Barua ya Papii Kocha kwa JK

watanzania wanafiki sana,mnaacha kuwaonea huruma ndugu zetu wanaosubiri kunyogwa huko china mnawaonea huruma hawa wabakaji!

alikubaka wewe nin?mbna una hasira?
hao waosubir kunyongwa China ni wauza sembe wenzio wabaya zaidi ya wabakaji pimbi wewe
 
Wakulu nimeiona hii ikizagaa za gaa kule kwa JayDee, naona kama watu wameogopa kuileta huku kwa haraka kama wafanyavyo kwa zengine. Labda kwa sababu ya history.

Hapa ni kwake mahara muafaka kwani ninaamini watu wengi wanasoma
JF (nadhani) hata mushemiwa rais.

Pia (siku moja kwenye taarifa ya habari ya TBC niliona akisoma habari furani kwenye page ya jf wakisisitiza habari kutoka kwenye chombo cha habari).

Sasa muheshimiwa kabla haijaja rasmi mezani kwako hii hapa barua.

Kuleta barua hiyo hapa jf mmekosea Rais ana ongoza nchi kwa sheria( not pressure groups)
 
Imekuaje mchungaji abake (mwanawe) kafungwa miaka kadhaa papii anaesemwa kabaka kifungo cha maisha!!!
CHEZO HILO
 
Hivi wale waliobakwa na kutoa ushahidi sasa wako wapi? Embu fanyeni upelelezi wenu muonee.... wanaoua maalbino wao vipi mbona sio kama Papii na Mzee Nguza? MIMI JMN NIKO NJIA PANDA ktk hii hukumu. But yupo MUNGU msemaji wa mwisho siku moja tutajuwa.
 
Wangapi mnaikumbuka barua ya Papii Kocha aliyoiandika kwa Rais Kikwete mwaka 2013 kuomba msamaha? Nakumbuka kaka Evarist Chahali aliichukua barua hii na kuiwasilisha kwa Waziri Lazaro Nyalandu aliyeahidi kuifikisha kwa Rais Kikwete. Kuanzia hapo sijui nini kiliendelea. Labda Chahali anaweza kutueleza what happened. Rais alijibu ile barua au aliipuuza?

Nimekumbuka barua hiyo kwa sababu June 25 mwaka huu, Papii Kocha na baba yake Nguza Vicking walitimiza miaka 12 gerezani. Nimeikumbuka barua hiyo kwa sababu kumekuwepo na sintofahamu nyingi kuhusu kesi hii. Nimeikumbuka barua hiyo kwa sababu baadhi ya watu wanaamini familia ya Babu Seya ilionewa. Nimeikumbuka barua hiyo kwa sababu inadaiwa kuna watoto waliowahi kukiri kwamba walifundishwa kutoa ushahidi wa uongo mahakamani.

Anyway mimi sio Hakimu, shahidi sala wakili wa kesi hii, lakini leo nimeipitia upya barua ya Papii Kocha na ikanigusa sana. Nimeipitia nikaona kama ni ya jana japo iliandikwa miaka mitatu iliyopita. Hebu na wewe isome tena:
____________________________________________________

Mfungwa NO:836'04
Gereza Ukonga,
S.L.P 9091
Dar es Salaam,

Mh.Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania,

YAH: MAOMBI YA KUPEWA MSAADA (MSAMAHA) WA KUFUTIWA ADHABU YA KIFUNGO NILIYOPEWA NA MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI KISUTU.

Husika na somo hilo hapo juu.
Mimi ni mfungwa katika gereza kuu la Ukonga. Kwa heshma na taadhima na kwa kutambua utu na huruma yako ya ki-MUNGU ulionayo dhidi ya binadamu wenzako pamoja na mamlaka uliokabidhiwa na Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Naanguka na kushika miguu yako mitukufu muheshimiwa rais.

Nakuomba msaada (msamaha) kwako muheshimiwa rais, kwa njia hii ya maandishi kusudi niweze kuondolewa adhabu ya kifungo cha maisha gerezani,niliyohukumiwa na mahakama tajwa hapo juu.

Mh.Rais mimi nimefungwa nikiwa bado kijana mwenye umri mdogo, na ukweli kutoka moyoni sikufanya kosa hilo. Si mimi, baba yangu Nguza wala ndugu yangu yeyote aliyefanya kitendo kile. Lakini wenye mamlaka wakatuona tuna hatia na kuamua kuteketeza kizazi chetu gerezani.

Natamani kiama ifike ili mwenyezi Mungu aweke wazi ukweli wote uliojificha nyuma ya pazia. Mpaka sasa natambua wazi hatima pamoja na dhamana ya maisha yangu ipo katika mikono yako mitukufu Mh. Rais Naomba huruma yako muheshimiwa Rais maana mimi ni mtoto wako ninaehitaji huruma yako wewe mzazi.

Lakini pia sisi ni binadamu wenye nafsi na miili kama wengine. Waliotumia mamlaka yao kutuweka gerezani nao ni binadamu pia, wenye miili na nafsi. Ipo siku nafsi zetu zitapaswa kutoa hesabu ya tuliyoyafanya hapa duniani. wakati huo miili yetu tunayoitumia
kunyanyasa wanyonge itakuwa imeoza mavumbini.

Natumaini kauli yako ya mwisho ndio itakayoleta pumzi ya uhai nafsini mwangu. Nakutakia kazi njema, afya njema na maisha marefu.

Mungu akubariki.

Wako mtiifu
Mfungwa NO:836'04
JOHNSON NGUZA (PAPII KOCHA)

[HASHTAG]#MyTake[/HASHTAG]:
Kama barua hii haikumfikia JK naomba Chahali afanye mpango imfikie JPM. Inaonekana kuna mengi tusiyoyajua nyuma ya pazia. Inawezekana wanaokwenda jela sio wote wana hatia. Hakimu wa haki anabaki kuwa MUNGU peke yake. Brother Chahali plz work on it the way u did last time na Mungu atakubariki.!
 
Kuna watu wanaishi kwenye hii dunia kana kwamba hawajui kama ipo siku nao watakufa! Mtu anafungwa bila hata kuwa na hatia!
 
:mwana wa adamu alikuja kufa msalabani ili tuokolewe dhidi ya dhambi waliyoifanya Adam na Hawa,
Yesu alituonea huruma,hivyo nasi twapaswa kuhurumiana,mi naona huyo bwana mdogo akitoka itakua baraka kwa mtoa msamaha:
 
Kumbe aliomba msamaha lakini hakupewa kipindi hicho. Nadhani wakati huo ilikuwa ni mapema sana! Si ajabu JK amemkumbushia JPM ya barua hii na kusema nadhani sasa inatosha na ni muda muafaka! Ni mawazo Yangu tu!
 
Mbona kwenye hyo Barua hawajakiri kama walitenda kosa wanaishia kuomba msamaha tu

Ova
 
Usirithi adui, jitengenezee adui yako. Uadui sio mzuri tuishi kwa amani na watu wote
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom