Barua: Kutoka kwa Mwalimu wa Shule ya Msingi kwenda kwa Rais wa JMT

Mwalimu Mwambije pole sana ni imani yangu kale ka falsafa ka FUKU (Fundisha Kadri Ulipwavyo) kataendelea kutesa taifa hili endapo maoni na uchambuzi wako havitazingatiwa kwa uzito wake...Umepresent vizuri sana Mwl wangu kazi kwa mwenye kuchanganya na za kwake kuamua
 
Japo barua imechelewa kufika hapa takribani wiki mbili lakini hakijaharibika kitu, mwalim huyu anaomba yeyote atakayeweza amsaidie kuifikisha hii barua katika meza ya mheshimiwa rais na itakuwa vizuri zaidi kama rais atakabidhiwa hii barua mkononi mwake!

BARUA YANGU KWA RAIS
(Serious).
Habari yako mheshimiwa Rais? Kwanza kabisa heshima yako, shikamoo na Pole sana na kazi za kulitumikia Taifa letu.
Mimi ni mwalimu wa shule ya msingi Matakapola, iliopo Ilala hapa Dar.

Haina aja ya utambulisho sana, naomba niende kwenye dhumuni la hii barua. (Ila ombi, naomba hii barua usome wewe mwenyewe Rais, kama kuna servant anakusomeaga, aishie hapa. Aiweke store siku ukiwa na muda wa ziada wewe ndio isome taratibu. Tafadhali sana).

Ijumaa iliopita mshahara wangu uliingia kwenye account yangu. Asante sana ingawa ni jasho langu.

Basi yafuatayo ni matumizi yangu yangu tokea Ijumaa hadi leo:

1. Kodi ya chumba (miezi 3)- Tsh 60,000, bili ya maji mwezi huu Tsh. 4,000 na ya umeme Tsh. 5,000

2. Chakula cha akiba kwa huu mwezi (Unga 10kg, Mchele 10kg, Maharage 5kg, Mafuta 2lts)-Tsh 42,000.

3. Mazaga zaga (Mazagazaga ni vitu vidogo vidogo ila vya muhimu sana) ya jikoni kama majani ya chai, chumvi, mkaa, kiberiti, mafuta ya taa-Tsh.10,000

4. Mwalimu usafi, imebidi nipitie mitumbani (huku ni sehemu unakoweza pata kitu cha bei kubwa kwa bei nafuu) nipate nguo za kubadilisha, maana hizi wanafunzi wamenizoea nazo. Hapa nili spend kama Tsh.15,000 na nkazipeleka kwa fundi kuzirekebisha (Efect (Madhara) mojawapo ya nguo za mitumbani ni kawaida kua oversize, ombea isiwe undersize, na ukishanunua hakuna guarantee wala kurudisha) hapa nkatumia tena Tsh 5,000.
Pia nikaenda duka la vipodozi kudaka body spray (Tsh.5000), Mafuta ya BabyCare (Tsh.1000).

5. Wazazi wangu wameteseka sana kunisomesha, hivyo fadhila muhimu kuwarudishia kwa hiki hiki kidogo nipatacho.
Nika wa M-Pesa Tsh.40,000 ili watumie kubadilisha mboga juma pili na nusu iwasaidie kumalizia ada ya mdogo wangu Riziki, yupo ile shule uliokuja izindua mwaka 2011/May/13 kijijini kwetu Mwankosi Mbozi Mbeya (au basi, sidhani kama unakumbuka, maana ulituhaidi visima, barabara, madawati shuleni na kujenga bweni la wasichana, ila hadi leo umetuachia manyoya. Umekumbuka? Siku ile Ulivaa tai nyekundu, suti nyeusi na shati la drafti drafti jeupe. Na ulikuja na mama, yeye alivaa full vitenge vya chama! Kumbuka?)

6. Kuna hela ya nauli kwenda na kurudi kila siku shuleni (Tsh.600 per day), vitafunwa asubuhi kila siku (Tsh.200 per day), na vitu visivyo nunulika kwa wingi, maana vitaharibika kama vitunguu, sabuni, nyanya, nazi,karoti, etc nakadilia Tsh.10,000 kwa mwezi.

7. Mheshimiwa kuna vitu havizuiliki kama vocha, nyama wakija wageni, kwenda hospitali, bado kutoka out mara moja moja (Yaani kama wewe unavoendaga Sydney kula mbuzi, na sisi tunaendaga kwa mama Lucy sinza, kula vifaranga).

8. Kuna Hiyo pesa tunaiita hela ya emergence kama michago ya mtaani, sadaka, misiba, kiatu/nguo kwa fundi...etc

Mheshimiwa kama ulisoma vizuri hesabu kama mimi, roughly hapo ni jumla kama Tsh.210,000 nikiongeza na pesa ya hitaji no.7&8 jumla kama Tsh.250,000.

Mheshimiwa kutaja mshahara wangu hapa si vizuri, lakini kwakua mama hapo nyumbani ameshawahi kua mwalimu naomba nikusumbue, ebu muulize walimu grade A, tunaoanza kazi tunalipwaje?

Kumbuka hapa bado niko peke yangu (Single Boy), sina ata mpenzi. Hivi nna ndoto za kuoa kweli ukitizama iko kipato? Nikiwa na mtoto je? Akianza kusoma je?

Nawaza sijui nikakope NMB au FINCA au VICOBA sijui Bay Port au SACCOS?

Yaani sijielewi. Sikushawishi uniongeze mshahara, ninachoomba tu, fananisha kazi yangu na hiyo wanayofanya wabunge "wako" niliowachagua, au ata kazi unayofanya wewe. Ndio, Wewe Mheshimiwa!

Kuna watu wananishauri nianzishe tuition, lakini mimi ni mzalendo wa pili baada ya Nyerere, itakuaje watoto wa maskini? Wasisome? Hapana, this is not fair (Sijui kama umeshawahi waza ili Mh.)

Wengine wamesema nianzishe biashara. Sijui hata pa kupata mtaji, pili sio vizuri maana ntaelekeza nguvu nyingi kwenye biashara kuliko kazi ya kuelimisha ili Taifa, narudia tena mm Mzalendo.

Hawa waliosema niache kazi wapotezee (achana nao).

Ok Mh, naomba nisiongee sana maana unakazi, safari na mambo mengi sana. Nisikuchoshe.

Natumaini ombi langu (Kama umesahau la kuweka hapo matumizi yako ya mshahara) litasikilizwa na kufanyiwa kazi.

Wako katika kujenga, kuelimisha na kuandaa Taifa lijalo
Mwl. G.C. Mwambije

Bora kuwa jobless kuliko kuwa mwalimu kihivyo achana na hiyo kazi mkuu
 
serikali imeahidi kupandisha mishahara ya walimu katika bajeti ya mwaka huu..kutakuwa na ongezeko kubwa sana tuvumilie kidogo
hello! Kwan hamjui kuwa serikali mufilisi ya ccm itapandisha kodi? Walim watarudisha mishahara kupitia kodi.polen walim 2015 tufanye maamuz kuchagua watakao tujali.
 
Mwalimu Mwambije pole sana ni imani yangu kale ka falsafa ka FUKU (Fundisha Kadri Ulipwavyo) kataendelea kutesa taifa hili endapo maoni na uchambuzi wako havitazingatiwa kwa uzito wake...Umepresent vizuri sana Mwl wangu kazi kwa mwenye kuchanganya na za kwake kuamua

:yo: HESHIMA KWAKO.UMENENA.
 
Huyu mwalimu inaonyesha hana watoto. Gharama ni zaidi ya haya. Me nimeondoka nyumbani naosha majicho huku nje kila siku mke wangu mwalimu anani-text, we maisha na watoto yanitesa. Hebu nitumie hela mwenzio.

Hahaaaaaaaaah. Walimu ni jangaa la dunia niliona hata kule Chicago wameandamana.
Kazi sana wakuu serikali iangalie upya maisha yao.

Inatia uchungua afadhali walimu wa vijijini,pamoja na mazingira magum hawana bajeti kubwa.!!
 
Nimecheka kwa namna alivyoiandika but ndio ukweli. It real pains

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Kweli kabisa. tunaomba wa samaria wema waanze kufanya patroo kule aliko okotwa kaka yake na huyo mwalimu G, Dr Olimboka
Hakika maoni yangu tofauti kidogo kwa kuwa ametaja Shule aliko na jina lake hilo hapo Mwl G C Mwambije, msije shangaa mkakuta ameokotwa Mabwepande akiwa hana meno wala kucha.
 
Umeona eeh! Maana hii serikali ya CCM ikiambiwa ukweli tu WANA KUULIMBOKA

Hana cha kupoteza...,maisha yenyewe yako wapi??, labda tu cha kuwaomba wakumbuke ganzi watakapokuwa wanamkibanda.
 
Ndio hivyo bwana,nilikimbia ualimu baada ya kufundisha kwa miaka 2.5,ukitaka kuelewa kuwa walimu waliowengi hawamiliki ATM kadi za bank zao we subiri mwisho wa mwezi ufike,utawaona wanavyohangaika na waliowapa kadi hizo wanawaita kwa jina la LIGONGA,wanafanya hivyo kwa kuwa mishahara yao haikidhi mahitaji yao.
poleni sana walimu wenzangu ndio ilivyo hivyo hakuna ujanja
 
Walimu wanataka wenyewe..mmekumbatia ccm leo mnalia tena..kikulacho kinguoni mwako..we subiri sale za ccm 2015 na nimeskia awamu hii eti watatoa hadi suruali kwa wanaume japo mmeremete...aaaana..mere..anameremeta mwalimu huyu..anameremeta?...anameremeta.
 
Japo barua imechelewa kufika hapa takribani wiki mbili lakini hakijaharibika kitu, mwalim huyu anaomba yeyote atakayeweza amsaidie kuifikisha hii barua katika meza ya mheshimiwa rais na itakuwa vizuri zaidi kama rais atakabidhiwa hii barua mkononi mwake!

BARUA YANGU KWA RAIS
(Serious).
Habari yako mheshimiwa Rais? Kwanza kabisa heshima yako, shikamoo na Pole sana na kazi za kulitumikia Taifa letu.
Mimi ni mwalimu wa shule ya msingi Matakapola, iliopo Ilala hapa Dar.

Haina aja ya utambulisho sana, naomba niende kwenye dhumuni la hii barua. (Ila ombi, naomba hii barua usome wewe mwenyewe Rais, kama kuna servant anakusomeaga, aishie hapa. Aiweke store siku ukiwa na muda wa ziada wewe ndio isome taratibu. Tafadhali sana).

Ijumaa iliopita mshahara wangu uliingia kwenye account yangu. Asante sana ingawa ni jasho langu.

Basi yafuatayo ni matumizi yangu yangu tokea Ijumaa hadi leo:

1. Kodi ya chumba (miezi 3)- Tsh 60,000, bili ya maji mwezi huu Tsh. 4,000 na ya umeme Tsh. 5,000

2. Chakula cha akiba kwa huu mwezi (Unga 10kg, Mchele 10kg, Maharage 5kg, Mafuta 2lts)-Tsh 42,000.

3. Mazaga zaga (Mazagazaga ni vitu vidogo vidogo ila vya muhimu sana) ya jikoni kama majani ya chai, chumvi, mkaa, kiberiti, mafuta ya taa-Tsh.10,000

4. Mwalimu usafi, imebidi nipitie mitumbani (huku ni sehemu unakoweza pata kitu cha bei kubwa kwa bei nafuu) nipate nguo za kubadilisha, maana hizi wanafunzi wamenizoea nazo. Hapa nili spend kama Tsh.15,000 na nkazipeleka kwa fundi kuzirekebisha (Efect (Madhara) mojawapo ya nguo za mitumbani ni kawaida kua oversize, ombea isiwe undersize, na ukishanunua hakuna guarantee wala kurudisha) hapa nkatumia tena Tsh 5,000.
Pia nikaenda duka la vipodozi kudaka body spray (Tsh.5000), Mafuta ya BabyCare (Tsh.1000).

5. Wazazi wangu wameteseka sana kunisomesha, hivyo fadhila muhimu kuwarudishia kwa hiki hiki kidogo nipatacho.
Nika wa M-Pesa Tsh.40,000 ili watumie kubadilisha mboga juma pili na nusu iwasaidie kumalizia ada ya mdogo wangu Riziki, yupo ile shule uliokuja izindua mwaka 2011/May/13 kijijini kwetu Mwankosi Mbozi Mbeya (au basi, sidhani kama unakumbuka, maana ulituhaidi visima, barabara, madawati shuleni na kujenga bweni la wasichana, ila hadi leo umetuachia manyoya. Umekumbuka? Siku ile Ulivaa tai nyekundu, suti nyeusi na shati la drafti drafti jeupe. Na ulikuja na mama, yeye alivaa full vitenge vya chama! Kumbuka?)

6. Kuna hela ya nauli kwenda na kurudi kila siku shuleni (Tsh.600 per day), vitafunwa asubuhi kila siku (Tsh.200 per day), na vitu visivyo nunulika kwa wingi, maana vitaharibika kama vitunguu, sabuni, nyanya, nazi,karoti, etc nakadilia Tsh.10,000 kwa mwezi.

7. Mheshimiwa kuna vitu havizuiliki kama vocha, nyama wakija wageni, kwenda hospitali, bado kutoka out mara moja moja (Yaani kama wewe unavoendaga Sydney kula mbuzi, na sisi tunaendaga kwa mama Lucy sinza, kula vifaranga).

8. Kuna Hiyo pesa tunaiita hela ya emergence kama michago ya mtaani, sadaka, misiba, kiatu/nguo kwa fundi...etc

Mheshimiwa kama ulisoma vizuri hesabu kama mimi, roughly hapo ni jumla kama Tsh.210,000 nikiongeza na pesa ya hitaji no.7&8 jumla kama Tsh.250,000.

Mheshimiwa kutaja mshahara wangu hapa si vizuri, lakini kwakua mama hapo nyumbani ameshawahi kua mwalimu naomba nikusumbue, ebu muulize walimu grade A, tunaoanza kazi tunalipwaje?

Kumbuka hapa bado niko peke yangu (Single Boy), sina ata mpenzi. Hivi nna ndoto za kuoa kweli ukitizama iko kipato? Nikiwa na mtoto je? Akianza kusoma je?

Nawaza sijui nikakope NMB au FINCA au VICOBA sijui Bay Port au SACCOS?

Yaani sijielewi. Sikushawishi uniongeze mshahara, ninachoomba tu, fananisha kazi yangu na hiyo wanayofanya wabunge "wako" niliowachagua, au ata kazi unayofanya wewe. Ndio, Wewe Mheshimiwa!

Kuna watu wananishauri nianzishe tuition, lakini mimi ni mzalendo wa pili baada ya Nyerere, itakuaje watoto wa maskini? Wasisome? Hapana, this is not fair (Sijui kama umeshawahi waza ili Mh.)

Wengine wamesema nianzishe biashara. Sijui hata pa kupata mtaji, pili sio vizuri maana ntaelekeza nguvu nyingi kwenye biashara kuliko kazi ya kuelimisha ili Taifa, narudia tena mm Mzalendo.

Hawa waliosema niache kazi wapotezee (achana nao).

Ok Mh, naomba nisiongee sana maana unakazi, safari na mambo mengi sana. Nisikuchoshe.

Natumaini ombi langu (Kama umesahau la kuweka hapo matumizi yako ya mshahara) litasikilizwa na kufanyiwa kazi.

Wako katika kujenga, kuelimisha na kuandaa Taifa lijalo
Mwl. G.C. Mwambije

mwalimu
umesahau kuwa bado ktk mishahara hiyo unataka kodi ya kichwa,CWT,BIMA ya afya na BIMA ya maisha
 
Back
Top Bottom