Baraza la mawaziri la mseto ni dawa au mbinu za kisiasa?

Unaonaje wizara kama tatu hivi wangepewa wapinzania waonyesha utendaji, ingawa kule Tanzania visiwani hatujui tofauti ya utendaji serikalini kati ya wanaotoka CCM na wanaotoka CUF.

Mkuu hakuna utendaji unaopimwa kwa viongozi/wawakilishi watatu wa upinzani kupokea uwaziri wakati tuna ile dhana ya collective responsibility chini ya chama tawala.... maana yake utakua umewafanya hao mawaziri waripoti kwa CCM na vikao vya baraza la mawaziri vinafuata miongozo ya kamati kuu cha chama twawala............. especially kwa rais huyu wa sasa

it will be suicidal to chadema
 
Mkuu hakuna utendaji unaopimwa kwa viongozi wa upinzani wakati tuna ile dhana ya collective responsibility chini ya chama tawala.... maana yake utakua umewafanya hao mawaziri waripoti kwa CCM na vikao vya baraza la mawaziri vinafuata miongozo ya kamati kuu cha chama twawala............. especially kwa rais huyu wa sasa

it will be suicidal to chadema

Unakumbuka ilani ya uchaguzi kutoka CCM inashindwa kufanya kazi hata kununua bajaji tu, kinachoendelea ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chadema. Katiba ulikuwa ni mluzi wa kampeni za uchaguzi mkuu uliopita kutoka Chadama.

Unaonaje kama wakienda kusimamia Chadema wenyewe ilani yao ya uchaguzi ambayo serikali imeridhia kuifanyia kazi?
 
Unaonaje wizara kama tatu hivi wangepewa wapinzania waonyesha utendaji, ingawa kule Tanzania visiwani hatujui tofauti ya utendaji serikalini kati ya wanaotoka CCM na wanaotoka CUF.

...Sidhani kama kutakuwa na mafanikio yoyote yale kati ya sasa na 2015. Kwanza Serikali imefilisika na sioni dalili ya kubadilika kwa ukwasi wa Serikali hivi karibuni hasa ukitilia maanani nchi za wafadhili zinasuasua kiuchumi hivyo kuna uwezekano mkubwa wa kupunguza misaada yao kutokana na uchumi wa dunia kuyumba. Pia magamba wameamua kuzigawa bure rasilimali zetu (madini na misitu) ambazo zingeweza kuliingizia Taifa pato kubwa sana ukilinganisha na ilivyo sasa....labda yafanyike mabadiliko ya kweli kwa mfano kuwataka wachukuaji katika sekta hasa ya madini kuongeza mrahaba na kuanza kutozwa kodi kubwa kama hawatakuwa tayari kufanya hivyo waambiwe wafunge virago.

Kwa maoni yangu kama kutakuwa na Serikali ya mseto basi nafasi hizo zitolewe kwa vyama mfu TLP, NCCR-Mageuzi na kile chama cha Cheyo ili tuone kama watapewa ushirikiano kutoka kwa magamba na hivyo kuleta ufanisi katika utendaji...lakini ukitilia maanani kwamba 2015 haiko mbali na kule magamba vurumai za makundi ili kupenyeza mtu wao katika kinyang'anyiro cha 2015 zimeshaanza sioni la maana kufanyika.
 
Mkuu hakuna utendaji unaopimwa kwa viongozi/wawakilishi watatu wa upinzani kupokea uwaziri wakati tuna ile dhana ya collective responsibility chini ya chama tawala.... maana yake utakua umewafanya hao mawaziri waripoti kwa CCM na vikao vya baraza la mawaziri vinafuata miongozo ya kamati kuu cha chama twawala............. especially kwa rais huyu wa sasa

it will be suicidal to chadema

Kamati kuu ya Chadema imefanyika majuzi tu, unajuaje kama kulikuwa na ajenda ya siri kuhusu Baraza la mawaziri kugawiwa kiti na Kikwete? Kikwete jeuri sana unajua hilo?
 
Kamati kuu ya Chadema imefanyika majuzi tu, unajuaje kama kulikuwa na ajenda ya siri kuhusu Baraza la mawaziri kugawiwa kiti na Kikwete? Kikwete jeuri sana unajua hilo?

....Sijui bana kama hili litatokea, lakini kwa maoni yangu CDM itafanya makosa makubwa sana kuingia kwenye Serikali ya mseto inayoongozwa na msanii.
 
...Sidhani kama kutakuwa na mafanikio yoyote yale kati ya sasa na 2015. Kwanza Serikali imefilisika na sioni dalili ya kubadilika kwa ukwasi wa Serikali hivi karibuni hasa ukitilia maanani nchi za wafadhili zinasuasua kiuchumi hivyo kuna uwezekano mkubwa wa kupunguza misaada yao kutokana na uchumi wa dunia kuyumba. Pia magamba wameamua kuzigawa bure rasilimali zetu (madini na misitu) ambazo zingeweza kuliingizia Taifa pato kubwa sana ukilinganisha na ilivyo sasa....labda yafanyike mabadiliko ya kweli kwa mfano kuwataka wachukuaji katika sekta hasa ya madini kuongeza mrahaba na kuanza kutozwa kodi kubwa kama hawatakuwa tayari kufanya hivyo waambiwe wafunge virago.

Kwa maoni yangu kama kutakuwa na Serikali ya mseto basi nafasi hizo zitolewe kwa vyama mfu TLP, NCCR-Mageuzi na kile chama cha Cheyo ili tuone kama watapewa ushirikiano kutoka kwa magamba na hivyo kuleta ufanisi katika utendaji...lakini ukitilia maanani kwamba 2015 haiko mbali na kule magamba vurumai za makundi ili kupenyeza mtu wao katika kinyang'anyiro cha 2015 zimeshaanza sioni la maana kufanyika.

Kwa kweli si mambo mabaya hivi, kuna baadhi ya miradi imeanza kushughulikiwa sasa hivi.

Majuzi nilienda kutalii mikoa ya Kusini Nyanda za Juu, kilichonifurahisha ni kuona upanuzi wa barabara kuu ya TANZAM kuwa two lane kila upande ili kupunguza tatizo la ajali kutokana na hatari ya kuendesha magari kwenye lane moja tu na inapotokea overtake basi ni risk kupata ajali.

Na maana machache kati ya mengi yasiyofanyika yanafanyika.
 
....Sijui bana kama hili litatokea, lakini kwa maoni yangu CDM itafanya makosa makubwa sana kuingia kwenye Serikali ya mseto inayoongozwa na msanii.

Mimi mwenyewe nimeliona hili, ila ninachoweza kusema ni juu ya upande wa pili dwa shilingi.
 
Kwa kweli si mambo mabaya hivi, kuna baadhi ya miradi imeanza kushughulikiwa sasa hivi.

Majuzi nilienda kutalii mikoa ya Kusini Nyanda za Juu, kilichonifurahisha ni kuona upanuzi wa barabara kuu ya TANZAM kuwa two lane kila upande ili kupunguza tatizo la ajali kutokana na hatari ya kuendesha magari kwenye lane moja tu na inapotokea overtake basi ni risk kupata ajali.

Na maana machache kati ya mengi yasiyofanyika yanafanyika.

...labda Mkuu lakini nakumbuka juzi kusoma katika gazeti moja kwamba ujenzi wa barabara nyingi umesimama kwa Serikali kutokuwa na pesa na pia kutaka kuyalipa kwanza madeni ya nyuma ambayo ni zaidi ya shilingi 600 billioni kabla ya kuendelea na awamu nyingine za ujenzi.
 
Unakumbuka ilani ya uchaguzi kutoka CCM inashindwa kufanya kazi hata kununua bajaji tu, kinachoendelea ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chadema. Katiba ulikuwa ni mluzi wa kampeni za uchaguzi mkuu uliopita kutoka Chadama.

Unaonaje kama wakienda kusimamia Chadema wenyewe ilani yao ya uchaguzi ambayo serikali imeridhia kuifanyia kazi?

Mkuu nakuelewa sana, ila wewe unaangalia kwa upande wa Rais, mimi naangalia upande wa CHAMA

Machelea kukubali approach yako kwani inamuangalia rais kama rais lakini upande wa pili unataka tena niangalie individuals.... labda kama tuko kibinafsi zaidi

Lakini kwa mtazamo wangu, we have to look at vyama kwani ndio challenge tuliyo nayo leo, tumefika kwenye janga hili kutokana na CCM kuendesha serikali kichama zaidi, hadi kikao cha juzi uliona jinsi walivyojaribu kuhamisha hoja iwe ni ya kichama zaidi, wameshabeza sana maamuzi ya maana ya wabunge wa chadema, walibeza kutoka nje wakati ule wa kuunda cabinet ya kipinzani, wakabeza wakati wa mchakato wa katiba nk. kujoin hapo bila kuwa na party reteat sio sahihi ... na hii si kwa vyama vya siasa, la hasha, sio sahihi kwa watanzania maskini (sio mimi na wewe kwani sisi tunaweza kujisemea) wasio na mtetezi
 
Kamati kuu ya Chadema imefanyika majuzi tu, unajuaje kama kulikuwa na ajenda ya siri kuhusu Baraza la mawaziri kugawiwa kiti na Kikwete? Kikwete jeuri sana unajua hilo?

I do agree wanaweza walikua na ajenda... lakini bado tutarudi palepale.... itakua suicidal

It is a simple logic.... wananchi wameanza kuona kwamba CCM si mkombozi, na wameona hivyo kutoka kwa M4C, sasa leo wakisikia M4C wamekubali ajira kwa chama tawala, then ile trust itatoka; ni kama leo umseme rafikiyo mzinzi mlevi, mbaya halafu kesho ukiwa na family (who were the audience of your smear) wakuone umeshikana mkono na yule rafiki mbaya mnaenda kwenye starehe

WHETHER CDM AGREED OR NOT, IT IS SUICIDAL.... CCM WILL GAIN FROM THIS KULIKO CHADEMA WATAKAVYOGAIN, CCM IS SINKING, SO ANY OBJECT TO CATCH IS MROE VALUABLE
 
dalili ya mvua ni mawingu, hata isiponyesha leo kuna mategemea kuwa mvua yaja. Rais kikwete kuteua wabunge wapya kipindi hiki kabla hajasuka baraza la mawaziri, mmoja akiwa kutoka chama cha upinzani, ni dalili ya kunukia kuwa na baraza la mawaziri mseto kutoka vyama kadhaa vya kisiasa nchini.

Kuna mambo kandaa ambayo yanaweza kumsukuma kikwete kuchukua hatua hiyo, machache ya mambo hayo ni kama ifuatavyo.

  1. kujulikana kwake kimataifa anataka kujijengea jina zuri kabla ya muda wake kumalizika duniani.
  2. anamwiga obama ambaye ana baraza la mawaziri mseto kutoak democratic na republican.
  3. kuingiza dawa mpya kutoka upinzani ili kubutua mtandao wa wanaccm walafi.
  4. amekata tamaa kwa kutegemea wa kutoka ccm tu, kwani wanamwangusha kiutendaji
  5. anatengeneza mazingira mazuri atakapomaliza muda wake akubalike kama biblia isemavyo juu ya karani mbaya.
  6. wengi ndani ya ccm wana kashfa ya ulafi.

kunaweza kuwa na tafsiri nyingi, lakini uamuzi huo ni uamuzi mgumu ambao kwa mtazamo wa harakaharaka wanaccm wenzake wanaweza kufikiria amesaliti chama, lakini kikwete ameangalia zaidi utaifa, na kujenga nchi yanye kujiamini, kwani kutegemea ccm pekee mambo yanazidi kuharibika, na nchi haitawaliki.

all of the above
 
Dalili ya mvua ni mawingu, hata isiponyesha leo kuna mategemea kuwa mvua yaja. Rais Kikwete kuteua wabunge wapya kipindi hiki kabla hajasuka baraza la mawaziri, mmoja akiwa kutoka chama cha upinzani, ni dalili ya kunukia kuwa na baraza la mawaziri mseto kutoka vyama kadhaa vya kisiasa nchini.

Kuna mambo kandaa ambayo yanaweza kumsukuma Kikwete kuchukua hatua hiyo, machache ya mambo hayo ni kama ifuatavyo.

  1. Kujulikana kwake kimataifa anataka kujijengea jina zuri kabla ya muda wake kumalizika duniani.
  2. Anamwiga Obama ambaye ana baraza la mawaziri mseto kutoak Democratic na Republican.
  3. Kuingiza dawa mpya kutoka upinzani ili kubutua mtandao wa wanaCCM walafi.
  4. Amekata tamaa kwa kutegemea wa kutoka CCM tu, kwani wanamwangusha kiutendaji
  5. Anatengeneza mazingira mazuri atakapomaliza muda wake akubalike kama Biblia isemavyo juu ya Karani mbaya.
  6. Wengi ndani ya CCM wana kashfa ya ulafi.

Kunaweza kuwa na tafsiri nyingi, lakini uamuzi huo ni uamuzi mgumu ambao kwa mtazamo wa harakaharaka WanaCCM wenzake wanaweza kufikiria amesaliti chama, lakini Kikwete ameangalia zaidi utaifa, na kujenga nchi yanye kujiamini, kwani kutegemea CCM pekee mambo yanazidi kuharibika, na nchi haitawaliki.

Nani aliyekwambia kikwete ataunda serikali ya mseto?!
 
Hakuna uhasama katika suala ya utumishi kwa umma, mradi Rais akipima kwamba baadhi ya wabunge wa Chadema anaweza kuwaaminisha majukumu ya kumsaidia katika utawala ni jambo jema. Tuweni wastaarabu jamani, nch hii ni moja na sote ni watanzania, na tunawapongeza ambao wako tayari kututumikia kwa moyo na roho njema kwa manufaa ya nchi yetu.

Strategically it will be a wrong move especially kama atachagua from CDM,Itakua wrong move kwa Opposition side.Why?

1.Chama cha upinzani kitakachotoa waziri hakitaepuka kuitwa CCM B,C,D na kadhalika.Baraza hili halitakua na jipya katika utendaji kwa sababu tatizo ni system,hivyo chama kitakachotoa waziri kutoka upinzani kitakua kimejiharibia mwisho wa siku.

2.Serikali inatekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi.Waziri kutoka NCCR atatekeleza ilani gani? Hilo haliwezekani.
 
Yote yawezekana, kudhoofisha upinzani au kuimarisha uwajibikaji serikalini. Ujue Kikwete huenda anakuwa peke yake, hakuna wa kumwunga mkono kwa vile wenzake wanaangalia zaidi masilahi binafsi na chama chao na kuweka kiporo mambo ya manufaa kitaifa.

KIKWETE ni mwizi kama hao wengine,Ni mwizi nyuma ya pazia.Time will tell
 
Katika chaguzi zetu watu wengi wamekuwa washiriki kwa kutumia rushwa. Tutegemee nini kutoka kwao?
 
Sio lazima ni dawa, pengine ni njia au namna ya kufa. Mseto unaufanya na nani kwa ridhaa ya nani? Kama wananchi ndo wanautaka na ukazingatia maoni yao kweli inaweza kuwa dawa, lakini kijanja janja unachagua wanyonge wasio na support yoyote kwa umma eti unafanya nao mseto, mi naona ni namna ya kufa maana hata baada ya huo mseto shida zitabaki palepale, hapo ndo kifo kitafuata. Dawa ya mseto wa kisiasa ikitumika vibaya kama krolokwini utakufa tu.
 
Back
Top Bottom