BASKETBALL: Ja Morant ndo master mpya wa court kwa sasa

kali linux

JF-Expert Member
May 21, 2017
1,996
5,054
Hello bosses and roses.

Huyu kijana anachezea Memphis ni hatari, aina yake ya mchezo ni ngumu sana kuiona kwa wachezaji wengine sasa na miaka kadhaa iliopita. Na bado ni kijana mbichi, 23 years.

Jamaa anafanya anachotaka uwanjani, uwezo wake wa kuruka juu ni mkubwa sana.

Last week kwenye mechi yao dhidi ya LA Lakers alidunk mbele ya Lebron James lakini lebron akaweka mabavu kumzuia dogo kitu kilichosababisha ajali moja mbaya sana kwa wote ila sidhan kama kuna majeruhi serious.

Ja anaweza kupenya kati yenu hata kama mnacheza D, anaweza kuwaruka kama vile visiki tu, ana uwezo wa kuzuia magoli kwa kuruka juu na kupangua mpira kabla haujaingia kwenye ring. Ni complete package ya mchezaji.

Mimi ni die hard fan wa LA Lakers lakini mechi zao walizocheza hivi karibuni against Memphis utaona uwezo wa Ja Morant sio wa kawaida, hasa ukiangalia anacheza against legends kama Lebron na AD.

Na ndo maana namuita 'The New Master of Court'. Naombea siku moja jamaa asainiwe LA Lakers.

Japo watu wengi wanam-critisize kwamba anafanya risky moves nyingi sana na ataishia kupata majeraha ya kumzuia kuendelea na game kwa muda mrefu lakini mimi namuona kama hungry, ambitious & calculated, sababu risky moves zake zote almost 80% zinatoa result nzuri. Na siku zote wanasema 'Never underestimate the struggle of an ambitious and hungry kid'. Namuona mbali sana Ja, atavunja records za hawa legends kwa miaka ijayo
 
Back
Top Bottom