Binti (Mwanafunzi wa Chuo) auliwa na maiti kufichwa

Dejane

JF-Expert Member
Jan 1, 2014
49,697
68,711
Inasikitisha jamanii na inauma kwa mauaji yanayotekea hapa Nchini, kuna binti alikuwa anasoma chuo cha Bagamoyo ni mkazi wa Mwanza, anaitwa Wanze au Ashura mrefu wastani,mweusi mzuri ,alitekwa na watu wasiojulikana wamemuua wakampiga picha kwa simu yake marehemu pia wakaisambaza kwa whatsapp kutumia simu yake ,wakatuma kwa namba zilizokuwemo kwenye simu ya marehemu.

Sasa jamani leo siku ya 11 hajulikani alipo mnataka kuifanyia nini hiyo maiti iwekeni sehemu basi watu waione watoe taarifa police ndugu wachukue binti yao wamzimke. Mmemuua bado mnaficha jamanii mlaaniwe mliofanya hivyo.

Jamani kwa waliosoma na Ashura au Wanze chuo cha Bagamoyo najua mtakuwemo humu tupeni taarifa yoyote mliyosikia jamanii.

Tiririkeni wadau bado maiti haijapatikana ila picha zimesambaa, ,na sijui kurusha picha humu.

Ee Mungu Wafariji ndugu zake na wazazi wake, Binaadamu tunatisha jamanii

Kinachoendelea, ,,maiti imekutwa Dar imetupwa wasamaria wameichukua na kuipeleka muhimbili hospital
Kwa uchunguzi zaidi

==========================
==========================

Picha kwa hisani ya Samuel Sasali (Blogger)
1450693_10152521791208581_3508405261326772003_n.jpg

10277921_10152521791318581_2186337517444446425_n.jpg

bina ina maana wamempiga picha akiwa ameshakufa afu ndo wanazituma picha kwa ndugu zake? Yani wamekaa na maiti siku 11?? Mbona unyama sana jamani, sijui ndugu zake wana hali gani jamani
 
bina ina maana wamempiga picha akiwa ameshakufa afu ndo wanazituma picha kwa ndugu zake? Yani wamekaa na maiti siku 11?? Mbona unyama sana jamani, sijui ndugu zake wana hali gani jamani

Ndio binam wamempiga halaf hana nguo wamemfunika na shuka,nilikutana na huyu binti mwaka huu mwanzoni kwenye hitma ya bibi yake,niliongea nae sana mchangafu mwenyewee,,
Meck Sadik ni mjomba wake
 
Dah mejikuta mwili unasisimka dah so sad jamani, binadamu tumekua na roho ngumu, mungu tuhurumie kwa kweli jaman jamani dah
Cc mamaafacebook
 
Last edited by a moderator:
Ndio binam wamempiga halaf hana nguo wamemfunika na shuka,nilikutana na huyu binti mwaka huu mwanzoni kwenye hitma ya bibi yake,niliongea nae sana mchangafu mwenyewee,,
Meck Sadik ni mjomba wake

sasa siku 11 zote hizo wanamfanyaje maiti wa watu??au washamtupa huko misituni jamani
 
Kama nambaye ingali hewani nadhani watu wa usalama wanaweza wakafanya trace ya location ya hao watumaji picha...
 
Ninaamini malipo na hapa duniani na ukiua kwa upanga utakufa kwa upanga. Mungu aiweke roho ya marehemu panapositahili. Amina
 
Angekuwa ameuawa kamanda wa polisi, sasa hivi wauaji wangekuwa mbaroni, lakini raia polisi haishughuliki ila itaomba raia wenyewe wawatafute wauaji!
 
Ni ukatili wa hali ya juu.
Ila ukiuwa na wewe lazima kitakula kwako tu hata ipite miaka kumi.
 
Kama nambaye ingali hewani nadhani watu wa usalama wanaweza wakafanya trace ya location ya hao watumaji picha...

Walivyotuma picha, walipiga hiyo namba ya marehemu haikupatikanaa
 
Angekuwa ameuawa kamanda wa polisi, sasa hivi wauaji wangekuwa mbaroni, lakini raia polisi haishughuliki ila itaomba raia wenyewe wawatafute wauaji!

Nadhan kuna kinachoendelea ili maiti ipatikane,,mkuu wa mkoa Meck huyu binti ni mtoto wa dada yake
 
Back
Top Bottom