Biashara ya Fuel Filling station

kanyagio

JF-Expert Member
Dec 10, 2009
1,021
365
Wadau wenye kufahamu.

Je katika kuanzisha Fuel filling station kubwa maeneo ya mjini kama Dar es salaam, Je kuna kigezo cha umbali kati kituo kimoja cha mafuta kwenda kingine vilivyo upande mmoja wa barabara.Kama kipo ni umbali gani?

Hapa namaanisha kama kama kuna hiki kigezo kipya maana siku za nyuma hakikuwepo
 
Sidhani Kama kuna umbali na Kama upo Ni mita chache... Kwa mfano sheli ya total Morocco mpaka sheli ya Victoria hapana umbali Wa km 1...

Pia kwa mbezi ya kimara kuna sheli mbezi kwa yusuphu mpaka mbezi chuo cha st Joseph umbali Wa pale haujazidi km 1...

Kwa maelezo zaidi unaweza kuwaona wahusika ewura na tanroad
 
Hamna kigezo cha umbali hata kama mnatenganishwa na ukuta mmoja we unafunguwa tu utajuwa wateja utapata wapi.Umbali so kigezo kabisa
 
Sidhani Kama kuna umbali na Kama upo Ni mita chache... Kwa mfano sheli ya total Morocco mpaka sheli ya Victoria hapana umbali Wa km 1...

Pia kwa mbezi ya kimara kuna sheli mbezi kwa yusuphu mpaka mbezi chuo cha st Joseph umbali Wa pale haujazidi km 1...

Kwa maelezo zaidi unaweza kuwaona wahusika ewura na tanroad
Jamani hivi hili neno SHELL, vipi?? "sheli ya total"?? Ndio ikoje hiyo?
 
Kama umeona kosa sahihi sio kuuliza kidananda...

Shell Ni jina LA kituo cha kuuzia mafuta Kama total na puma.. Tunaita sheli kwa mazoea Ila inaitwa filling station au kituo cha mafuta...

Narudia tena Acha udananda
 
Sio mambo ya kimazoea!! Watu watajuaje kama unafahamu ila umeandika ki mazoea? Mkuu? Kwani hilo ni tatizo karibu la taifa zima hasa kizazi cha sasa ambao hata hiyo kampuni ya shell hawakuiona!! Take it easy. Wala sio kesi
 
Wadau wenye kufahamu.

Je katika kuanzisha Fuel filling station kubwa maeneo ya mjini kama Dar es salaam, Je kuna kigezo cha umbali kati kituo kimoja cha mafuta kwenda kingine vilivyo upande mmoja wa barabara.Kama kipo ni umbali gani?

Hapa namaanisha kama kama kuna hiki kigezo kipya maana siku za nyuma hakikuwepo
Sidhani kama kuna kigezo kama hicho,ila biashra ya petrol statio inatumia mara nyingi mfumo wa Frachise so kwa baadhi ya maeneo utakuta kama unataka watumia Puma na hapo kuna Puma karibu hawatakubali.Nafikiri ndio inakuwaga hivo
 
Kama kituo ni chako jenga tu hakuna tabu wateja watakuja lkn kama unataka kampuni au mtu awekeze atangalia eneo na movement yake na pia ataangalia ukaribu wa kituo sabb panapokuwa na ukaribu wa kituo ni bora zaiid kuwekeza kwani wateja wa Jiran watavutiwa pia na ww
 
Sidhani kama kuna kigezo kama hicho,ila biashra ya petrol statio inatumia mara nyingi mfumo wa Frachise so kwa baadhi ya maeneo utakuta kama unataka watumia Puma na hapo kuna Puma karibu hawatakubali.Nafikiri ndio inakuwaga hivo
Ahsante kwa maelezo
 
Sio mambo ya kimazoea!! Watu watajuaje kama unafahamu ila umeandika ki mazoea? Mkuu? Kwani hilo ni tatizo karibu la taifa zima hasa kizazi cha sasa ambao hata hiyo kampuni ya shell hawakuiona!! Take it easy. Wala sio kesi
Kama umeona kosa sahihi sio kuuliza kidananda...

Shell Ni jina LA kituo cha kuuzia mafuta Kama total na puma.. Tunaita sheli kwa mazoea Ila inaitwa filling station au kituo cha mafuta...

Narudia tena Acha udananda
Kwa kusaidia, kuna maneno yalliyokubalika na jamii fulani pale yatumikapo kwa maana kusudiwa. Hivyo hakuna cha ajabu, muhimu ni hoja kuu.
 
Kama umeona kosa sahihi sio kuuliza kidananda...

Shell Ni jina LA kituo cha kuuzia mafuta Kama total na puma.. Tunaita sheli kwa mazoea Ila inaitwa filling station au kituo cha mafuta...

Narudia tena Acha udananda
Ila katika watu huku jf wanao nichekesha wewe jamaa uko makini ngoja nikucheki pm
 
Back
Top Bottom