Baunsa

mwl

JF-Expert Member
May 25, 2011
1,101
913
Jamaa mmoja alikwenda hoteli hana pesa akataka apewe chakula, akakataliwa. Basi jamaa akawatisha alipowaambia nitafanya kama alivyofanya kaka yangu jana. Wale watu wakaogopa wakijua kwamba jamaa ni mkorofi au kaka yake baunsa, wakampa chakula. Alipomaliza wakamuuliza tuambie kaka yako alifanya nini jana, jamaa akawaambia alilala bila ya kula.
 
duh, umenikumbusha mbali sana aisee..
Kipindi hicho nimekuja dar zamani kiasi, tukapanda basi la mabgala yani limejaa vibaya.
Basi konda akaanza kuitisha nauli..jamaa mmoja kujisachi akajikuta wallet yake haipo!
Akaanza kuongea kwa sauti ya juu, full hasira..
"Aisee, aliyenichukulia wallet yangu anirudishie!"
watu kimya..
akasimama tena, akasema, "Washkaji eeh, sitaki utani leo, aliyenichukulia wallet yangu anirudishie kabla sijafanya kitu nisichokipenda"
watu kimya wengine wakaanza kumcheka kimyakimya..
Ghafla, mshkaji akaanza kutoa shati akabaki na vesti, shati kaweka kwenye begi la mgongoni, akarudia,
"Aliyechukua wallet yangu, anirudhishie kabla sijafanya nilichokifanya jana!"
Watu kimya baada ya kuona jamaa anakuwa serious..
Akainama, akaanza kufunga kamba za viatu vizuri. afu mi ndo nimekaa jirani yake, jamaa amejazia, full kuunga ze body!
akasimama tena,
"Kwa mara ya mwisho ntasema kabla sijasimamisha gari, ALIYECHUKUA WALLET YANGU ANIRUDISHIE KABLA SIJAFANYA NILICHOFANYA JANA! SIPENDI KUKIFANYA ILA UTANILAZIMISHA.."
Akaaa..
haikupita dakika, mara tukaona wallet imerushwa kutoka nyuma..
jamaa akachukua nauli akalipa akaendelea kukaa.
Sasa mimi kwa curiosity nkamuuliza, "Kakae kwani jana ulifanya nini?"
akaniambia, "Acha tu mdogo wangu, jana pia waliniibia wallet ikanibidi nitembee kutoka kwa Azizi Ali mpaka Kizuyani kwa miguu. Hapa yenyewe nlikua najiandaa kuanza kutembea tena."
Duh..
 
Nyingine hii:

Washikaji wawili wamekutana na maneno yakaanza kama ifuatavyo..........

Mshikaji 1: Aisee jana nona ile mbaya maana NIMELALA NA NJAA.

Mshikaji 2: Heri yako wewe umeLALA NA NJAA, mwenzio jana nimelela peke yangu.
 
duh, umenikumbusha mbali sana aisee..Kipindi hicho nimekuja dar zamani kiasi, tukapanda basi la mabgala yani limejaa vibaya.Basi konda akaanza kuitisha nauli..jamaa mmoja kujisachi akajikuta wallet yake haipo!Akaanza kuongea kwa sauti ya juu, full hasira.."Aisee, aliyenichukulia wallet yangu anirudishie!"watu kimya..akasimama tena, akasema, "Washkaji eeh, sitaki utani leo, aliyenichukulia wallet yangu anirudishie kabla sijafanya kitu nisichokipenda"watu kimya wengine wakaanza kumcheka kimyakimya..Ghafla, mshkaji akaanza kutoa shati akabaki na vesti, shati kaweka kwenye begi la mgongoni, akarudia,"Aliyechukua wallet yangu, anirudhishie kabla sijafanya nilichokifanya jana!"Watu kimya baada ya kuona jamaa anakuwa serious..Akainama, akaanza kufunga kamba za viatu vizuri. afu mi ndo nimekaa jirani yake, jamaa amejazia, full kuunga ze body!akasimama tena,"Kwa mara ya mwisho ntasema kabla sijasimamisha gari, ALIYECHUKUA WALLET YANGU ANIRUDISHIE KABLA SIJAFANYA NILICHOFANYA JANA! SIPENDI KUKIFANYA ILA UTANILAZIMISHA.."Akaaa..haikupita dakika, mara tukaona wallet imerushwa kutoka nyuma..jamaa akachukua nauli akalipa akaendelea kukaa.Sasa mimi kwa curiosity nkamuuliza, "Kakae kwani jana ulifanya nini?"akaniambia, "Acha tu mdogo wangu, jana pia waliniibia wallet ikanibidi nitembee kutoka kwa Azizi Ali mpaka Kizuyani kwa miguu. Hapa yenyewe nlikua najiandaa kuanza kutembea tena."Duh..
Duh! Hii ndo imetisha
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom