Zawadi Ngoda
JF-Expert Member
- Aug 13, 2009
- 3,805
- 1,873
Mtikisiko wa uchumi Ulaya umezilazimisha Benki nyingi za Ulaya kushusha Riba mara kadhaa kwa kipindi cha miaka 5. Mwezi uliopita ECB- Benki kuu ya Ulaya imeshusha Riba yake na kufikia 1.25 % ni kiwango cha chini kabisa toka Benki hiyo ianzishwe. Akielezea hatua hiyo, mkuu wa Benki hiyo ameeleza kuwa uongozi umefikia hatua hiyo ikiwa ni uamuzi muhimu sana wa kudumisha uchumi wa nchi hizo na hasa hatua hiyo inalenga kuwaondolea mzigo kwa watu wenye kipato cha chini kuweza kukopa fedha na kulipa bila kuogopa ukubwa wa RIBA.
Benki hiyo imeshusha RIBA mara kumi kwa kipindi cha miaka 5. Swali kubwa ninalojiuliza, kama Benki hizo zinaikubali idiolojia ya Benki za kiislam za kutokubali RIBA kama ni wizi wa wazi hasa kwa watu wenye kipato cha chini. Nakumbuka mara tu baada ya mtikisiko wa uchumi kuanza, Ulaya ilituma wataalamu wake kwenda nchi za KIISLAM kuchunguza jinsi wanavyoendesha BENKI ZAO. Waliporudi ndio tulishuhudia kushuka kwa RIBA kwa Benki nyingi za Ulaya. Kwa ushahidi huu ninaamini kabisa kuwa Mabenki ya Ulaya ynafuata kwa kiwango kikubwa sana idiolojia za mabenki ya KIISLAM.
Ukitaka kujua kuwa RIBA ni wizi wa wazi, ni pale ambapo BENKI inaweza kupandisha Riba wakati wowote bila kukubaliana na mkopaji. Kwa maana nyingine ni kwamba kama unakopa leo sh 1 milioni kwa riba ya 10%, baada ya miezi 5 benki inaweza kupandisha riba mpaka 20% bila kukutaarifu mkopaji. Hii ina maanisha kuwa benki hata siku moja haina kikomo cha kupandisha RIBA, hata kama wakitaka kusema RIBA yetu kuanzia leo ni 40% wanauwezo wa kisheria kufanya hivyo na itawahusu wakopaji wote hata wale waliokopa siku za nyuma wakati riba ilikuwa 12%.
Suala jingine linaloonyesha wizi, ni kwa vipi Benki zao zinazokopesha wananchi wao wanashusha RIBA, lakini Mabenki yao ya KImataifa kama IMF na WORLD BANK yanayokopesha nchi masikini hawajashusha RIBA ni tofauti wanapandisha. Hapa utajiuliza ni nani walala hoi zaidi wananchi wao au akina Masanja na Okonko wa Afrika. Jibu unalo Msomaji, La msingi ni kuikataa hii RIBA kwa mabenki yote ili kuleta haki kwa Wote kama mabenki ya KIISLAM. NA HUKO NDIKO ULAYA WANAKOKWENDA.