kuna vitu vinaitwa MALENGO na MKAKATI_lengo la wanaharakati wote kwasasa nikuona kunakuwa na Mabadiliko ya Kiutawala_mambo mengine yote ni Mikakati_hali kadhalika tuandikapo Posts huwa ni Mikakati kwa ajili ya mambo fulan tunayoyalenga_ni vema kufikiri sana kabla hujafanya jambo_kwa post hii nadhan umetuma wakati ukijisaidia choon_haimsaidii yeyote hata familia yako hainufaiki kwa post hii_otherwise mnatukatisha tamaa waislam tuliomo chadema kwamba inawezekana chadema ni ukiristo na sisi tunawasindikiza kwenye move zenu_kwann harakat za kisiasa zizungumzie iman wakat wanaharakat ni wenye iman tofaut na tunaunganishwa na MALENGO? Hii inanitia shaka na kunifanya niamin kuwa inawezekana mh. Zitto yupo sahih kuwa kuna udin ndan ya cdm_nimekuwa kwa muda mrefu nikikemea mambo haya na kuwaomba mods kupinga vitu_lakin posts zinazofutwa ni zile zinazokemea mambo haya ndizo hufutwa
Kwani ni lazima walaani kwa kupitia vyombo vya habari?Am just curious......hivi BAKWATA wanaweza kutoa tamko la kulaani mauaji yaliyotokea Arusha???
Usipoangalia unakaribia kupata ugonjwa unaowapata wengi wanaothamini dini kuliko haki unaoitwa fikramgandoosis. Unajua mission ya dini yoyote duniani? unapoona haki inakiukwa ni wajibu wa wapenda haki wote kukemea. kumbuka leo kwa mwenzio, kesho kwako. hakuna binadamu mwenye akili timamu awezaye kukaribisha hali hatarishi ya maisha ya viumbe wenye thamani kupita wote duniani-Binaadamu. Ni jukumu siyo la wapenda haki tu, bali la watanzania wote kulaani matumizi ya nguvu katika shughuli halali zenye haki za kikatiba ili kuilinda katiba yetu pamoja na mapungufu yake. Hapa natarajia hata viongozi wa serikali kulaani tabia za namna hii. hujasoma magazeti leo kwamba hata Rais Kikwete amesoneshwa na kilichotokea arusha na kuahidi kuwa hakitatokea tena? Hivi unadhani ni kwa nini serikali imefikia kuomba meza ya mazungumzo na wawakilishi wa wananchi-cdm kwa tukio la arusha? THINK THINK THINK kabla hujamwaga mawazo yako janvini
Habari ya mwembechai ilikuwa na maslahi kwa kundi moja katika jamii, habari ya Arusha ina maslahi kwa taifa zima
Mtu yoyote kuwawa sio kitu cha kufurahisha ispokua ni lazima tukubali mazingira aliyouwawa mtu yana mchango mkubwa ktk kufikia uamuzi kua aliuwawa kimakosa au hapana. Sidhani kua ni hekima kusema kua mauaji ya muembe chai yalikua ni halali kwa kua wale watu walipigania maslahi binafsi na maandamano ya juzi yalikua na maslahi kwa taifa zima.
Ni muhimu kua na utaratibu ktk ufanyaji wa mambo na ni lazima utaratibu ufuate, Ninafikiri kua maandamano yalizuiwa na serikali kwa sababu zinazohusiana na uslama, sasa kama kituo cha polisi kilitiwa moto na watu wengine walitaka kuwatoa watu ktk kituo cha polisi kwa nguvu. yoyote anaweza kuona kua hiyo haikukaa sawa.
Mpaka sasa tunapata sana information za upande mmoja ule unaolaumu kua umefanyiwa dhuluma, tusubiri serikali nayo itoe maelezo kua kwanini hali ilikua vile au mazingira gani yalipelekea ile hali kutokea.
Wengi hawaoni kua kuna change yoyote kubwa inayoweza kufanyika hasa ukizingatia ni juzi tu tumemaliza uchaguzi.
BAKWATA ni chombo ya WAGALA ambao wako Serikalini
pia msisahau kuwa BAKWATA iliunda na Serikali
majority ya waislam hawaitambui
In otherwords Bakwata is just one of many organisations kama vile Baraza kuu, Shura ya Maimam, SUPTAM na wengineo sema BAKWATA wanaenjoy kupewa niceties na serikali
And dont get me started on Sheikh Mkuu wa BAKWATA wa DSM....
I means seriously Bakwata inaongozwa na mtu iliterate halafu mnataka muone Tamko lao?
Hivi mnawa rate so high hawa jamaa?
Mimi natowa tamko la kuwalaani wote walioanzisha na kushadidia maandamano yaliyozuiliwa na polisi kufanyika.
Walaaniwe wote waliolazimisha ya fanyike na damu za hawa waliofariki ziwasute maisha yao yote.
Hivi KKT nao walilaani maiuaji ya MWEMBECHAI?
Am just curious......hivi BAKWATA wanaweza kutoa tamko la kulaani mauaji yaliyotokea Arusha???
Bakwata hawajaungana na Chama Cha Domo Endelevu la Maaskofu(CHADEMA)
Kanisa heri linyamaze na kufunga mdomo maana kila nikikumbuka mauaji ya kimbari Rwanda huwa nasikitika sana Kanisa linapoongelea juu ya haki! kila nikikumbuka mauaji ya Mwembechai Dar, na kauli alieitoa Padri Lwambano kuwa Serikali iwashugulikie Waislamu wa Msikiti wa Mwembechai na siku ya pili Polisi waliitikia wito huo na kuuwa wananchi wenzetu! nasikitika tena Kanisa kuhubiri haki!
Kila nikikumbuka mauaji ya raia huko visiwani na kauli ya Muadhama Kardinali Pengo kuwa waliouliwa na Polisi huko Zenji ndio wabebe lawama kwa kutokutii amri ya Serikali ya kutokuandamana!!
Sasa, leo Kanisa na Baraza la Maaskofu watakuwa na ubavu gani wa kujitokeza na kulaani mauaji ya Arusha?
Kuna watu wengine wapumbavu watakao fikiri kuwa mimi nafurahia mauaji ya Arusha lakini kwa hakika kila binaadamu mwenye hisia hatafurahia kitendo hicho cha Askari wetu kufyatua risasi za moto na kuua wananchi! ni tendo la kulaaniwa lakini sio Maaskofu wajitokeze leo ghafla na kutoa kilio cha kinafiki! kwanza waombe msamaha kwa maovu waliofanya huko nyuma kwa kuunga mkono maamuzi ya Serikali ya Benjamin Mkapa ya kuuwa raia wa nchi hii na ndipo wafungue ukurasa mpya wa kudai haki za wananchi kinyume chake itakuwa vigumu kuelewa lengo la Kanisa ni nini!
BAKWATA si chombo halali cha waislamu wala chombo hiki hakina ridhaa ya Waislamu bali Serikali inaibeba kwa amri ya Mwalimu Nyerere ambae kwa hakika ndie alie asisi mwaka 1968 huko Iringa baada ya kuvunja jumuiya ya Waislamu ya EAMWAS! ambayo iliwaletea Waislamu maendeleo makubwa na kutaka kujenga chuo kikuu cha kiislamu cha Afrika Mashariki ndipo Nyerere akafikia uamuzi huo wa kuivunjilia mbali! soma: Mwembechai Killings
Hivyo BAKWATA walaani au wasilaani hiyo sio issue kwa Waislamu bali Waislamu wanajumuiya zao zinazowakilisha maslahi yao na kama kutoa kauli basi ni viongozi wao ndio watatoa lakini sio BAKWATA!
Cityboy hebu rudi tena.....Maaskofu wana ubia na CDM au wana 'memorandum of understanding' na serikali kama mlivyokuwa mnadai hapo awali?
Ndio serikali ina MOU na kanisa.MOU uliingiwa wakati wa mkapa na kanisa lilikua na sauti kuu juu ya serikali.Soma fact za Kadogoo hapo juu.Wakati huu wakristo na matamko ya kilaleo ili tu nafasi irudi huku wakitafuta mbadala ambao ni kupitia cdm.Tazama humo cdm kulivyo na udini,tena ukatoliki ukiwa zaidi ya waunga mkono wengine.Kanisa lina hangaikia nguvu za kuuangamiza uislam na JK amewasoma ndo maana mwaka2010 hakua chaguo la Mungu tena kwani mlivyoni ni wa kuburuza tu sivyo!Kampeni zenu tunazijua A to Z upo hapo?
Unataka kuniambia kuwa viongozi wa dini hawaruhusiwi kukemea uovu uliofanywa na vyombo vya Serikali, km Jeshi la Polisi, eti kwa hofu ya kuogopa kuchanganya dini vs siasa?
Rejea tamko la kanisa juu ya mauaji ya Zanzibar.Kama unakumbukumbu naomba unijibu. Zanzibar walokufa ni waislam.Kanisa na cdm lao moja! Upo?
Kwa hiyo MoU ukomo wake ilikuwa ni 2010?