Bajeti Mbadala Ya Upinzani 2008/2009.

UFISADI MWINGINE SIJUI VIONGOZI WETU NI VIPOFU? AU NDIYO WANAONUFAIKA?

79. Mheshimiwa Spika, Taarifa mbalimbali za kitafiti zinaonesha kuwa Tanzania inapoteza mapato mengi sana katika madini ya vito kwa sababu ya uzembe na ufisadi. Kwa mfano, Katika soko la dunia mauzo ya Tanzanite mwaka 2005 yalikuwa na thamani ya Dola za kimarekani 400m. Hata hivyo rekodi ya Tanzania ni Dola 16m tu.Tuna taarifa kuwa Kenya ilipata tuzo kwa kusafirisha Tanzanite nyingi duniani wakati hawana Tanzanite.
 
Bajeti ya wapinzania hata ya mwaka jana ilikuwa imesoma shule sana. Lakini kuna watu wanaendelea kuwaaminisha watanzania kwamba wapinzani bado hawawezi kutawala!

WAtanzania tu wazembe sana kwa kutoweza kuwafukuza watawala vilaza/wababaishaji madarakani.
 
UFISADI MWINGINE SIJUI VIONGOZI WETU NI VIPOFU? AU NDIYO WANAONUFAIKA?

79. Mheshimiwa Spika, Taarifa mbalimbali za kitafiti zinaonesha kuwa Tanzania inapoteza mapato mengi sana katika madini ya vito kwa sababu ya uzembe na ufisadi. Kwa mfano, Katika soko la dunia mauzo ya Tanzanite mwaka 2005 yalikuwa na thamani ya Dola za kimarekani 400m. Hata hivyo rekodi ya Tanzania ni Dola 16m tu.Tuna taarifa kuwa Kenya ilipata tuzo kwa kusafirisha Tanzanite nyingi duniani wakati hawana Tanzanite.

Sisi ni Wajinga. Kama balozi zetu zinaajiri Wakenya (Sweden, kama tulivyoambiwa na wana JF wa huko) tunategemea nini?
 
Sisi ni Wajinga. Kama balozi zetu zinaajiri Wakenya (Sweden, kama tulivyoambiwa na wana JF wa huko) tunategemea nini?

Tunafanyaje hili kuondoa ujinga wetu? Lakini kwa suala la Tanzanite nasikia Kenya wana sheria ukiweza kuuza kitu chochote nje ya nchi, iwe maua, tanzanite, dhahabu, kahawa nk hata kama haipatikani Kenya, ukitoa udhibitisho serikali inakulipa percent fulani.

Na hili ndilo limekuwa kichocheo ktk kupata malighafi kutoka Tanzania.
 
Ndesamburo ,anasema kuwa kuongeza pombe iwe ghali itawafanya wananchi kwenda kunywa Gongo ,na hilo litaongeza gharama za kuwatibia kwani watapatwa na magonjwa ya figo.

Haipongezi TRA kwani wao hawaji na njia mpya za kukusanya kodi bali ni zilezile na kila kukicha wanaongeza na kiuangalia hapo hapo.
 
35. Mheshimiwa Spika, matumizi halisi ya sekta hizi katika mwaka 2007/08 kama yalivyochambuliwa katika Hali ya Uchumi wa Taifa Jedwali na. 26, Elimu imetumia Shilingi bilioni 552.7 sawa na asilimia 51 tu ya fedha zilizotengwa. Sekta ya Ujenzi imetumia Shillingi bilioni 596.3 ikilinganishwa na shilingi bilioni 777.2 zilizotengwa kwa sekta ya Miundombinu ya barabara peke yake sawa na asilimia 76.7. Sekta ya Afya imetumia shilingi bilioni 373.9 ikilinganishwa na shilingi bilioni 589.9 zilizotengwa sawa na asilimia 63.4. Sekta ya Kilimo imetumia shilingi bilioni 151.4 ikilinganishwa na shilingi bilioni 379 zilizotengwa sawa na asilimia 39.9. Sekta ya Maji imetumia shilingi bilioni 208.3 ikilinganishwa na shilingi bilioni 309.1 zilizotengwa sawa na asilimia 67.4.

sasa kuna maana gani ya kuwa na bajeti kama haifuatwi?
 
Well, Ni upuuzi kujadili kitu ambacho ni uhakika100% no one will bother on it! Alafu kwani kuna tofauti gani na Kasheshe kufikiri angeifunga Taifa Stars siku ile walivyocheza na Cameroun... Hii naina tofauti... ukitaka kujua uhondo wa ngoma uingie kuicheza...

Hawa wako nje... na no-body anawa-question kwa kusema... hayo waliyosema and no body responsible...

Bajeti ya Serikali inaandaliwa na watu wengi sana... kuliko tunavyodhani... sasa ukiniambia watu watano...au kumi wanaweza kutengeneza bajeti ya Serikali... naona ndio upuuzi ule ule wa watanzania waku-dhani kila kitu chaweza kupatikana same day!!!
 
Mkuu Kasheshe

Kwa hiyo unataka kumaanisha kuwa walio tengeneza bajeti wa serikali mambo yanawapiga chenga?

Maana hao wachache wameonyesha mapungufu ya kutosha na pia kwa mtazamo wangu ni kama waandaaji wa serikali wamepelekwa shule.
 
Tutakaposikiliza upande wa pili tutajua ukweli!!! ... tatizo ni kwamba kwa kuwa tunaandika tu hapa!!! tukikosea sawa... tukiandika upuuzi sawa... ndio maana tunajiona sisi maprofessa wa bajeti ... wakati hakuna lolote!!!

Hakuna kazi rahisi huku duniani kama kukosea mwingine!!!
 
Ni kweli kuwa hakuna kazi rahisi huku duniani kama kukosea wengine.......

kama wewe unavyofanya kila siku ni kwa kuwa ni rahisi eehh
 
Back
Top Bottom