Binti wa Karume azua mtafaruku kortini Dar

Semanao

JF-Expert Member
Jul 25, 2007
208
16
*Amfokea Hakimu Kisutu wakati akiendesha kesi
*Ainuka kumvaa, wasikiliza kesi, karani wamzuia

Na Rabia Bakari

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, binti wa Rais Amani Abeid Karume wa Zanzibar, Bi Fatma Karume, amemtishia kwa maneno makali huku akitaka kumshambulia Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Bibi Addy Lyamuya.

Tukio hilo la aina yake lilitokea mahakamani hapo jana, wakati Hakimu Lyamuya akisikiliza kesi ya madai ya mtoto kati ya Bw. Sadiq Walju na Bi Saeda Hassam ambapo Bi. Fatma alikuwa akimtetea Bw. Walju.

Awali, ilidaiwa mahakamani hapo kuwa, kesi hiyo namba 60 ya mwaka jana, ilikuwa ikisikilizwa na Hakimu Mkazi, Bw. Adolf Mahay, lakini baada ya kutokea kutokuelewana na wakili huyo (Fatma), hakimu Mahay alijitoa kusikiliza .

Septemba 20 mwaka huu, kesi hiyo ilipangwa kwa Hakimu Mkazi, Bibi Euphemia Mingi na ilipofika Oktoba 8 mwaka huu, Hakimu Mingi alijitoa kusikiliza kwa kile kilichoelezwa kufokewa mahakamani na wakili Bi Fatma na kushinikizwa kujitoa katika kesi hiyo kwa madai ya kutoiendesha ipasavyo.

Jana kwa mara ya kwanza, kesi hiyo ilikuwa ianze kusikilizwa na Hakimu Mkazi, Bibi Lyamuya lakini kutokana na sababu za kimahakama aliiahirisha hadi Januari 13 mwakani.

Baada ya Hakimu Lyamuya kupanga tarehe hiyo, Bi. Fatma aliipinga na kumwambia anataka kesi hiyo isikilizwe Novemba 23 mwaka huu.

Karani alimwambia Hakimu kuwa tarehe iliyopendekezwa na wakili Fatma, imejaa hivyo hakutakuwa na nafasi, ndipo wakili huyo alipopendekeza isogezwe na kusikilizwa Januari 2 mwakani.

Baada ya pendekezo hilo, Hakimu Lyamuya alimwambia wakili huyo kwamba hatakuwa na nafasi tarehe anazolamizisha, hivyo anaomba kujitoa kusikiliza kesi hiyo na badala yake apangiwe hakimu mwingine, mwenye nafasi katika siku hizo.

Kutokana na kauli hiyo, ndipo, Bi. Fatma alianza kufoka mahakamani hapo kwa sauti hali iliyozua tafrani na watu waliokuwapo kubaki wameduwaa kwa kilichokuwa kikiendelea.

"Umeniona kwa mara ya kwanza, hunijui mimi ni nani, nitakuonesha kwanza hujui kazi, nitaandika barua kwa wakuu wako wa kazi," wakili huyo alifoka kwa jazba huku akimnyooshea kidole Hakimu Lyamuya na kumfuata alipokuwa amekaa.

Hata hivyo, Bi. Fatma alizuiwa na karani wa mahakama pamoja na watu waliokuwamo mahakamani hapo, ambao walifanikiwa kudhibiti mtafaruku huo.

Akizungumzia tukio hilo, Hakimu Mkuu Mkazi Mfawidhi, Bw. Sivangilwa Mwangesi alisema amepata taarifa ya tukio hilo na atalifanyia uchunguzi.

"Nimepata malalamiko ya wote wawili, yaani wakili Bi. Fatma na Hakimu Lyamuya, nitafanya uchunguzi kwani kitendo hicho ni kinyume cha sheria, zogo wala ugomvi haviruhusiwi mahakamani, hata kama umegombana na mtu msubiri nje ya mahakama si kuleta vurugu ndani ya mahakama," alisema Bw. Mwangesi.

Aidha, Hakimu Lyamuya alisema awali wakati Bi. Fatma akimtolea maneno ya vitisho, alidhani ni utani, lakini alipomwambia kuwa ataandika barua kwa wakuu wake wa kazi, ilibidi awe makini zaidi na jambo hilo.

"Nina mashahidi, maana nimejua kwamba hafanyi mzaha, shahidi wangu wa kwanza ni Bw. Jerome Msemwa, Bw. Jabiri Mkongo, Bw. Juma Magota, Bw. Derick Ngoro na watu waliokuwa mahakamani wakati kesi hiyo ikiendelea," alisema Hakimu huyo.
Source-MAjira (22/11/2007)
 
Bila shaka kama angekuwa mtoto wa mkulima wa kawaida tu kwanza angetiwa ndani kwa shitaka la kidhalilisha mahakama na kumpa vitisho hakimu. Lakini kwa kuwa ni mtoto wa mkubwa hiyo ni ndoto kwani ana immunity hadi mahakamani, ingawa sidhani. :(
 
hapa ndipo natamanigi niwe bongo.. ningemswekwa Lupango halafu nione askari gani atamtia pingu! Tukiwaambia wamelewa ugimbi wa madaraka wanatushangaa, sasa hadi watoto wao wameanza kupata ganzi kisa baba ndio kala mbilimbi!
 
Nafikiri unaona maneno ya hakimu anaposema ilibidi awe makini yule mtoto aliposema ataandika barua kwa wakubwa wake. Na ndipo utajua kuwa mahakama zetu haziko HURU kabisa.
 
Mimi ningekuwa ndo Hakimu.. naanza na kumsweka ndani kwanza kwa masaa kadhaa hadi akili imrudie!
 
hapa ndipo natamanigi niwe bongo.. ningemswekwa Lupango halafu nione askari gani atamtia pingu! Tukiwaambia wamelewa ugimbi wa madaraka wanatushangaa, sasa hadi watoto wao wameanza kupata ganzi kisa baba ndio kala mbilimbi!

wewe kama nani ? hivi ni kitu gani ambacho unadhani huwezi kufanya wewe ? maana kazi za wanasiasa wee unatilia mguu, mahakimu unatia mguu, yaani kila kitu unadhani unaweza kufanya bobu ?? kila jambo na mtu wake,wee andika mashairi mzee !
 
Polisi walikuwa wapi wakati Wakili huyo akitishia amani na akidharau mahakama? Hilo ni kosa la jinai na Polisi lazima wamfungulie mashitaka ya kudharau mahakama na kuvuruga amani na pia Polisi, Idara ya Mahakama,na Wizara ya Sheria na Mambo ya Katiba watoe tamko kuhusu hilo; pia Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) wamchukulie hatua wakili huyu asiyefuata sheria na kuheshimu mahakama. Tutavumulia upuuzi huu hadi lini?
 
wewe kama nani ? hivi ni kitu gani ambacho unadhani huwezi kufanya wewe ? maana kazi za wanasiasa wee unatilia mguu, mahakimu unatia mguu, yaani kila kitu unadhani unaweza kufanya bobu ?? kila jambo na mtu wake,wee andika mashairi mzee !

Kada,

MKJJ, kajiweka katika nafasi kama Hakimu Lyamuya. Unless you have personal grudge with MwanaKijiji, your comments above clearly shows us the rotten mentality that has been circulating in minds of Watanzania Watendaji who are afraid to govern using principles and bend to influencial powers and supremacy!
 
Court house ina rules zake. Court is the house of judge, don't come in my house and tell me what to do. That is where i like US court system. Sababu Judge anakutupa lupango kisha yeye ndio anajadili bond yako, now you do the math.

I'm fed up with Tanzania rule of law, this non sense need to stop.
 
Mimi ningekuwa ndo Hakimu.. naanza na kumsweka ndani kwanza kwa masaa kadhaa hadi akili imrudie!

nadhani hapa huyu Hakimu alikusa point za bure. Mbona hapo ndio alikosa point za bure kabisa? watu hawajui kutumia nafasi kujenga umaarufu kwenye kazi zao? Angemweka ndani kwa masaa walau matatu
 
Mimi ningekuwa ndo Hakimu.. naanza na kumsweka ndani kwanza kwa masaa kadhaa hadi akili imrudie!

Mie nimeanza kukumbuka maneno ya Mzee Mwanakijiji,Tuwadhilie hawa viongozi..mtoto yeyote wa mkubwa akinipa maneno ya madharau,namtoa macho ..siko tayari kuendelaza upuuzi huu..Mie nataka achukuliwe hatua.Ipo siku nitamtoa mtoto roho
 
Lakini mimi ninadhani huyo Fatma Karume na hakimu go back a long way, because binti huyu amekuwa akipambana na mahakimu wengi lakini safari hii imeripotiwa.
Tunamtetea Hakimu lakini ukiangalia threads zetu hapo nyuma tumekuwa tukilaani sana mahakimu kuwa walarushwa. Sasa katika kesi kama hizi za alimony unakuta mawakili wanaotetea akina mama na watoto wanajikuta wakipewa wakati mgumu.
I think that Fatma just snapped but she really fights for her clients! I know that. However, I must admit she overstepped na kwa kweli angestahili kupewa adhabu, kwani hata kama aliona kuwa hakimu amefanya kosa, angefuata utaratibu. I believe the bar association itabidi imweke chini na hata kumpa adhabu ili ajifunze kucontrol her temper.
 
Tatizo la viongozi wa kiafrika ni miungu watu. Nina hakika kama hakimu angelifuata sheria kama inavyokuwa kwa watoto wa wakulima kwa kumsweka ndani Fatma, basi kibarua kingeota mbawa. Mambo haya yatakuja isha tu, kwani lini tulitegemea raia wangevamia ama kuchoma kituo cha polisi.

Pili, nafikiri huyu kada pinzani ndiye Fatma, ila akiwa hapa JF anajiita kada pinzani.
 
Hakimu huyu si ndiye aliyewatupa lupango kina Nguza & Co. maisha.

Mbona kashindwa kutumia makali yale yale hapa?
 
huwezi ukasema kama ungekuwa bongo ungemuweka lupango ! wewe nani ?? ina maana hata huku nje mtu akikosea basi random personal achukue kazi ya polisi ??
 
wewe kama nani ? hivi ni kitu gani ambacho unadhani huwezi kufanya wewe ? maana kazi za wanasiasa wee unatilia mguu, mahakimu unatia mguu, yaani kila kitu unadhani unaweza kufanya bobu ?? kila jambo na mtu wake,wee andika mashairi mzee !

Tatizo la viongozi wa kiafrika ni miungu watu. Nina hakika kama hakimu angelifuata sheria kama inavyokuwa kwa watoto wa wakulima kwa kumsweka ndani Fatma, basi kibarua kingeota mbawa. Mambo haya yatakuja isha tu, kwani lini tulitegemea raia wangevamia ama kuchoma kituo cha polisi.

Pili, nafikiri huyu kada pinzani ndiye Fatma, ila akiwa hapa JF anajiita kada pinzani.

Hapana huyu KadaMpinzania alichosema hadi ukamshitukia kama yeye ndiye Bi Fatma ni sahihi kabisa wala hakuwa na negative impact kwa maoni yake. Aliposema kwamaba kila jambo na watu wake alimaanisha kwamba kwa taratibu zilizopo za kukiuka zile za kisheria mtu wa kawaida huwezi ukafanya hivyo na isitoshe yule ni mtoto wa > fulani kwa maana hiyo anayatumia madaraka vibaya. Sijamnukuu KadaMpinzani nina dhania likuwa anamaanisha hivyo kwa mbaaaaaaaaaaaaaaaali.
 
Itakuwa Jambo la Ajabu na la kushtusha kama Chama Cha mawakili (TLS),Hakitomchukulia Hatua huyu Dada,ambaye amemdharau Hakimu na Kudharau Mahakama.Inawezekana kabisa alikuwa anatofautiana na maelezo ya Hakimu,lakini kitendo chake cha kauli za dharau,na ukali ni kuivunjia Heshima Mahakama na Watendaji wake.Ni wazi kabisa sheria itachukua Mkondo wake dhidi ya Advocate Fatma.
 
Hakimu huyu si ndiye aliyewatupa lupango kina Nguza & Co. maisha.

Mbona kashindwa kutumia makali yale yale hapa?

Ndiye huyo huyo utadhani kawa mwingine kumbe ni yule yule na long experience za uzoefu wa muda mrefu maana tangu kesi ya Nguza hadi leo amepata uzoefu lakini kwa Bi Karume ka-gwaya.
 
Back
Top Bottom