BAVICHA vs UvCCM: Walipo watoto wa Viongozi wa CCM na CHADEMA

Kama Tz hatuna chama mbadala ungetaka wawe cham gani zaidi ya ccm?
WanaJF,

Kuna msemo niliwahi kuusoma zamani, 'mimi sio nyoka kwa sababu baba yangu hakuwa nyoka'...

Pia, wengi wetu (sio wote) ni wakristo au waislamu kwa sababu wazazi wetu ni wakristo au waislamu. Au kwa sababu tumelelewa kwenye mazingira hayo.

Hali hiyo imewakuta wengi linapokuja suala la ufuasi wa vyama hasa kwa vijana ambao wazazi wao walikuwa au ni viongozi wa ccm. Ukiangalia vijana walio kwenye baraza la vijana la chadema na wale walio kwenye umoja wa vijana wa ccm utaona hilo. Hata wale ambao umri umesogea kidogo na sio vijana tena.

Hapa nitatoa mifano michache;

1. Ridhiwani Kikwete

2. January Makamba

3. Nape Nnauye

4. William Malecela

5. Hussein Mwinyi

6. Abdulla Mwinyi

7. H. Kawawa

8. Mboni Mhita

Hawa ni baadhi ya wengi ambao kuwa kwao CCM ni dhahiri kumetokana na malezi na sio kwa kutaka kwao. Ndio maana wanafuata dini na makabila ya wazazi wao. Wamelazimika pia kufuata 'uanachama' wa wazazi wao.

Swali linabaki inawezekanaje wakawa na lolote jipya? Je wana uwezo kiasi gani kuwa na mawazo binafsi? Itawezekanaje wajivue gamba walilozaliwa nalo?

Kuna watu kama kina Makongoro Nyerere waliwahi kwenda tofauti lakini baadae tena wakarudi walikotoka.

Freeman Mbowe ni mmoja wa watoto wa makada wa CCM ambae ameweza kusimama na kubaki kwenye upinzani daima. Je ni kutokana na kutokuwa na njaa? Ni kutokana na yeye kuweza kufanya biashara zake bila kutegemea mzazi hivyo kuweza kuwa na mawazo binafsi? Au ni influence ya Mzee Mtei?

Kikubwa zaidi ni kwamba hakuna mtoto wa kiongozi wa ccm anayeweza kuthubutu kwenda kinyume na baba au mama yake. Kwa nini? Uoga na unafiki!
 
Uko hivyo ulivyo kwa sababu kadhaa na miongoni ni hizi zifuatazo:

1. Wazazi wako
2. Sehemu na wakati ulikozaliwa
3. Shule ulizosomea, ikiwa ni pamoja na fani yako
4. Exposure yako
5. Unafanya nini na ni zipi jitihada zako juu ya hali ulionayo
5. Ndoto na chaguo la maisha yako
6. n.k

Wako watu wengi wamezaliwa familia za hali ya chini sana, lakini wameibuka na kufanikiwa aidha kwenye medani za siasa, elimu, biashara, muziki n.k

Pia wako watu wengi sana wa watu waliokuwa mashuhuri na wasomi wakubwa lakini wameishia kuwa wavuta bangi na walevi wakubwa.

Rai yangu: Akina Nape, January, David, Hussen n.k tutakuwa hatuwatendei haki tunapowasema vibaya juu ya success yao katika medani za siasa hapa nchini. Ebu soma profile ya Mh. January kwenye website yake, uone alivyo smart...Ukweli, ata lile wazo la kupost profile yake kwenye mtandao ni kuonyesha inajibidiisha. Fuatilia kwa umakini ata mawazo na posting za watu hapa JF utaona baadhi yetu tuko weak kwenye mijadala. Soma rambirambi za Mh. Zitto kwa aliyekuwa M/Kiti wa CDM Shinyanga, utaona Mh. Zitto ata asingekuwa Mbunge bado mchango wake kwa jamii ungeonekana tu. VIJANA TUJIBIDIISHE POPOTE TULIPO NA TUENDELEE KUFANYIA KAZI NDOTO ZETU KWA UMAKINI, ONE DAY YES!
 
Adam na Eva walikuwa wana wa Mungu hapo Mwanzo. Walipotaka kuwa kama Baba yao yaani Mungu, ndiyo mwanzo wa mauti, taabu, shida, chuki, udini, ukanda, ukabila n.k ambavyo tumerithi mimi na wewe.

"Mtoto amuleavyo ndivyo akuavyo". Binafsi sioni kwa nini wote uliowataja wasiwe wanasiasa na viongozi. Ni haki yao kikatiba ni hii nchi ni yetu sote.

Sijasema kwamba wasiwe wanasiasa na viongozi. Hakuna tatizo wao kuwa wanasiasa na viongozi. Je ni kutokana na malezi ndio maana wamekuwa wanasiasa na viongozi kupitia CCM au ni kwa sababu wanaamini CCM ni chama bora? Je kutokuwa kwao upinzani ni kwa sababu hawataki kuwaudhi wazazi wao au ni kwa sababu vyama vya upinzani ni dhaifu?
 
cdm nayo ina wenyewe muulize zitto kabwe

Zitto Kabwe aulizwe nini? yeye ni mbunge kwa tiketi ya CDM. Ni Naibu Katibu Mkuu na Naibu wa Kiongozi wa Upinzani Bungeni. Sasa kama yeye sio mwenyewe basi mwenyewe atakuwa nani?
 
Uko hivyo ulivyo kwa sababu kadhaa na miongoni ni hizi zifuatazo:

1. Wazazi wako
2. Sehemu na wakati ulikozaliwa
3. Shule ulizosomea, ikiwa ni pamoja na fani yako
4. Exposure yako
5. Unafanya nini na ni zipi jitihada zako juu ya hali ulionayo
5. Ndoto na chaguo la maisha yako
6. n.k

Wako watu wengi wamezaliwa familia za hali ya chini sana, lakini wameibuka na kufanikiwa aidha kwenye medani za siasa, elimu, biashara, muziki n.k

Pia wako watu wengi sana wa watu waliokuwa mashuhuri na wasomi wakubwa lakini wameishia kuwa wavuta bangi na walevi wakubwa.

Rai yangu: Akina Nape, January, David, Hussen n.k tutakuwa hatuwatendei haki tunapowasema vibaya juu ya success yao katika medani za siasa hapa nchini. Ebu soma profile ya Mh. January kwenye website yake, uone alivyo smart...Ukweli, ata lile wazo la kupost profile yake kwenye mtandao ni kuonyesha inajibidiisha. Fuatilia kwa umakini ata mawazo na posting za watu hapa JF utaona baadhi yetu tuko weak kwenye mijadala. Soma rambirambi za Mh. Zitto kwa aliyekuwa M/Kiti wa CDM Shinyanga, utaona Mh. Zitto ata asingekuwa Mbunge bado mchango wake kwa jamii ungeonekana tu. VIJANA TUJIBIDIISHE POPOTE TULIPO NA TUENDELEE KUFANYIA KAZI NDOTO ZETU KWA UMAKINI, ONE DAY YES!

tutakuwa hatuwatendei haki tunapowasema vibaya juu ya success yao katika medani za siasa hapa nchini.

Ni wapi nimewasema vibaya? Au maswali niliyouliza ni kuwasema vibaya? Labda niulize kwa lugha nyepesi zaidi, je wanasiasa na vingozi hao wanaweza kujiunga na upinzani na kupingana na mawazo ya wazazi wao? Kuna kijana yeyote mwenye umri usiozidi miaka 35 mtoto wa kiongozi wa CCM ambaye yuko upinzani? Kuna kijana yeyote mtoto wa kiongozi wa upinzani mwenye umri usiozidi miaka 35 ambaye yupo CCM na ni kiongozi?

Hoja ya msingi hapa ni kwa nini vijana wanafuata ufuasi wa wazazi wao kwenye siasa? Ni kwa sababu mawazo yao na imani yao ndiyo inawatuma hivyo au ni matakwa ya wazazi na maslahi?
 
Una maana gani kwa hili swali lako la pili? si umesema mwenyewe kuwa Freeman Mbowe ni mmoja wa watoto wa kada wa CCM?

Freeman Mbowe ameanza siasa miaka ya 90. Kwa sasa hivi sio kijana tena. Ila najaribu kujiuliza kwa nini vijana wa sasa (age 35 - 18) ambao wazazi wao ni viongozi au wanasiasa wanakimbilia kule waliko wazazi wao? Je hawana mawazo yao binafsi? Au siasa ni kama ilivyo dini na kabila la mzazi kwamba lazima uvifuate?
 
Kuna mmoja aliwahi kukiri: "Ndiyo nimembeba mwanangu, ....lakini nimefanya hivyo kama mzazi si kama katibu mkuu" Kwa kauli hii alifanikiwa kuhadaa wanamagamba wenzake.
 
Mtoto wa nyoka ni nyoka, jibu unalo. Hii ni kweli kutokana na malezi waliyokulia lazima utafuta mkondo, kuna msemo mwingine husema maji hufuata mkondo. Mfano mzuri wa nyumbani kwetu, watu wa nyumbani hawakupenda siasa isipokuwa mmoja au tuseme walikuwa ssm mamluki, sasa huyu mmoja ni cdm na mwaka jana kagombea ubunge, kwenye pilikapilka za kampeni watu wetu wamevutika na cdm, sasa wanazungumza kicdm cdm na wanipenda cdm, ni kwamba huyu kawaambikiza ucdm. So maji hufuata mkondo

Hoja ni kwamba je hawa watu watakuwa na mabadiliko? inategema na dhamira ya mtu husika, mabadiliko yanawezekana au yasiwepo, Ila mi ninachojua vijana wa leo si kama wale wa juzi.

Issue ya Mbowe naweza sema pengine kwasababu hafuati pesa kwenye siasa ndo maana kabaki pale alipo, au naweza sema cdm ni kama yake amedhaminiwa na mkwe au pengine vyama vya siasa pengine ni biashara hatuwezi jua, kafika ametua mabegi.
 
Uko hivyo ulivyo kwa sababu kadhaa na miongoni ni hizi zifuatazo:

1. Wazazi wako
2. Sehemu na wakati ulikozaliwa
3. Shule ulizosomea, ikiwa ni pamoja na fani yako
4. Exposure yako
5. Unafanya nini na ni zipi jitihada zako juu ya hali ulionayo
5. Ndoto na chaguo la maisha yako
6. n.k

Wako watu wengi wamezaliwa familia za hali ya chini sana, lakini wameibuka na kufanikiwa aidha kwenye medani za siasa, elimu, biashara, muziki n.k

Pia wako watu wengi sana wa watu waliokuwa mashuhuri na wasomi wakubwa lakini wameishia kuwa wavuta bangi na walevi wakubwa.

Rai yangu: Akina Nape, January, David, Hussen n.k tutakuwa hatuwatendei haki tunapowasema vibaya juu ya success yao katika medani za siasa hapa nchini. Ebu soma profile ya Mh. January kwenye website yake, uone alivyo smart...Ukweli, ata lile wazo la kupost profile yake kwenye mtandao ni kuonyesha inajibidiisha. Fuatilia kwa umakini ata mawazo na posting za watu hapa JF utaona baadhi yetu tuko weak kwenye mijadala. Soma rambirambi za Mh. Zitto kwa aliyekuwa M/Kiti wa CDM Shinyanga, utaona Mh. Zitto ata asingekuwa Mbunge bado mchango wake kwa jamii ungeonekana tu. VIJANA TUJIBIDIISHE POPOTE TULIPO NA TUENDELEE KUFANYIA KAZI NDOTO ZETU KWA UMAKINI, ONE DAY YES!

Hapo umenena! twaweza fanya makubwa popote pale, suala ni dhamira ya dhati, iwe babako ni bosi au la.
 
viongozi walioshinda bavicha wote ni watoto wa viongoz wa chadema na ndugu zao.me naendelea kusema cdm hawana tofauti na ccc na kinachowatofautisha wao na ccm ni kwamba wao hawana dola.tena bora ccm imejivua gamba kuliko cdm ambayo imejaa wanafiki na wezi na wachochezi wa fujo.
 
Nani amewambia Nape mtoto wa Nnauye? Mbona wale dada zake waliwahi kuripitiwa kwenye vyombo vya habari wakimkana? Muondoeni humo Nape katika orodha ya watoto wa vigogo. Huyu ana baba yake, lakini si Nnauye.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom