Asante Bwana
Bajeti ya serikali ya Tanzania 2012/2013 (kiswahili). Kama kawaida inang'ata na kupuliza.
See the attachment.
Wana JF,
Baada ya kuisikiliza kwa makini hotuba ya bajeti jana naomba niseme hii sala fupi kumshukuru Mungu.
Mwenyezi Mungu, Muumba wa mbingu na Dunia, Wewe uliyeumba kila kitu. Tunakushukuru kwa mpango wako wa kuikomboa nchi hii toka mikononi mwa Ufisadi uliodumu miaka mingi. Tunakushukuru kwa mpango wako mzima wa kuwaamsha watanzania ili waamke toka usingizi wa uzembe, uvivu na woga kwa kuwawekea bajeti itakayowasababishia maisha magumu ili waanze kufikiria vinginevyo. Tunakushukuru kwa kuwa bajeti hii itawafanya watambue kuwa serikali waloiweka madarakani haina dhamira ya kujali maisha yao bali ni kujali maslahi ya viongozi na wawekezaji Mungu. Tunashukuru kwa kuwa bajeti hii haijaweza kuona ni wapi serikali inapoteza pesa nyingi Mungu. Bajeti inayolinda posho za vikao ambazo ni kwa ajili ya viongozi na wafanyakazi wa kawaida hawaingii kwenye vikao hivyo hawazipati. Tunashukuru kwa kuwa bado umezidi kuwatia upofu ili wasione umuhimu wa kukusanya kodi toka kwenye makampuni ya madini na mahoteli ya wawekezaji Mungu. Tunashukuru kwa kuwa umewaelekeza kuwa wazidi kutegemea kuendesha nchi kwa kutegemea walevi. Tunakushukuru kwa kuwa umewaonyesha kuwa mapato yanaweza tu kupatikana kwa kuwakaba wafanyakazi kwa PAYE na kuingiza kodi kwa machinga jambo litakaloifanya CCM izidi kuchukiwa. La zaidi Mungu tunakushukuru kwa kuwa bajeti hii haina mkakati wa kulipa malimbikizo ya mishahara na wala haina mkakati wa kuwalipa wakulima wa Korosho ambako CCM inadai ni ngome yake. Tunashukuru kwa kuwa chuki ya wakulima na wafanyakazi itaongezeka Bwana.
Baba Mungu tunazidi kukuomba ukazidi kuwatia hata wabunge wa CCM upofu ili wakazidi kuipigia makofu bajeti hii bila kujua kuwa malimbikizo ya mishahara na kutowalipa wakulima ni kifo kwa CCM.
Kwa hayo machache tunaomba na kushukuru. Amen.