Mke wangu amepata changamoto ya kupumua na sauti haitoki punde baada ya kujifungua

Rurakha

Senior Member
Oct 20, 2019
121
209
Habari za leo

Ninaomba ushauri kutokana na changamoto inaomkabili mke wangu leo siku ya 11 tangu ajifungue tarehe 5 February 2024.

Ilikuwa hivi mke wangu alikua na changamoto ya uchache wa damu wakati anajifungua hivyo ikapelelea akaongezewa damu.

Baadae akaruhusiwa na kuna dawa tumepewa sasa changamoto anaopata mke wangu anapumua kwa shida sana, Mbavu zinabana, na anakohoa kikohozi kizito mpaka napata hofu na sauti haitoki.

Hali inazidi kuwa mbaya tumeona kesho tumrejeshe hospital

Wadau naomba kama kuna mtu anauzoefu na changamoto kama yangu anisaidie walau ushaurin

MREJESHO
Nilifuata ushauri wa wadau nilimpeleka mke wangu hospital ya Rufaa ya Mwananyamala walimpokea na kisha walimpima alionekana ana changamoto ya TB ambayo ilikua imeathiri mapafu hivyo mpaka leo ni siku ya 5 mke wangu Kipenzi yupo ICU anatumia Machine kupumua lakini tayari kaishaanza kutumia Dozi ya TB

Naomba mniombee ndugu zangu napitia kipindi kiugm sana
 
Rudisha hospital haraka sana. Usisubiri ifike kesho

Narudia tena mpeleke mkeo hospital sasa hivi.. tena mpeleke hospital kubwa yenye vipimo vyote. Usimpeleke zahanati za kuunga unga

Hiyo ni serious case.

Mtu sauti ikiwa inakata na changamoto ya kupumua maana yake ni muscle weakness. Hiyo dalili sio nzuri

Usije ukazika mtu kama utani


Nakupa facts Binadamu yoyote akikaribia kufa kauli huwa inakata na anapata changamoto ya kupumua
 
Back
Top Bottom