Bahari ni kiboko ya usafiri wa wachawi

Tulia wewe Mama,bado unafikra ya kuwa kuandika English ndio kujua?! I told u ukishindana na mimi na huo upuuzi wako na vineno vya kike hapa patakuwa pachungu kwako.
Wacha wee...joker of the post! I am enjoying you to the fullest
 
samahani kwa udadisi,wakati mchawi au mganga anapopandisha mapepo anaita mapepo'majini gani?
Kuna uchawi wa kutumia majini unaitwa uchawi wa kitabu
Kuna huo wa kuyaita mapepo
Halafu kuna huu wa tunguli
 
Clear King nafikiri ww Ndo huelewi issues, kama issue unaona haikuhusu Ni better kukaa kimya kuliko kUzidi kuongea! Kuna Upumbavu mwingi katika maneno
 
Kuongezea kidogo......uchawi wote duniani baba yake ni ibilisi (shetani) ila sasa wachawi ni binadam na wanatumia nguvu za giza kwa faida yao (wanayoiona wao)

Majini hawa ni automatical katika nguvu wanazotumia na hawategemei dawa ili kufanya maisha yake tofauti na mchawi, mganga anatumia majini na si mganga yeyote anaweza kuwatumia majini pindi akionyeshwa njia na kufuata maagano.

MGANGA ANATUMIAJE MAJINI?

Asili ya uganga asilimia kubwa upo njia mbili, uganga wa kurithi kutoka kwa babu, baba, bibi, mama nk haswa pale anapokufa na mikoba inataka kurithiwa ili iendelee kufanya kazi......na hapa sio kurithi tunguli au vitabu tu bali wapo majini wenye kusimamia vitu vyao na ndio maana ikiwa wewe ndio mrithi na ukakataa unaweza usibaki salama.

Njia ya pili ni uganga wa kukuchunuku, hapa majini hutokea kukuchunuku na wakakupa matatizo mbali mbali na mwisho wa siku kumbe wanataka uwe mganga.

Hapo nimekuonyesha ushirika wa majini na uganga (sio hawa matapeli)
Ipo njia nyingine ambayo ni uganga wa kujifunza ingawa haina nguvu sana ki utendaji.

Nikitulia nitaeleza juu ya tofauti ya majini na mashetani

Tofauti ya jini aliyeumbwa na aliyetengenezwa na binadamu

Tofauti ya majini wa bara na pwani nk
Na haitakua ni story bali ninayoona kwa macho
Asante sana
 
Mshana nimeshasikia watu wakisema kwamba mwanga anapokuja usiku kukuwangia anafanikiwa kama umelala ukiwa umezima taa na hivyo chumba Kuwa na giza totoro na kwamba kama umewasha taa hawezi kukuwangia? Hii umeshawahi kuisikia? Ina ukweli wowote? Pili nimesikia kama umeweka mifupa ya nguruwe kwenye pembe za nyumba yako mchawi hushindwa kuingia. Hii nayo ni kweli? Tatu Je kwa mfano kama nataka kumkamata mchawi aliyeingia ndani ya nyumba yangu kuna namna yoyote anaweza kunasa?
 
Hapa ngoja nimualike jichawi aseme neno
 
JE, KWENYE MWANGA MCHAWI HAWEZI KUKUDHURU?

Mchawi anaweza kukudhuru mda wowote iwe giza au mwanga au usiku au mchana, wengi hudhani wachawi hufanya yao usiku tu lakini hata mchana wanawajibika tena katika mambo ya kutisha iwapo ukiona unaweza kuogopa hata kutembea.

MIFUPA YA NGURUWE, BANGI JE NI KINGA YA WACHAWI?

Kwa kuwa uchawi ni mjumuiko wa madawa na yana masharti kama zilivyo dawa nyingine, vitu vyao vinakinzana na mifupa ya nguruwe na bangi kiasi cha kuwapa tabu wakati mwengine.
Ila pamoja na hayo uchawi ni sayansi kama nyingine, tafiti hufanyika na kugundua vyombo vizito zaidi hivyo achilia mbali bangi au mifupa ya nguruwe......unaweza wekewa zundiko la maana na wakatafuta mbinu zake baada ya mda wakaliuwa.

NAWEZA KUMKAMATA MCHAWI

Wanakamatwa wachawi na haswa pale wanapoingia pasipoingilika ila kumkamata sio ujanja ila kujikinga mwenyewe.

KWA NINI?

Kumkamata dawa zipo ila akianguka mmoja mda mfupi tu wachawi wa miji mbali mbali huitana kwa kikao cha dharura kujadili juu ya mwenzao na mbinu zilizomkamatisha, baada ya hapo wanahesabu umeidhalilisha tasnia yao na hukumu yao ni kukuuwa (iwapo utakuwa mwepesi)
Duh. Kazi kwelikweli
Ahsante jichawi.
 
Je wanaweza kuniua iwapo hawanijui? Si binadamu tungekua tunauwawa sana na hawa wachawi?
 
Mambo ya freemason viapo maagano ibada na hukumu zao ni vitu visivyojulikana kutokana na usiri unaotawala...hata haya tunayoandika ni mambo ya juu juu tu
lakini si kuna waty waliokuwepo kwenye iko chama wakajakujitoa badae na kutoboa siri zao.wengine waliuwawa wengine wapo.je hao c wametoa siri zao za maagano yao ??
 
lakini si kuna waty waliokuwepo kwenye iko chama wakajakujitoa badae na kutoboa siri zao.wengine waliuwawa wengine wapo.je hao c wametoa siri zao za maagano yao ??
Hao waliojitoa na wakabaki hai hawana madhara kwakuwa hawajui mengi na waliishia level za chini
 
Naam ila ukifuata nyendo zozote za wachawi hakikisha ni mzima kweli kweli na sio kufuata kwa kuwa huamini uwepo wao, utatafuta matatizo bure.

Umenikumbusha miaka mingi kidogo iliyopita tulikuwa mahali fulani katika milki za majini mimi na baba mzaa babu, nilikuwa bado kijana mdogo na kulikuwa kuna vitu vya kimizimu vinafanyika.

Akatokea mtu mwanamume wa dini fulani na kuanza kumuandama mzee kuwa hakuna majini duniani, uchawi wala chochote hivyo pale tunapoteza muda tu, mzee alikasirika na mimi nikawa nacheka (rabda kutokana na umri wangu wakati ule)
Mzee akampaka dawa fulani kijana na kumwambia tuongozane aone dunia.

Tukaondoka na kupanda gari la abiria na yule kijana maana nae alikuwa anaelekea tunakokwenda maana tunaishi nae mtaa mmoja, njian aliambia atakachoona asishangae akasema hakuna lolote.....ghafla akamtazama dereva na kumuona yupo uchi wa mnyama huku kiunoni kumejaa mahirizi!
Akahamaki, tukashuka na kuingia katika gulio akaona mama anauza maandazi huku anapepea na mkono wa mtoto mchanga unavuja damu! Kwa kuwa ni mara yake ya kwanza alipiga kelele na kuwehuka.......mama yule akamwambia "si umeniona? Na mimi nitakuona,,
Akh! Muhimu tumuombe Mungu lakini dunia ina mengi kama asemavyo Mkuu wangu Mshana
Akhsante mkuu kwa majibu murua
 
Kuua si kwamba ndio jambo la kipaumbele kwao ila pia inategemea iwapo umewakosea au la, ila pia wakati mwengine wanaweza kukudhuru bila hata kosa......baadhi ya mambo wanayodhuru watu ni kuwafunga rizki, kuwafunga uzazi, kuwapa maradhi, kufarakanisha, mikosi, vitimbi nk

Kuhusu kukujua wana uwezo wa kukujua iwapo wakitaka, hata uende ulaya wanaweza kukufuata (hapa ni wale wenye vyeo katika uchawi).
Kama ilivyo dunia ina mengi, majoka, majini, wanyama nk lakini bado tunaishi ndivyo dunia ilivyo
Dah we are leaving in a very strange world aisee. Kuna haja ya kusali kila unapopata upenyo kidogo katika kila siku. Asubuh mchana usiku. Sasa naona mana ya swala tano wanazofanya waislamu. Kuna pastor mmoja mnigeria aliniambia "pray when you cannot and pray when you can" "pray without ceasing and god will be on your side you will always be a winner". Sasa naona umuhimu wa kufuata maneno ya pastor yule
 
Jichawi: je wachawi wanapotaka kumdhuru mtu halafu wakakuta jamaa ni mtu wa mungu kwrlikweli (kwa sisi wakristo tunasema kampokea yesu) huwa wanapata shida gani? Wakikuta ni aliyetubu dhambi na kumpokea na kumuomba na kumtegea mungu kisawasawa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom