Baraza la wawakilishi Zanzibar latetea matumizi ya bendera ya taifa kwa meli za Iran

Keynez,

..I just dont understand your line of thinking.

..Yaani wa-Tanzania hatuwezi kuamka mpaka tuwekewe vikwazo??

..Na huku kupeperusha bendera yetu kwenye tankers za Iran is our attempt "kuamka" frm ur slumber, or what??

..Huyo Fidel mwenyewe mbona kila siku analilia vikwazo viondolewe?? When did u hear him akisema vikwazo vimemsaidia?

JokaKuu,

Hamna anayependa kuwekewa vikwazo, si Cuba, Zimbabwe, Iran au Tanzania. Ninachosema tu ni kwamba huu mchezo ni mpana na mrefu. Ni muhimu kuangalia mambo kwa tafsiri pana iwezekanavyo hasa ukiwa unaongelea hizi siasa za dunia ili upate picha kamili. Nisingependa kuanza kuorodhesha mambo mbalimbali yanayoshawishi fikra zangu, itanichukua muda mrefu sana kuweza kujieleza kwa ufasaha. Nimeshawahi kuanzisha thread fupi humu miaka ya nyuma ya jinsi gani urafiki wa marekani na Tanzania ni 'machiavellian' (wa ki-hilahila??) kwa pande zote mbili.

Labda kama kuna wapanga sera na mikakati humu wanaweza wakawa wamenisoma vizuri.

Nikiweza kupanga mawazo yangu sawa na kwa ufupi nitajaribu kujielezea vizuri zaidi.
 
Wakati mataifa ya Magharibi yanatishia kuiwekea vikwazo Tanzania kwa kuruhusu usajili ya meli za mafuta za Iran na kutumia bendera ya Taifa, baraza la wawakishi Zanzibar, limesema Zanzibar kama sehemu ya Muungano wa haki ya kusajili meli ya Iran au nchi yoyote ile kwa maslahi ya Wazanzibar na kuwa taarifa na kelele zinazoendelea ni njia ya kutaka kuwakatika tamaa Wazanzibar kujiletea maendeleo.

My take:

Huu ni mwendelezo wa kutaka kuhalalisha kuvunjika kwa muungano.

Hakuna uhusianao wa muungano na swala hili ispokua wazungu wanapenda kutisha tu wanakataa kabisa kusoma alama za nyakati. Inaonekana wengi wameshindwa kuielewa na kuichambua barua hiyo ya marekani kama ni barua kweli na sio vitisho tu. Hebu tujaribu kuitupia macho kidogo.

Ktk jumla ya maneno ya kwenye barua yanasema 'Tanzania must stop' kwahiyo kinachotakiwa ni Tanzania kuacha kama imefanya. Ingawaje haikowazi kwamba hiyo ni amri au ni ombi. Kipengele cha pili ni kile kinachosema 'Tanzania will face threat of sunction or damage its ties with Washington' Hii nayo sio Tanzania tu amby itaathirika na vikwazo hivyo na hadi sasa iliyopo ni dhana tu kitu kwamba kitu fulani kimefanyika kama walivyotumia neno accused. Huwezi kumuadhibu mtu yoyote kwa kutumia dhana.

Kuna maswali mengi ya kujadili ktk hili, kwa mfano je sheria inasemaje kuhusu kusajili meli? Baadae kuna ule wasiwasi wa kua Tanzania kwa kufanya hivyo itakua imesaidia Iran neclear enrichment ambayo Iran wenyewe walishaeleza kwamba nuclear yao ni kwa peaceful purpose.

Kinachotakiwa kufahamika ni kwamba Tanzania ni nchi kamili yenye uhuru kamili hakuna haja ya kuogopa kama inahisi imefanya kitu ambacho hakiko kinyume na sheria let say International law. Ni vyema wakafahamishwa wowote wale kwamba uhusiano mzuri ni muhimu kwa pande zote na kama ikibidi kua uvunjike kwa sababu ya shaka tu, Tanzania nayo haitakua na choice baadae tuone watajibu nini. Tumeshadanganywa sana tokea vita kuu ya pili ya dunia hadi leo Africa haina maendeleo, huu ni wakati wa kujaribu plan mbadala kama vile china badala ya kuogopaogopa ambako hakusaidii chichote.

Waelezwe tu kwamba' We are not aware of such activities taking place, even if that was the case, it was within international law boundaries as far as we are concerned. We ll look into the matter closely and if we believe that something was wrong we will hold responsilities those responsible. We undestand that our ties are important not only for Tanznaian but for both side, however, we don't believe that such ties can be jeopadise by accusation as your letter suggested. Our believes is that it will unwise to reach such conclusion without enough evidences. Until the whole circumstances surrounnding the episode are clear nothing can be justified. By for now.
 
FIFA imekataa kwa nini? Umejiuliza kama hizo sababu za FIFA ndio hizo hizo mashirika mengine ya Kimataifa zimetumia?

Besides, hawajavunja kanuni na taratibu tulizojiwekea. Tanganyika haitumii bendera ikifanya mambo nje ya Muungano na Zanzibar haikulazimika kufanya hivyo

Waziri husika wa Zanzibar amesema anataka Serikali ya Muungano impe idhini, ili ifanye hivyo.

The ball is in Mwakyembe and Pinda's court.

Gaijin,

..Tanganyika haina serikali, na vilevile haina bendera. madaraka ya serikali ya Tanganyika yalikasimiwa kwa serikali ya muungano tangu mwaka 64. Sababu hizo ndizo zinazopelekea Tanganyika kupeperusha bendera ya muungano hata katika mambo yasiyohusu muungano.

..Zanzibar kwa upande wake ilikataa "kumezwa." Zaidi ina serikali yake, mahakama zake, bunge, bendera, wimbo wa taifa etc etc. Kuna mambo machache tu ambayo Zanzibar imeyakasimu kwa serikali ya muungano. Hili suala la kusajili meli halimo kati ya yale masuala ya muungano. Kwa msingi huo Zanzibar inaposajili meli inapaswa kuhakikisha kwamba haitumii bendera ya muungano.

..Nilivyoelewa mimi ni kwamba Waziri wa Zanzibar amesema, serikali yake ina mamlaka ya kusajili meli, na haipaswi kuingiliwa na serikali ya muungano ktk suala hilo. Sasa kama Zanzibar wana mamlaka ya kusajili meli, kwanini wakose mamlaka ya kupeperusha bendera yao? Mbona mnapocheza mpira mashindano ya Kagame hampeperushi bendera ya muungano, badala yake mnapeperusha bendera yenu, na kupiga wimbo wa taifa wa Zanzibar??
 
Sasa ndo wakat muafaka kwa AMERIKA NA ULAYA KUANZA KUTUYUMBISHA,,,,,,, na watatuyumbisha sana maana hao waliojipa madaraka ni dhaifu kama mbu wa jangwani
 
Wakati mataifa ya Magharibi yanatishia kuiwekea vikwazo Tanzania kwa kuruhusu usajili ya meli za mafuta za Iran na kutumia bendera ya Taifa, baraza la wawakishi Zanzibar, limesema Zanzibar kama sehemu ya Muungano wa haki ya kusajili meli ya Iran au nchi yoyote ile kwa maslahi ya Wazanzibar na kuwa taarifa na kelele zinazoendelea ni njia ya kutaka kuwakatika tamaa Wazanzibar kujiletea maendeleo.

My take:

Huu ni mwendelezo wa kutaka kuhalalisha kuvunjika kwa muungano.

Hawa jamaa si wavivu wa mwili tu bali ni wavivu wa kufikiri pia.
 
Wewe kweli bongolala!!

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Nadhani kwa hili Zanzibar walikuwa sahihi.

Ni lazima tukumbuke Zanzibar haina mamlaka kwenye mambo ya kimataifa,hivyo wasingeweza kutumia bendera yao kwenye hili.

Iran ina ubalozi wake hapa nchini,kudhihirisha diplomatic relations na Tanzania!
Haiwezekani adui wa marekani wawe adui wetu!Hii inaondoa sovereignty yetu kama taifa huru.
Na hapa ndipo umuhimu wa kutumia rasilimali zetu za ndani kujiendeleza inaonekana,badala ya kudhalilishwa na misaada!
Mungu ibariki Tanzania.
 
Gaijin,

..Tanganyika haina serikali, na vilevile haina bendera. madaraka ya serikali ya Tanganyika yalikasimiwa kwa serikali ya muungano tangu mwaka 64. Sababu hizo ndizo zinazopelekea Tanganyika kupeperusha bendera ya muungano hata katika mambo yasiyohusu muungano.

How convinient!
 
tungeonyeshwa mkataba tujue tunafaidika vipi na wairan kutumia bendera yetu, isije ikawa wametuletea kontena la juzuu wenyewe wakapige hela na kutuachia mzozo. kwanini hawatumii bendera yao! au iran haina bendera nowadays! huku ndio kumbeba tip tip mabegani. jifunzeni kuitumia historia.
 
Sasa hawa Wazanzibari wanataka kutuingiza kwenye matatizo, si tuvunje tu Muungano na wao? kwi kwi kwi teh teh teh!

Moja kati ya sababu za kuuanzisha Muungano wetu ilikuwa ni suala la kiusalama, Lakini kwa hili naona kama wazanzibar wanakwenda kinyume kwa lengo la kutimiza matakwa yao. Something has to be done katika mchakato wa kukusanya maoni ya katiba kwani naona ni suluhisho pekee kwa hivi karibuni, Kundi la usuluhishi wa kero za Muungano limeshindwa kabisa kuweka mambo sawa kwani katika kero zaidi ya kumi za kimuungano wamefanikiwa kuzitatua mbili tu katika vikao lukuki walivyokaa
 
Wakati mataifa ya Magharibi yanatishia kuiwekea vikwazo Tanzania kwa kuruhusu usajili ya meli za mafuta za Iran na kutumia bendera ya Taifa, baraza la wawakishi Zanzibar, limesema Zanzibar kama sehemu ya Muungano wa haki ya kusajili meli ya Iran au nchi yoyote ile kwa maslahi ya Wazanzibar na kuwa taarifa na kelele zinazoendelea ni njia ya kutaka kuwakatika tamaa Wazanzibar kujiletea maendeleo..
Jamani WZNZ hawajui wanataka nini. Leo wamekubali kuwa ni sehemu ya muungano! si huwa wanasema ni nchi yenye bendera na wimbo wa Taifa sasa hii bendera ya Tanzania inawahusuje! Hawa watu hawajui wanasema nini leo na kesho watasema nini.
Haya yametokea ndani ya BLW! ZNZ ni tatizo, LET ZNZ GO!
 
Moja kati ya sababu za kuuanzisha Muungano wetu ilikuwa ni suala la kiusalama, Lakini kwa hili naona kama wazanzibar wanakwenda kinyume kwa lengo la kutimiza matakwa yao. Something has to be done katika mchakato wa kukusanya maoni ya katiba kwani naona ni suluhisho pekee kwa hivi karibuni, Kundi la usuluhishi wa kero za Muungano limeshindwa kabisa kuweka mambo sawa kwani katika kero zaidi ya kumi za kimuungano wamefanikiwa kuzitatua mbili tu katika vikao lukuki walivyokaa

Kwa upande wangu sina tatizo kabisa na Muungano, tatizo ni namna na aina ya Muungano. Kero za Muungano hazitakwisha kwa mfumo wa muungano tulionao, kwa sababu nchi hizi ni "dynamic" kila siku kuna mapya na kila siku kutahitaji mabadiliko, njia nzuri ni kuuvunja muungano uliokuwa wa watu wawili na kuufanya wa watu wengi, kwa sheria na njia na namna ambayo inakubalika na wananchi wa pande zote na kimataifa.

Mfano hili suala la Meli, hapa inajulikana Tanzania kimataifa lakini ukweli ni kwamba Zanzibar wana kanuni zao za usajili wa meli na huku bara tuna kanuni na sheria zetu za usajili wa meli ambazo zote zinakubalika kimataifa lakini zote kwa vigezo vyake.

Ukitazama kwa mfano huu na Muungano uliokuwepo utaona mapungufu yake, nadhani mfumo wa Muungano wetu uwe wa nchi mbili tofauti na kila moja iwe imekamilika "autonomous" na Muungano uwe kama huu tunaoujenga sasa wa Afrika Mashariki.
 
kinachonishngaza ni ujasili wa nchi kama tz kudefy orders za mtawala wa dunia yaani usa wakati nchi hata zinazotupamisaada zinafyta mkia! huyu jk safari hii ndo amekali kuti kavu? hivi watanzania hatujui kua bajeti yetu zaidi ya 40% inatoka kwa hawa jamaa wanaosema tusishirikiane na iran? je iran anaweza fidia iyo cut hawa jamaa wanayotoa iwapo wakikata hiyo misaada?
 
Back
Top Bottom