?- Hiyo inawezekana ikawa ni standard procedure na sioni tatizo liko wapi

-Tusisahau kuwa moja kati ya kazi ya media ni kudramtize mambo hivyo tusi rule out hilo

-Vile vile je kuna mtu anayo statement toka kwa Fatma na huyo mwenzie?

That said, naungana na wengi kwamba jamii yetu ya Tanzania leo ina resent sana hawa watoto wa wakubwa ambao wengi wanajua wana nafasi hizo kwa sababu Baba zao wamewapa hizo nafasi, na pili watanzania wenye uwezo zaidi wamekosa hizo nafasi hivyo Fatma ajiandae vilivyo kukabiliana na hii resentment hata kama haki itakuwa iko upande wake kwani hii ni nafasi nzuri ya wenye ma gridge na hawa watoto wa kishua kumaliza hasira zao

Na zaidi ya yote hayo, kwa jinsi Judiciary ya Tanzania inavyonuka RUSHWA wengi huwa hawapati mwanza wa kuwapa au kutoa duku duku lao kuhusu Rushwa kwenye mahakama zetu sasa in the end wakitokea watu kama akina FATMA ambao eidha kwa ujasiri wao au kwa nafasi zao wakalisema hili then inakua ni ahueni kwa wengi...


Hivi MWANAISHA CHANDE bado yuko pale au?
 
jamani kama nilivyosema awali wakili ni ofisa wa mahakama kuu kwa hiyo hakimu wa mahakama ya hakimu mkazi hawezi kumwadhibu kwa namana yoyote ile. yeye anachoweza kufanya ni kupeleka malalamiko kwa hakimu mkazi mwandamizi ili awasilishe malalamiko yake kwenye kamati maalumu ya malalamiko. ndiyo maana hakimu lyamuya alitafuta mashahidi wake na kusema wako tayari kutoa ushahidi wakati muafaka ukifika!!

kamati hiyo ina majukumu haya

ADVOCATES ACT (CAP 341)
section 13. Powers of Committee
(1) The Committee shall have jurisdiction to hear and determine–
(a) any application by an advocate to procure the removal of his name from the Roll;
(b) any application by any person to remove the name of any advocate from the Roll; or
(c) any allegation of misconduct made against any advocate by any person.

(2) Where an application or allegation of misconduct is made under paragraph (b) or paragraph (c) of subsection (1), the Committee shall have power to require the advocate in respect of whom such application is made, or in respect of whom such allegation is made, to show cause why his name should not be removed from the Roll of advocates or to answer the allegation made, as the case may be:
Provided that where, in the opinion of the Committee, an application under paragraph (b) of subsection (1), or an allegation under paragraph (c) of that subsection does not disclose a prima facie case, the Committee may refuse such application or may dismiss the allegation without requiring the advocate to whom the application or allegation relates to show cause why his name should not be removed from the Roll or to answer the allegation, as the case may be.

(3) On the hearing of an application under paragraph (b) of subsection (1) or any allegation under paragraph (c) of that subsection–

(a) the Committee shall give the advocate to whom the application relates or against whom the allegation is made an opportunity to appear and be heard by it, and for that purpose shall, not less than seven days before the date fixed for the hearing, inform him of such date and of the particulars of the application or allegation, furnish to him a copy of any affidavit made in respect of the application or allegation, and notify him of the time and place when and where he may inspect and make a copy of any other document in the possession of the Committee which it deems relevant to the application or allegation;

(b) the Committee may in the course of the hearing, hear such witnesses and receive such documentary evidence as in its opinion may assist it in coming to a conclusion as to the truth or otherwise of any allegation made against the advocate.

(4) Upon the conclusion of a hearing subsection (3) the Committee may, if it is satisfied of the truth of the allegations upon which an application under paragraph (b) of subsection (1) is founded or of any allegation of misconduct made against the advocate–

(a) direct that the name of the advocate be removed from the Roll;

(b) admonish the advocate; or

(c) suspend the advocate from practising for such period as the Committee may direct.

(5) In any proceedings under this section the Committee shall have power to make any such order as to payment by any party of any costs or witness expenses as it may think fit, and any such order shall be deemed to be an order of the High Court and may be enforced in like manner.

(6) If in the course of any hearing before the Committee after the whole or any part of the evidence has been heard and recorded, there is for any reason a change of the members of the Committee, the Committee may act on the evidence so recorded before such change, or partly recorded before and partly recorded after such change, as the case may be, or the Committee may re-summon the witnesses and recommence the hearing:
Provided that the advocate whose misconduct is the subject matter of the proceedings may, when the Committee resumes its proceedings after such change, demand that all the witnesses or any of them be re-summoned and reheard and shall be informed of such right by the Committee when it so resumes its proceedings.



Mzee unajua fika kuwa hapa inatafutwa FITNA na kama haionekani then utakuwa unatwanga maji kwenye kinu

Kuja na emperical evidence kusupport argument yako kwa kweli si style ya JF na ni wachache sana watakubali hili

Tatizo ni kuwa watu wanamjadili FATMA kama mtoto wa karume na si kama wakili

Now the question would be je watu wako tayari kuwajadili hawa watoto wa wakubwa bila wengine kusema hapa si mahala pake? I am not sure kama kuna watu wako tayari kusoma wanayotenda marafiki zao humu

On a flip side nakusifu kwa kuchukua mwelekeo tofaut wa kutetea hoja yako na naomba unedelee namna hiyo...and this will be the best way to separate men from boys JF style

Sasa kama kuna mtu ana rebuttal ya hiyo quote ya CHAUMBEYA then aje
 

...That said, naungana na wengi kwamba jamii yetu ya Tanzania leo ina resent sana hawa watoto wa wakubwa ambao wengi wanajua wana nafasi hizo kwa sababu Baba zao wamewapa hizo nafasi, na pili watanzania wenye uwezo zaidi wamekosa hizo nafasi hivyo Fatma ajiandae vilivyo kukabiliana na hii resentment hata kama haki itakuwa iko upande wake kwani hii ni nafasi nzuri ya wenye ma gridge na hawa watoto wa kishua kumaliza hasira zao...



game nakubaliana nawe katika hili.
aidha napenda kuongeza kwamba pamoja na uwezekano kwamba bi fatma amefanya kosa la kutofuata utaratibu, inawezekana pia ameweza kusema yale yanayowasibu mawakili " wasio watoto wa vizito" ambao wanashindwa kutekeleza wajibu wao kwa sababu ya rushwa iliyokithiri katika mahakama zetu. kama kumbukumbu zangu ni sahihi hata jaji samatta alieleza kusikitishwa kwake na rushwa katika mahakama zetu.
 

Mzee unajua fika kuwa hapa inatafutwa FITNA na kama haionekani then utakuwa unatwanga maji kwenye kinu

Kuja na emperical evidence kusupport argument yako kwa kweli si style ya JF na ni wachache sana watakubali hili

Tatizo ni kuwa watu wanamjadili FATMA kama mtoto wa karume na si kama wakili
Now the question would be je watu wako tayari kuwajadili hawa watoto wa wakubwa bila wengine kusema hapa si mahala pake? I am not sure kama kuna watu wako tayari kusoma wanayotenda marafiki zao humu

On a flip side nakusifu kwa kuchukua mwelekeo tofaut wa kutetea hoja yako na naomba unedelee namna hiyo...and this will be the best way to separate men from boys JF style

Sasa kama kuna mtu ana rebuttal ya hiyo quote ya CHAUMBEYA then aje

Hapa anajadiliwa kama mtoto wa raisi kutokana na maneno yake mwenyewe namnukuu

'Wewe hunijui mimi ni ..wala hunifahamu.. hujui kazi yako.. nitaandika barua kwa wakubwa zako...

nadhani yeye ndiye anajitambulisha zaidi kuwa mtoto wa mkubwa kaliko kazi yake ( I stand to be corrected)
 
jamani huyu binti kweli amefanya kosa,,ila naona kila sehemu wanangania upande mmoja amearibu mahakamani,,labda napenda kuwaeleza pengine huyu ndie atakaekuwa nabii wa walalhoi pale MAHAKAMA ya KISUTU,,Ndugu zangu kisutu imejaa rushwa chafu chafu hata ukisema ufisadi itakuwa haifai ni aibu,,
Kwanza nampongeza sana huyu bibi kwa kuwafumbua watu macho,,mimi nilikuwa na kaka yangu anaitwa EDGAR,jamani mtoto wa mamayngu mkubwa,bahati mbaya akaja kuwa mwizi wa kimataifa
huyu bwana amekuwa akisumbua kiasi cha kwamba ndugu wengine wanaomba apigwe maisha,wengine wakasali atoke,,katika mvutano huu
mama mmoja alisimamia hii kesi ,,sisi tulikuwa wahusika wakupeleka kiasi kinachotakiwa,,jamani huyu dada mwa cheni ni mwokozi,pamoja na kaka yetu alitoka kwa dhamana akakimbia,,na kesi ufutwa wengine walibaki maskini mpaka sasa tunavyoongea
Ndugu zanguni hali ni mbaya kisutu mbaya,,rushwa kuanzia mlangoni kwa mfagizi mpaka wanaokohfadhi mafaili ,,huku ni balaa zaidi aitamaniki,,kuja kumwona pp huyu ndie connector wa rushwa za mahakimu,,hata ukijitahidi kumwona hakimu wapi,,hivyo huyu jamaaa ana uwezo wa kula zaidi hata ya hakimu
 
mbaya ni pale kila alipopelekewa pesa anaongeza akifatwa karibu na kesi anapiga simu mama amesema mgao mdogo kama hamna mkifika kesi simple inaairishwa hiyooooooo,jamani msione huyu dada amefika hivyo yalimfika shingoni ,,na wale jamaa wakiona huna hela na washakula hela yako wanaairisha kesi ukileta ujinga ndio hivyo wanabadilisha mahakimu,,huyu dada hata kama amekoseza msameheni ila amefungua ukurasa mpya labda walalahoi kesi zao zinaweza kwenda kwa haraka kuliko hapo nyuma

Waziri wa sheria nilimnukuu alisema siku moja hivi sasa wanajitagdi kupeleka kesi mapema ziishe mapema,,lakini hiyo ni mchanga wa macho rushwa haishi,,watu wanateseka jamani ,wengine
wanaamua umemkasirisha au umemnyima dili ankubakimbizia kesi
ukifika anatoa hela ,,na kuamua siku utakayotoka,,mungu ikomboe tanzania,,mungu ibariki tanzania,ni hayo tu jamani nikiwaeleza na huyo akimu ni nani inasikitisha wengine inawezekana msiandike tena na kulia,wadau tusadiane kukomboa wananchi
 
Pdidy:
Kama hayo uliyoyaeleza ndivyo yalivyo hapo Kisutu, basi huyo mtoto wa mkubwa Fatma angewasaidia sana waTanzania kuondokana na uozo huo kwa kutumia njia nyingine za kuondoa matatizo kama hayo unayoyazungumzia.
Linaloonekana hapa ni kuwa yeye anatumia kifua cha jina lake kukiuka taratibu za kazi.

Kama nia yake ni kuwasaidia walalahoi na kuondoa uozo hapo Kisutu, wengi tutamuunga mkono sana hapa, bila hata kujali yeye ni mkubwa. Tena wengi tutaanza hata kupiga mbiu ya kurithishwa kiti, kama ilivyo kawaida. Njia anazozitumia sasa zinatufanya tuamini kuwa si kwa maslahi ya walalahoi.
 
Back
Top Bottom