Barua toka kwa.....

Magulumangu

JF-Expert Member
Jan 7, 2010
3,047
455
Dear Magulu....
Najua utakuwa unajiuliza maswali mengi kuhusu mimi kuondoka bila kuaga....Nimeamua kufanya hivyo ili kukupa nafasi ya kuweza kusonga mbele na mipango yako. Magulu najua nimechelewa kufanya hivi kwani nimekufanya uamini mengi na kuniweka kila katika mpango wako bila kujua nini mimi nawaza...
Kwanza naomba unisamehe kutokana na mengi mabaya nilokufanyia na visa vya bila wewe kujua, Magulu ulikuwa na utabaki kuwa mutu muhimu sana katika maisha yangu, nitakukumbuka kwa mengi mazuri na machache sana mabaya ulonifanyia kipindi nikiwa na wewe...Ulijua jinsi ya kupatia ufumbuzi kila kuwapo na tatizo, pasipo kujali nani mwenye makosa ulikuwa wa kwanza kuomba msamaha, hukuwa na papala kuwapo tatizo hata kama lipo juu ya uwezo wako ulijaribu kulitatua na kulitolea mbandala.
Magulu, nilifanya juu chini kukatisha uhusiano wetu lakini nilichelewa, unakumbuka rafiki yangu Monica alipokutaka na ukamkatalia hata kuweza kumkalisha kitako na kumweleza jinsi utakavyoniumiza pindi nikijua unauhusiano na rafiki yangu? Nisamehe kwa hilo magulu maana nilidhani utamkubalia hivyo kukuwezesha kuendelea bila mimi pindi mtego wangu ungefanikiwa...
Nakumbuka siku uliponitongoza Magulu, siku uliponishika mkono na kuniongoza baharini, ukashika kichwa changu ukiwa kwa nyuma na kunionyesha jua linakotokea, uliniambia nitazame mahali Mbingu inapokutana na bahari, ulinambia jinsi unavotamani kuwa kama maji,"Maji kila siku hupata suluhisho yahitajipo njia", kwangu umekuwa maji Magulu....
Umenifanya nijue nini maana ya mwanamke na umuhimu wa mwanamke hapa Duniani, umenifanya nijue jinsi ya kupambana na maisha na kujali wengine bila kuangalia kipato cha mtu wala familia atokayo....
Magulu, umenifundisha kupenda kwa gharama zote, umenifundisha nini maana ya mapenzi na jinsi ya kuyaenzi mapenzi, nilijifunza mengi kutoka kwako magulu, ulijua jinsi ya kuniita niwapo na mawazo na kunifanya nifurahi nisikiapo sauti yako, ulijua jinsi ya kunibembeleza na kunifanya nisahau mimi ni nani na nini natakiwa kufanya juu yako, lakini ulisahau kunifundisha jinsi ya kuishi bila wewe, ulisahau kunifundisha mara niondokapo usiumie maana hukupenda niumie......
Magulu, niahidi kitu kimoja kama ulivyokuwa unaniahidi tukiwa wote, najua si muda mrefu naweza kuwa mbali na wewe daima, Magulu mie ni mwasirika ndo maana sikutaka kufanya na wewe mapenzi mpaka imefikia sina sababu tena kukunyima wewe......
Magulu nitakupenda mpaka mwisho wa maisha yangu na naomba siku nikiaga dunia njoo nibusu na nambie neno moja tu...
Utanipenda hata baada ya Kifo....
ni mimi
Janneti......
 
Weka jina la mwandishi ujumbe ni mzito anahitaji SHUKURANI ZETU.


Mkuu lipo chini ni Janneti msichana nilompenda tukatenganishwa masomo baadae tukaja kukutana tena......Hiyo ni moja ya barua mbili baada ya yeye kuondoka, ni miaka kumi sasa ila ninzo hizo barua....ya pili nitaiweka soon....
 
Mkuu lipo chini ni Janneti msichana nilompenda tukatenganishwa masomo baadae tukaja kukutana tena......Hiyo ni moja ya barua mbili baada ya yeye kuondoka, ni miaka kumi sasa ila ninzo hizo barua....ya pili nitaiweka soon....
Kama kweli uliandikiwa wewe samahani,usioe mwanamke janeti anakusubiri huko mbele ya safari USIMSALITI !
 
Duh! Mkuu, kwa ukweli imenigusa sana hii stori, naamini Janet alikuwa muaminifu sana hakupenda kukuweka matatizoni. Ingekuwa vizuri kama ungetupa full story ilikuaje mpaka hayo yakamkuta Janet maana inaonekana kuna kubwa umetuficha juu yake. Pole sana mkuu.
 
Duh! Mkuu, kwa ukweli imenigusa sana hii stori, naamini Janet alikuwa muaminifu sana hakupenda kukuweka matatizoni. Ingekuwa vizuri kama ungetupa full story ilikuaje mpaka hayo yakamkuta Janet maana inaonekana kuna kubwa umetuficha juu yake. Pole sana mkuu.


mkuu uko sawa kweli ni story ndefu lkn ipo siku hapa JF nitailweka maana nilimjua toka watoto, shule ikatutenganisha, tukaja kutana wakubwa wote after school with all our promises.....
 
Sio kweli ingekuwa hivyo ungejuwa hapendi jina lake lifupishwe hivyo kwakuwa lina maana tofauti kabisa lol!

hahahha mkuu unakomelea tu, muache BJ wangu alale jana nimeongea nae sana tu kwa simu, anakupa hi sana anauliza ile zawadi yake mbona hujamtumia tena?
 
I always hate people who create HI virus 4 their own benefit,my God give them a nice reward!
 
as a scientist u are not deemed to think that way broda! well,it has had its benefit, who knowa maybe overpopulation ingelemea dunia! tunavyopenda kujamiiana siku hizi bila hiv si mimba zingekutana mwilini?
I always hate people who create HI virus 4 their own benefit,my God give them a nice reward!
 
Oooh...Magulu, pole sana Mangi..
at least Jannet alikupenda kwa dhati...alikupenda akakulinda!
Ninapatwa na hofu nikifikiria Jannets wa siku hizi...si atasema tufe wote tu!??
mh...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom