Bigirita
Platinum Member
- Feb 12, 2007
- 15,986
- 7,367
Unajua ukibishana na kenge, utaonekana unamuonea wifu kwa vile ana magamba..........Hii hoja ya kuingia Ubungo Terminal imeanzia mbali kidogo lakini wenye akili zao wakaipuuza kwa sababu haina mashiko wala mantiki kwa somo lililopo mezani.
Naomba kuuliza, T.Shs. 200/= za kuingia Ubungo Terminal ni nauli?
Kinachozungumziwa hapa ni nauli tena ya Pantoni Kigamboni na siyo viingilio vya kuingilia sijui wapi; mtaanza pia kuhoji na sadaka tunazotoa sijui wapi ni za nini. Jamani, lets use common sense.
Labda tuwaulize hwa die hard wa Maghufuli, mbona hawatolei mfano wa parking ya Julius Nyerere International Airport.........kuingia na kumshusha mtu tu, ni Sh 500, ukikaa zaidi ya 1hr/2hr, charge inaongezeka to 1,000/=, Je mbunge wa eneo hilo anaona ni sawa?
Hilo linaitwa swali la kijinga, SAWA NA WANAOULIZA KIINGILIO CHA UBUNGO BUS TERMINAL NA NAULI YA KIBAHA TO UBUNGO.
NB: Sio kweli kwamba nauli ya Kiluvya Ubungo ni sh 900. Nauli ya Kongowe - Ubungo ni sh 900, hiyo ya Kiluvya Ubungo iweje iwe 900??