Binti huyu ametupanga wanaume kumi na moja

BATTO

JF-Expert Member
Feb 7, 2014
282
208
Ukimuona kwa macho utasema huyu ndio mwanamke kumbe ni bonge la kimeo.

Ilikuwa mida ya jioni natoka zangu kazini mara ikaingia massage baby uko wapi nimekumisi, nikamjibu ndo natoka kazini now yeye.

Basi naomba upitie nyumbani japo nikuone nimekumiss sana we mwanaume.

Nikaona isiwe shida ngoja nikamuone roho yake itulie nipo njiani wazo likanijia. Nikapitia duka moja maarufu Sinza na kumnunulia zawadi ya viatu kama suprize nimejikoki mwenyewe naenda kwa babybaby, mademu bwana.

Kufika akanipokea kwa bashasha na mabusu motomoto dady's home.

Yeye najua umechoka baby wangu kaa kwa kochi upumzike nataka nikutengenezee juice fresh unayo ipendaga..nikamwambia ngoja kwanza nikupe zawadi yako nikatoa vile viatu na kumpatia akafurahi sana na kuvijaribisha vilimtosha na kumpendeza , nikapewa busu lingine la sekunde kazaa.

Akatoka kwenda kuandaa juice huku simu yake na vile viatu akiwa ameviacha jirani na kochi nililokaa nikamuuliza simu yako inabando akanijibu ndio.

Nikaichukua nakuingia sehemu ya kubrowse internent akili ikanituma nifanye udukuzi kidogo nikafungua application yake ya watsupp mbona nilichoka.

Nilikuta msururu wa wanaume anaochati nao nakuwatumiana picha akiwa amevaa pichu tu nakukaa kimitego huku wakiambiana ni jinsi gani wamemisiana kupeana utamu kijasho kikanitoka, nikajikaza mwenyewe na kuendelea kuperuzi kwa wote idadi ikafikia wanaume kumi na moja na kwa mtiririko wa chating yao wote waonekana wameshapewa utamu.

Napenda kusema kitu kimoja hapa tangu nimeanza mahusioano nae tumefikisha mwaka sasa sikuwahi hata siku moja kuishika simu yake.

Nilishikwa na hasira sana yani huduma zote ninazo mpatia kumbe nahudumia kahaba nikamwita na kumuuliza aniambie hao watu ni akina nani.

Utetezi alionipa anasema ni marafiki zake nisimfikirie vibaya.

Nilitamani nimkate kofi moja la nguvu yani ushahidi wote ninao hapa unanijibu rejareja hivyo nikamuuliza huo urafiki pamoja nakugongana we kweli kiboko sasa unataka nikupe cheo gani huu ni umalaya au kipaji.

Akaanza kulia huku akiomba nimsamehe.

Kwakweli nilichanganyikiwa nakujiuliza hivi huyu binti anawezaje kutupanga wengi hivi nilichofanya nikuchukua viatu nilivyokuja navyo nikamwambia nimejitoa kwenye hiyo cheni na kama viatu atakuleta mwingine hivi naondoka navyo.

Nipo njiani kurudi home massage za kuomba asemehewe na kuto rudia tena zinamiminika kwenye simu yangu huku akijuta na kudai mimi ndo ananipenda kiukweli nikimwacha hatopata furaha ya maisha nakuomba nimpe last chance abadilike nikamjibu nakumwambia huwa natoa msamaha kwa makosa mengine lakini sio kwa hilo la kuchapiwa naomba tuachane kwa amani tu mama.

Akanipigia simu sikupokea akarudia tena na tena nikapokea.

Nikamuuliza unasemaje akanimbia ananipenda sana na hawezi kuishi bila mimi uku akilia..nilichomjibu ni kwamba siwezi kuendelea nae.

Kitu kingine kinacho nichanganya hapa nikwamba ametishia kujiua na yupo chini ya uangalizi wa dada yake jamani hata kama ni msamaha nikifiria idadi yake ya wanaume nachefuka kabisa..napigiwa simu kila mara kuombwa nirudishe moyo na ndugu zake ninachowajibu ni kwamba siwezi ajaribu kumchagua mwingine atakayempenda sana mpaka nafikia hatua ya kuwaandikia hii habari huyu binti amelazwa hospital presha imeshuka.

Hapa nafanyaje wakuu kiukweli huyu mwanamke amenitoka kabisaa..hofu yangu ni hiyo ya kulazwa kisa mimi inamaana nikigoma hata kwenda hospital si ndio majanga yataongezeka msaada wenu wakuu kichwa changu kimevurugwa kabisa.
 
nenda kamuone hospitali,mwambie umemsamehe,mengine mtaongea akiruhusiwa kutoka hospitali,endelea kuwasiliana nae as a friend taratibu atakuelewa,inawezekana kweli wewe ndie aliyekuwa anakupenda huko kwengine ni tamaa ya pesa ndio iliyompeleka.
viatu naviomba mimi..............just kidding
 
Zungumza na moyo wako vizuri kisha utoe jibu!na pia jiangalia na wewe una michepuko au huna,jibu utalipata tu!

Najipenda sana Mkuu sina mchepuko nilikuwa namwandaa aje kuwa mke kumbe majanga tu..
 
nenda kamuone hospitali,mwambie umemsamehe,mengine mtaongea akiruhusiwa kutoka hospitali,endelea kuwasiliana nae as a friend taratibu atakuelewa,inawezekana kweli wewe ndie aliyekuwa anakupenda huko kwengine ni tamaa ya pesa ndio iliyompeleka.
viatu naviomba mimi..............just kidding

Asante Mkuu kwa ushauri Dah! sijui hata naanzaje ila nitaufanyia kazi...na niheli viatu nikupe wewe.,
 
  • Thanks
Reactions: lin
Watsap bwana.

Pole ndugu, mie mwenyewe imenikuta, hivi karibuni, ila sisi hatukuwa wengi, tulikuwa 7 tu.

Na nikimuuliza alikuwa anatoa majibu kama ya huyo wa kwako, niliamua, kumpa mimba, na hivi sasa anamimba yangu, amekuwa mpoleeeeeeee na anahangaika kuitoa anashindwa.

Ananing'ang'ania mda huu, n mm najiweka pembeni.
 
I once had the same type of the girl! Watch out

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
aisee hapana kaka, 11 uwo ni ukahaba
mwache , maradhi atapoa, hosptaili ataruhusiwa akiipata nafuu
11 kw kweli haingii akilini kua ni makosa, bora awe anagongwa ni miwaume 50 badae anawapotezea, ila yeye bado anakuaga nao
uyo ni kahaba mubiiin
 
Watsap bwana.

Pole ndugu, mie mwenyewe imenikuta, hivi karibuni, ila sisi hatukuwa wengi, tulikuwa 7 tu.

Na nikimuuliza alikuwa anatoa majibu kama ya huyo wa kwako, niliamua, kumpa mimba, na hivi sasa anamimba yangu, amekuwa mpoleeeeeeee na anahangaika kuitoa anashindwa.

Ananing'ang'ania mda huu, n mm najiweka pembeni.

Asante sana Mkuu ila kwangu wamezidi aisee pole na wewe.,
 
Kuna vitu vinavyosameheka jamani sio kwa mazingira haya; 11!!! Hata mbwa hafanyi ushenzi wa namna hii. Kwa ubinadamu fanya uwezalo atoke kwenye hiyo hali then kaa na hao ndugu zake wape msimamo wako na yeye wamuelekeze afanye ustaarabu wake. Kama wanakutakia mema watamuelekeza ndugu yao. Hayo ni majanga kijana coz ukiikwepa ngwengwe ipo siku unaweza ua mtu uishie segerea.
 
Pole sana, I can imagine how you are suffering......ilintokea mimi demu kaning'ang'ania kama kupe, nlimfumania na sms za wadau wengine, nkamwambia tuachane, si akanywa mavidonge eti anajiua....

Bro yaani niliona uhusiano wangu na Kamuhanda unakaribia........niliogopa kishenzi, ila alipona, na nilikaza mwanzo mwisho sitaki uhusiano nae.....
 
Back
Top Bottom