...labda Mkuu lakini nakumbuka juzi kusoma katika gazeti moja kwamba ujenzi wa barabara nyingi umesimama kwa Serikali kutokuwa na pesa na pia kutaka kuyalipa kwanza madeni ya nyuma ambayo ni zaidi ya shilingi 600 billioni kabla ya kuendelea na awamu nyingine za ujenzi.
Mkuu nakuelewa sana, ila wewe unaangalia kwa upande wa Rais, mimi naangalia upande wa CHAMA
Machelea kukubali approach yako kwani inamuangalia rais kama rais lakini upande wa pili unataka tena niangalie individuals.... labda kama tuko kibinafsi zaidi
Lakini kwa mtazamo wangu, we have to look at vyama kwani ndio challenge tuliyo nayo leo, tumefika kwenye janga hili kutokana na CCM kuendesha serikali kichama zaidi, hadi kikao cha juzi uliona jinsi walivyojaribu kuhamisha hoja iwe ni ya kichama zaidi, wameshabeza sana maamuzi ya maana ya wabunge wa chadema, walibeza kutoka nje wakati ule wa kuunda cabinet ya kipinzani, wakabeza wakati wa mchakato wa katiba nk. kujoin hapo bila kuwa na party reteat sio sahihi ... na hii si kwa vyama vya siasa, la hasha, sio sahihi kwa watanzania maskini (sio mimi na wewe kwani sisi tunaweza kujisemea) wasio na mtetezi
Nani aliyekwambia kikwete ataunda serikali ya mseto?!
Strategically it will be a wrong move especially kama atachagua from CDM,Itakua wrong move kwa Opposition side.Why?
1.Chama cha upinzani kitakachotoa waziri hakitaepuka kuitwa CCM B,C,D na kadhalika.Baraza hili halitakua na jipya katika utendaji kwa sababu tatizo ni system,hivyo chama kitakachotoa waziri kutoka upinzani kitakua kimejiharibia mwisho wa siku.
2.Serikali inatekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi.Waziri kutoka NCCR atatekeleza ilani gani? Hilo haliwezekani.
Asiguse CDM awatumie cuf na nccr
Kweli kabisa, wabunge walioteuliwa toka vyama vya upinzani watakuwa wanatekeleza ilani ya CCM katika baraza jipya la mawaziri. Hii itazidi kuipa nguvu CCM na kuzorotesha upinzani. Chadema wasikubali kabisa kuingia kichwakichwa kama NCCR
NI DAWA.Hatuwezi tukawaacha watu wazuri (tunavyosikia) kama huyo Janet, Mbatia, na Lipumba. Ila sidhani kama atachukua wengi, atajaribisha mmoja.Ila ni faida kuweka zadi ya mmoja, inaweza kuanza kuleta revolution ya kiuchumi
Nakubaliana na hoja zako, lakini kumbuka suala la uwaziri ni mtu binafsi na wala si chama. Hata kama chama wangekubali kuwa mbali na nafasi hizo, mtu binafsi mradi ni mbunge anaweza kukubali kuwa waziri kadiri ya dhamiri yake.
This is not proper. Huwezi kusimama peke yako bila kusimamia kwenye miguu ya chama chako. Na ukumbuke kuwa ubunge ulipatikana kupitia chama na sio mgombea binafsi.
Anaweza kugusa/kutumia chama chochote kwa maslahi ya kulijenga Taifa hili bila ulafi wa madaraka.
Asiguse CHADEMA awatumie CUF na NCCR
...CDM sioni mtu wa kuukubali uwaziri toka kwa Kikwete isipokuwa yule mganga njaa Shibuda....