Kenya: Safari ya saluni ilivyokatisha uhai wa mwanafunzi Chuo Kikuu

Dalton elijah

JF-Expert Member
Jul 19, 2022
208
462
Familia moja katika Kijiji cha Kabuboni, Kaunti ya Tharaka-Nithi, inapambana kutafuta haki ya binti yao mwenye umri wa miaka 21, aliyeuawa kikatili.

Mwili wa Ann Kambura ulikutwa umetupwa kisimani huku mikono yake ikiwa imefungwa kwa nyuma wakati blauzi na sidiria yake vikiwa vimefungwa kwa nguvu shingoni kwake na hivyo kuashiria kuwa aliuawa kwa kunyongwa.

Ann ambaye alikuwa mwanafuzi mwaka wa kwanza katika Chuo Kikuu cha Kiriri, aliondoka nyumbani Ijumaa Mei 12, mwaka huu saa 8.30 mchana kuelekea saluni kusuka ili kujiandaa na kurudi chuoni jijini Nairobi siku iliyofuata, hata hivyo hakurejea tena

James Mwiti, baba wa Ann na mkewe Frida Gaceri wameuambia mtandao wa ‘Nation’ kuwa walimpigia simu binti yao muda wa saa 7 usiku kujua kama alikuwa amehudumiwa kwa sababu muda ulikuwa umeenda, hata hivyo; simu hiyo hakupokea.

Wazazi waliendelea kupiga simu lakini hakupokea na baada ya saa chache simu ilizima na walidhani kwamba binti yao aliamua kulala nyumbani kwa msusi wa nywele maana baada ya giza kuingia.
Kesho yake asubuhi, walimpigia tena simu ambayo ilikuwa bado imezimwa, kitu kilichosababisha wakahisi huenda kuna kitu kibaya kimetemtokea na hivyo kuamua kwenda huko saluni kupata taarifa kamili.

Hata hivyo, Msusi aliwaeleza kuwa Ann alifika kwenye saluni hiyo saa tatu usiku na kuondoka mwendo wa saa 06:30 baada ya kumaliza kusuka nywele zake.

Wazazi hao ambao walikuwa na wasiwasi juu ya binti yao, waliamua kumtafuta mwendesha bodaboda aliyempeleka saluni na akathibitisha kwamba Ann alikuwa amefika saluni, lakini hakuwa amempigia simu kumrudisha nyumbani.

Baada ya majibu hayo, wazazi waliamua kupigia simu marafiki wa Ann chuoni Nairobi, ili kujilidhisha ikiwa binti yao aliamua kurudi chuoni kitu ambacho walisema chumba chake kilikuwa kimefungwa.

"Ijumaa hiyo, nilitumia siku nzima kufuatilia mkopo nilioomba kwaajili ya kumlipia ada, japo ndiyo siku aliyouawa,” alisema Gaceri.

Wazazi hao waliripoti suala hilo kwa chifu wa eneo hilo na matangazo yakatolewa katika makanisa ya eneo hilo, huku msako ukianza.

Siku ya Jumatano, rafiki wa familia hiyo, Jeremy Thirika, aliwashauri pia kuripoti kisa hicho katika Kituo cha Polisi cha Chuka, lakini walipofika huko, walishauriwa kwenda kutoa taarifa katika kituo cha Polisi karibu na makazi yao.

Wakati wanaandikisha taarifa za tukio hilo kituoni hapo, taarifa za kipolisi kutoka kwa afisa wa polisi, zilikitaarifu kituo hicho juu ya kupatikana kwa mwili uliokuwa umetupwa katika kisima kimoja kijijini hapo.
Gaceri alisema kwamba kutokana na maelezo ya saizi na mavazi, alikuwa na uhakika kwamba taarifa hiyo ilimhusu binti yake.

Kwa pamoja na Polisi, walielekea eneo la tukio na, baada ya kuopoa maiti, familia ilithibitisha kwamba alikuwa Ann.

Mwili huo ulipelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali ya Rufaa ya Chuka huku Polisi wakianza uchunguzi kuhusu tukio hilo.

“Binti yangu ameuawa kikatili kwa sababu kisima kilifunikwa vizuri, mikono na kichwa chake vilikuwa vimefungwa kwa blauzi yake iliyochanika na ilikuwa imefungwa kwa nguvu shingoni,” baba wa marehemu alisema kwa hisia kali.

Mwiti ameambia ‘Nation’ kuwa ripoti ya uchunguzi wa maiti ilionyesha mtoto wake wa kwanza alibakwa kabla ya kuuawa. Alijiapiza kutomzika hadi hadi watu waliofanya uhalifu huo kukamatwa na kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za mauaji.

Hata hivyo, mpaka tunaenda mitamboni, polisi walikuwa hawajamkamata mshukiwa yeyote kuhusiana na kitendo hicho cha kinyama, huku wazazi wakiendelea kuomba haki kutendeka kwa binti yao ambaye walikuwa na matarajio makubwa.

Katika taarifa yake, Gavana wa Kaunti hiyo, Muthomi Njuki ameelezea wasiwasi wake kutokana na visa vya uvunjaji sheria katika kaunti yake.

"Nimesikitishwa sana kwamba msichana wa miaka 21, Ann Kambura Mwiti, ambaye alikuwa akijiandaa kurejea chuo, alibakwa na kuuawa kikatili katika eneo letu tena mtaani kwake," Njuki amesema katika taarifa hoyo, na kuongeza;

"Hii haikubaliki kabisa na inatishia amani na utulivu ambao tumekuwa tukifurahia. Haiwezi kuwa kwamba kama viongozi wa kaunti hii, tunaketi chini na kutazama hali hii ya sasa inayoendelea.”

Gavana huyo amesisitiza kuwa familia ya Ann inastahili haki na kutoa wito kwa vyombo vya uchunguzi kuharakisha kesi na hivyo kuhakikisha kuwa wote waliohusika wahusika wanafikishwa mahakamani.


SOURCES :Mwanannchi
 
Natoa pole kubwa kwa familia, wachukue DNA ya mbakaji kama itapatikana kisha waanze kuitest kwa watu wa eneo hilo wasioeleweka, watapata a match tu. DNA ya mbakaji lazimaitakuwepo kwenye finger nail scraping wakati anaparuana na mbalaji. Pia kwenye Sperm kama alibaka bila kinga atakuwa ameacha mbegu, watapata DNA tu.

Haya ndio madhara ya kuoiga vita Uchangudoa, PEPFAR ya Marekani ijitathmini, unapotaka kuondoa machangua 80,000 mtaani mnafanya kwa malengo yapi hasa? Hamasisheni matumizi ya kinga.
 
nimejaribu kusoma second paragraphs ambayo Ume Andika sijatoka na hoja yoyote ile mtaaalam
;ulikuwa unajaribu kutanabahisha usemi upi huo ili tupate dokezzo jadidi ......................
 
Poleni sana wafiwa
Ila kwenye mda ndio sijaelewa.maana unachanganya kiswahili na kizungu
Saa Tatu usiku na aliondoka 06:30
 
Back
Top Bottom