Barua ya Papii Kocha kwa JK

We bado hadi leo unaamini kwamba jamii fulani ndiyo hodari kwa kitu au jambo fulani?

Hujaniellewa,,,, siamini kama kuna huo uchawi na sijawahi kisikia watu wakifanya hivo. ni comment yako ndo imeelezea hayo.
 
Hujaniellewa,,,, siamini kama kuna huo uchawi na sijawahi kisikia watu wakifanya hivo. ni comment yako ndo imeelezea hayo.
Na mimi hoja yangu ni kwamba, wengi wanaona haiingii akilini kwa kitu kama hicho kufanywa na mzazi akishirikiana na watoto wake!! Yaani, kama zile tuhuma ingekuwa ni za mzee peke yake, au Papii peke yake; kuna wengine labda wangeamini lakini wanapata taabu kuamini kusikia ulikuwa ni "mtungo" wa baba na wanae! Kutokana na hilo, ndio maana nikasema ikiwa watu kwenye imani zao za kishirikina wanafikia kulala na mama zao wazazi, sasa kuna lipi la ajabu mtu kushiriki mtungo na wanae? Lipi gumu? Kupiga mother au kupiga mtungo kwa kushirikiana na watoto wako? So, binafsi naamini kwamba katika hali ya kawaida, haiingii akilini mtu mzima kushiriki mtungo na wanae lakini linapokuja suala la ushirikika, yawezekana!
 
mwache afungwe huyu jamaa wangapi wamefungwa na hawaandiki barua kwa Rais kaonewa peke yake sasa si aandika kwaniaba ya wafungwa wote walioonewa!! acha afungwe mwache akae huko,wapo wengi tu lkn hapa huyo babu seya utafikiri taifa bila yeye halitoenda mkata viuno tu yule .
 
Mangi na penda kukupa pongezi sana kwa maelezo yako mafupi lakini yenye maana sana, ukweli kuwa wengi humu ndani wanakurupuka tuu kuhukumu watu bila sababu za msingi.

Lakini Tanzania kila jambo lina wezekana kwani siku mbili tumesikia Lema alivyo shinda kesi hivyo sina imani sana na watoa hukumu kwani hoja iliyo mfanya lema ashinde ilikuwa ndogo sana hata mimi ningeweza kuona kuwa hakupaswa kuvuliwa ubunge wake.

Ila ndio ilivyo tokea, turudi kwenye kesi ya Nguza na vijana wake, kuna wale wawili waliwekwa ndani pia kwa hukumu hiyo hiyo ila ilipo kwenda huku na kule ikaonekana hawakuhusika ni mahakama hizi hizi za tanzania zilifanya jambo hili. ukweli ni kwamba ningekuwa ni wale watoto ningeweza kufunga mashitaka kwa walio nizushia na kwa serekali pia kunifunga bila kosa.

Hivyo na imani kuwa hawa jamaa wameonewa sana hivyo kijana kama ameandika barua hiyo hakuna haja ya kumshambulia amesha sema mara nyingi hakuhusika sifahamu hao wanaotaka kwanza akiri kama alifanya au hakufanya wanataka kujua nini?

Ukiambiwa udhibitishe Kwa kucngziwa kwao utaweza?acha kubeba story za mtaani na kujifanya we ndiye ulikuwepo wakati wanacngiziwa kesi.akili yako changanya na ya kuambiwa
 
Raisi mwenyewe anaitaji msamaha kutoka mbinguni
sijui nani amsamhe mwenzake
 
Walisingiziwa? Ushahidi wa picha mpaka za video ulitolewa mahakamani, walikuwa wanawala na kuwalawiti watoto wadogo wa shule za msingi. Hao ilikuwa wauliwe tu. Si wakuhurumiwa hata kidogo, fikiria wale watoto sasa hivi wanaojiita hizi nyuzi na waneshakuwa watu wazima. Roho zao zinawauma vipi wakikumbuka unyama waliofanyiwa kwa kudanganywa kwa chipsi na biskuti!

Kweli wewe Zombi, unahasira...
 
Na mimi hoja yangu ni kwamba, wengi wanaona haiingii akilini kwa kitu kama hicho kufanywa na mzazi akishirikiana na watoto wake!! Yaani, kama zile tuhuma ingekuwa ni za mzee peke yake, au Papii peke yake; kuna wengine labda wangeamini lakini wanapata taabu kuamini kusikia ulikuwa ni "mtungo" wa baba na wanae! Kutokana na hilo, ndio maana nikasema ikiwa watu kwenye imani zao za kishirikina wanafikia kulala na mama zao wazazi, sasa kuna lipi la ajabu mtu kushiriki mtungo na wanae? Lipi gumu? Kupiga mother au kupiga mtungo kwa kushirikiana na watoto wako? So, binafsi naamini kwamba katika hali ya kawaida, haiingii akilini mtu mzima kushiriki mtungo na wanae lakini linapokuja suala la ushirikika, yawezekana!

Tatzo la watz tunaamini sana story za vijiweni..tubadilike jamani.mtu utaombaje msamaha bila kosa?
 
kumbukumbu zangu ni kwamba vile vitoto vilihojiwa na mEDIA MBALIMBALI (ITV Ikiwamo) japo havikuoneshwa nyuso zao,na jinsi vilivyokua vinaelezea kama ni maigizo they deserve ''ACADEMY AWARD NOMINATION''

Angefanyiwa mtu anaekuhusu Kwa karibu Ndio ungempa hyo tuzo maana ungeelewa vema Kua anaugiza
 
Wairejee vipi wakati rufani walikata na ikasikilizwa lakini bado ikaonekana wana hatia kasoro dogo mmoja ambae ilikuja kuthibitika kwamba wakati yale yanatokea yeye alikuwa yupo mkoa....huyu aliachia lakini wengine wote wakaonekana wana hatia....!! Tena hata Mabere Marando ambae alikuwa ni Wakili wao aliwahi kuhojiwa kama yule dogo anaweza kudai fidia; nae akajibu "ili mradi yupo huru, hayo mengine aachane nayo" na wala hakuonesha kutoridhishwa na hukumu!

Wambie,maana kulalamika kwingi ila hawafatilii mambo.mahakama ya rufaa haiwezi Kufanya upuuzi huo
 
BARUA YA PAPII KOCHA
KWA RAIS
JAKAYA KIKWETE... KWA
WALE
AMBAO HAMJAISOMA HÍI
HAPA.

MF/NA: 836'04
Johnson Nguza
(Papii Kocha)
Gereza Kuu Ukonga
S.L.P 9091
Dar es Salaam
Mh. Rais Jamuhuri ya
Muungano
Tanzania
YAH: MAOMBI YA
KUPEWA MSAADA
(MSAMAHA) WA
KUFUTIWA ADHABU
YA KIFUNGO NILIYOPEWA
NA
MAHAKAMA YA HAKIMU
MKAZI
KISUTU.

Husika na somo hilo hapo
juu.

Mimi ni mfungwa katika
gereza
kuu Ukonga. Kwa heshma
na
taadhima na kwa
kutambua utu
na huruma yako ya
kiMUNGU
ulionayo dhidi ya
binadamu
wenzako pamoja na
mamlaka
uliokabidhiwa na Jamuhuri
ya
Muungano wa Tanzania.
Naanguka na kushika
miguu yako
mitukufu muheshimiwa
rais.
Nakuomba msaada
(msamaha)
kwako muheshimiwa
rais, kwa
njia hii ya maandishi
kusudi
niweze kuondolewa
adhabu ya
kifungo cha maisha
gerezani,niliyohukumiwa
na
mahakama tajwa hapo
juu.
Mh.Rais mimi
nimefungwa nikiwa
bado kijana mwenye umri
mdogo,
na ukweli kutoka moyoni
sikufanya kosa hilo. Si
mimi, baba
yangu Nguza wala ndugu
yangu
yeyote aliyefanya
kitendo kile.
Lakini wenye mamlaka
wakatuona tuna hatia na
kuamua
kuteketeza kizazi chetu
gerezani.
Natamani kiama ifike ili
mwenyezi
Mungu aweke wazi
ukweli wote
uliojificha nyuma ya pazia.
Mpaka
sasa natambua wazi
hatima
pamoja na dhamana ya
maisha
yangu ipo katika mikono
yako
mitukufu Mh. Rais
Naomba huruma yako
muheshimiwa Rais
maana mimi ni
mtoto wako ninaehitaji
huruma
yako wewe mzazi. Lakini
pia sisi
ni binadamu wenye nafsi
na miili
kama wengine.
Waliotumia mamlaka yao
kutuweka gerezani nao ni
binadamu pia, wenye miili
na
nafsi. Ipo siku nafsi zetu
zitapaswa kutoa hesabu
ya
tuliyoyafanya hapa
duniani.
wakati huo miili yetu
tunayoitumia
kunyanyasa
wanyonge itakuwa
imeoza
mavumbini.
Natumaini kauli yako ya
mwisho
ndio itakayoleta pumzi ya
uhai
nafsini mwangu.
Nakutakia kazi
njema, afya njema na
maisha
marefu.
Mungu akubariki.
Wako mtiifu
Mfungwa NO:836'04
JOHNSON
NGUZA (PAPII KOCHA)
 
Kati ya hukumu za hovyo duniani na muendekezo wa madaraka ya kipumbavu,hukumu hii haikosi kwenye top 5!!

Nasubiri barua ya yule jamaa wa BoT aliefungwa,akampgia simu prezidaa wa wasafi na wanyuka suti akiwa gerezani kumuomba msamaha huku mtoto wake wa kike nae akikamatwa kwa kesi ya sembe!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom