Kama Tz hatuna chama mbadala ungetaka wawe cham gani zaidi ya ccm?
WanaJF,
Kuna msemo niliwahi kuusoma zamani, 'mimi sio nyoka kwa sababu baba yangu hakuwa nyoka'...
Pia, wengi wetu (sio wote) ni wakristo au waislamu kwa sababu wazazi wetu ni wakristo au waislamu. Au kwa sababu tumelelewa kwenye mazingira hayo.
Hali hiyo imewakuta wengi linapokuja suala la ufuasi wa vyama hasa kwa vijana ambao wazazi wao walikuwa au ni viongozi wa ccm. Ukiangalia vijana walio kwenye baraza la vijana la chadema na wale walio kwenye umoja wa vijana wa ccm utaona hilo. Hata wale ambao umri umesogea kidogo na sio vijana tena.
Hapa nitatoa mifano michache;
1. Ridhiwani Kikwete
2. January Makamba
3. Nape Nnauye
4. William Malecela
5. Hussein Mwinyi
6. Abdulla Mwinyi
7. H. Kawawa
8. Mboni Mhita
Hawa ni baadhi ya wengi ambao kuwa kwao CCM ni dhahiri kumetokana na malezi na sio kwa kutaka kwao. Ndio maana wanafuata dini na makabila ya wazazi wao. Wamelazimika pia kufuata 'uanachama' wa wazazi wao.
Swali linabaki inawezekanaje wakawa na lolote jipya? Je wana uwezo kiasi gani kuwa na mawazo binafsi? Itawezekanaje wajivue gamba walilozaliwa nalo?
Kuna watu kama kina Makongoro Nyerere waliwahi kwenda tofauti lakini baadae tena wakarudi walikotoka.
Freeman Mbowe ni mmoja wa watoto wa makada wa CCM ambae ameweza kusimama na kubaki kwenye upinzani daima. Je ni kutokana na kutokuwa na njaa? Ni kutokana na yeye kuweza kufanya biashara zake bila kutegemea mzazi hivyo kuweza kuwa na mawazo binafsi? Au ni influence ya Mzee Mtei?
Kikubwa zaidi ni kwamba hakuna mtoto wa kiongozi wa ccm anayeweza kuthubutu kwenda kinyume na baba au mama yake. Kwa nini? Uoga na unafiki!