Edwin Chapa
Member
- Jun 3, 2011
- 54
- 12
Wewe ni GREAT THINKER...
Wewe niGREAT THINKER..Sipendi kusema bakwata wana njaa, sipendi kusema bakwata wanatumiwa kama condm au t.paper, sipendi kusema waislamu wantumiwa. Napenda kusema kuwa imekuwa rahisi kwa CCM kutumia vikundi vya watu wachache kwa jina la Bakwata, kwa sababu ya udhaifu wa ama sheria, au taratibu au katiba inayoongoza bakwata. Sio rahisi ukasikia paroko wa kanisa fulani, pengine na halmashauri ya walei ya parokia husika, imekutana na waandishi wa habari na kusema 'kanisa katoliki linatoa msimamo huu wa kisiasa'. Sio kwamba katika kanisa katoliki hakuna mapadri wanaoweza kutumika, ila kwa sababu akijitokeza padri akaongea havyo hawezi kusikilizwa kwani utaratibu ni kwamba, mambo kama hayo lazima yapitie katika baraza la maaskofu Tanzania.
Kama mtu anataka 'kuwatumia' viongozi wa wakatoliki kisiasa, inabidi alinune baraza zima la maaskofu Tanzania, ili waweze kuwa na msimamo mmoja, hata kama ni issue inayohusu wilaya au hata kijiji fulani peke yake.
Tatizo la BAKWATA kama nilivyoeleza awali ni kuwa kiongozi yeyote wa Bakwata katika level hata ya wilaya, anaweza kuitisha mkutano wa waandishi wa habari na kutoa msimamo wa BAKWATA (inafanana na UVCCM).
Hii inaweza kuonekena just a simple thing, lakini niwaambie tu kuwa bila shaka itaathiri sana mshikamano wa waislamu nchini, hasa yanapoguswa maslahi ya kitaifa kama siasa. Kwa kipindi kifupi kisichozidi mwaka mmoja, kumekuwa na matamko mengi ya kisiasa yanayotoka BAKWATA. ijui ni kwa kiasi gani yanakuwa yamefanyiwa utafiti, lakini nahisi haya ndiyo yatakayoifarakanisha jamii ya waislamu tanzania...