Benki kuu ya Ulaya yafuata mfumo wa Benki za Kiislam

Zawadi Ngoda

JF-Expert Member
Aug 13, 2009
3,768
1,817
Mtikisiko wa uchumi Ulaya umezilazimisha Benki nyingi za Ulaya kushusha Riba mara kadhaa kwa kipindi cha miaka 5. Mwezi uliopita ECB- Benki kuu ya Ulaya imeshusha Riba yake na kufikia 1.25 % ni kiwango cha chini kabisa toka Benki hiyo ianzishwe. Akielezea hatua hiyo, mkuu wa Benki hiyo ameeleza kuwa uongozi umefikia hatua hiyo ikiwa ni uamuzi muhimu sana wa kudumisha uchumi wa nchi hizo na hasa hatua hiyo inalenga kuwaondolea mzigo kwa watu wenye kipato cha chini kuweza kukopa fedha na kulipa bila kuogopa ukubwa wa RIBA.

Benki hiyo imeshusha RIBA mara kumi kwa kipindi cha miaka 5. Swali kubwa ninalojiuliza, kama Benki hizo zinaikubali idiolojia ya Benki za kiislam za kutokubali RIBA kama ni wizi wa wazi hasa kwa watu wenye kipato cha chini. Nakumbuka mara tu baada ya mtikisiko wa uchumi kuanza, Ulaya ilituma wataalamu wake kwenda nchi za KIISLAM kuchunguza jinsi wanavyoendesha BENKI ZAO. Waliporudi ndio tulishuhudia kushuka kwa RIBA kwa Benki nyingi za Ulaya. Kwa ushahidi huu ninaamini kabisa kuwa Mabenki ya Ulaya ynafuata kwa kiwango kikubwa sana idiolojia za mabenki ya KIISLAM.

Ukitaka kujua kuwa RIBA ni wizi wa wazi, ni pale ambapo BENKI inaweza kupandisha Riba wakati wowote bila kukubaliana na mkopaji. Kwa maana nyingine ni kwamba kama unakopa leo sh 1 milioni kwa riba ya 10%, baada ya miezi 5 benki inaweza kupandisha riba mpaka 20% bila kukutaarifu mkopaji. Hii ina maanisha kuwa benki hata siku moja haina kikomo cha kupandisha RIBA, hata kama wakitaka kusema RIBA yetu kuanzia leo ni 40% wanauwezo wa kisheria kufanya hivyo na itawahusu wakopaji wote hata wale waliokopa siku za nyuma wakati riba ilikuwa 12%.

Suala jingine linaloonyesha wizi, ni kwa vipi Benki zao zinazokopesha wananchi wao wanashusha RIBA, lakini Mabenki yao ya KImataifa kama IMF na WORLD BANK yanayokopesha nchi masikini hawajashusha RIBA ni tofauti wanapandisha. Hapa utajiuliza ni nani walala hoi zaidi wananchi wao au akina Masanja na Okonko wa Afrika. Jibu unalo Msomaji, La msingi ni kuikataa hii RIBA kwa mabenki yote ili kuleta haki kwa Wote kama mabenki ya KIISLAM. NA HUKO NDIKO ULAYA WANAKOKWENDA.
 
asante sana... Mi nilishaapa sitakuja kukopa benki au sehemu yoyote yenye riba hasa baada ya kugundua naibiwa.. Na nina mpango wa kuacha kupeleka hela benki kwa sababu wananiibia sana.
 
taratibu aiseee

hivi mnajua maana ya currency depreciation?
mnajua maana ya inflation??????

msibwabwaje tu humu...
 
Hebu tujulishe mkuu, maana hapa ndipo kwenye 'GREAT THINKERS'. Lakini usisahau kunukuu maneno ya wakuu wa Benki hizo za Ulaya waliyoyatoa kama SABABU YA KUSHUSHA RIBA.

Maana sikusikia 'inflation au currency depreciation' kama moja ya sababu za kushusha RIBA.
 
ahsante sana kwa taarifa mkuu. Nalog off

Log off, lakini ujumbe umeupata. Na mbaya zaidi kwa jinsi system ilivyo hata kama binafsi hujakopa lakini utahusika tu kulipa lile deni kuu la IMF kupitia kodi.

La msingi hapa ni kujiuliza kwa nini kama wanataka kutusaidia hawajashusha ile RIBA ya IMF?
 
naam mfumo wa bank wa kiislam ni mzuri sana.... kuna bank hapa tanzania imeanzisha huo mfumo ... kwa wateja waislamu wasiotaka riba... kuna watu humu waliamua ati kuhama hiyo bank while hawakulazimishwa kujiunga nayo...
 
Source? Let me guess..ni wewe menyewe..(What else is NEW??)
Halafu skujua kwamba kumbe benki za kisilamu zinatoza riba ya 1.25%
 
Mtikisiko wa uchumi Ulaya umezilazimisha Benki nyingi za Ulaya kushusha Riba mara kadhaa kwa kipindi cha miaka 5. Mwezi uliopita ECB- Benki kuu ya Ulaya imeshusha Riba yake na kufikia 1.25 % ni kiwango cha chini kabisa toka Benki hiyo ianzishwe. Akielezea hatua hiyo, mkuu wa Benki hiyo ameeleza kuwa uongozi umefikia hatua hiyo ikiwa ni uamuzi muhimu sana wa kudumisha uchumi wa nchi hizo na hasa hatua hiyo inalenga kuwaondolea mzigo kwa watu wenye kipato cha chini kuweza kukopa fedha na kulipa bila kuogopa ukubwa wa RIBA.

Benki hiyo imeshusha RIBA mara kumi kwa kipindi cha miaka 5. Swali kubwa ninalojiuliza, kama Benki hizo zinaikubali idiolojia ya Benki za kiislam za kutokubali RIBA kama ni wizi wa wazi hasa kwa watu wenye kipato cha chini. Nakumbuka mara tu baada ya mtikisiko wa uchumi kuanza, Ulaya ilituma wataalamu wake kwenda nchi za KIISLAM kuchunguza jinsi wanavyoendesha BENKI ZAO. Waliporudi ndio tulishuhudia kushuka kwa RIBA kwa Benki nyingi za Ulaya. Kwa ushahidi huu ninaamini kabisa kuwa Mabenki ya Ulaya ynafuata kwa kiwango kikubwa sana idiolojia za mabenki ya KIISLAM.

Ukitaka kujua kuwa RIBA ni wizi wa wazi, ni pale ambapo BENKI inaweza kupandisha Riba wakati wowote bila kukubaliana na mkopaji. Kwa maana nyingine ni kwamba kama unakopa leo sh 1 milioni kwa riba ya 10%, baada ya miezi 5 benki inaweza kupandisha riba mpaka 20% bila kukutaarifu mkopaji. Hii ina maanisha kuwa benki hata siku moja haina kikomo cha kupandisha RIBA, hata kama wakitaka kusema RIBA yetu kuanzia leo ni 40% wanauwezo wa kisheria kufanya hivyo na itawahusu wakopaji wote hata wale waliokopa siku za nyuma wakati riba ilikuwa 12%.

Suala jingine linaloonyesha wizi, ni kwa vipi Benki zao zinazokopesha wananchi wao wanashusha RIBA, lakini Mabenki yao ya KImataifa kama IMF na WORLD BANK yanayokopesha nchi masikini hawajashusha RIBA ni tofauti wanapandisha. Hapa utajiuliza ni nani walala hoi zaidi wananchi wao au akina Masanja na Okonko wa Afrika. Jibu unalo Msomaji, La msingi ni kuikataa hii RIBA kwa mabenki yote ili kuleta haki kwa Wote kama mabenki ya KIISLAM. NA HUKO NDIKO ULAYA WANAKOKWENDA.

Mkuu nadhani hauko sahihi,

Benki za kiislamu zina mifumo yake ya mikopo ambayo ukiangalia riba inakuwaga ni zero % Hata hivyo ukichunguza kwa undani kuna kitu wanakiiita profit sharing na incremental income wanayoipata kutoka humo haina tofauti na riba yenyewe. ECB au Fed wamepunguza riba sio kupunguza mzigo wa riba kwa wakopaji bali kuifanya mikopo iwe rahisi kwa ajili kusaidia uchumi wao usianguke. Hata hivyo benki zao zinachaji riba kama kawa ijapokuwa iko chini lakini ni riba. Sijakuelewa ulipokuwa unapoipinga riba kwani ndio pato la benki kwa kukuhifadhia hela zako na kukukopesha hela unapoihitaji kufanyia shughuli za maendeleo.

Sijui malengo ya muanzishaji mada ni yapi nilikuwapo.
 
Source? Let me guess..ni wewe menyewe..(What else is NEW??)
Halafu skujua kwamba kumbe benki za kisilamu zinatoza riba ya 1.25%

Benki za kiislam hazina RIBA kabisa, yaani Riba =0. Nilichotaka kukieleza mporomoko huu wa Riba unakaribia Benki za Kiislam, yaani kwa speed hii ya miaka mitano iliyopita jinsi walivyoshusha kama wataendelea kwa mwendokasi huo huo kwa kipindi cha miaka mitano ijayo basi kiwango cha RIBA KITAKUWA "0".
 
Mkuu nadhani hauko sahihi,

Benki za kiislamu zina mifumo yake ya mikopo ambayo ukiangalia riba inakuwaga ni zero % Hata hivyo ukichunguza kwa undani kuna kitu wanakiiita profit sharing na incremental income wanayoipata kutoka humo haina tofauti na riba yenyewe. ECB au Fed wamepunguza riba sio kupunguza mzigo wa riba kwa wakopaji bali kuifanya mikopo iwe rahisi kwa ajili kusaidia uchumi wao usianguke. Hata hivyo benki zao zinachaji riba kama kawa ijapokuwa iko chini lakini ni riba. Sijakuelewa ulipokuwa unapoipinga riba kwani ndio pato la benki kwa kukuhifadhia hela zako na kukukopesha hela unapoihitaji kufanyia shughuli za maendeleo.

Sijui malengo ya muanzishaji mada ni yapi nilikuwapo.

Kwanza Benki za Kiislama hazina Riba kabisa.

Pili, Lengo lilikuwa kuziangalia idiolojia hizi mbili zilizotofauti. Kwa Benki za kiisla hzitozi riba kwa vile zinaamini kuwa Riba ni wizi kwa mkopaji. Kwa Benki zinazotoza Riba huchukulia hiyo kama ndio kipato cha Benki. Baada ya mtikisiko wa Uchumi Ulaya, vyombo vya habari vinatoa sana Mabilioni ya Dola ambazo Benki za Ulaya zinapata kutokana na RIBA. Nchi nyingi za Ulaya wananchi wake wameanza kuuhoji mfumo huo na kwa kweli umeangusha Ethic and moral values za wananchi hasa wenye kipato cha chini.

Kwa hiyo swali ni kama huu ndio mwisho wa utozaji wa RIBA Katika Mabenki ya Ulaya.

Ukitaka kufahamu vizuri swala la RIBA fuatilia historia yake na ilianzishwa na nani?
 
Title "Benki Kuu za Ulaya zafuata mfumo wa Kiislamu" haiendani kabisa na maelezo yako! Kwa mujibu wa maelezo yako, Benki zimeshusha riba hadi 1.2% huku ukidai pia kwamba Benki za Kiislamu riba yake ni 0%! Kwanza, Sasa huoni unajichanganya mwenyewe? Pili, Je, Benki hizo Kuu za Ulaya zimedai zenyewe kwamba zinafuata mfumo wa Kiislamu au wewe ndio umekuwa "msemaji wa kujitolea" wa Benki hizo? Tatu, source ya taarifa yako ni ipi?
 
Kwanza Benki za Kiislama hazina Riba kabisa.

Pili, Lengo lilikuwa kuziangalia idiolojia hizi mbili zilizotofauti. Kwa Benki za kiisla hzitozi riba kwa vile zinaamini kuwa Riba ni wizi kwa mkopaji. Kwa Benki zinazotoza Riba huchukulia hiyo kama ndio kipato cha Benki. Baada ya mtikisiko wa Uchumi Ulaya, vyombo vya habari vinatoa sana Mabilioni ya Dola ambazo Benki za Ulaya zinapata kutokana na RIBA. Nchi nyingi za Ulaya wananchi wake wameanza kuuhoji mfumo huo na kwa kweli umeangusha Ethic and moral values za wananchi hasa wenye kipato cha chini.

Kwa hiyo swali ni kama huu ndio mwisho wa utozaji wa RIBA Katika Mabenki ya Ulaya.

Ukitaka kufahamu vizuri swala la RIBA fuatilia historia yake na ilianzishwa na nani?

Kwanza asili ya riba imetokea kwa wayahudi enzi ya nabii Isa au Jesus (A.S) pamoja na nabii zakariya (a.s). Wakati wayahudi walipokuwa wakicharge ziada katika biashara yao kama ujira wa kazi au kukopeshana.

Pili benki za kiislamu hazina riba but ukichunguza murabaha,sukuk, musharakah na mudharabah na Ijar wanafanya katika mazingira ya kuwagawana faida. This is key intergral part of islamic banking katika kushare profit and loss and risk and return kwa mtumiaji wa huduma za benki.

Hata hivyo ukiangalia faida uliyoipata kutoka products hizo na interest on loan uliyolipa kwenye benki au huduma za benki utaona tofauti ni ndogo sana.

Mkuu ukilinganisha na ECB ndio unapokosea kwani ECB wanachokifanya au Feds ni Keynisian Economics ambapo Milton Keynes anasema wakati wa matatizo ya mdororo wa kiuchumi ni vizuri serikali zikawasaidia private sectors. Lowering interest rate ni kujaribu kuwahamasisha private sector kukopa na kukuza uchumi.

Ni vema ulinganisha Islamic banking na benki za kawaida. Hapo nakuunga mkono kwakuwa Islamic Banking nafahamu nyingi wakati wa matatizo ya kibenki 2008 hazikuyumba kwakuwa zilikuwa ziko stable katika utendaji wake.
 
Benki za kiislam hazina RIBA kabisa, yaani Riba =0. Nilichotaka kukieleza mporomoko huu wa Riba unakaribia Benki za Kiislam, yaani kwa speed hii ya miaka mitano iliyopita jinsi walivyoshusha kama wataendelea kwa mwendokasi huo huo kwa kipindi cha miaka mitano ijayo basi kiwango cha RIBA KITAKUWA "0".
lolz @ this deluded Islamist..sasa tangu lini 0% = 1 1/4%?
We mchemfu na hupo hapa kuelimisha bali kujitilia ndimu..tumeshakuzoeeni.
 
Mkuu nadhani hauko sahihi,

Benki za kiislamu zina mifumo yake ya mikopo ambayo ukiangalia riba inakuwaga ni zero % Hata hivyo ukichunguza kwa undani kuna kitu wanakiiita profit sharing na incremental income wanayoipata kutoka humo haina tofauti na riba yenyewe. ECB au Fed wamepunguza riba sio kupunguza mzigo wa riba kwa wakopaji bali kuifanya mikopo iwe rahisi kwa ajili kusaidia uchumi wao usianguke. Hata hivyo benki zao zinachaji riba kama kawa ijapokuwa iko chini lakini ni riba. Sijakuelewa ulipokuwa unapoipinga riba kwani ndio pato la benki kwa kukuhifadhia hela zako na kukukopesha hela unapoihitaji kufanyia shughuli za maendeleo.

Sijui malengo ya muanzishaji mada ni yapi nilikuwapo.

Nimefurahi sana jinsi ulivyoielimisha jamii kuhusu asili ya RIBA. Hii ni sahihi kabisa, na ukweli na kwamba hizo riba wakati huo zilileta uadui mkubwa sana kati ya matajiri na masikini. Riba zilikuwa kubwa na ziliongezeka kila mwezi kwa anayeshindwa kulipa deni, wakati mwingine zilifikia mpaka 100%. Ilikuwa ni mateso kwani matatizo ya watu yalitumiwa kama mtaji. Kifupi, mfumo wa uchumi na hasa mabenki unaotumiwa leo hii katika nchi zilizoendelea ni mfumo ule wa Kiyahudi.

Swali la kujiuliza, ni nani anayefaidika na ni nani anayepoteza? Kuna uwezekano wa kujikomboa kutokana na mfumo huo hasa kwa wanaopoteza ikiwemo Afrika.

Hoja yako nyingine umesema: "Benki za kiislamu zina mifumo yake ya mikopo ambayo ukiangalia riba inakuwaga ni zero % Hata hivyo ukichunguza kwa undani kuna kitu wanakiiita profit sharing na incremental income wanayoipata kutoka humo haina tofauti na riba yenyewe"
Unajua tatizo si usawa wa kiwango cha pesa bali ni 'ETHIC and MORAL VALUES' ya suala lenyewe. Faida ni swala linalokubalika kwa mwanadamu yeyote yule. Unayefanya biashara ya kuuza nyama, Mchele, Dala Dala, Kiwanda cha Urafiki, shule za Private n.k. Ziwe biashara ndogo au Kubwa suala ni moja tu.

Lakini unapozungumzia RIBA ni neno lenye idiolojia nyingine kabisa. Na ukweli ukichunguza asili yake ilikuwa ni wizi kwa kutumia shida ya mtu. Ni biashara iliyokuwa haina utu hata kidogo. Isitoshe mkopaji hashirikishwi katika kujadili Riba inapoongezwa.

Umeeleza juu ya ECB, ni sawa kabisa maelezo yako. Lakini ulichosahau ni vitu viwili muhimu.
  • Riba ya ECB ina athiri RIBA za Mabenki mengine Mengi. ECB ndio inakopesha hata Mabenki mengine ya Ulaya ambayo nayo yameshusha RIBA kutokana na kushuka kwa RIBA ya ECB. Kwa hiyo kushuka kwa RIBA kwa ECB ndio ni Muhimu sana kwani system ya Mabenki iko kama PYRAMID. Kwa Ulaya Juu ya kilele cha PYRAMID ndio ECB.
  • Umeeleza :"ECB au Fed wamepunguza riba sio kupunguza mzigo wa riba kwa wakopaji bali kuifanya mikopo iwe rahisi kwa ajili kusaidia uchumi wao usianguke." Ukipunguza riba ndio umepunguza mzigo kwa mkopaji, na ukimpunguzia mzigo mkopaji umempa urahisi wa kukopa, na Benki bila mkopaji haiendi maana huko kwa mfumo wao ndiko wanakofanya faida. Na Ulaya si kama Afrika, kwani wenzetu 90% ya wananchi wao wana mkopo wa aina moja au nyingine. Hivyo Mabenki walichoona ni kupungua kwa wakopaji baada ya mtikisiko wa wa uchumi na hii iliwaathiri wote nikimaanisha Serikali (kodi) na uchumi wa mwananchi mwenyewe na mabenki. Kwa hiyo kupunguza mzigo ni suala ambalo halikuweza kuepukika.
Swali ni kuwa JE HUO NDIO MWISHO WA MCHEZO HUKO ULAYA? Na IMF na WORLD BANK JE? AU Afrika ndio matajiri kwa hiyo hatuhitaji kupunguziwa mzigo?
 
What if interest wakipunguza na kuwa sawa na faida anayoipata mtu mkishare profit je riba itakuwa na ubaya? Na kwanini duniani kuna wengine wana shida ya mtaji na wengine wanakuwa na uwezo wa kuwapa watu wengine mtaji?
 
Bado kuna Tatizo. Tatizo ni kwamba Faida na Riba zinajengwa katika mazingira tofauti sana. Mfano Rahisi ni pale ambapo mkopaji wa IMF hawezi hata kidogo kuwa na sauti juu ya RIBA ipangwae na Benki hiyo. Sasa niambie kwanini hawajashusha RIBA ya IMF, wakati walala hopi ndio wa Afrika ndio tunalipa hiyo Riba.

Nikija kwenye swala la ETHIC na MORAL VALUES ni muhimu kuelewa kuwa kama umeiba sh 1000 na mwingine ameiba milioni 100. Katika Ethic na Moral values nyie ni sawa kwani swala hapo si kiwango bali ile tabia ya wizi. Kwa hiyo Riba ipo katika mazingira ya WIZI bila ya kujali kiwango. Hata nadharia ya kuongezwa na kupunguzwa kwake kama umeielewa vizuri utakubaliana nami. Na hapo ndio tatizo.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom