BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,377
- 8,121
Ndugu Rais, naamini una uzima wa kutosha asubuhi ya leo. Ukiiangalia video hii kwa haraka haraka utawaona “wahuni” na “watu wasiokuwa na maadili” wakifanya biashara ya “ukahaba.” Lakini ukiangalia kwa umakini, hautowaona wahuni, utaona kundi kubwa la watanzania maskini wanaoishi maisha ya tabu na mateso. Ukiangalia kwa umakini zaidi, utawaona wapiga kura wako ambao umaskini umewalazimisha leo waonekane kama wadhambi kuliko watanzania wote.
Mhe. Rais, kinachofanywa na Mkuu wa Mkoa hapa wala sio kukamata “makahaba” na “kufungia madanguro,” kinachofanyika ni kumdhalilisha maskini kwa sababu ya umaskini wake. Nasema hivi kwa sababu wenzao wanaofanyia “ukahaba” kwenye guest houses za elfu thelathini kule Sinza kuhudumia wateja wa tabaka la kati au wale wanaofanyia kwenye mahoteli yaliyopo ufukweni wakihudumia wateja wa tabaka la wenye nacho, wao hawabughudhiwi. Kwa hiyo hawa kwenye video wanaadhibiwa kwa sababu umaskini wao unaonekana wazi na unawakera viongozi.
Mhe. Rais, usinielewe vibaya. Sipingi kinachofanywa na Mhe. Mkuu wa Mkoa, ila najiuliza, kwa nini viongozi mnakerwa na muonekano wa maisha ya watu wenu lakini hamkerwi na mambo yanayosababisha hawa watu waishi maisha haya? Kwa mujibu wa taasisi ya UNAIDS, Tanzania kuna zaidi ya wanawake 150,000 wanaojihusisha na biashara ya ukahaba. Wametoka wapi wote hawa? Wala usiumize kichwa sana Mhe. Rais, nitakukumbusha. Hawa ndio wale vijana waliomaliza kidato cha nne wakarudi nyumbani bila maarifa yoyote yenye tija. Ndio wale ambao NECTA wanasemaga “asilimia 75% wamepata Division Four na Zero.” Wengine ndio wale waliomaliza vyuo vikuu wakakosa ajira na elimu waliyopewa haijawaandaa kujiajiri, waende wapi? Walio pambana sana ndio wale wamekuwa waendesha bodaboda na wengine mama ntilie, hizo ndio zimekuwa kazi za ndoto zao.
Mhe. Rais, kama hawa wangeweza kupewa mafunzo mbadala, kukuzwa na kuendeleza vipaji vyao, na kukopeshwa mitaji, labda leo wasingekuwa wanatweza utu wao kwa kiwango hiki. Hata hivyo zile fedha za kufanyia haya ndio serikali yako imeamua iwanunulie viongozi magari ya kifahari; iwaongezee wabunge mishahara kimono; na hivi karibuni itawagawia wake wa viongozi ambao tayari wanaogelea kwenye utajiri. Fedha nyingine ndio zile zimepigwa kwa mabilioni kwenye report ya kamati ya kudumu ya bunge hesabu za serikali (PAC). Hizi ndio fedha zinazotumika kutengeneza wale vijana mashuhuri unaowaona kule Israel, Singapore, China, Finland, etc. Hawana uchawi wowote Mhe. Rais, wameamua kujali tu.
Nihitimishe Mhe. Rais, hawa maskini ambao leo wanasambazwa kwenye media kama object of mockery kwa taifa hawakuchagua kufanya haya. Nikuone basi, tunapoenda kuwanyanyasa kwa umaskini wao, basi angalau hata tuwatunzie utu wao kwa kuficha sura zao. Kuwapa adhabu ya public shame juu ya mzigo wa umaskini wanaoubeba ni sawa na kuwaua angali bado wapo hai. Na la mwisho, Mhe. Rais, ikikupendeza, basi mwambie mkuu wa Mkoa anapowaambia waondoke na waache kufanya wanachokifanya, basi awaambie pia waende wapi na wakafanye nini kama mbadala wa hiki.
Nakushuru sana kwa muda wako.
Wako
Onesmo Mushi