Viongozi wa BAVICHA wakishiba na kuvimbiwa, wanawaza maandamano bila kujali hali za vijana wanaowataka kuandamana.

KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
2,591
4,604
Nawapongeza sana UVCCM maana wanachofanya siku zote ni kuwaheshimisha vijana, huwezi kukuta UVCCM wanapanga kufanya maandamano huku wakijua vijana wanatakiwa kutafuta ugali wao muda huo.

Maandamano ya UVCCM yananifurahisha Kwa sababu yanakuja baada ya vijana kushiba tofauti na ya BAVICHA ambayo yanashindisha vijana njaa. Unakuta UVCCM inafanya maandamano ya kuipongeza Serikali kutoa ajira nyingi kwa vijana ambalo ni jambo zuri au kuishukuru Serikali kutoa mitaji na ujuzi Kwa vijana ambalo ni jambo zuri zaidi Kwa sababu vijana wanakuwa wameshiba ujuzi

Sasa BAVICHA kufanya maandamano hali wakijua wameshiba wao huku wanaowaandamisha wana njaa ,ni jambo la ajabu na aibu kidogo kwangu
 
Tangu mama aanze kutoa ruzuku Pambalu na Mnyika wananenepa sana, mashavu hatari
 
Back
Top Bottom