BAKWATA itakufa CCM ikiondoka madarakani

Wewe ni GREAT THINKER...
Sipendi kusema bakwata wana njaa, sipendi kusema bakwata wanatumiwa kama condm au t.paper, sipendi kusema waislamu wantumiwa. Napenda kusema kuwa imekuwa rahisi kwa CCM kutumia vikundi vya watu wachache kwa jina la Bakwata, kwa sababu ya udhaifu wa ama sheria, au taratibu au katiba inayoongoza bakwata. Sio rahisi ukasikia paroko wa kanisa fulani, pengine na halmashauri ya walei ya parokia husika, imekutana na waandishi wa habari na kusema 'kanisa katoliki linatoa msimamo huu wa kisiasa'. Sio kwamba katika kanisa katoliki hakuna mapadri wanaoweza kutumika, ila kwa sababu akijitokeza padri akaongea havyo hawezi kusikilizwa kwani utaratibu ni kwamba, mambo kama hayo lazima yapitie katika baraza la maaskofu Tanzania.
Kama mtu anataka 'kuwatumia' viongozi wa wakatoliki kisiasa, inabidi alinune baraza zima la maaskofu Tanzania, ili waweze kuwa na msimamo mmoja, hata kama ni issue inayohusu wilaya au hata kijiji fulani peke yake.
Tatizo la BAKWATA kama nilivyoeleza awali ni kuwa kiongozi yeyote wa Bakwata katika level hata ya wilaya, anaweza kuitisha mkutano wa waandishi wa habari na kutoa msimamo wa BAKWATA (inafanana na UVCCM).

Hii inaweza kuonekena just a simple thing, lakini niwaambie tu kuwa bila shaka itaathiri sana mshikamano wa waislamu nchini, hasa yanapoguswa maslahi ya kitaifa kama siasa. Kwa kipindi kifupi kisichozidi mwaka mmoja, kumekuwa na matamko mengi ya kisiasa yanayotoka BAKWATA. ijui ni kwa kiasi gani yanakuwa yamefanyiwa utafiti, lakini nahisi haya ndiyo yatakayoifarakanisha jamii ya waislamu tanzania...
Wewe niGREAT THINKER..
 
Tatizo la waislamu ni kuwa uongozi wao hauna hierarchy, (hirakia). Mtu yeyote hata kama ni kiongozi wa msikiti wa mtaa, anaweza kuibuka akaita waandishi wa habari akasema 'waislamu tunato msimamo fulani'. Nadhani hii itawafanya waislamu wafarakane sana hasa katika kipindi cha vuguvugu la kisiasa.

mkuu umenena sisi waislamu ktk mfumo wetu.. Hatuna hierarchy uongoz ndio maana hata ustaadh maalim wa madrasa anatoa tamko linalotuhusu waislamu wote.
 
Kwa muda mrefu nilikuwa nikisikia kuwa Bakwata haipo kwa maslahi ya waislam,nikawa siamini kwa kuzani huenda kulikuwa na chuki miongoni mwa madhehebu ya kiislam.Tamko la bakwata tabora limenifanya niamini kuwa wapo kisiaza zaidi kuliko kidini.Kwamba wanawataka waislamu wote igunga wasimpigie kura mgombea wa chadema inaonyesha kuwa wanapiga kampeni.Hivi ni nani asiyejua kwamba suala la mkuu wa wilaya igunga lipo mahakamani? Bakwata inadhani waislam wote akili zao zinafanana na wao, hapana tumewastukia.Eti kabla ya kutolewa kwa tamko hilo walifanya kikao cha pamoja ccm kwenye hotel kwa mujibu wa Radio five Arusha 2:30 usiku ,hii ni aibu. Waislam tunapenda kuona chombo kinachotoa matamko baada kufanya utafiti sio kisiasa. Mfano mzuri ni namna kikwete alivyoijibu bakwata wakati wa baraza la Idd,ile ni aibu,hivi zile shule za bakwata zilizopo zinafanana na seminari za kikristo kwa ufaulu na uendeshaji wake.Haya ndio mambo ya kujadiliwa na bakwata na si kupigia kampeni ccm.
Mimi nimewaelewa Bakwata, wao walichokasirishwa ni kauli iliyotumika wakati wanamkamata mama kimario walisema hivi "....unadhani hapa ni msikitini....." na wakamvua mtandio wake, sema wao waislam wamekosa msamiati wa kuibuka nao juu ya suala zima. Sema sasa ukweli kuufahamu ni ngumu mpaka wahusika wa pande zote waseme ni kauli gani zilizungumzwa, na hapo inavyoonekana mama kimario naye ni mzushi maana ameongea vitu vya kiongo mfano "...nimepoteza simu ya ...laki nne...." ni maneno ya kimtaani zaidi, so the wholly issue is dump!!
 
Tatizo la waislamu ni kuwa uongozi wao hauna hierarchy, (hirakia). Mtu yeyote hata kama ni kiongozi wa msikiti wa mtaa, anaweza kuibuka akaita waandishi wa habari akasema 'waislamu tunato msimamo fulani'. Nadhani hii itawafanya waislamu wafarakane sana hasa katika kipindi cha vuguvugu la kisiasa.
Jamani, hapa tunazungumzia BAKWATA na sio waislamu. Kufanya hivi mnawaonea waislamu wasio na uhusiano wowote na BAKWATA.
 
Tatizo waislam kupitia Bakwata tunatumiwa kama Kondom na ccm kwa kuwalinda na wakimaliza shughuli yako hututupa na kutotukumbuka tena. Jamani tuamke, tutatumiwa mpaka lini kwa masilahi ya wanasiasa??

Chagueni viongozi wenye elimuuuuuuuuuuuuuu! mwe hivi hamjui tatizo lenu kweli au ni makusudi
 
Tulisha wajua na yaleyale Siasa za magamba za "maji ya chooni" sasa ni ushirikiano wa BAKWATA..
 
WAISLAMU na BAKWATA mimi mbona nimechanganyikiwa? Mara tuambiwe kuwa CHADEMA hawawapendi Waislamu! Halafu hapo hapo Katibu wa CCM tena anaitwa WILLSON Mkama anasema CHADEMA imeleta makomandoo 'magaidi' toka nchi za Kiislamu, Afghanstan, Pakistan na Libya na palestina! Du! Siwezi kugombana na rafiki zangu Waislam kwa sababu za wachumia tumbo wachache wanaoutumia Uislamu kama daraja la dharura! Tena hao CCM wanajifanya kutetea suala la mkuu wa Wilaya wengi wao ni Wakristo! kweli wanatuonea huruma Waislam au njaa zinawasumbua?
 
Kuweni makini sana na hawa wachumia matumbo wanaoitwa CCM, walaghai na wezi wakubwa hawa
 
Hee -- mnabishania nini? Kuna thread moja katika Jukwaa la habari Mchanganyiko inasema DC huyo, fatuma kimarion wala siyo Muisilamu, ni Mkatoliki aliyebatizwa katika porakia ya Mbezi Beach, na kuna ushahidi pale. Mme wake Joseph Kimario ni Mkatoliki.

Hivyo huyo DC ni tapeli mkubwa anayetaka kuleta vurugu za udini hapa nchini na tonangoja kuona serikali hii ya kidhalimu itamfanya nini.
 
Misimamo hii inaongeza mvuto wa CHADEMA kwa waislamu..hongera

waislamu hawajaambiwa waichague cdm kwa uislamu wao, wala hawajaelekezwa waipinge ccm kwa sababu wao ni waislam, sababu zipo kwenye utaifa.
 
Mimi ni muslim, ila nakiri kuwa viongozi wengi wa bakwata elimu dunia hawana kichwani. Wanatumiwa kwakuwa hawana shule kichwani.
Maskini BAKWATA! Imegunduliwa kuwa huyo mkuu wa wilaya ya Igunga hata siyo mwislamu! Sasa mtuambie tamko lenu la laana kwa chadema bado ni halali au feki? Siku nyingine msikurupuke na matamko bila kufanya utafiti! Haya ndiyo matatizo ya kuwa na mashehe uchwara wa darasa la nne!
 
09_11_72rf7k.jpg

Huyu Maulid Athman Mussa, katibu wa BAKWATA, alifanya hamaki na haraka kutoa tamko lake, wakati alipopata maelekezo toka ngazi ya juu, na ilimpasa awakusanye wazee ambao ndio wenye bakwata pale Igunga, kisha angewaeleza msimamo huo na wangemshauri.. tunasikitika kwa kitendo chake cha kudhalilisha umma wa waislam kwamba ndio wametoa tamko hilo..BAKWATA ina wasomi na watu watulivu, sidhani kama ni busara mtu akisema sisi wakristo, au sisi waislam tunasema hivi au vile. nadhani ni busara kusema mimi hapa nasema hivi au vile.
lakini pia Mtoto akimtukana Jirani yako, na wewe usimuonye ni wazi jirani yako atajua umemtuma, na umekubaliana na matusi yake, nashauri wazee wa BAKWATA, naojua ni watu wastaarabu wangeweka msimamo wao na kukomesha udhia wa kutumia dini kama kinga ya kupata kura.
na hii mambo ya kuwaita hawa masheikh, hawa mapadre, hawa masista.. mie siipendi sana humu jamvini..
hayo Fatma mwenyewe huyo.. siku ya pili yake ofisini kwake akiongea na waandishi wa habari, haya sasa hijabu iko wapi, mama wa watu mkristo mla kitimoto kwa kwenda mbele, kisha watu wengine wanatuchanganyia habari.
hata kama farma angekuwa muislam, basi bakwata wangewanyoshea vidole wale vijana waliomtoa baibui lake, ambao ni waislam akina Anwaar kashanga. na si kuhukumu chama fulani cha kisiasa. ni mchezo mchafu sana huo. ni dhambi..
 
Bakwata at least sasa inaanza kujua wajbu wake ilikuwa ipo kisiasa zaid sasa kimeamka ni kuwatetea waislam kwenda mbele l
Maskini BAKWATA! Imegunduliwa kuwa huyo mkuu wa wilaya ya Igunga hata siyo mwislamu! Sasa mtuambie tamko lenu la laana kwa chadema bado ni halali au feki? Siku nyingine msikurupuke na matamko bila kufanya utafiti! Haya ndiyo matatizo ya kuwa na mashehe uchwara wa darasa la nne!
 
Sorry wadau, tunavyotoa comment za kukejeli dini ya watu, tunaonesha wazi nia yetu sisi wakristo kama tunawakeli waislam, ambao ndio hao hao wapiga kura wa CHADEMA, tuache jazba tujadili hoja, hivi ni kweli waislam wala ubwabwa, darasa la pili, wacheza bao, hivi hakuna waislam waliosoma. Tuache jazba kwa maneno haya tunaoneka tunaongea maneno ya kijiweni na hatuna maana kuliko hata hao wacheza bao jamani
 
Me sijafamu Bakwata, wanatetea mtu au Vazi! nasi tusikirupuke maana kesho anaweza kuvuliwa m2 msalaba, na kukashifu ukristo, ina maana wakristo tukae kimya maana aliyevaa msalaba c mkristo, nadhan umakini wa fikra unahitajika ktk suala hili
 
Hivi sasa hivi ndio tumekumbuka kuwa udini haufai?.Uchaguz wa mwaka jana CDM ililalamikiwa sana na waislam kutumiwa na TEC.Waraka wa maaskofu na kauli zao zilionesha dhahiri chuki dhidi ya JK na sio CCM. Lengo lilikuwa kumuangusha ili waislam waonekane hawafai, maana alitishia interests zao kama madhehebu yote kulipa kodi na ukiangalia wanufaika wakubwa ni wao.

Hivyo ndg zangu tuache kusema ooh waislam hawajasoma wanatumiwa.Nakumbuka ktk kampen za 2010 dk slaa kule bukoba alipanda jukwaani na masista 5 huku wamevaa vilemba vyao wanashangilia sana na mapadri walikua wamejazana wengi wamevaa kiraia.Wana bukoba wanafaham CDM ni nini.

HEBU TUITISHE KONGAMANO LA KITAIFA KUJADILI MAMBO HAYA TUACHANE NA KUSHUTUMIANA.
 
Back
Top Bottom