BAKWATA na Mauaji Arusha

Kwa hiyo haulaani mauaji ya Arusha kwa vile tu wakatoliki wamelaani? Halafu unajigamba kuwa haufuati mkumbo!

Amandla.....

Hapana Fundi Mchundo!!!,

Pitia thread zangu za nyuma nimeyalaani na kila mtanzania anapaswa kuyalaaani ila nachokipinga ni UNAFIKI WA KANISA KATOLIKI, kama unakumbuka mauaji ya mwembechai alitokea kasisi mmoja akadai serikali iwashungulikie waislamu, sasa leo imetokea arusha wanalaani. This is double standard. Sidhani wewe kama fundi mchundo utakubaliana nalo unless wewe huna morals!!!
 
There you are>>>>> changamsha ubongo ndugu, MWEMBECHAI hayakua maandamano ya waTanzania wapenda mabadiliko chanya kisiasa, ilikua ni suala la imani, katiba ya nchi iliyopo haitambui mambo ya Uislam wala Ukristo, inatambua kila mtu kwa imani yake...zaidi, kama Wakristo hawakutoa tamko kuhusu MWEMBECHAI wakati damu ya waTanzania ilimwagika, SHAME on them!!! Kosa na upumbavu wao isiwe sababu ya BAKWATA kunyamaza, kwanza CDM sio wakristo, ni Watanzania bila kujali imani....BAKWATA-Arusha wakinyamaza katika hili, na Wakristo wenye akili finyu wataanza kusema Serikali iliyopo ni ya Kiislam, tunaelekea wapi sasa?? Acha mawazo mgando, think BIG!!!
Nani alikuambia maandamano ya mwembechai yalikuwa ya kiroho? Nyie ndio mnafikra mgando mkuki ukikuchomeni mnataka kila mtanzania awaunge mkono ila ukiwachoma waislamu mnasema serikali imefanya vizuri sana. This era my friend hakuna mjinga stop whinning my friend katika hili muache kila mtu na mtazamo wake.
 
Usidharau Waislam pia,unaweza kutuambia tofauti ya Waislam wa sasa na wa Zamani??? Ujinga wa zamani ni upi na Ujanja wa sasa ni upi?? Nitajie wazee waliofuata mkumbo zamani...Acha kuandika utumbo...

Sijadharau ila nasema ukweli walifuata mkumbo ndio maana leo kuna matatizo mbali mbali kwasababu vitu vimefanyika kienyeji. Na ujinga sio tusi ni kutokufahamu ningelikuwa nimesema wapumbavu ningelikuwa nimewakosea adabu na mie sio mtovu wa nidhamu hivyo. NARUDIA TENA WAISLAMU WA SASA SIO WAJINGA MKUU STOP WHINNING WAACHENI BAKWATA WANAMAMBO MENGI YA KUFANYA TAMKO LA KKKT LINATOSHA.
 
Am just curious......hivi BAKWATA wanaweza kutoa tamko la kulaani mauaji yaliyotokea Arusha???
Tujiulize walifanya nini walipouwawa Wapemba 32? Hivyo nanyi tunakuulizeni mlikuwepo wakati ule au wale waliouwawa hawakuwa binaadamu?
 
Hapana Fundi Mchundo!!!,

Pitia thread zangu za nyuma nimeyalaani na kila mtanzania anapaswa kuyalaaani ila nachokipinga ni UNAFIKI WA KANISA KATOLIKI, kama unakumbuka mauaji ya mwembechai alitokea kasisi mmoja akadai serikali iwashungulikie waislamu, sasa leo imetokea arusha wanalaani. This is double standard. Sidhani wewe kama fundo mchundo utakubaliana nalo unless wewe huna morals!!!

Mkuu nisamehe sana kwa kukosea jina lako nimejaribu kuedit inakataa sasa sijui tatizo ni nini MOD naomba msaada pengine ni kijicomputer kangu kameishiwa nguvu
 
Msemaji wa Kanisa Katoliki ni Pope na sijamsikia akilaani mauaji ya Mwembechai au Arusha. Unakosea kulaani kanisa lote kutokana na udhaifu wa wafuasi wao. Kasisi wa kanisa katoliki si msemaji wa wakatoliki kama ilivyo mashehe wachache wanaoutukana ukristu wasivyo wasemaji wa waislamu. Umekuwa sensitive mno kwenye ishu hii. Kunyamaza kwa Bakwata hakupunguzi uzito wa msimamo wako wa kulaani mauaji haya kama ambavyo ukimya na upuuzi wa kasisi mmoja wa kanisa katoliki haukupunguza uzito wa wakristu wengine waliolaani mauaji ya Mwembechai. Ingekuwa Kasisi yule yule aliyeshangilia mauaji ya mwembechai angejitokeza kulaani haya ya Arusha, ningekuelewa.

Amandla.....
 
Bakwata wao wako after Kadhi na OIC they don't bother what is happening so long haihusu Kadhi mkuu ungewasikia kama askari wangeingia msikitini na mabuti shame on them.
Shame on you so much times!! Ulifanya nini walipouwawa watu kule Zanzibar ?
 
Mkuu nisamehe sana kwa kukosea jina lako nimejaribu kuedit inakataa sasa sijui tatizo ni nini MOD naomba msaada pengine ni kijicomputer kangu kameishiwa nguvu

Wala hamna haja ya kuniomba msamaha. Najua ni typo. Mbona mimi najiita Fundi Utumbo. Hata hivyo nashukuru sana kwa uungwana uliouonyesha.

Kama unataka ku-edit pengine ungejaribu baadae wakati hakuna watu wengi wanaojaribu kuingia kwenye sait. Lakini hata ukiacha hivyo hivyo hamna tatizo.

Amandla.....
 
Msemaji wa Kanisa Katoliki ni Pope na sijamsikia akilaani mauaji ya Mwembechai au Arusha. Unakosea kulaani kanisa lote kutokana na udhaifu wa wafuasi wao. Kasisi wa kanisa katoliki si msemaji wa wakatoliki kama ilivyo mashehe wachache wanaoutukana ukristu wasivyo wasemaji wa waislamu. Umekuwa sensitive mno kwenye ishu hii. Kunyamaza kwa Bakwata hakupunguzi uzito wa msimamo wako wa kulaani mauaji haya kama ambavyo ukimya na upuuzi wa kasisi mmoja wa kanisa katoliki haukupunguza uzito wa wakristu wengine waliolaani mauaji ya Mwembechai. Ingekuwa Kasisi yule yule aliyeshangilia mauaji ya mwembechai angejitokeza kulaani haya ya Arusha, ningekuelewa.

Amandla.....

Ok tuseme uko sahihi, ngoja nikuulize swali moja Kanisa Katoliki la Tanzania lilikuwa wapi kutokuomba radhi kwa matamshi ya yule paroko aliyoyatoa au alifikiri waislamu wana roho za mbao? Nimekuwa sensitive mkuu kwasababu vitu kama hivi ndio chachu ya ugomvi mie nadhani kanisa katoliki needs to reconcile na waislamu wakitaka ushirikiano na wao. Venginevyo mkuu itakuwa ni unafiki tu
 
Mimi natowa tamko la kuwalaani wote walioanzisha na kushadidia maandamano yaliyozuiliwa na polisi kufanyika.

Walaaniwe wote waliolazimisha ya fanyike na damu za hawa waliofariki ziwasute maisha yao yote.

WE KWELI TUTUSA KAMA SIO ZEZETA AU TAHILA.WEWE NI BAKWATA? You a fool person
 
Habari ya mwembechai ilikuwa na maslahi kwa kundi moja katika jamii, habari ya Arusha ina maslahi kwa taifa zima
Tunachozungumza ni roho za binaadamu. Hivyo wewe kitu cha mwanzo kwako kilikuwa kipa imara au CHADEMA? Hivyo waliouwawa kwa siasa na dini huwa tofauti kwako? DUH!
 
Ok tuseme uko sahihi, ngoja nikuulize swali moja Kanisa Katoliki la Tanzania lilikuwa wapi kutokuomba radhi kwa matamshi ya yule paroko aliyoyatoa au alifikiri waislamu wana roho za mbao? Nimekuwa sensitive mkuu kwasababu vitu kama hivi ndio chachu ya ugomvi mie nadhani kanisa katoliki needs to reconcile na waislamu wakitaka ushirikiano na wao. Venginevyo mkuu itakuwa ni unafiki tu

Lakini kwa nini unakazania Kanisa Katoliki likuombe msamaha? Yule hakuwa mwakilishi wa kanisa alipotoa maneno hayo sasa kwa nini Kanisa lihusishwe? Hivi kweli kila ambapo kasisi, buruda au mkatoliki mwingine akifanya kosa itakuwa haki Pope au Kadinali aombe msamaha? Mabaya mangapi wanafanya waislamu lakini hatuwasikii viongozi wao wakiyalaani? Ni hivyo hivyo ilivyo kwa wakristu. Wako wanaofanya maovu mengi tu lakini hauwezi kuhukumu kanisa zima. Kanisa halina ugomvi na waislamu sasa hiyo reconcilation ya nini? Au waislamu mna ugomvi na kanisa?

Amandla.......
 
Unataka kuniambia kuwa viongozi wa dini hawaruhusiwi kukemea uovu uliofanywa na vyombo vya Serikali, km Jeshi la Polisi, eti kwa hofu ya kuogopa kuchanganya dini vs siasa?

Ndio kwanza unaliona hilo leo? Haya si mauwaji ya kwanza hapa Tanzania.
 
Tunachozungumza ni roho za binaadamu. Hivyo wewe kitu cha mwanzo kwako kilikuwa kipa imara au CHADEMA? Hivyo waliouwawa kwa siasa na dini huwa tofauti kwako? DUH!

Ngekewa muulize huyu jamaa waliokufa mwembechai au Pemba walikuwa nani au walikuwa sio watanzania na walikuwa hawana roho? This is ridiculous Hebu kaeni kimya!!!
 
Lakini kwa nini unakazania Kanisa Katoliki likuombe msamaha? Yule hakuwa mwakilishi wa kanisa alipotoa maneno hayo sasa kwa nini Kanisa lihusishwe? Hivi kweli kila ambapo kasisi, buruda au mkatoliki mwingine akifanya kosa itakuwa haki Pope au Kadinali aombe msamaha? Mabaya mangapi wanafanya waislamu lakini hatuwasikii viongozi wao wakiyalaani? Ni hivyo hivyo ilivyo kwa wakristu. Wako wanaofanya maovu mengi tu lakini hauwezi kuhukumu kanisa zima. Kanisa halina ugomvi na waislamu sasa hiyo reconcilation ya nini? Au waislamu mna ugomvi na kanisa?

Amandla.......

Hujajibu swali ndugu kama umekasirika sina jinsi ya kukusaidia. Jibu swali langu do you think yule paroko wa kanisa katoliki tamko lake alolitoa wakati ule wa mwembechai kwanini kanisa lisitoe tamko la kuomba radhi!!!!
 
Usipoangalia unakaribia kupata ugonjwa unaowapata wengi wanaothamini dini kuliko haki unaoitwa fikramgandoosis. Unajua mission ya dini yoyote duniani? unapoona haki inakiukwa ni wajibu wa wapenda haki wote kukemea. kumbuka leo kwa mwenzio, kesho kwako. hakuna binadamu mwenye akili timamu awezaye kukaribisha hali hatarishi ya maisha ya viumbe wenye thamani kupita wote duniani-Binaadamu. Ni jukumu siyo la wapenda haki tu, bali la watanzania wote kulaani matumizi ya nguvu katika shughuli halali zenye haki za kikatiba ili kuilinda katiba yetu pamoja na mapungufu yake. Hapa natarajia hata viongozi wa serikali kulaani tabia za namna hii. hujasoma magazeti leo kwamba hata Rais Kikwete amesoneshwa na kilichotokea arusha na kuahidi kuwa hakitatokea tena? Hivi unadhani ni kwa nini serikali imefikia kuomba meza ya mazungumzo na wawakilishi wa wananchi-cdm kwa tukio la arusha? THINK THINK THINK kabla hujamwaga mawazo yako janvini
Hivyo dini yako haijali haki?
 
Ngekewa muulize huyu jamaa waliokufa mwembechai au Pemba walikuwa nani au walikuwa sio watanzania na walikuwa hawana roho? This is ridiculous Hebu kaeni kimya!!!

Hivi Bakwata waliwahi kuiomba msamaha jamii ya watanzania kwa kiendo cha Fupi na wenzake kulipua ubalozi wa Marekani? Au waliokufa na kujeruhiwa hawakuwa watanzania au watu? Mnaona how ridiculous hii blame game inavyoweza kuwa?

Amandla......
 
Wakati mwingine inasikitisha sana kuona ni jinsi gani hisia za kidini zinavyopofua watu katika jamii na kuleta mfarakano usio kuwa na msingi.
 
Back
Top Bottom