Bajeti yetu

OGOPASANA

JF-Expert Member
Apr 30, 2009
262
144
Habari wakuu, binafsi sijui lolote kuhusu mwanasiasa wala sina elimu kuubwa ila nahitaji kujua yafuatayo:
1 - Kuna ulazima wa kukopa fedha kwa wahisani (hasa mataifa ya wazungu) kwa rasilimali tulizonazo??
2 - Kuna umuhimu wa kufanya usiri kwa fedha zinazokopwa kwa manufaa ya taifa??
3 - Kwa idadi ya watu tulionao, ardi nzuri yenye rutuba, baadhi ya viongozi bora, sera na mikakati tuliyonayo inatushinda kupata mapato ya kuweza kukidhi haja ya bajeti yetu??
4 - Watanzania tuna haki ya kujua kiasi cha madeni tunayodaiwa kama nchi hadi sasa na nani wanaotudai kwa mujibu wa sheria na katiba???
5 - Watanzania wanaweza kupata nafasi ya kutoa maoni yao kuhusu uandaaji wa bajeti zetu kila mwaka kama tunavyofanya katika uundwaji wa katiba????
6 - Wananchi tunaweza kupewa haki na ruhusa ya kupitisha bajeti zilizowasilishwa bungeti na viongozi husika mara baada ya bunge kupitia na kupitisha???? (maana ni rahisi waziri kuwahonga wabunge ili bajeti yake ipitishwe)

nawasilisha.
 
Back
Top Bottom