Binti wa Karume azua mtafaruku kortini Dar

mtu pekee ambaye anaweza kutoa uamuzi wa kumsimamisha wakili kwa kumkosea adabu ni jaji wa mahakama kuu!! jaji wa mahakam kuu anaweza kufanya hivyo kwa sababu wakili ni court officer wa mahakama kuu kwa hiyo yuko chini yake!!!

haki hii ya jaji wa mahakam kuu inapatikana

ADVOCATES ACT (CAP 341
22. Disciplinary powers of Judges and High Court apart from inquiry by Committee
(1) Nothing in this Act contained shall supersede, or interfere with the powers vested in the Chief Justice or any of the Judges of the High Court to deal with misconduct or offences by advocates.
(2) Without prejudice to the generality of the foregoing subsection, notwithstanding that no inquiry may have been made by the Committee–
(a) the Chief Justice or the High Court shall have power, for any reasonable cause to admonish any advocate or to suspend him from practising during any specified period or make an order of removing his name from the Roll;
(b) any Judge of the High Court shall have power to suspend any advocate in like manner temporarily, pending a reference to, or disallowance of such suspension by, the High Court;
(c) any advocate aggrieved by any decision or order of the Chief Justice or a judge of the High Court made in pursuance to paragraph (a), may, within thirty days of such decision or order appeal–
(i) in the case of a decision or order by a judge of the High Court, to the Advocates' Committee; and
(ii) in the case of a decision or order of the Chief Justice, to the Court of Appeal:
Provided that where the decision or order appealed against was made by a judge of the High Court nominated by the Chief Justice to be a member of the Advocates' Committee under section 4(1)(a) of this Act, such judge shall not sit at the hearing of the appeal by the Committee, and in such case, the Chief Justice may nominate another judge of the High Court as provided under subsection (3) of section 4 of this Act; and save further that in an appeal to the Court of Appeal against a decision or order of the Chief Justice the latter shall not sit to hear the appeal.
 
FORMULA YA KISUTU

Kama kesi yako inawakilishwa na wakili inakuwa hivi:
Wakili anaonana na hakimu kabla ya kesi kuanza na wanakubaliana masuala kadhaa ikiwemo rushwa. Then, wanapoingia kwenye court room inakuwa ni kazi ya hakimu kutekeleza makubaliano.

Kama unajiwakilisha mwenyewe inakuwa hivi:
Unamwona karani wa hakimu husika mwenye kesi yako unatoa mapendekezo yako, then anayapeleka kwa hakimu, majibu yakirudi yataeleza ni kiasi gani cha rushwa kitatakiwa. Baada ya hapo mkienda kwenye court room hakimu kazi yake ni kutekeleza.

ATHARI:
Kama Wakili akionekana mgumu kuonana na hakimu mapema basi mengi yatamkuta, inabidi awe jasiri kweli kweli.

Kama unajiwakilisha mwenyewe na hujafuata formula ya hapo juu, usione ajabu kesi yako ikawa inapangiwa tarehe kila inapoitwa mahakamani. Au ukashukiwa na balaa usiyoitegemea (kesi yako kuwa fundisho kwa wengine wote)

ONYO: Maelezo yangu yanatokana na uzoefu nilioupata katika mahakama ya Kisutu na hayana uhusiano wowote na sakata la hakimu Lyamuya na Wakili Fatma.
 
Asubuhi ya leo huyo bibie alikuwa Clouds fm akielezea yaliyojitokeza.
Kwanza kabisa anasema mambo yaliyoripotiwa sivyo yalivyokuwa, kwani waandishi waliitwa na wakapewa hadithi hiyo na wakili wa utetezi; kwa hisia zake ni kuwa wakili huyo na hakimu wana lao jambo.

Hume
Mbona hapa kuna utata kidogo, kwanini huyo wakili wa utetezi aliamua kuwaita waandika habari na kuwapa maelezo yeye juu ya kilichotokea? au aliamua ku-dramatize?
 
Hume
Mbona hapa kuna utata kidogo, kwanini huyo wakili wa utetezi aliamua kuwaita waandika habari na kuwapa maelezo yeye juu ya kilichotokea? au aliamua ku-dramatize?

wenye akiri ni rahisi kupambanua yalio kweli na uongo hujitenga penye ukweli.
Kwa uchacxhe nimemsikia Bint. akieleza upande wake wa hadithi,inaonyesha kwa sababu ya kuficha hiyo rushwa(ufisadi) wao wakiri wa utatezi na Mahakimu wa Court ile tukufu ndio maana wakiri wa utetezi akaona awahi kwenye vyombo vya habari kumchafua Bint eti kwa sababu baba yake Rais.
Hii inaonyesha ss waTz ni watu wanamna gani!
Sasa Bint anayo recorded conversation ambayo wakiri wa kwanza kwenye kesi hiyo akiaomba ruswa LIVE.kwa kujua hilo hakimu huyo ana wainfluence wenziwe wamwoonyeshe kama kabint ni kakorofi wakati in real sense wao wanaficha rushwa yao.
wapi tunaenda huko wandugu PCCB na hata Hat mahakama imeshindwa kumtia hatian hakimu huo toka mwezi wa nane!
 
Ninafikiri Fatma alichemsha, nionavyo mimi ni kwamba kuna kila dalili kuwa mtoto wa mkubwa ndio kumefanya awe jeuri namna hiyo. Pamoja na kwamba alikuwa na haki katika kuuliza hayo aliyouliza,lakini kitendo cha kutoka na kumfata hakimu alipo na kumfokea na maneno ya aibu, kinatia hasira sana, ukizingatia kuwa Fatma mwenyewe ni wakili hivyo tunaamini sheria anazijua labda kama uwakili aliupata kwa kuonga. Nafikiri angefutiwa kazi ya uwakili kwa muda kama adhabu aliyopoewa Masumbuko Lamwai. Lakini kama wenzangu walivyosema, Fatma kwa kuwa ni mtoto wa mkubwa yataisha haya kimya kimya kimya......kama kesi ya ditopile.

Nshomile hapa naungana nawe kuhusu kuchemsha kwa huyu Wakili Karume,Ukiangalia na kufuatilia sokomoko lote,utaona kuwa Wakili Karume aliingia Mahakamani akijua kuwa haki haitotendeka,na neno lake la kwanza hapo Mahakamani lilikuwa kuomba kuahirishwa kesi,na kwa matakwa yake alitaka kesi isikilizwe kesho yake(20.11.07),kwa kufuata Utaratibu wa kawaida wa Mahakama Hakimu Lyamuya akamuuliza karani kama kesho kuna nafasi,Karani akamjibu Hakimu mbele ya macho ya Wakili(Karume) kuwa hakuna nafasi wazi mpaka tarehe 13.01.08.Hakimu alipomfahamisha Wakili Karume ,yeye alikataa kwa madai kwamba tarehe hiyo ni mbali mno,nae akataka kesi isikilizwe 02/01/08.Hakimu alimwambia Wakili tarehe hiyo haiwezekani kwani ni siku ya Mapumziko ya Mwaka mpya.

Baada ya kauli hiyo ya Hakimu ndipo Wakili Karume alipotoka kwenye platform yake na kumwambia Hakimu kwa kumnyooshea kidole nanukuu "Kwanza wewe hujui kazi,na ni mara yako ya kwanza kuniona mimi".sasa kwa mtazamo wangu sielewi kumjua Wakili kuna uhusiano gani na kesi,tukitaka haki itendeke ni wazi kabisa wakili Karume approach yake haikuwa nzuri.

Hakimu wa kwanza wa case hiyo (#60/2006) alijitoa kwenye case baada ya kupatwa kwenye Mtego wa Hongo tarehe 26.08.07 huko seacliff,shauri lake lipo Takukuru na Jaji Kiongozi(Amir Manento) ana ufahamu wa shauri hilo.Hakimu huyo Adolph Mahayi bado yupo kazini.

Hakimu wa pili wa case hiyo Bibi Euphemia Mingi aliomba asiendelee na shauri hilo baada ya kupokea maneno mazito kutoka kwa wakili Karume,maneno hayo yalisababishwa na Mh.Hakimu kuchelewa kuingia kwenye chumba cha mahakama.

Sasa kwa namna yoyote ile,pamoja na Wakili kwenda kwenye vyombo vya Habari bado ana tatizo la kudharau Mahakama,kwa vyovyote itakavyokuwa TLS itasubiri uchunguzi na kuchukua hatua za kinidhamu.
 
Yaani watu kwa kijifanya wanajua kila kitu tu hawajambo...
Kwa nini msisubiri sheria ichukue mkondo wake../manake wengine mshaanza kutoa hukumu tayari...
 
Naungana Na Pundamilia Kumuuliza Hume Kuwa Kwa Nini Anakubali Maelezo Ya Fatma Karume Kuwa Waandishi Wa Habari Kuwa Hawakuwepo Wakati Yanatokea? Kwa Uhakika Kabisa Naomba Nikuhakikishie Kuwa Mwandishi Wa The Guardian Alikuwepo Wakati Huo. Nimeongea Naye Na Anakiri. Pia Kama Umesikiliza Maelezo Ya Clouds Na Hata Ya Tanzania Daima Wakili Fatma Anakiri Kufanya Aliyotuhumiwa Ila Anasema Kuwa Alilazimika Kufanya Hayo Kwa Sabau Ya Rushwa.

Tunachokisema Sisi Ni Kuwa Chamber Ya Hakimu Sio Forum Nzuri Ya Kutoa Tuhuma Za Rushwa. Kwa Kuwa Alishazipeleka Pccb Asubiri Wachukue Hatua. Sasa Swala Linakuja. Kwa Nini Pccb Hawajachukua Hatua Kwa Hakimu Aliyerekodiwa? Ina Maana Hawamwogopi Mtoto Wa Rais Aliyekuja Na Ushahidi Madhubuti Usiopingika Katika Kaseti?

Mimi Nasema Kuna Mengi Sana Hapa Yamejificha!!

Na Kama Ni Kweli Fatma Karume Ameweka Kanda Ya Mazungumzo Ya Hakimu Akiomba Rushwa Kwenye Redio Ya Clouds Basi Atakuwa Ametenda Kosa!! Kwa Sheria Mpya Ya Rushwa Ya Mwaka 2007 Kifungu Cha 27 Nadhani Ni Kosa La Jina Kwa Mtu Kutoa Taarifa Ya Mambo Yanayochunguzwa Na Pccb. Anayetakiwa Kutoa Hayo Maelezo Ni Mkurugenzi Wa Pccb!!
 
Kwa maoni yangu ni kwamba.Ni vizuri tukamhukumu mtu kutokana na mazingira.Lakini kwanza tuelewe kuwa rushwa katika mahakama zetu mna hasa kisutu imekithiri.baya zaidi mfumo wa mahakama zetu inalinda sana mahakimu.aidha mahakimu nao wanalindana sana.Kutokana na hali hii inawafanya hata mawakili wetu wawe ni watu wa kujipendekeza kwa mahakimu na baadhi yao ndio wanaowachukulia mahakimu rushwa kutoka kwa wateja na kuwapelekea.Kweli ingelikuwa karume si mtoto wa mkubwa angetiwa ndani.lakini ni vyema kwa kutumia hadhi yake ametumbua jipu.Kapigania haki ya kutokupuuzwa katiaka kesi zake.Tuache kumlaumu kwa kuonea gere.inaelekea watanzania tumejenga chuki kwa viongozi na familia zao ambapo viongozi hao hao tunawachagua wenyewe.tuache fikira za kimachinga za kuchukia waliofanikiwa kimaisha ili hali sisi wenyewe tulikimbia umande tukabweteka.Tukio la Fatma kwa mtazamo wangu unaamsha hoja kuchunguza wizara idara nzima ya mahakama nchini watu wananyimwa haki.Nadhani ukiwa na kesi dhiidi ya mtu mwenye pesa ndipo utajua ubuvu wa mahaka zetu
 
Hume
Mbona hapa kuna utata kidogo, kwanini huyo wakili wa utetezi aliamua kuwaita waandika habari na kuwapa maelezo yeye juu ya kilichotokea? au aliamua ku-dramatize?

Hali hii ndo inazidisha utata juu ya mambo yaliyojitokeza.

Lengo lake ilikuwa kumfanya huyu binti aonekane ana hatia, kabla hajasikilizwa.

Maelezo yake yanaonyesha kuwa kuna ukaribu uliopitiliza kati ya wakili na hakimu Lyamuya.

Kwanza wakili wa utetezi alichelewa kufika mahakamani, hakimu akasema hawezi kuamua lini kesi isikilizwe hadi huyo wakili afike, kinyume na taratibu za kawaida.

Kuna mengi yanafukuta hapa.

Nani anasema kweli, nani anasema uongo tusubiri kwani wote wamelalamika panapohusika, yaani hakimu na Binti karume wote wamefaili complaints!
 
Nshomile hapa naungana nawe kuhusu kuchemsha kwa huyu Wakili Karume,Ukiangalia na kufuatilia sokomoko lote,utaona kuwa Wakili Karume aliingia Mahakamani akijua kuwa haki haitotendeka,na neno lake la kwanza hapo Mahakamani lilikuwa kuomba kuahirishwa kesi,na kwa matakwa yake alitaka kesi isikilizwe kesho yake(20.11.07),kwa kufuata Utaratibu wa kawaida wa Mahakama Hakimu Lyamuya akamuuliza karani kama kesho kuna nafasi,Karani akamjibu Hakimu mbele ya macho ya Wakili(Karume) kuwa hakuna nafasi wazi mpaka tarehe 13.01.08.Hakimu alipomfahamisha Wakili Karume ,yeye alikataa kwa madai kwamba tarehe hiyo ni mbali mno,nae akataka kesi isikilizwe 02/01/08.Hakimu alimwambia Wakili tarehe hiyo haiwezekani kwani ni siku ya Mapumziko ya Mwaka mpya.

Baada ya kauli hiyo ya Hakimu ndipo Wakili Karume alipotoka kwenye platform yake na kumwambia Hakimu kwa kumnyooshea kidole nanukuu "Kwanza wewe hujui kazi,na ni mara yako ya kwanza kuniona mimi".sasa kwa mtazamo wangu sielewi kumjua Wakili kuna uhusiano gani na kesi,tukitaka haki itendeke ni wazi kabisa wakili Karume approach yake haikuwa nzuri.

Hakimu wa kwanza wa case hiyo (#60/2006) alijitoa kwenye case baada ya kupatwa kwenye Mtego wa Hongo tarehe 26.08.07 huko seacliff,shauri lake lipo Takukuru na Jaji Kiongozi(Amir Manento) ana ufahamu wa shauri hilo.Hakimu huyo Adolph Mahayi bado yupo kazini.

Hakimu wa pili wa case hiyo Bibi Euphemia Mingi aliomba asiendelee na shauri hilo baada ya kupokea maneno mazito kutoka kwa wakili Karume,maneno hayo yalisababishwa na Mh.Hakimu kuchelewa kuingia kwenye chumba cha mahakama.

Sasa kwa namna yoyote ile,pamoja na Wakili kwenda kwenye vyombo vya Habari bado ana tatizo la kudharau Mahakama,kwa vyovyote itakavyokuwa TLS itasubiri uchunguzi na kuchukua hatua za kinidhamu.


Mwawado,
Nimesoma comments zako, je unaweza kutupatia uzoefu wako katika shauri lolote pale mahakama ya kisutu?
 
hivi kati ya hakimu na uyo wakili Fatma nani ambaye ameongea na waandishi wa habari kujua ukweli?
 
Yaani watu kwa kijifanya wanajua kila kitu tu hawajambo...
Kwa nini msisubiri sheria ichukue mkondo wake../manake wengine mshaanza kutoa hukumu tayari...

I SALUTE YOU,MKUBWA NYANI,
Kwanini watu hapa mna hivi vijitabia vya kutetea uozo na ku-side na wale wenye dhamana wengine aman eenda mbali mpaka kuhukumu this is too much.......
 
MI NAPENDA KUWEKA WAZI.

Kitendo cha bi Fatma kupeleka kanda iliyopelekwa PCCB kwa uchunguzi kwenye radio ni KOSA la jinai. Achana na vurugu zake za hapo mahakamani.

Je PCCB watamchukulia hatua Mtoto wa Rais wa Mkoa wa Zanzibar?!!!!!!!!!!!

Au ile sheria ni kosa la jinai kwa akina kabwela sie???!
 
Hume
Inaonyesha Huna Ufahamu Wa Kina Kuhusu Sheria Na Taratibu Za Kimahakama!!! Huwezi Kupanga Tarehe Ya Kusikiliza Shauri Bila Ya Wakili Wa Utetezi Kuwepo Ili Tarehe Ipangwe Kwa Pamoja. Tatizo La Kupanga Tarehe Bila Mawakili Wote Kuwepo Ni Kwamba Unaweza Kukuta Tarehe Iliyopangwa Wakili Wa Utetezi Ana Kesi Mahakama Kuu Au Mahakama Ya Rufaa.

Kwa Kukufahamisha Tu Ni Kuwa Kama Wakili Ana Case Mahakama Ya Rufaa Au Mahakama Kuu Na Nyingine Mahakama Ya Hakimu Mkazi Basi Kesi Ya Mahakama Ya Hakimu Mkazi Itaaahirishwa. Kwenye Sheria Hii Tunaiita Precedence Of Appearance.
 
Naam Ndg.Pundamilia,naweza kuwa sina uzoefu wa mambo yanavyokwenda pale Kisutu.Lakini kwenye Ukweli na usemwe,na tusikwepe kusema ukweli ati kwa sababu kisutu pananuka Hongo!!!.Kuna kila sababu ya kuona kuwa Wakili Karume alimkosea Heshima Hakimu na Mahakama kwa kitendo chake cha kutoa maneno yasiyostahili Mahakamani.Kuna Malalamiko mengi ya Rushwa ktk vyombo vyetu vya Sheria,si kisutu tu!,ni kwenye Mahakama nyingi tu!,Lakini ni vyema kuripoti vitendo hivyo kwa vyombo Husika,na kuendelea na utaratibu wa kawaida wa kuheshimu process za Mahakama,Nafikiri utakuwa umenielewa Mh.Pundamilia.Si nia yangu kutetea Mahakimu wetu!!!La Hasha,ninachogombania hapa ni kuheshimu Utawala wa Sheria...
 
MI NAPENDA KUWEKA WAZI.

Kitendo cha bi Fatma kupeleka kanda iliyopelekwa PCCB kwa uchunguzi kwenye radio ni KOSA la jinai. Achana na vurugu zake za hapo mahakamani.

Je PCCB watamchukulia hatua Mtoto wa Rais wa Mkoa wa Zanzibar?!!!!!!!!!!!

Au ile sheria ni kosa la jinai kwa akina kabwela sie???!

Ohoooo, mkuu haya mengine tena. Uzanzibari na uzanzibara,
Zanzibar umekuwa mkoa tena!!!!!!
Nawe umetenda kosa la jinai, jitokeze ushtakiwe.

Kweli kakiuka kupeleka ushahidi wa pccb redioni, ni sawa na kuchukua sheria mkononi au siyo, atasema ameshtaki kwenye mahakama ya UMMA! kama walivyofanya wapinzani.

Shitaka litaanzia kwa mmiliki wa redio, watangazaji waliokuwepo na hatimaye Fatma mwenyewe si sawa na yale ya mwanahalisi?

Yangu macho!
 
Hume
Inaonyesha Huna Ufahamu Wa Kina Kuhusu Sheria Na Taratibu Za Kimahakama!!! Huwezi Kupanga Tarehe Ya Kusikiliza Shauri Bila Ya Wakili Wa Utetezi Kuwepo Ili Tarehe Ipangwe Kwa Pamoja. Tatizo La Kupanga Tarehe Bila Mawakili Wote Kuwepo Ni Kwamba Unaweza Kukuta Tarehe Iliyopangwa Wakili Wa Utetezi Ana Kesi Mahakama Kuu Au Mahakama Ya Rufaa.

Kwa Kukufahamisha Tu Ni Kuwa Kama Wakili Ana Case Mahakama Ya Rufaa Au Mahakama Kuu Na Nyingine Mahakama Ya Hakimu Mkazi Basi Kesi Ya Mahakama Ya Hakimu Mkazi Itaaahirishwa. Kwenye Sheria Hii Tunaiita Precedence Of Appearance.

Inawezekana sina ufahamu wa kina,
ingekuwaje kama wakili asingefika kabisa?
Hivi ni kazi ya wakili wa mlalamikaji na hakimu kumbembeleza wakili wa utetezi afike ili wapange tarehe?

Hebu we mtaalam wa sheria nieleze katika mazingira hayo sheria inasemaje?
 
Jamani this is only one sided story, lets wait for the other side of the story!

Leo asubuhi Binti Karume ametembelea Claoud FM katika "Power Break Fast" kinachoendeshwa na Masoud Kipanya na Finna Mango. Kitu cha kwanza ambacho nimegundua ni kuwa huyu Binti ni jasiri sana (labda kwa kuwa ni mtoo wa Kigogo). Lakini kitu cha pili ni kuwa huenda hii story ikawa imekuzwa na Wahandisi wa habari.

Kwa mujibu wa madai yake ni kuwa hakufanya kama jinsi ilivyolipotiwa na magazeti na tena Mahakamani hakukuwa na Waandishi wa Habari. Kwa mijibu wa madai yake ni kuwa Wahandisi hao wa habari waliitwa na Hakimu Addy Mamuya baadaye kabisa na Hakimu huyo akaanza kuwaeleza hayo yaliyotolewa kwenye Magazeti. Binti KArume anasema kuwa habari hizo amepewa na mmoja wa Waandishi wa Habari yaani Hakimu Mamuya aliwaita Wanahabari na kuwaeleza hayo ili kumkomoa.

KAtika kipindi hicho cha Clouds FM pia Wakili Karume alieleza kuhusu kujitoa kwa hakimu wa awali anayejulikana kwa jina kla Euphemia Mingi amabcho pia ni kichekesho!

Swali la kujiuliza hapa ni hili: ikiwa ni kweli Wakili KArume alimvamia Hakimu Lyamuya; Je, kwa nini hakuripoti suala hilo kwa Polisi wa Pale Mahakamani au kwenda Kituo chsa Polisi kulalamika, au hata kutoa amri ya kumkamata Wakili huyo na kutoa adhabu papo hapo kwa kosa la kuidharau Mahakama au kuhatarisha Amani?

Mambo mengine hata kama ni mabaya, yanaotkea ili kutufunulia yaliyojificha na kutusaidia kujifunza na kujirekebisha. Naamini ninaelekea pazuri zaidi.
 
actually kwa wale msiomfahamu fatma karume ni
1. wakili ambaye ni mshari sana na siku zote anapenda kuwanyanyasa mahakimu na majaji. mara nyingi ameonywa lakini kwa kuwa ni mtoto wa mkubwa haguswi. kama mnavyoelewa kitendo cha kugusa familia ya karume ni kutishia muungano wa nchi yetu(kama huamini uliza watu)

2.kwa sasa yuko kwenye ile law firm ya IMMA advocates yenye uhusiano mkubwa na maskendo ya deep green finance na tangold kama partner na sasa inaitwa IMMA and Karume Advocates!! mi nahisi ameenda pale kulinda maslahi ya chama tawala!! sasa labda anahisi mama lyamuya kwa kuwa ni mchaga basi atakuwa chadema!!

Duh! Mheshimiwa hii information umetoa wapi? Huyu dada alikuwa anafanya kazi kwa Mkono,na alipotoka hapo akaanzisha kampuni yake binafsi.Kile kiwanja kilipojengwa Sea Cliff Village ni cha bibi yake,na yeye ofisi yake iko hapo.

Mimi kwenye hili nina mtazamo kidogo tofauti.Kwa wale ambao wanaishi huku,rushwa mahakamani ni kitu cha kawaida sana.Hata wale wakina Nguza ni kwa sababu tu walikuwa hawana pesa,lakini kila mtu anajua kama wale wangekuwa ni watoto wa wakubwa au wana uhusiano na mkubwa yeyote,au wangekuwa wana pesa wasingefungwa!Kila mtu atakubali pia kuwa kama Ditto angekuwa ni mwananchi wa kawaida angekuwa yuko ndani mpaka leo!Mifano kama hii iko mingi sana.Kwa hio,ni kweli kama Bi Karume angekuwa ni mwananchi wa kawaida angeswekwa ndani,je ni kweli tusingesema kuwa 'kaonewa' kwa sababu kamueleza hakimu ukweli? Kuna mtu hapa katoa mfano kuwa huyo Hakimu Lyamuya alishamfunga mtu kwa kuwa simu yake iliita wakati yuko ndani ya mahakama.Hio ndio jeuri aliyokuwa nayo,sasa anaogopa nini kumfunga huyu kama ni ndani ya uwezo wake? Kama kweli anaogopa kwa sababu ni mtoto wa mkubwa,basi hafai kuwa hakimu in the first place,maana kama mimi nikimshtaki huyo Binti Karume kwa kosa kama hilo,sitategemea haki kutoka kwake.Mimi namsifu huyo dada kwa kuweka wazi haya mambo.Hawa mahakimu hudai rushwa sana,tena rushwa zenyewe ni mbuzi kwelikweli.Naweza nisikubaliane na mtindo aliotumia,lakini i feel its high time mtu akasimama kuusemea uozo wa hawa mahakimu.Sasa kama mtu mwenyewe ni mtoto wa mkubwa,so what!Hakuwa anajitetea yeye mahakamani,alikuwa anamtetea raia wa kawaida,ambaye angeweza kupoteza haki yake kwa sababu ya rushwa.Huyu dada katumia nafasi yake kama mtoto wa mkubwa kutetea maslahi ya mwananchi wa kawaida(i assume he is)

Ni mtazamo wangu
 
Hii stori inatuambia mengi. Kwanza bado nina msimamo kuwa yule Hakimu ni kilaza, kwa sababu kwa nini asingemchukulia hatua huyo wakili? mbona kuna mkuu wa wilaya alimjia juu Lowassa pale iLowassa alivyojaribu kumdhalilisha mbele za watu?

Kutokana na maelezo ya rushwa hapo mahakamini nina hisia kuwa huyo Hakimu kilichomzuia kumfundisha adabu Wakili ilikuwa si kuogopa jina la Karume, bali huyo Hakimu ana jambo lingine analoogopa in this case ni hayo mambo ya rushwa. Hapa ni shari kuzaa heri, maofisa wa kuzuia rushwa wanatakiwa wateremke pale wawapige watu jamba jamba hata kama hawatamkamata mtu basi waonyeshe presence yao pale na wachimbe biti kishenzi kwamba tumeweka mitego na tunawatumiwa washtaki na washtakiwa kwa hiyo muhusika wa kesi akiombwa rushwa tu tutajua na Hakimu anayeshughulikia kesi hiyo tutamuabisha, yaani hapo ni scare tactics za kuzuia watu kuomba rushwa kabla hata hawajaomba, unajua unaweza kuzuia rushwa kisaikolojia tu! Mambondia kama kina Mohamed Ally walikuwa kwanza kabla ya ngumi wanampiga mtu kisaikolojia mtu anatishwa wewe ntakufanyizia leo ntakuteremshia ngumi kama nyuki, jamaa anakuwa anapigwa pambano la kifikra kabla la ngumi halijaanza.

Hii inawezekana mahakamani, mahakimu wataogopa kupokea rushwa na serikali iwaongezee mishahara na mambo yataenda na haki itatendeka.
 
Back
Top Bottom