Macos
JF-Expert Member
- May 12, 2008
- 1,979
- 1,416
bajeti yetu imesomwa...napenda kuuliza ni vipi bajeti hii itasaidia kuondoa umaskini ? Vipi itaongeza ajira? Vipi itapunguza vifo vitokanavyo na maradhi kwa masikini wasio kuwa na uwezo wa kujilipia matibabu? Vipi serikali inapanga kupunguza vifo vya wazazi na watoto ? Vipi inapanga kupunguza ama kuzuia maambukizi mapya ya h.i.v ,...
Kwa ufupi bajeti ya mara hii ukichambua inaonesha kama mwandishi alikua ana harkaa tu ya kuandika andika mambo ambayo haya jafanyiwa utafiti ama wasomi wetu wamechoka . Na nimesikia wachambuzi wengi lakini nao pia wame shindwa kuona mapungufu makubwa yaliopo
yafuatayo ni mapungufu na ambayo inafanya nbajeti hii kuwa mbovu kuliko zote duniani!!
Ubovu wa bajet ni mkubwa ila sasa naachia hapo kwa wengine kuchangia..ama kukusoa
Kwa ufupi bajeti ya mara hii ukichambua inaonesha kama mwandishi alikua ana harkaa tu ya kuandika andika mambo ambayo haya jafanyiwa utafiti ama wasomi wetu wamechoka . Na nimesikia wachambuzi wengi lakini nao pia wame shindwa kuona mapungufu makubwa yaliopo
yafuatayo ni mapungufu na ambayo inafanya nbajeti hii kuwa mbovu kuliko zote duniani!!
- kilimo...bajeti haijazungumza kabisa mikakati ya kuendeleza kilimo, japo bado tunaamini kilimo ndio uti wa mgongo wa uchumi wetu...waziri ameshindwa ama hakutaja kilimo kama ni priority..kuna matatizo ya chakula, kuna matatizo ya wakulima wa korosho , mahindi na mpunga(mchele) ameshindwa kueleza kilimo kinachangia kiasi gani katika bajeti ya taifa ama inachangia kiasi gani katika gdp ya taifa !!
- hakuna mipango yoyoyte mfano ya umwagiliaji maji mashamba, ama kuanzisha kilimo cha umwagiliaji , jinsi ya kutafuta masoko ya mazao ya kilimo
- waziri ameshindwa kueleza akiba ya chakula iliyopo na mikakati ya kuongeza akiba zaidi ili kupunguza bei ya chakula ..hakuna mipango yoyote iliyoitajwa kuhusu ruzuku ya mbolea ama matrekta.kwa ufupi waziri hakutaja chochote katika bajeti yake kuhusiana na kilimo...neno kilimo halikuwemo ndani bajeti hii isipokuwa kwenye msamaha kwa wazalishaji wa zabibu kwa ajili ya mvinyo!! Hiii ni ya mwaka kwa taifa linalojidai kilimo mwanzo lakini bajeti yake imesahau kuweka mikakati ya kuendeleza kilimo
- elimu..education...hakuna taifa litaloendelea kiuchumi bila ya kuweka mkakati madhubuti kuhusu kuendeleza elimu...waziri tulitegemea atasema mfano serikali itatoa ruzuku ya vitabu na madaftari bure kwa deprived community ama watoto wa masikini wasio jiweza,mipango ya kujenga nyumba zaid za walimu, mipango ya kuangalia maslahi zaidi ya walimu, mipango ya kuondoa tatizo la manamano ya wanafunzi wanao andamana kufatilia mikopo ya elimu..tulitarajia waziri atatenga bajeti ya kuwa na japi library katika shule za secondary ,kuzidisha uchapaji wa vitabu nk,...jee imetenga kiasi gani kuwapeleka watanzania njee kusomea fani muhimu za kukuza uchumi? Au ndio nafasi hizi mpaka tupate msaada tu? Ni wakati kwa serikali kuwa na mipango ya kupata wataalam walo bobea...na isongejee scholarship za bure.
- china walipo jua wanahitaji wasomi wali peleka watoto wao marekani kwa wingi kusomea fani mbali mbali..leo usione vya elea vimeundwa....bila ya elimu taifa huwa la wajinga
- kwa ajabu kabisa waziri ameshindwa kutaja elimu kama ni muhimu na kipaumbele katika bajeti yake ya ajabu...kwa ufupi neno elimu limetajwa mara mbili tu katika bajeti hii na halihusiani na sera ya elimu
- madini..na gas...waziri wetu ameogopa ana ameshidwa kabisa kutaja pato litokanalo na uchimbaji wa madini...waziri hakutaja mfano uchimbaji wa dhahabu na tanzanite una changia kiasi gani katika pato la taifa ama gnp.
- waziri ameshindwa kueleza makampuni hayo ya madini yatachangaia kiasi gani katika bajeti ya tanzania, wakati gold inapanda bei kila siku makampuni hayo yanashindwa kuwekea kodi itokanayo na faida wana yopata.
- serikali ingeweza kuongeza corporate tax kwa makampuni haya ya madini mpaka 35%
- windfall tax ingetozwa kwa makampuni haya ...na 10% ingesaidia kuondoa malalamiko kwamba sekta hii haisadii chochote kwa taifa.
- waziri ameshindwa kutaja kiasi ambacho kitachangiwa katika bajeti kutoka kwenye madini badala yake ..anataja sigara, bia , soda ,,,hii inashangaza sana
- waziri pia ameshindwa kutaja kampuni ya pan african inayo chimba gas songo songo itachangia kiasi gani katika bajeti ya taifa..hii kampuni inafanya faida kubwa sana kutokana na gas yetu
- waziri haku eleza taifa litapata kodi kiasi gani kutikna na watafutaji wapya wa gas , madini na mafuta, kume kuwapo na ugawaji mkubwa wa vitalu vya mafuta na gas,...na waziri ana shindwa kueleza hawa wata changia kiasi gani katika bajeti ijayo
- kuna wageni hawa wanao pewa vitalu vya madini na mafuta ..kuna mtindo wa kuuza hisa zao mara wanapo gundua upatikanaji wa mafuta ama gas...haya mauzo hufanyika nje na kwa mabilion ya dollari...bila ya tanzania kupata chochote .,..tungetarajia serikali ikaanzisha tax regime ya 25% kwa mauzo yoyote yatokanayo na vitalu hivi
- pia serikali inashindwa kuweka utaratibu wa ku-tax uuzaji wa shares kwa makampuni ya ndani kwa ma share wa nje...mfano ilipo uzwa celtell..na sasa royal palm kwa serena
- kwa ufupi waziri ameshindwa kufanya haya amabyo yangesaidia sana pato la taifa na ingesaidia kupunguza payee hadi tshs 500,000 badala ya kumkata kodi mlala hoi anepata mshahara wa 170,000...
- waziri hakugusia chochote kuhusu madini gas na oil exploration
- waziri hakugusia kabisa kuhusu afya ya watanzania na serikali imepanga kutumia kiasi gani kupuza maradhi na vifo kutokana na ukosefu wa huduma bora za afya
- maji nayo haya kutajwa....
- ama mambo mengine mengi mfano kubadili sheria za soko la hisa, ukweli utabaki kwamba soko hili letu ni kama halipo..jee mikakati gani serikali inayo kulifanya likue na lisaidie ukuaji uchumi? Mfano sheria zake za kwa makampuni kuweza ku ji list? Jee hazi hitaji kubadishwa? Jee hakuna uwezekano wa sheria kuruhusu kamapuni ndogo ( sme) kuweza kuwa listed?
- yapo mengi niliyo yaona katika bajeti hii ila ukweli sioni ni kwa vipi bajeti hii ina msaidia mlalahoi....labda kama yupo anaweza kunielimasha zaidi
Ubovu wa bajet ni mkubwa ila sasa naachia hapo kwa wengine kuchangia..ama kukusoa