Barua: Kutoka kwa Mwalimu wa Shule ya Msingi kwenda kwa Rais wa JMT

..........mawazo kama yako yaliyokufa ni mbolea ya umaskini wetu...........
Barua inazua maswali mengi kama vile kifo cha sokoine. Je ni kweli huyu jamaa ni mwalim anafundisha shule gani na anuani yake kamili ni ipi. Acheni kutudhalilisha walimu kwa kutunga visa na majina ya uongo.Hata hivyo haya ni matatizo ya walimu wa mjini wa voda fasta wenye tamaa ya kuingia kazini na kununua magari kwa mshahara wa walimu. Kalalamikie chama cha walimu ambacho hakimsaidii mwalimu bali kukata makato ya mishahara yetu na kuwekeza katika vitega uchumi. Sisi walimu wa kijijini tunajishughulisha na kilimo, bustani mboga,mboga nk. Tunahitaji kuwa wabunifu siyo kutegemea mshahara kwa mwalimu. Historia haioneshi walimu kulalama ulimwenguni kote kuliwaondolea matatizo binafsi-jitume bwana mdogo badala kulalama-jiendeleze kielimu au tafuta ajira unayofikiri itakulipa.
 
Hakika maoni yangu tofauti kidogo kwa kuwa ametaja Shule aliko na jina lake hilo hapo Mwl G C Mwambije, msije shangaa mkakuta ameokotwa Mabwepande akiwa hana meno wala kucha.
Mpaka ameandika hivyo nadhani amekata tamaa ameamua liwalo na liwe au ameona heri mmoja afe kwa ajili ya wengine.
 
Mpwa wangu, nilishaandika hapa makala moja ngoja niitafute; ok ok hii hapa nimeipata Mpwa https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...uhuda-nilikimbia-ualimu-kuepuka-matatizo.html yaani ni kwamba kuna tisha huko na kingine hawa wafanyakazi wa Halmashauri wananyodo kupita maelezo...nilifika pale na degree yangu nimepigika miaka minne (enzi zile ni fours - education) halafu nakuta kuanzia mtu wa masijala hadi mlinzi wote ni nyodo kumuona afisa elimu kama vile unamuona Mungu...it pains so much
Mpwa Elli njoo huku uone mateso ya walimu!
 
Barua inazua maswali mengi kama vile kifo cha sokoine. Je ni kweli huyu jamaa ni mwalim anafundisha shule gani na anuani yake kamili ni ipi. Acheni kutudhalilisha walimu kwa kutunga visa na majina ya uongo.Hata hivyo haya ni matatizo ya walimu wa mjini wa voda fasta wenye tamaa ya kuingia kazini na kununua magari kwa mshahara wa walimu. Kalalamikie chama cha walimu ambacho hakimsaidii mwalimu bali kukata makato ya mishahara yetu na kuwekeza katika vitega uchumi. Sisi walimu wa kijijini tunajishughulisha na kilimo, bustani mboga,mboga nk. Tunahitaji kuwa wabunifu siyo kutegemea mshahara kwa mwalimu. Historia haioneshi walimu kulalama ulimwenguni kote kuliwaondolea matatizo binafsi-jitume bwana mdogo badala kulalama-jiendeleze kielimu au tafuta ajira unayofikiri itakulipa.
Ndiyo maana watoto wetu wanapata sifuri muda mwingi unatumia kulima bustani au unawatuma wanafunzi kulima badala ya kusoma.
 
Mpwa mimi ni Mwalimu kabisaaaa ila napinga sana ulichokiandika hapa, japo silazimishwi kukubaliana na mawazo yako mimi nakubaliana na mawazo yamleta hoja....Nilipangiwa shule fulani maeneo ya Ikwiriri, shule haina chochote, unafundisha wananfunzi hawajala kitu, hakuna vifaaa, hakuna maabara, hakuna vitabu ukienda huko Wilayani Utete unaishia kudhalilishwa tu, mshahara wangu ulikua Tshs. 374,000/ japo sijawahi kuipata kama ilivyo maana kila siku utakua makato yasiyo na msingi, hata mimi nilishaweka Uzi kama huo, usiome hapa...https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...uhuda-nilikimbia-ualimu-kuepuka-matatizo.html
Barua inazua maswali mengi kama vile kifo cha sokoine. Je ni kweli huyu jamaa ni mwalim anafundisha shule gani na anuani yake kamili ni ipi. Acheni kutudhalilisha walimu kwa kutunga visa na majina ya uongo.Hata hivyo haya ni matatizo ya walimu wa mjini wa voda fasta wenye tamaa ya kuingia kazini na kununua magari kwa mshahara wa walimu. Kalalamikie chama cha walimu ambacho hakimsaidii mwalimu bali kukata makato ya mishahara yetu na kuwekeza katika vitega uchumi. Sisi walimu wa kijijini tunajishughulisha na kilimo, bustani mboga,mboga nk. Tunahitaji kuwa wabunifu siyo kutegemea mshahara kwa mwalimu. Historia haioneshi walimu kulalama ulimwenguni kote kuliwaondolea matatizo binafsi-jitume bwana mdogo badala kulalama-jiendeleze kielimu au tafuta ajira unayofikiri itakulipa.
 
Maisha ni magumu kila mahali hata huku mtaani pia, afadhali ya wewe mwalim ambaye unapata mshahara. Kinachotakiwa ni kufanya kazi kwa bidii, kufikiria hata biashara ndogo ya kukupatia kipato mbadala tofauti na mshahara. Hata wanaolipwa milioni kumi kwa mwezi haziwatoshi nao wanataka waongezewe. Don over spend, don misuse...be economical
Mtumishi wa UMMA awe mfanya bihashara!!!!!!!!! si hajabu watu wanafanya bihashara IKULU!.

ZERO zitazidi kuongezeka!.
 
Mpwa wangu, nilishaandika hapa makala moja ngoja niitafute; ok ok hii hapa nimeipata Mpwa https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...uhuda-nilikimbia-ualimu-kuepuka-matatizo.html yaani ni kwamba kuna tisha huko na kingine hawa wafanyakazi wa Halmashauri wananyodo kupita maelezo...nilifika pale na degree yangu nimepigika miaka minne (enzi zile ni fours - education) halafu nakuta kuanzia mtu wa masijala hadi mlinzi wote ni nyodo kumuona afisa elimu kama vile unamuona Mungu...it pains so much

Mpwa kwa kweli inasikitisha sana! Nina ndugu zangu wako huko mmoja ni dadaangu na mwingine mwanangu, yaaani kama huyo dada toka mimi niko form one late 70's lakini hali yake kwa kweli inakatisha tamaa huyu mwenetu tutamtoa huko tu hakuna njia !
 
Ninaomba tukumbuke kuwa zipo profession ambazo ukifanya kazi za ziada huwezi fanya kazi yako vizuri, zipo profession unaweza fanyakazi hata ukiwa nyumbani, au kwa ratiba yako BUT mwalimu ni lazima awe pale mwanafunzi alipo, Dr lazima awe pale mgonjwa alipo, Askari magereza lazima awe pale mfungwa alipo n.k. Kazi ya mwl lazima ukubali kufanya kazi muda wa ziada kama utakuwa na nia ya kuwasaidia wanafunzi. Ni lazima uandae Azimio, Andalio, notes, uandae exercise, H/W, test na ufanye hayo maswali mwenyewe kwanza ili kujua ugumu wake, usahihishe madaftarin.k. Mwl. kufundisha tution ni uhaini kwa profession. Binafsi nimekuja na mapendekezo ya bajeti ya malipo aliyostahili Mwambije ili aishi na sio awe na maendeleo (mf. kiwanja, nyumba, usafiri n.k)
Bajeti ya Mwl. Mwambije Angalau ilipaswa iwe hivi.
Pango (vyumba 2)
30,000*2
60,000.00
Chakula (With reference to 7500 per day as meal allowance for undergraduate student as per Jully 2011)
7,500*30
225,000.00
Umeme & Maji

30,000.00
Mavazi
60,000.00
60,000.00
Usafi
25,000.00
25,000.00
Relatives(Wazazi, wadogo, michango misiba & harusi (>50000))
100,000.00
100,000.00
Usafiri(Gari 2 kwenda)
400*2*2*30
48,000.00
Sadaka (Zaka(10%) +sadaka nyingine+masikini & wahitaji)

90,000.00
Mawasiliano(Najiunga Yatosha @ siku)
1,500*30
45,000.00
Others(Kumbuka ndo Mwambije anaanza kazi, hana kijiko, godoro, sufuria, kigoda n.k)

100,000.00
TAKE HOME(Take home)

783,000.00

Walimu wanaanzisha tuitions
Madaktari wanafungua Zahanati Binafsi...
Wanasheria wanakua Mawakili...
Ma-engineer nao wana firms zao...
Kosa ni ni kwa Polisi nae kuwa na kituo chake cha Polisi? Hakimu awe na Mahakama yake pia.....kama ile story ya Yule Hakimu kule mkoani???

Changamoto kwa Taifa; kila mtu aanzishe business yake kutokana na ujuzi wake.....
CC: zumbemkuu MANI Paloma saudari Invisible Bujibuji et al
 
Last edited by a moderator:
Hivi mama Kikwete naye si alikuwaga ticha wa zamu?
Najua mkulu anaijua vyema mishahara ya waalimu.
Asijisahau sana na kufikiria kila mwalimu atakuwa Rais kama Nyerere au first lady kama mama Kikwete
Huyu mama kuna siku alikuwa anahutubia mabinti wa shule za sekondari akawaambia, 'ukisoma unaweza kuwa daktari, mhandisi, mke wa rais, n.k'.
 
Kweli Serikali inahitajika iwaongezee walimu mishahara maisha yao ni ya kuunga unga sana
Kweli kabisa mkuu, waache kuwafanya walimu wa kike pool ya kuchukuwa 'viburudisho' pindi wanapofiwa na wake zao. Mwenyekiti na makamu wa chama fulani hii habari inawahusu.
 
wakuu,mbona mada kama hizi akina Ritz,tandaleone,Sumu na vivaraka wengine wa lumumba hawapiti??
 
mwalimu,jiandae kutolewa kucha bila ganzi watasema hii barua imejaa uchochezi!!ohoooo
 
Maisha ni magumu kila mahali hata huku mtaani pia, afadhali ya wewe mwalim ambaye unapata mshahara. Kinachotakiwa ni kufanya kazi kwa bidii, kufikiria hata biashara ndogo ya kukupatia kipato mbadala tofauti na mshahara. Hata wanaolipwa milioni kumi kwa mwezi haziwatoshi nao wanataka waongezewe. Don over spend, don misuse...be economical

Huwezi kulinganisha chai ya mtu anayelipwa 10m na mtu wa laki 2!
Akianzisha hizo biashara ndogondogo atakaa darasani saa ngapi! Ni lazima aibe ule muda wa vipindi aende kariakoo akanunue vitu if at all ameajiri msaidizi wa kuuza hiyo biashara! Kama umesoma barua ya mwalimu hata tuition hataki kufundisha as wenye uwezo wa kulipia tuition ni watoto wa vigogo na wafanyabiashara kwa sie walala hoi tutaweza wapi! Kila siku tunaendelea kujenga daraja la walionacho na wasiokuwa nacho! Wakati wengine wanasinzia huko bungeni kwako wanalipwa 200,000 kwa kikao ambazo ni mshahara wa mwalimu mmoja mwalimu anaambiwa ni marufuku kufanya tuition! Halafu tunaimba SISI WOTE NI SAWA NA AFRICA NI MOJA! Pole sana mwalimu ingawa wewe ndiye uliyeafikisha hapo wabunge walipo leo! Watanznia wengi hawawezi kuwa wazalendo kama wengine wanajigawia keki kubwa wakati wengine wanaambulia punje zinazodondoka mvungu mwa meza! Uzalendo wa kweli huanzia tangu mtoto anapozaliwa! Anenda shule wa gharama ya serekali! Apate matibabu kwa gharama ya serekali!
Sasa hivi kama huna hela mtoto haanzi nursery! Kama huna hela mwanao hapati matibabu! Kama huna hela mkeo hajifungui salama! Then unatakwa watu wawe wazalendo? Mfano Norway! Huna kazi unalipwa nearly 5,000USD! Kwa nini asiwe mzalendo! Lazima akipata kazi alipe kodi ili ajenge nchi yake!
Kuna Nyani wanakaa pale Loduare Gate Ngorongoro! Wamechoka kuona makapu ya vyakula yanapita machoni pao kila uchao! Kwenye magari ya watalii! Sasa wameamua kujichukulia wenyewe kwa nguvu! Wanachukua vyakula vya wenyewe kila wapatapo fursa. Soon Watanzania watachoka kama hawatataka kugawana hiki kidogo tulichonacho kwa faida ya wote. Ingawa Tanzania sio maskini kama wanavyofikiri! Mungu ibariki Tanzania
 
Ofcoz walim wa daraja la 3A mishahara yao ni hafifu sn haivuki 270,000,hua nawaza wanaishi vp kwakweli mjini hapa!...halafu hawana semina,wala vikao vya kupata sitting allowance!!serikali iwaonee huruma kwakweli!
 
Hii Barua ni baada ya nauli kupanda pia? Maana kama nauli ilikuwa bado inabidi kiwango kiongezeke pia.

Ndio maisha ya waalimu haya then tunategemea nini kwenye matokeo ya wnafunzi ikiwa mwalimu anafundisha na mawazo na njaa?
 
Walimu wanaanzisha tuitions
Madaktari wanafungua Zahanati Binafsi...
Wanasheria wanakua Mawakili...
Ma-engineer nao wana firms zao...
Kosa ni ni kwa Polisi nae kuwa na kituo chake cha Polisi? Hakimu awe na Mahakama yake pia.....kama ile story ya Yule Hakimu kule mkoani???

Changamoto kwa Taifa; kila mtu aanzishe business yake kutokana na ujuzi wake.....
CC: zumbemkuu MANI Paloma saudari Invisible Bujibuji et al

Mpwa kila mtu anakula kwa urefu wa kamba yake! Lakini hili la vituo binafsi vya polisi itakuwa balaa !
 
46 Reactions
Reply
Back
Top Bottom