Biashara ya salon za kiume na kike

sc-10blk_new_2_.jpg $120 sc-27blk-53_900px_1_.jpg $220 su-70blkp_angle_900px.jpg $380 - 400

Unapokusudia kufungua biashara yako jambo la msingi angalia vifaa ambavyo havitakuletea maumivu ya kichwa soon, bora fanya kitu ambacho kikusahaulisha ununuzi wa dhana mara kwa mara hasi biashara yako inatulia.

Kwa barbashop jambo la msingi ni ununuzi wa zana hizo hapo juu, vitu vingine vinapatikana kwa bei rahisi na upatikanaji wake nirahisi.

Binafsi huwa nawafikishia watu bidhaa kama hizi wanaozihitaji, ninachofanya si kuwauzia, ila kwa ufafanuzi wote bei na manunusi, tax na usafirishaji kisha kuna ongezeko la komisheni yangu ya 5-10 % inategemea na gharama za bidhaa. Hakuna cha bei ya masikilizano hizo nibe toka kwa wauzaji.
 
View attachment 134831 $120 View attachment 134832 $220 View attachment 134833 $380 - 400

Unapokusudia kufungua biashara yako jambo la msingi angalia vifaa ambavyo havitakuletea maumivu ya kichwa soon, bora fanya kitu ambacho kikusahaulisha ununuzi wa dhana mara kwa mara hasi biashara yako inatulia.

Kwa barbashop jambo la msingi ni ununuzi wa zana hizo hapo juu, vitu vingine vinapatikana kwa bei rahisi na upatikanaji wake nirahisi.

Binafsi huwa nawafikishia watu bidhaa kama hizi wanaozihitaji, ninachofanya si kuwauzia, ila kwa ufafanuzi wote bei na manunusi, tax na usafirishaji kisha kuna ongezeko la komisheni yangu ya 5-10 % inategemea na gharama za bidhaa. Hakuna cha bei ya masikilizano hizo nibe toka kwa wauzaji.

well mkuu,nimeelimika
 
Haya mambo yakaugiza mpaka mwezi ndio mzigo uje na meli .

Nenda Pale Radium Salon Equipments company limited
Kuna kila kitu
Niliwahi kununua pale kama miaka mitatu iliyopia Full Set ya salon equipments.Yaani ukitoka pale hununui kitu sehem nyingine wana hadi mataulo.
Ukifika pale utapata wazim kwa jinsi walivyosheheni vifaa.

Wapo Town,mitaa ya kueleka Swahili Street
Ukipotea wapigie 0713 608681 watakuelekezo walipo

Nio bora uende pale then ndio utapata tathmini ya Gharama ya Salon kamili.Maana hata mie ndio nilivyofanya
Sio kwamba nawafagilia ila ni Dar nzima hawa ndio jamaa walio sheheni vifaa vyote vya Salon.
 
Ningependa kujua ni biashara ipi inalipa zaidi kati ya biashara ya saloon ya kawaida ya kike au ya kiume katika maeneo ya miji midogo(Mikoani na wilayani) kwa kuzingatia Mtaji wa chini wa kuanzisha, Gharama za Uendeshaji, Wingi wa wateja, Changamoto, Pato na Faida.

Pia ningependa kufahamu ni wapi vifaa muhimu vyenye ubora vya saloon za kike na kiume kama Machine za kukaushia nywele(Dryer), Hair Steamer, Sterizer nk. zinapatikana na gharama zake zikoje.

Naamini topic hii itakuwa msaada kwa watu wengi sana.
 
Tatizo hasemi yupo wapi.
Kila sehem na kila mkoa au wilaya inachangamoto zake .
Ni sawa na kuuza Chai Maharage Bar,badala ya supu.
Lakini hao hao wateja wa supu ndio wateja wa chai maharage kwa maeneo mengine.
Hapo akili kumkichwa mkono kumpumbu

Na pia Salon za kike nakiume zinatfautiana pia maeneo,so jamaa afunguke ili watu wamsaidie,ukiwe kwa style ya kuficha ficha ndio tabu inakuja ya kukaa kama ubao wa viziwi
 
Saloon ya kiume ni rahisi kuisimamia kuliko ya kike. Saloon ya kiume mnawekeana malipo kwa mwezi au week. So gharama nyingine zi za operators mf, spirit, luku, maji, kuajiri wale wanasafisha watu after kunyoa. Saloon ya kike ina changamoto nyingi sana mf, mtu anaweza kuja na dawa yake so akalipa costs za kuwekwa tu, utawezaje kucontrol mtu kusuka? Ni ngumu aisee.
Upande wangu nakushauri fungua ya kiume

Sent from my Nokia Lumia using Tapatalk
 
Ningependa kujua ni biashara ipi inalipa zaidi kati ya biashara ya saloon ya kawaida ya kike au ya kiume katika maeneo ya miji midogo(Mikoani na wilayani) kwa kuzingatia Mtaji wa chini wa kuanzisha, Gharama za Uendeshaji, Wingi wa wateja, Changamoto, Pato na Faida.

Pia ningependa kufahamu ni wapi vifaa muhimu vyenye ubora vya saloon za kike na kiume kama Machine za kukaushia nywele(Dryer), Hair Steamer, Sterizer nk. zinapatikana na gharama zake zikoje.

Naamini topic hii itakuwa msaada kwa watu wengi sana.

Bila ya shaka wala hofu…salon ya kike ndiyo inayolipa zaidi kuliko ya kiume iwapo utafanya yafuatayo -

Kwanza hakikisha unapata location mzuri kwa biashara yako kulingana na mtaji wako.
Pili hakikisha unapata profesional staffs wenye kuiheshimu kazi na wawe waaminifu.
Tatu hakikisha mnatoa huduma bora na siyo bora huduma…umbeya na uswahili swahili ni mwiko.

Kuhusu faniture na vitu vidogo vidogo nenda RUDIUM(fire kariakoo) SH AMON(posta) na LEILA COSMETICS(kisutu,opposite Sewa Haji Hospital)

Angalizo: ili pesa yako irudi na uone faida…salon ya kike inahitaji uangalizi na ufuatiliaji wa hali ya juu sana
vinginevyo hesabu maumivu makali sana.
 
Salute Mrembo,
Radium Salon Equipments wapo vizuri sana kwa vifaa hivi.

Unajua tatizo la jamaa hapo juu ni kwamba Salon ya kike inahitaji usimamizi kila wakati,wakati ya kiume unachukua hesabu ya siku na wao vinyozi na watu wa scrub watajipanga
 
Heshima kwenu.

Naomba kama kuna mtu ana uzoefu na saloon za kunyoa anipe uzoefu, tena zile za 1000 kichwa maana kwa hesabu zangu nikilipa chumba 40,000/50,000 na nikiongea na kinyozi anipe 10,000 kila siku na nikaiboresha si nitapata?
au mnanishauri vip?
 
Mawazo yako ndio mtaji wako salsa yafanyie kazi kwanza cha muhimu no kubolesha huduma yako kinyozi mwenye uzoefu'usafi kwa ujumla,kuweka vivutio mbali mbali kama TV
 
Heshima kwenu.

Naomba kama kuna mtu ana uzoefu na saloon za kunyoa anipe uzoefu, tena zile za 1000 kichwa maana kwa hesabu zangu nikilipa chumba 40,000/50,000 na nikiongea na kinyozi anipe 10,000 kila siku na nikaiboresha si nitapata?
au mnanishauri vip?

Tembelea wadau wa sekta hiyo hapo mtaani kwako watakupa ushauri mzuri zaidi...
 
Back
Top Bottom