Mapito ya dunia!

Chawa wa lumumbashi

JF-Expert Member
Nov 19, 2022
793
1,749
THE HUSTLER - 2

Nilipata hela ya kulipa baada ya kama wiki na kitu hivi, nyumbani mpaka sehemu niliyoambiwa nitapandia gari ni mbali kwahiyo asb ya alfajiri yule mtu wa sait alikuja na baiskeli mbili akanipakia na mama akapanda nyingine.

Kufika huko tulikaa sehemu jamaa akasema tusubiri gari inakuja. Hapo sasa ni pale *** mjini kabisa

Laura mama yangu aliamka kama saa tisa hivi kusali kiasi na mm sikulala tena alisali mwisho akaanza kulia kichinichini nilijisikia vibaya tukaamka wanawe wote kukakaa naye. Maneno yake mengi yalikuwa kunisihi kama mambo yasipokuwa sawa ni heri tu nirudi nyumbani

Palipokucha nikaagana na ndugu zangu tukaondoka. sasa hapo tulipokaa mama alikuwa anainama anasali ananishika bega bila kukaza roho ningemuambia mama turudi tu nyumbani ila maisha laura maisha yanakufanya unakaza roho

Basi kukatokea sintofahamu flani, gari aliyoitegemea kumbe iliondoka jana yake saa kumi jioni hapo nikatakiwa nipande gari nyingine yule jamaa wa sait akawa anasita sababu sio gari ya mtu anamjua tulichelewa mno kuondoka mwisho nikalipa nikaondoka ni lori flani lilikuwa na vitunguu na humo nyuma tulikuwa watatu

Ilikuwa safari ya ukimya sana kulikuwa na sehemu za kula ambazo sikushuka na sikuwa hata na hiyo hela ya kula. Tulisafiri muda mrefu sometimes tulishuka tukaambiwa tutembee kuvuka sehemu fulani kisha mnapandia gari mbele nahisi kuna sehemu walikuwa wanakwepa vitu na gari ilikuwa mbovu pia kuharibika kila mara

Nilifika kibaha kama saa tano asb au sita hv kesho yake, dereva akaniambia ndio hapo yeye kazi imeisha, nilikuwa na namba ya kupiga, nikaomba simu sehemu nikapiga nikafuatwa pale

Ni kweli ilikuwa kazi ya kuangalia mifugo ng'ombe na mbuzi wengi lakini Laura mlo ulikuwa ni mmoja tu tena kama unafanyiwa hisani na kutumwa kazi za ndani na bustani hupumziki

Matusi ndio usiseme mabosi wakijisikia hapa vibao unapigwa, watoto humo ndani wanakutend kama mtumwa wao, nilifanya kaz miezi nane hivi au tisa kamili bila kupokea chochote Laura yaani hata shilingi mia sikupewa kila siku maneno na ahadi badae nikaanza kufokewa nakula bure nalala bure kila nikikumbushia hela yangu

Niliondoka pale baada ya kulala polisi kuwa nimeiba jenereta nikauza, naapa kwa Mungu sikuwai kuiba hata ukoko nikiwa na njaa achia hiyo jenereta ambayo sikuwahigi kuiona.

Nikafukuzwa nikaondoka bila chochte hata nguo zangu ambako kulikuwa kuna namba za mawasiliano ya mtu kule nyumbani yule jamaa wa sait alinipa ili nikipata tatizo niipige ila nilijikaza kutoipiga kwa hofu asione nalalamika sana huku kanisaidia nilikuwa na matumaini nitalipwa hela yangu, so nikaondoka mikono mitupu walininyima hata ndala laura shahidi Mungu wangu

Na jua kali nilitembea peku toka pale mpaka barabara kubwa kuna mwendo aiseee na vipori vidogo vidogo, nikajaribu kuomba msaada lakini watu wakawa hawaniamini wananiona tapeli mmoja ndo alinisaidia ndala basi

sijawahi kulala nje Ila siku ile nililala nje asb nikaendelea tu kutembea bila mwelekeo mpka nilipohisi naishiwa nguvu kidogo sababu njaa na uchovu nilifika sehemu kuna stendi ya daladala nikajilaza hapo kwa muda sana baadae nikaona nitakufa

nikamfata kaka fulani anauza machungwa kwenye meza nikamuomba anisaidie chungwa sina hela akanipa na tukaongea, yule jamaa akanipa mtu akasema atanisaidia

Yote ni katika kutafuta riziki yangu, nilianza na vibarua nikapiga dege sana Kibaha stendi nikapata gari nikawa konda kila hela napata nje ya chakula yote naweka sikuwahigi kusahau sura ya mama akilia, kaka yangu akiumwa na dhiki niliyoiacha nyumbani

Gari nililokuwa Konda lilipata ajali nikanusurika kufa ila niliumia vibaya sana watu kibao walikufa basi akiba yote ikaniuguza nikarudi nyuma hatua mia ikawa kama naanza moja tena

Sikuweza kurudia kwenye ukonda nikaingia sokoni kujaribu kubeba mizigo na kuuza mifuko huku natafta japo duka la kuuza ile kazi ya mizigo niliacha baada ya kupoteza fahamu nikiwa na mzigo begani, kiukweli tangu kupata ajali nilikuwa dhaifu sana na mkono mmoja ulikuwa na maumivu kila mara

hapo ninakolala lilikuwa geto tu lina watu kama 11 hivi, asb wote mnaingia mtaani kutafuta usiku mnabanana hata hewa safi shida lakini utafanya nini sasa utaenda wapi? Sasa nilipopoteza fahamu niliamua kupumzika kidogo sikuwa sawa ikatokea mchana kuna mtu yy mishe zake sometime mchana yupo akaanza kuniletea mambo ya ajabu pale geto nikamwambia sijihusishi na hizo vitu ila kama ikawa ananiharaz sana mwisho siku moja akataka kama kutumia nguvu kwa sababu yy mkubwa nikamchomoka nikakimbilia kijiweni kwa mshikaji flani nae tupo nae geto huwa ana mishe sizijui kumueleza nikaona aibu haijakaa kiume kusema yale mambo ila ndani nilikuwa naogopa na sikutaka kurudi pale maana alinishikia kisu cha koo

Pale geto niliondoka nikawa nalala duka flani hivi niliomba hifadhi ya muda na muuzaji alikuwa mtu poa. Hapo natafuta inshu sioni na mwili unaniuma kila siku ukishika hata 5000 unaona kutoa mia 200 ununue panado hela itaisha

Nikahangaika sana hadi kuzibua vyoo na mitaro nilijaribuni aisee nilitapika sana nikaona nitafia kwenye mashimo ya watu

Huku na kule nilijikuta kwenye ishu flani za wizi nikaona labda nitatusua Mungu anisamehe ilikuwa kama mara mbili ya tatu tuliingia sehemu nia ilikuwa kuiba na kuondoka ila bahati mbaya mwenzetu akajeruhi katika kujihami ikawa nuksi tupu akapigwa akatiwa tairi tumejificha tunaona yaani ile picha aliuungua na kulia ilinitia wehu kweli kweli, Laura niliambiwaga nivute hiki mara nilambe sijui maunga gani nitakaa sawa nitaacha wuoga na sauti ya mama ilikuwa kama inakuja inaniita

Yale sio maisha nilitaka kuishi nilitoka pale nilipohifadhiwa nikatembea mpaka sehemu nikawa sijui nifanyeje naona moto matairi mtu anaungua kwa kweli nilipata kiwewe kikubwa nikaona msikiti mbele japo mimi mkristo nilienda tu nikavua viatu nikaingia mule ndani hakukuwa na watu wengi walikuwa wachache sana

Nikaweka mikono kichwani sikuwa nimelia kwa kipindi kirefu cha mapito yangu ila pale nilianza kulia kwa sauti kubwa nikimuita Mungu aniokoe
Basi wle jamaa msikitini walinifuata wakanishika wakaniweka pembeni kidogo na kunihoji nikasaidiwa chakula na hela kiasi

Nilikaa na ipe hela nawaza nirudi nyumbani nikiwa hv au niendelee kupambana? Nikasema mi mwanaume nitaanza moja ile hela nikaanza kufata maji ya jumla nauza kwa kutembeza faida ni ndogo kwa sababu mtaji mdogo, hela mwingine anaipata kwa siku we unaidunduliza wiki ndo itimie bila hivyo hutoboi,

nimeuza sana maji juani mtaji ulipokua kidogo nikatafuta mwamvuli wa kuweka stendi afya yangu pia ilikuwq inazidi kuwa ovyo juani, nilisogea hadi maeneo ya Kimara nikawa napata angalau ya kutunza na kuishi geto la mbavu za mbwa ukiona huwez amini mtu anaishi

Nikawa naongeza vitu kidogo kidogo, nikawaza nikaona nahitaji ujuzi siku biashara hii ikiyumba nipate pa kuegemea basi nikaona nijifunze kufyatua matofali pia kilikuwa na mshikaji site flani tulizoeana basi nikawa siku nyingine naenda na biashara sait nasaidia kufyatua ili nipate ujuzi lakini nalipwa kidogo

Siku moja niko na mwamvuli barabani stend akaja yule mshikaji akasema kuna dili la kufyatua matofali sait ya mtu Bunju ile dili ndiyo ilinipa hela nyingi kiasi kwa pamoja, kukaa kidogo yule mtu akatuunganisha na rafiki yake nikapata tena hela kilichonisaidia sikuwa na tamaa ya kutumia ela ovyo

Nilipambana sana nikakuza kimtaji changu cha biashara nikawekeza hela yangu kubwa mpaka siku nilipokuta sehemu natunza vitu na bidhaa wamevunja na vitu vimeibiwa vyote. Ile siku nilijiuliza kama Mungu ni wa kila mtu, kuna vitu nilikaribia kufanya kwa msongo niliokuwa nao kuna vishawishi na shida ngumu bila uimara tamaa inakuvua uanaume wako na utu Laura amini nakwambia

Sijui nikusimulie nn niache nn katika yote niliyopitia nikitafuta maisha, kuna sehemu nilianza moja kabisa huku umri unaenda unapata unapoteza

mwisho wa siku nilirudi nyumbani nikiwa sina kikubwa walau nilikuwa na kiasi mkononi, nikakuta kaka yangu mgonjwa alishafariki, mdogo wangu mmoja naye alifariki akijifungua, dada mkubwa alifariki kwa kuugua, mdogo wangu mmoja ni teja na baba amefariki.

Mama kuniona alilala chini akasujudu kushukuru Mungu nimerudi hai ilikuwa kama nimeamsha misiba yote ilotokea nikiwa sipo

sikuwa na hela kubwa sana ila alinipokea hivyo hivyo. Ile hela mama aliniambia tulime na kaka yangu anajua maeneo ya kukodi na yeye ni kibarua eneo flani

Basi niliongea na kaka tukaanza kufanya wote mipango. Tuna miaka kadhaa tunapambana. Leo hii sijafika pakubwa sana ninakotaka lakini angalau naishi maisha yanayoeleweka na nina miradi kadhaa, mama yangu leo angalau huzuni yake imepungua. Ingawa mm naziona kabisa athari za msongo ndani yangu ila napambana nikae sawa

Leo nikipita sehemu nikiona watu wanafanya vibarua nilivyofanya nawapigia saluti kiroho safi. Nawaheshimu sana maana nayaelewa vizuri maumivu yao na dharau wanazoziishi kutoka kwa watu.

Nawapenda Hustlers!!
Much respect. 👊🏽
 
Back
Top Bottom